viongozi wenye mali nyingi hawatufai

ngapu

Member
Nov 18, 2012
41
1
Hawa viongozi wenye mali nyingi huwa hawana fikra na wenzao katika maslahi ya maisha kwa ujumla hivi utakuta vijiji hakuna maji safi hakuna hospitali bora hakuna barabara nzuri hakuna umeme lakini yeye huwa hana habari na hayo yote nakama akiamua kufanya msaada wala huwa hafilisiki halafu wananchi wanamchagua tena huko ni kuto kujua haki zenu hao muwakatae pia wasikushawishini hao hata kidogo
 

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,276
1,519
jana nilibahatika kufika maeneo ya Kongowe - vikuge , mkoa wa Pwani, kule nilikuta shamba zuri saana la serikali, linaloljihusisha na upandaji na uvunaji nyasi kwa ajili ya mifugo, nilipoliona shamba lile nilifarijika na kukasirishwa vilevile, kilichonikasirisha ni matunzo mabovu ya karakana , magari na matrekta pamoja na majengo. ukiyaangalia majengo yale utaona kuwa niyasiku nyingi na kukupa taswira kuwa mradi ule ni toka enzi ya MWALIMU NYERERE,kwa kiasi fulani nilifanya mazungumzo na maneja wa eneo lile na kugundua kuwa ni mtu mwenye upeo mkubwa saana na akiwezeshwa anaweza kufanya mambo makubwa saana. nilipomdadisi ni viongozi gani? waliwahi kufika hapa na kutoa msaada bila kusita aliniambia kuwa kiongozi pekee aliyewahi kufika na kutoa msaada wa gari na trekta ni EDWARD LOWASSA, kilichonifurahisha saana ni ukubwa wa shamba la nyasi na matunzo yake, hakika wanastahili pongezi na kuungwa mkono, nikirudi kwenye mada yako, binafsi siiungi mkono na zaidi inalenga kuwafanya viongozi wetu kuwa waoga ,kutumia fursa walizonazo kujitajirisha na kurudisha utajiri huo kwa wananchi. shamba lile nililoliona hata ww kama umeliona au ukibahatika kuliona na ukajenga mawazo kuwa yawepo mashamba kama yale 10, ktk mkoa wa DSM yakiwa yanamilkiwa na wananchi wakiwemo viongozi wetu, yatatoa ajira ngapi?, na yatashawishi wakazi wengi wa jiji, kufanya ufugaji na kuongeza kipato na lishe bora, vinginevyo hivi sasa kiongozi wa umma akiwa mbunifu na kutumia fursa zake vzr akiwa na shamba kubwa mithili ya yale niliyoyaona , tutamwita fisadi , hakika neno hili limeletwa na shetani kuwatisha viongozi wetu, ili tuwe masikini masikini wakutupwa,huku viongozi wetu wakishangaa umaskini wetu unaletwa nanini?,nendeni Kenya kamtazameni CHARLES NJONJO anashamba kubwa kubwa saana katikati ya shamba kaweka kiwanda, viongozi wetu igeni hilo, acheni kujaza madaladala,mnayogombania barabara na wastaafu wa ngazi ya chini, jengeni viwanda, fungueni mashamba makubwa mtupe ajira ,tuwapigie kura za ndiyo tukiwa wananchi wenu na watumishi wenu, hongera saana, EDWARD LOWASSA na hongera saana JOSEPH MUNGAI mmejaribu lkn bado.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom