Viongozi wa kisiasa wana kinga maalumu ya kiroho

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Kuna machungu watanzania tunapitia na imenikumbusha ‘fact’ moja inayowatofautisha mtu mwenye cheo kama cha uraisi na mtu wa kawaida.

Kwa muda mrefu nimewaza hivi Rais mfano wa Marekani anaweza kuwa na kinga gani hadi anakuwa hadhuriki na laana anazopewa. Yaani unakuta waarabu huko hawakeshi lakini jamaa yuko fresh tu anaenda kuangalia baseball game!

Nakumbuka kuona video clip moja ya Donald Trump baada tu ya kuchaguliwa akiwekewa mikono na viongozi labda zaidi ya saba wakimuombea mmoja baada ya mwingine. You can feel power fulani ilikuwepo pale. Sasa hivi ni kama fashion kumsema Trump, si waarabu, si wapalestina, si waafrika, si waingereza, si walatino. Wote kwa njia moja ama nyingine wanamlaani. Ila huyu Trump haonekani kudhurika!

Mimi nimetokea kufahamu na kuamini nguvu katika kauli tunazotoa kama nilivyoelezea katika uzi wangu mmoja ambao umepotea. Nadhani mods wamefanya yao.

Ni nini hawa viongozi wa juu kama maraisi wanapewa inayowapa kinga za namna hii?

NB. Naomba kichwa cha habari kisomeke ‘Rais wa nchi ana kinga maalumu ya kiroho’

6670963D-AEC5-494D-9D6C-2F946D02205F.jpeg
 
Hakuna cha kinga wala nini hapo, Ukiona hadhuriki ujue kwamba muda bado haujafika. Time will tell. Umewasahau akina Sadam Hussein, Nduli Idd Amin Dadaa?,n. K. Muda wa zile Laana kufanya kazi ulipofika nini walikipata?. Utajijibu wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom