'Viongozi wastaafu fikirini kama Plato'

'Viongozi wastaafu fikirini kama Plato'

MpendaNchi1

Member
Joined
Sep 25, 2021
Posts
7
Reaction score
4
Na. Mwandishi Maalum

Siasa chafu, za chuki na fitina zimetakiwa kusitishwa Afrika ili bara hilo liweze kupiga hatua za kimaendeleo.

Siasa hizo zinazoripotiwa miongoni mwa wanasiasa vijana na wakongwe kwenye majukwaa na vyombo vya habari, wanaharakati mitandaoni na baadhi ya viongozi wa dini, zimeelezwa hazina afya kwa amani, umoja, mshikamano, ustawi na maendeleo.

Demokrasia isiyozingatia mazingira na tamaduni za Kiafrika kwa upande mmoja, vyama vingi na chaguzi zake kwa upande wa pili, zimetajwa kuwa cheche ambazo hutumika kuwasha mioto na milipuko maeneo mbalimbali ya bara hilo ambapo imekuwa ikiulizwa wako wapi watu aina ya kina Nkrumah, Kaunda, Mondlane, Nyerere, Samora, Neto, Nujoma na wenzao wengine wanaoweza kufikiri kizalendo kuweza kuyaunganisha mataifa ya Afrika kwa mazingira ya sasa.

Wanasayansi ya siasa na utawala wanafahamisha, katika kila taifa suala la upigaji hatua haraka, jambo la kwanza linaloweza kufanyika ni wazalendo wa taifa hilo kuweka pembeni uchu wa madaraka na tamaa ya mali iliyopindukia na kuchora mipaka kati ya maslahi binafsi na maslahi ya taifa.

Hata hivyo, katika nchi nyingi za Afrika, pamoja na Tanzania kwa namna ya pekee, bado inashuhudiwa namna wanasiasa wanaojumuisha wastaafu serikalini wakigeukia uanaharakati wa kucheza kifitna mchezo wa siasa kwa gharama ya uhai na maendeleo ya wananchi.

Wanafalsafa wakongwe wa Ugiriki walikuwa mstari wa mbele katika kufundisha kwamba jamii isiyokuwa na umoja ni jamii iliyohukumiwa kuangamia.

Plato katika kitabu chake " Republic" akisisitiza nadharia yake ya "Philosopher King", alisema kwamba, wanasiasa wanapoongozwa na tamaa badala ya hekima, wanaligeuza Taifa lao kuwa jangwa la machafuko.

Aristotle naye aliongeza kuwa binadamu ni mnyama wa kijamii, na hivyo siasa inapaswa kutumika kuunganisha watu, siyo kuwatenganisha.

Wanasiasa kwa ujumla lakini wakongwe kwa namna ya pekee wangeyazingatia maandishi hayo wanayoyajua vema, wangetambua kuwa siasa za chuki wanazojaribu kuzipandikiza kwa vijana, ni kinyume cha mantiki ya uzee wenye hekima.

Hali halisi ni kwamba wakati baadhi ya viongozi wastaafu wangetakiwa kuwa mstari wa mbele kuhimiza umoja, mshikamano, amani na utulivu, wengi wao wamekuwa vinara wa kuchochea chuki na mifarakano kwa maslahi yao binafsi.

Wanapozungumza kana kwamba kwa niaba ya jamii, lakini kimya kimya lugha zao ni za kichochezi kugawanya kidini na kiitikadi ambapo kufikiri kwao ni kwa niaba ya kikundi chao kidogo, wakisahau kuwa historia haijawahi kuwasamehe wale waliotumia utu uzima wao, ukongwe wao na nafasi zao kuidanganya na kuivunja jamii waliyopaswa kuijenga.

Waalimu nguli wa taaluma za siasa na utawala kama Machiavelli na Max Weber walionyesha kuwa Taifa bila maadili huwa na maisha mafupi.

Machiavelli alisema kuwa mwenye hekima hutumia siasa kujenga uimara wa dola, siyo kuivunja.

Katika nyanja ya intelijensia na usalama, taifa lolote lisilokuwa na amani ya ndani haliwezi kuwa na akili ya pamoja ya kitaifa.

