vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 1,468
- 2,668
Kuna matukio mawili yameongozana yamedhihirisha ni wazi TFF ina watu wasiokuwa na uadilifu, wasiokuwa na maono na hawana upeo wa kufikiria, kuchambua vitu kwa kina.
Tukio la kwanza ilikuwa ni kitendo cha kupeleka fainali ya kombe la CRDB federation cup Manyara. Tukio la pili ni kitendo cha kuhamishia Zanzibar badala ya Manyara.
Tukio la tatu ni kitendo cha Simba kuamisha uwanja dhidi ya KMC na nyie TFF na bodi ya ligi mkalibariki.
Hiyo sio haki, timu za mpira wa miguu ni taasisi ambazo zinakuwa na mipango na mikakati yake kulingana na ratiba iliyokuwepo. Kitendo KMC kujulishwa kuwa mechi atacheza mechi na Simba Dar kwenye uwanja wa Isamuhyo, inawafanya wapange bajeti zao na ratiba zao kulingana na taarifa waliyoipata.
Ghafla timu iliyoomba uwanja wa Isamuhyo inabadili kwenda Arusha, ni kutowatendea haki KMC. Kuna gharama za safari hapo inajitokeza kitu ambacho KMC hawakuliwaza wala kujiandaa nayo. Simba wao wamejiamulia kwavile inauwezo wa kupanda ndege na pia wamesha organize mambo yao, je vipi huyu mpinzani wake? Au kwavile ni timu ndogo?
KMC hutumia usafiri wa bus kwenda mkoani, kucheza mechi hapo kuna muda kwaajili ya kusafiri, kuna muda kwaajili ya kupumzika kutokana na uchovu wa safari, na kuna muda kwa ajili ya kujiandaa na mchezo je hilo limefikiriwa kwa KMC? Au ndio KMC wanafanyiwa hujuma ili apoteze mechi au ashindwe kusafiri ili Simba ipewe point tatu na magoli
3. Hii ni hujuma ya wazi kwa KMC ambao wanagombea nafasi ya 4 dhidi ya Coastal union na pia upendeleo wa wazi kwa Simba ili washinde mechi kiurahisi. Kinachofanyika kwa KMC sio haki ni uonevu huo.