opwa
Member
- Jun 10, 2010
- 66
- 5
tangau kipindi nakua miaka ya 1980 sikuwahi kujiuliza hasa udini ni nini kwani niliamini dini ni njia tu ya kutukutanisha na mwenyezi mungu kama kweli yupo. lakini sasa nashangaa kuona kuwa viongozi tena top figures wanapojaribu moja kwa moja kuhusisha neno na matendo yanayo wagawa watanzania kwa mlengo wa dini zao, leo naona kabisa element za ubaguzi wa kidinn katika utendaji pia uwezeshaji katika sehemu mbali mbali hususani zenye mkono wa serikali, mwalimu wangu mmoja aliwahi kuniaminisha kuwa '' religion is nothing than opium of mind '' tena akaongeza kwa kuniambia '' religion kills reasoning and arose emossions '' sasa najiuliza hawa viongozi wanataka tutumie imani zinazotufanya mabubu kuchukiana wenyewe? au wanatakaje? elimu ye tanzania ya uraia inasema tanzania ni nchi isiyofungamaona na uzio wa dini yoyote, lakini katika hili viongozi wa sasa ni viziwi na vipofu, nikiuangalia mfimo wa uongozi napatwa na makanganyiko, nimedokezwa kuwa eti dodoma chuoni kuna mwananchi katishiwa hadi kutoweshwa uhai wake ikibidi kwa kuitwa adui kisa ni frateri wa kikatoriki....... roho inaniuma napoona hata zile sehemu nyeti ambazo vigezo nyeti vingetumika kutoa maamuzi basi dini flani ndo inawekeza vilaza wake pale. mataifa tunayo yapigia magoti kuomba misaada yakija jua ni vipi mnazifuja tena kwa kigezo cha udini mtapoeana huko magogoni, machaguo secondari na vyuo vikuu pia bodi ya mikopo nayatupia jicho la nne tu kwa kushauri kuwa mpeni anaye stahili anachostahili, tofauti na hapo tutarudisha taifa katika zile zama za ukabila na ukanda ikibidi uchama.....