Nilikuwa nafuatilia mazishi ya hayati BW Mkapa tangu mwanzo hadi mwisho. Niliona jinsi ambavyo rais wetu alivyo mtaka rais wa Zanzibar kuzungumza na wananchi wa Masasi na Shein alionesha kushtuka kwa hilo kwani hakuwa amearifiwa lakini alikwenda.
Pia akafuata Kikwete na baadaye Mwinyi. Wote walionesha kutofurahishwa na kitendo cha kukurupushwa kuongea bila kutaafiwa.
Anyway, kilichonifurahisha ni kitendo cha mh. Kikwete kuweka mambo sawa kuhusu ukuaji wa uchumi na mambo mengine mengi kama ninavyoyaweka hapa chini kwa kifupi:
1. Mpango wa kufikia uchumi wa kati uliasisiwa na Mkapa na lengo ni kufikia $3000 mwaka 2025 na kusema mpango huo serikali zote zimeufanyia kazi kwa hatua na sio jambo la serikali hii tu
2. Kikwete alionesha ujasiri mkubwa kwa kusema Mkapa alifanya mengi sana lakini hakuwa anapenda kusifiwa. Alitumia neno la kiingereza "populist" na kusema wazi kuwa Mkapa hakuwa populist ila wengi hawakumwelewa alimaanisha nini. Ukiwa kiongozi halafu ukawa populist ni mbaya sana na populist wanachukiwa sana popote kwani huvuruga siasa kwa kujipendekeza kwa namna sisizo nzuri kwa wananchi.
3. Kiwete aliweka wazi wazi kuwa mwaka 1995 kwenye round ya kwanza ya kura za maoni alimshinda Mkapa ila maamuzi ya chama yalimwelekea Mkapa. Na kwamba hata baada ya mchuano huo mkali Mkapa baadaye alifanya kazi kwa karibu na Kikwete na hapakuwepo na uadui. Rejea hatima ya Membe mwaka huu ndani ya CCM kwa kujaribu kumshindanisha JPM.
4. Kikwete aliweka wazi kuwa bado serikali hii ina kazi kubwa kufikia lengo la $3000 mwaka 2025 na kwamba sasa wamefikia $1080 tu bado $1920.
Kikwete alimaliza hatuba yake kwa kusema kuwa hiyo ndio gharama ya kukurupushwa kuongea. Ama kweli Kikwete aliuweka wazi ukweli bila kuogopa, sikutegemea hayo pale msibani.