Henry Kissinger alisema kuwa nguvu halisi ya taifa haipimwi kwa silaha zake, bali kwa uwezo wake wa kuweka msimamo mmoja wa kitaifa.

Afrika imepoteza miongo mingi katika vita vya ndani, mapigano ya kikabila na migawanyiko ya kisiasa ambayo ingeweza kuepukwa kama wanasiasa wangekuwa wazalendo, wangechagua njia ya mazungumzo chanya badala ya chuki, lugha chafu na fitina.

Kiuchumi, nchi zinazogombana haziwezi kuvutia uwekezaji wala kutengeneza ajira endelevu.

Adam Smith katika "The Wealth of Nations", alieleza kuwa utajiri wa taifa hutegemea utulivu, sheria na imani ya wananchi katika mfumo wao.

Hali ya sasa barani Afrika ni kwamba mabilioni ya dola yanapotea kila mwaka katika migogoro ya kisiasa ambayo ingeweza kutumika kujenga shule, barabara, viwanda na kuwaletea hali bora wananchi.

Tanzania yenyewe imepoteza fursa nyingi kwa sababu ya siasa za mitaani, wanasiasa wenye uchu wa madaraka na wakongwe wasiotumia hazina za busara walizonazo kuleta maelewano katika jamii.

Wahitimu na wasomi wa fani ya sayansi ya siasa, utawala na uhusiano wa kimataifa wanafahamu kuwa, Historia ya Bara la Ulaya ilijengwa upya baada ya kusitishwa kwa migogoro na kusainiwa kwa Mkataba wa Westphalia mwaka 1648.

Kabla ya hapo, Ulaya ilikuwa uwanja wa vita na machafuko ya kijamii yakiongozwa na kanisa na yale ya kikabila yaliyodumu kwa miongo kadhaa.

Baada ya Westphalia, viongozi walielewa kuwa bila amani hakuna maendeleo.

Leo Ulaya ni kielezeo cha umoja wa kiuchumi na kisiasa, siyo kwa sababu walikuwa bora zaidi kuliko Waafrika bali kwa sababu walichagua kuacha chuki, fitina, majungu na kujenga mifumo ya pamoja.

Tanzania imebarikiwa kuwa na historia ya uongozi wa umoja kabla ya uhuru kwenye vyama vya TAA, AA na TANU na enzi za Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume.

Siasa ya Ujamaa ilifeli kiuchumi, lakini ilifaulu kisiasa kwa kuweka msingi wa UTU na UMOJA wa kitaifa.

Leo inaposhuhudiwa lugha za kugawanya zikitolewa na wale waliokuwepo zama.za Mwalimu , inapasa kujiuliza kama kinachotakiwa ni kurudi nyuma au kusonga mbele.

Maendeleo hayawezi kujengwa kwenye msingi wa chuki, kwa sababu chuki hutafuna hata ule msingi wenyewe.

Wanafikra wa kisasa wa maendeleo kama Amartya Sen wamesema kuwa maendeleo halisi yanapimwa kwa uhuru wa binadamu kuishi maisha anayoyataka.

Lakini uhuru huo hauwezi kupatikana katika jamii iliyogawanyika na yenye chuki.

Wakati vijana wanapoeneza fikra na kelele za chuki kwenye mitandao na majukwaa ya kisiasa, wazee wangetumia busara zao badala ya kuunga bogi hilo, wakijua wazi kufanya hivyo Taifa linajikosesha akili na nguvu kazi ya kizazi kipya kinachotakiwa kulelewa.

Afrika kwa ujumla ina rasilimali za kutosha kubadilisha uso wake ndani ya miongo michache. Ina ardhi, ina madini, ina vijana, ina soko kubwa la watu bilioni 1.4.

Kinachokwaza si ukosefu wa rasilimali, bali ukosefu wa uzalendo, visima vya fikra, busara, mifumo na dira.

Wanasiasa wengi wanatumia siasa kama mtaji wa kuwatoa kimaisha, kichaka cha biashara binafsi, na matokeo yake ni umasikini unaodumu miongoni mwa wananchi na vijana wanaokata tamaa.

Ili kuepuka mtego huo, ni lazima kuanza kusema wazi kuwa siasa za fitina ni uhalifu dhidi ya kizazi kijacho.

