Viongozi wakuu wa UKAWA watazungumza na waandishi wa habari jioni hii Colosseum Hotel

Naamini kabisa watatoka salama salimini kwa uwezo wa mwenyezi mungu .walianza na mungu na watamaliza na mungu .vivaa ukawaaa .
 
Baada ya majadiliano ya leo, kuanzia asubuhi, viongozi wakuu wa UKAWA watazungumza na waandishi wa habari jioni hii.

Vyombo vya habari tayari vimeshaalikwa kufika hapa Colosseum Hotel.

Tutawajuza kitakachozungumzwa. Tunajua Watanzania wanasubiri mwanga wa Tanzania ijayo chini ya uongozi wa UKAWA. Wanajua kupitia viongozi wa UKAWA, nchi itakuwa kwenye mikono salama kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Tanzania yetu.

Makene

Unajua wewe ni mtu mkubwa sana, sasa kutudanganya tunakuwa hatukuelewi. Si bora ukae kimya tu? halafu itakuwa chadema wanataka kila kitu wawe wao. Kama ukawa ikivurugika, najua ni chadema ndo chanzo. hivyo binafsi sitawaelewa kabisa
 
Toka jana najizuia kuandika nasoma tu maana... Dah

Anyway subira yavuta Heri, unajua ile ya Majambazi siri zilikuwa zinavuja zinakuja huku uraiani ila hii ya kwetu ni subira na usiri ukisindikiza kwa nyuma

Nitarud kukomenti kesho
 
kweli mpaka saa hii hakuna mpya! Kama walikuwa hawajaafikiana kwanini kutuweka roho juu juu hivi si wangesubiri wawe tayari ndiyo waseme! Inachosa sana
 
Maccm wenyewe kidogo wafarakane kwenye mchakato ni bahati .mzee wa mamvi amewahi kusaliti amri la sivyo mambo yangekuwa mengine.kwa nini iwe kwa ukawa ?
 
Unajua wewe ni mtu mkubwa sana, sasa kutudanganya tunakuwa hatukuelewi. Si bora ukae kimya tu? halafu itakuwa chadema wanataka kila kitu wawe wao. Kama ukawa ikivurugika, najua ni chadema ndo chanzo. hivyo binafsi sitawaelewa kabisa

Mkuu sio wewe tu hata mi sitawaelewa na sitapga kura kabisaa
 
Baada ya majadiliano ya leo, kuanzia asubuhi, viongozi wakuu wa UKAWA watazungumza na waandishi wa habari jioni hii.

Vyombo vya habari tayari vimeshaalikwa kufika hapa Colosseum Hotel.

Tutawajuza kitakachozungumzwa. Tunajua Watanzania wanasubiri mwanga wa Tanzania ijayo chini ya uongozi wa UKAWA. Wanajua kupitia viongozi wa UKAWA, nchi itakuwa kwenye mikono salama kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Tanzania yetu.

Makene

Hivi jioni huwa ni saa ngapi vile?
 
Mzee Vuta tuvutane jambo la muhimu tupate upinzani wenye nguvu ili wenye hila washindwe kupitisha mambo ya hovyo kwa mgongo wa bunge.
 
Hadi nachukia, upinzani gani huu? Siendi kupiga kura ng'o!!! Wale tuliowategemea ndio hao! Kila mmoja anataka aongoze yeye. Mpoto hakukosea aliposema:-
"...Waliopo hatuwatki, wanaotaka tuwape hatuwaamini"
 
mnajua utofauti wa huu mkutano wa UKAWA na ule wa CCM ni kwamba ule wa wale jamaa siri zilikuwa zinavuja zinatoka zinakuja humu jf fasta kwahiyo watu tulikuwa updated kabla hawajatoa habari rasmi.Sasa hawa UKAWA akuna kinachovuja yan hawa majamaa ni hatariii,wanatuacha tunahemea juu juu tu kwa shauku.
 
Ninyi mnavanya utani,tutakuwa katika mikono salama hata Lowassa akiwa Raisi!?Nawaonya mapema, mkimsimamisha Lowasa kama Mbowe anavyotaka na kung'ang'ania CDM imekwisha.Acheni tabia ya kuchumia tumbo.

Back
Top Bottom