Mwanasiasa yeyote anayechochea chuki anapaswa kukumbushwa kuwa historia haiandikwi na hotuba zake kwenye mahojiano wala kelele majukwaani, bali na athari za matendo yake kwa maisha ya watu wa kawaida.

Mwananchi wa Morogoro, Tanga, Mwanza au Mtwara hawezi kunufaika na mahojiano ya chuki wala kufarijika na hotuba za fitina, alitaka anufaike wakati ukiwa kiongozi ikashindikana, hivi sasa anataka barabara, maji, shule, hospitali na maisha mazuri.

Mfano wa Rwanda baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 unafundisha mengi.

Nchi hiyo iliamua kusitisha siasa ya chuki na kuanzisha siasa ya uwajibikaji na umoja.

Leo Rwanda ni miongoni mwa nchi zinazokua kwa kasi barani Afrika, na sababu kubwa ni kwamba viongozi waliamua kuwa maisha ya mwananchi ni muhimu zaidi kuliko nafasi yao ya kisiasa.

Kwa upande mwingine, nchi zilizoshindwa kufanya hivyo zimebaki nyuma, siasa za chuki na "kukinukisha" hazIwezi kujenga taifa.

Wakati fitna na uchochezi ukiendelea kabla ya Oktoba 29, 2025 wazee wakongwe ama walikoleza au walipiga kimya kusubiri "litokee la kutokea", leo wanasimama kuhoji na kuzungumzia yaliyojiri kwa lugha za kichochezi.

Afrika mabilioni yanatumika kununua silaha, wakati shule zinafungwa na hospitali zinakosa dawa. Hilo ni somo kwa Watanzania wasilichezee.

Wakati dunia inaelekea kwenye uchumi wa maarifa na teknolojia, Afrika haiwezi kuendelea kuburuzwa kurejea kwenye siasa za karne ya 19.

Leo vita havipiganwi tena kwa mikuki, vinapiganwa kwa mawazo, ubunifu, vumbuzi, teknolojia na ushindani wa kiuchumi.

Nchi itakayoshinda ni ile inayoweza kuweka pamoja akili zote za watoto na wazee wake bila kujali kabila, dini au mkoa.

Hivyo basi, wajibu wa viongozi wakongwe ni kuwa nguzo ya amani, siyo miale ya moto.

Wana nafasi ya kipekee ya kushauri, kuelekeza na kukemea kila aina ya siasa inayogawanya na kuleta mifarakano. Sio wao kuwa sehemu ya kuchochea na kuleta mifarakano

Kama hawatafanya hivyo, historia itawahukumu kama watu walioleleka kwenye umoja na mshikamano na kuwa na ufunguo za umoja lakini baadaye wakachagua funguo za uharibifu.

Ni wakati sasa kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla kuamua wazi kuwa siasa za chuki hazitakiwi. Mleta chuki na mfarakano akanywe bila kujali umri na ukongwe wake.

Chaguzi, lazima ziwe na mstari mwekundu kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya jinai ya kuvunja amani ya taifa kwa ajili ya maslahi yake ya kisiasa.

Maendeleo yanahitaji "kafara" "na "dhabihu", na hiyo ni kuacha maslahi binafsi kwa ajili ya taifa.

Taifa lenye umoja ni taifa lisiloshindika. Kama Plato, Aristotle, Machiavelli na Weber wangesimama mbele leo, wangeongea kwa sauti moja ya jengeni nchi kwa hekima, wazee wakongwe ni kisima cha busara, si wapanda chuki.

"Westphalia" ya Afrika haiwezi kuja kutoka nje, inatakiwa ianze ndani, katika moyo wa kila mwanasiasa, kila mwananchi na kila kiongozi hasa wakongwe na wastaafu. Maendeleo ya Afrika yanategemea uamuzi huo.
WhatsApp Image 2026-05-13 at 20.26.33.jpeg
 
"Westphalia" ya Afrika haiwezi kuja kutoka nje, inatakiwa ianze ndani, katika moyo wa kila mwanasiasa, kila mwananchi na kila kiongozi hasa wakongwe na wastaafu. Maendeleo ya Afrika yanategemea uamuzi huo.View attachment 3588300
well done gentleman:KasugaYeah:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom