Kiroho na kiuchawi; Watoto hawana Kinga binafsi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,893
KIROHO NA KIUCHAWI; WATOTO HAWANA KINGA BINAFSI

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu Jeusi.

Kumdhuru mtoto Mdogo Kwa namna yoyote Ile ni Jambo rahisi Sana. Kwa sababu mtoto Mdogo hana kinga binafsi.

Unaweza kumdhuru mtoto kimwili, kiroho, kihisia, Kiakili yaani kivyovyote vile.
Ndio maana Jambo la Kwanza ambalo mzazi hulitoa Kwa mtoto ni Ulinzi Hii hi Kwa sababu mtoto Hana ulinzi wala kinga binafsi.

Kuna Aina nyingi za Kinga, nazo ni;
1. Kinga ya kimwili
2. Kinga ya Kiroho
3. Kinga ya kihisia
4. Kinga ya kifikra.

Vyote hivyo mtoto atavipata aidha Kutoka Kwa Wazazi wake au Walezi wake.. vyovyote vile iwavyo, mtoto anapodhurika Kwa namna moja au nyingine basi wazazi na Walezi wake wanahusika Kwa kiwango kikubwa.

1. Kinga ya Kimwili.
Hii ni kinga ambayo mtoto anazaliwa nayo, na mara nyingi huirithi Kutoka Kwa Wazazi wake, Mara nyingi kinga ni ishu ya kijenetiki yaani yakurithishwa. Kinga dhidi ya kupambana na magonjwa.
Kama wazazi wa mtoto kinga zao hazikuwa thabiti basi kuna uwezekano mkubwa hata mtoto kuwa vivyohivyo.

Kinga ya kimwili pia inahusu Vyakula mtoto apewavyo, kama tunavyojua mtoto hajiamulii ale chakula gani, mtoto atakula kile apewacho na Wazazi wake.
Na hapa nazungumzia mtoto mwenye umri wa miaka kuanzia 0 - 15 na wengine wanakuwa Watoto mpaka miaka 20 kutegemeana na nature ya Ukoo atokao.

Kwa upande wa Mimba, Kijusi kilichopo tumboni kinga yake pia inatokana na kinga ya Mama.
Ni rahisi kuidhuru mimba kwa namna moja ama nyingine Kwa sababu mimba kama mimba na Kijusi havina kinga. Ndio maana Mama wa mtoto kuna vitu atakatazwa asivile na vingine ataambiwa avitumie kwaajili ya mtoto.
Kijusi(kitoto kilichopo tumboni) endapo kitadhurika Kwa namna yoyote Ile iwe NI kimwili au Kiroho basi ni rahisi kitoto hicho kufia tumboni. Hii inaweza kupelekea Mimba kuchomoka hasa ikiwa Chini ya wiki 20 kwani ndio kipindi ambacho Kijusi kinakuwa kichanga na hakijiwezi.
Bado tupo kwenye kinga,

2. Kinga ya Kiroho.
Mtoto Mdogo kuanzia akiwa tumboni mwa mamaye hutegemea zaidi kinga ya Mzazi wake. Mtoto Hana kinga yake binafsi, sio ajabu mtoto apatapo madhara Mtu wakwanza Kupata uchungu ni mama yake Kutokana na kuwa yeye ndiye mtu wa Kwanza mwenye kinga ya mtoto iwe Kiroho au Kimwili.
Ndio maana Taikon ninashaurigi, ni vizuri mwanaume Kabla haujamzalisha Mkeo au Mwanamke yeyote lazima Muwekane Sawa kwenye ishu ya Imani, Kwa sababu Imani ndio kinga ya Roho ya MTU.
Usikimbilie Matako, sijui uzuri wa Sura, hayo ni muhimu lakini kuna yamuhimu zaidi ikiwemo Imani.

Elewa kuwa, Wakati Mwanamke ni Mjamzito, popote atakapoenda ataenda na huyo mtoto, chochote atakachotumia ata-share na mtoto aliyetumboni,
Kumbuka Imani chanzo chake ni kusikia na kuona, kisha kutafakari. Mtoto aliyetumboni huanza Kupata Imani yake kuanzia wiki ya ishirini na tano mpaka ishirini na sita yaani mwezi wa nne unusu kuelekea mwezi wa tano.
Ingawaje Imani yake itakuwa sifuri lakini sio kila sifuri inamaanisha hakuna kitu.
Mtoto husikia katika miezi ya tano, sita mpaka atakapozaliwa. Chochote atakachokisikia hata kama hakielewi kitabaki kama sehemu ya Imani yake Kiroho. Imani ya mtoto aliyetumboni hutokana zaidi na Mama na wanaomzunguka Mama yake.
Mama Mjamzito mbali na masharti mengine ya kiafya ya mwili anayopewa lakini hapo masharti ya Kiroho ambayo anatakiwa kuyazingatia kulingana na mtoto anayetaka kumzaa aweje,

Mfano,
I) Mjamzito hapaswi kusema maneno ya chuki, matusi au kupewa maneno ya chuki au kutukanwa.
ii) Mjamzito hapaswi kukaa maeneo yenye makelele na kusikia Lugha chafu kusikiliza muziki au kuangalia filamu zenye namna yoyote ya kuathiri Imani chanya iwe Imani yake au ya mtoto Mdogo. Haijalishi Akili yake itamuambia Hii NI filamu tuu ya kuigiza, lakini ubongo na Imani hautatafsiri hivyo katika kuweka kumbukumbu katika ung'amuzi bwete. Kwani itatafsiri kwamba ni Kweli ingawaje kiuhalisia itakuwa NI Uongo. Hii itajidhihirisha Kwa baadhi ya ndoto atakazoota mtu, sio ajabu mtu Kuota filamu aliyoiona lakini ikamsumbua kwenye ndoto kama tukio la kweli.
Hii huathiri mtoto aliyetumboni.

iii) Mjamzito anapaswa kutunzwa Kwa upendo na heshima. Hii huimarisha afya kimwili na Kiroho ya mtoto aliyetumboni.
iv) Mjamzito kuna vyakula ambavyo Kiroho ni sumu(haramu) ingawaje kimwili havidhuru. Vyakula hivyo hatakiwi kuvitumia kama chakula.

v) Mjamzito hatakiwi kuitoa mimba Kwa dhamiri yake au dhamiri ya Baba wa mtoto au mtu yeyote. Labda mimba Itoke yenyewe na sababu za mimba Kutoka zinajulika, kubwa kuliko NI kudhurika Kwa Kijusi kimwili au Kiroho.
Kijusi kinapodhurika kimwili au Kiroho hupelekea kuumwa na kama hatua hazitachukuliwa Kijusi hicho kinaweza Kufa, kikifa basi mimba lazima ichomoke.

Sababu nyingine ya mimba Kutoka ni Eneo la mfuko wa Uzazi kugeuka Kaburi hasa ikiwa Mimba zilitolewa Kwa Makusudi.
Kama tujuavyo, kitu kilichohai hakiwezi kuishi makaburini, mimba inapotungwa hasa kwenye mji wa Mimba ambao umekuwa Kaburi ni rahisi kuchomoka,
Ingawaje zipo sababu za kisayansi kama uwepo wa makovu katika Kuta za kizazi, na vivimbe au uteute usiosapoti Kijusi kujipachika katika Kuta za Uzazi, lakini Kiroho ni ngumu Kwa roho hai kuishi Kaburini.
Taikon hashauri mtu kujaribu kutoa mimba ingawaje pia hatahukumu ikiwa kuna aliyefanya hivyo.

Ni muhimu na lazima ikiwa MTU alitoa mimba, kufanya ibada ya kujitakasa na kuliondoa hilo Kaburi lililopo katika mji WA mimba ili kuruhusu ujio wa watoto wengine. Vinginevyo ni Jambo la kawaida Kwa MTU aliyetoa mimba, kukutwa na mambo ya Miscarriage (mimba kuchomoka au mtoto kufia tumboni). Hata hivyo miscarriage nyingine hutokana na mazingira au Ulaji wa vyakula Fulani ambacho huchochea homoni za Uzazi kupanda au kushuka Sana Hali inayoathiri ukuaji WA mimba.

Pia sio vizuri Kutumia vidonge vya Uzazi au Kutumia Tembe kama P2 Kwa lengo la kudhibiti mimba. Ingefaa hayo yatumike Baada ya MTU kumaliza Kupata watoto.

"Taikon unaongea Sana, umetoka nje ya mada"
Sawa, ngoja turudi.

Kumloga mtoto ni Jambo rahisi Mno Kwa sababu Watoto Imani zao zinatokana na Wazazi wao.
Mzazi akiwa na kinga ndogo ya Kiroho hupelekea na mtoto kuwa na kinga ndogo,
Na kinachoondoa Imani ya mtu ni Matendo yake. Halikadhalika kinachoongeza Imani ya mtu ni Matendo yake.
Kadiri unavyokuwa Mwema ndivyo Imani yako inavyoimarika. Kadiri unavyokuwa mwovu ndivyo Imani yako inavyodhoofika.
Matendo mara nyingi huathiriwa na kile MTU asikiacho na aonacho.
Ni ngumu kutenda Jambo ambalo hujawahi kuliona au kulisikia.

Ili Imani Ife kabisa yapo Makosa lazima uyafanye, mfano Kufanya Mauaji ya Makusudi hasa Kwa MTU asiye na hatia, kuwa mchawi au mshirikina WA namna yoyote Ile. Kufanya uzinzi hovyohovyo hasa na Watu uliokatazwa mfano, Ndugu yako, baba au Mama yako, Binti au kijana wako au MKE wa MTU.
Wachawi na waganga wote wanajua kuwa ni rahisi kumloga mtu mwenye Matendo ya hivyo. Yaani hauhitaji nguvu kubwa kumloga mtu mshirikina.

Mtoto wako anaweza kudhuriwa na Uchawi Kwa sababu yako kama mzazi au mlezi. Ni kweli mtoto Hana kosa lakini pia kumbuka pia Hana kinga hivyo Njia rahisi ya kukuumiza wewe ni kumloga yeye ili uumie wewe.
Mtu anaweza kumloga au kumdhuru mtoto wako Kwa sababu nyingi lakini kubwa zaidi ni Kisasi Fulani, lakini kuna kitu inaitwa Karma.

Unapotenda Jambo lolote Baya, Jambo Hilo linasajiliwa katika Ulimwengu wa Ubaya, hivyo linakuwa pending kama Akiba yako ambayo itatumika baadaye.
Mtu akitaka kukufanyia ubaya mara nyingi hutumia Akiba yako ya ubaya kukulipa mabaya iwe Kwa kujua au kwakutokujua.

Halikadhalika MTU akifanya Mema, Wema wake unasajiliwa katika Ulimwengu wa Mema. Hivyo Wema huo utabaki kuwa pending kama Akiba yake ambayo itatumika baadaye.

Kama tunavyojua kila kitu kina riba.
Kadiri malipo ya mtu yanapochelewa iwe ni Wema au Ubaya, ndivyo riba yake itakavyokuwa kubwa,

Mtoto anapokutwa na tatizo lolote basi Jambo la Kwanza ni kuangalia mzizi WA tatizo Hilo.
Mfano mtoto anaumwa malaria, basi chanzo cha tatizo Hilo ni kumuacha mtoto sehemu isiyosalama yenye Mbu.
Mtoto kuharisha basi hapo utajua aidha anaota Meno, au Kala chakula chenye uchafu,

Mtoto ili alogwe au apigwe juu basi hapo wakuangalia ni wazazi wake au Walezi wake, full stop.

Tutaendelea na kinga zingine, Mimi ngoja nipumzike.

Ni Yule Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili zenye nguvu na utukufu,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ivi watoto wanaopona katika ajali za magari / matetemeko ya ardhi / ajali za ndege etc ili hali watu wenye umri mkubwa wanaangamiaaa huwa wana kinga ipi?

Nafikiri katika Law of Extinction inaeleza kuwa ni rahisi kiumbe chenye umbo kubwa kuangamia kunapotokea janga kama tetemeko, ajali za kuanguka aidha nyumba, au magari au hata ndege.

Lakini viumbe wenye maumbile madogo ni rahisi kusustain Kutokana na maumbile Yao kuwa madogo.
Hiyo inaweza kuwa sababu yenye mantiki.

Kiroho ishu ya Kufa au kutokufa ni ngumu kuielezea Kwa sababu pia mtoto anaweza Kufa lakini Watu wazima wakabaki.
 
Uko sahihi naweza sema kwa kiasi kikubwa sanaa mkuu.Na katika mambo mawili hapo nathibitisha kuwa ni kwel.

1. Kutoa mimba mwanamke na akakosa kufanya ibada ya toba ya kumaanisha kabisa toka rohoni aisee huwa na madhara sana

2. Kufanya fanya ngono hovyo na hao watu uliowataja hapo kuna ua kabisa utashi wa nafsi ya mtu, na impli ations zake ni kubwa mnoo, hili mtu hawez kuliona haraka kwa walio wengi na zaid kama huna utaratibu wa kuji asses kiroho, ila kama una huo utaratibu basi utajua madhara ya zinaa kwako
 
Napenda Watu mnaojua ku- summarizing
 
Sio kwamba upewe Elimu ili usiwe mjinga WA vitu hivyo.

Vitu ambavyo havithibitiki ni vingi mno lakini vipo.

Kusema hakuna Uchawi ni Sawa na kusema hakuna Nafsi au Roho kisa havionekani
Ni wapumbavu tu mnakua na mawazo kama hayo. Uchawi haupo.

Hizo hadithi za kitaahira kawape mataahira wenzio.
 
Wewe mwenyewe haupo, mawazo ya kusema wewe upo ni upumbavu.
Kwa wengine wasiokujua wakiambiwa kuna MTU anaitwa The Assassin watasema ni Uongo na haupo.
Ni mpumbavu ambaye kitu asichokijua kusema KUWA hakipo
 
Mifano yako ya kitaahira hii kawape mataahira wenzio. Mimi nipo, naweza kuthibitika kwa kupelekwa huko wanakosema sipo. Uchawi haujawahi na wala hautawahi kuthibitika. Kama wewe ni mchawi niroge sada hivi. Kama huwezi kuniroga huo uchawi haupo.

Uwe unafikiria kabla ya kutoa mifano isiyo na maana yoyote.
 
Na Uchawi upo na unaweza kuthibitishwa Kwa ninyi mnaosema haupo.

Ni taahira kama wewe unayekataa Uchawi haupo Wakati hukuomba uthibitisho
 
Thibitha basi kwa kuniroga. Nimekuruhusu uniroge kuthibitisha uchawi upo.

😂😂😂
Aliyekuambia Uchawi ni kuroga tuu NI Nani?
Ndio maana nikakuambia kitu kama hujui ni Bora uombe kujulishwa.

Unaweza ukawa na hoja inayohitaji uthibitisho lakini kutukana na kudhihaki Watu wanaojua Jambo Fulani lipo alafu wewe hujawahi kulithibitisha ni dalili ya upumbavu
 
Acheni mawazo ya kipumbavu uchawi haupo.
 
KIROHO NA KIUCHAWI; WATOTO HAWANA KINGA BINAFSI

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani katika Hekalu Jeusi.

Kumdhuru mtoto Mdogo Kwa namna yoyote Ile ni Jambo rahisi Sana. Kwa sababu mtoto Mdogo hana kinga binafsi.

Unaweza kumdhuru mtoto kimwili, kiroho, kihisia, Kiakili yaani kivyovyote vile.
Ndio maana Jambo la Kwanza ambalo mzazi hulitoa Kwa mtoto ni Ulinzi Hii hi Kwa sababu mtoto Hana ulinzi wala kinga binafsi.

Kuna Aina nyingi za Kinga, nazo ni;
1. Kinga ya kimwili
2. Kinga ya Kiroho
3. Kinga ya kihisia
4. Kinga ya kifikra.

Vyote hivyo mtoto atavipata aidha Kutoka Kwa Wazazi wake au Walezi wake.. vyovyote vile iwavyo, mtoto anapodhurika Kwa namna moja au nyingine basi wazazi na Walezi wake wanahusika Kwa kiwango kikubwa.

1. Kinga ya Kimwili.
Hii ni kinga ambayo mtoto anazaliwa nayo, na mara nyingi huirithi Kutoka Kwa Wazazi wake, Mara nyingi kinga ni ishu ya kijenetiki yaani yakurithishwa. Kinga dhidi ya kupambana na magonjwa.
Kama wazazi wa mtoto kinga zao hazikuwa thabiti basi kuna uwezekano mkubwa hata mtoto kuwa vivyohivyo.

Kinga ya kimwili pia inahusu Vyakula mtoto apewavyo, kama tunavyojua mtoto hajiamulii ale chakula gani, mtoto atakula kile apewacho na Wazazi wake.
Na hapa nazungumzia mtoto mwenye umri wa miaka kuanzia 0 - 15 na wengine wanakuwa Watoto mpaka miaka 20 kutegemeana na nature ya Ukoo atokao.

Kwa upande wa Mimba, Kijusi kilichopo tumboni kinga yake pia inatokana na kinga ya Mama.
Ni rahisi kuidhuru mimba kwa namna moja ama nyingine Kwa sababu mimba kama mimba na Kijusi havina kinga. Ndio maana Mama wa mtoto kuna vitu atakatazwa asivile na vingine ataambiwa avitumie kwaajili ya mtoto.
Kijusi(kitoto kilichopo tumboni) endapo kitadhurika Kwa namna yoyote Ile iwe NI kimwili au Kiroho basi ni rahisi kitoto hicho kufia tumboni. Hii inaweza kupelekea Mimba kuchomoka hasa ikiwa Chini ya wiki 20 kwani ndio kipindi ambacho Kijusi kinakuwa kichanga na hakijiwezi.
Bado tupo kwenye kinga,

2. Kinga ya Kiroho.
Mtoto Mdogo kuanzia akiwa tumboni mwa mamaye hutegemea zaidi kinga ya Mzazi wake. Mtoto Hana kinga yake binafsi, sio ajabu mtoto apatapo madhara Mtu wakwanza Kupata uchungu ni mama yake Kutokana na kuwa yeye ndiye mtu wa Kwanza mwenye kinga ya mtoto iwe Kiroho au Kimwili.
Ndio maana Taikon ninashaurigi, ni vizuri mwanaume Kabla haujamzalisha Mkeo au Mwanamke yeyote lazima Muwekane Sawa kwenye ishu ya Imani, Kwa sababu Imani ndio kinga ya Roho ya MTU.
Usikimbilie Matako, sijui uzuri wa Sura, hayo ni muhimu lakini kuna yamuhimu zaidi ikiwemo Imani.

Elewa kuwa, Wakati Mwanamke ni Mjamzito, popote atakapoenda ataenda na huyo mtoto, chochote atakachotumia ata-share na mtoto aliyetumboni,
Kumbuka Imani chanzo chake ni kusikia na kuona, kisha kutafakari. Mtoto aliyetumboni huanza Kupata Imani yake kuanzia wiki ya ishirini na tano mpaka ishirini na sita yaani mwezi wa nne unusu kuelekea mwezi wa tano.
Ingawaje Imani yake itakuwa sifuri lakini sio kila sifuri inamaanisha hakuna kitu.
Mtoto husikia katika miezi ya tano, sita mpaka atakapozaliwa. Chochote atakachokisikia hata kama hakielewi kitabaki kama sehemu ya Imani yake Kiroho. Imani ya mtoto aliyetumboni hutokana zaidi na Mama na wanaomzunguka Mama yake.
Mama Mjamzito mbali na masharti mengine ya kiafya ya mwili anayopewa lakini hapo masharti ya Kiroho ambayo anatakiwa kuyazingatia kulingana na mtoto anayetaka kumzaa aweje,

Mfano,
I) Mjamzito hapaswi kusema maneno ya chuki, matusi au kupewa maneno ya chuki au kutukanwa.
ii) Mjamzito hapaswi kukaa maeneo yenye makelele na kusikia Lugha chafu kusikiliza muziki au kuangalia filamu zenye namna yoyote ya kuathiri Imani chanya iwe Imani yake au ya mtoto Mdogo. Haijalishi Akili yake itamuambia Hii NI filamu tuu ya kuigiza, lakini ubongo na Imani hautatafsiri hivyo katika kuweka kumbukumbu katika ung'amuzi bwete. Kwani itatafsiri kwamba ni Kweli ingawaje kiuhalisia itakuwa NI Uongo. Hii itajidhihirisha Kwa baadhi ya ndoto atakazoota mtu, sio ajabu mtu Kuota filamu aliyoiona lakini ikamsumbua kwenye ndoto kama tukio la kweli.
Hii huathiri mtoto aliyetumboni.

iii) Mjamzito anapaswa kutunzwa Kwa upendo na heshima. Hii huimarisha afya kimwili na Kiroho ya mtoto aliyetumboni.
iv) Mjamzito kuna vyakula ambavyo Kiroho ni sumu(haramu) ingawaje kimwili havidhuru. Vyakula hivyo hatakiwi kuvitumia kama chakula.

v) Mjamzito hatakiwi kuitoa mimba Kwa dhamiri yake au dhamiri ya Baba wa mtoto au mtu yeyote. Labda mimba Itoke yenyewe na sababu za mimba Kutoka zinajulika, kubwa kuliko NI kudhurika Kwa Kijusi kimwili au Kiroho.
Kijusi kinapodhurika kimwili au Kiroho hupelekea kuumwa na kama hatua hazitachukuliwa Kijusi hicho kinaweza Kufa, kikifa basi mimba lazima ichomoke.

Sababu nyingine ya mimba Kutoka ni Eneo la mfuko wa Uzazi kugeuka Kaburi hasa ikiwa Mimba zilitolewa Kwa Makusudi.
Kama tujuavyo, kitu kilichohai hakiwezi kuishi makaburini, mimba inapotungwa hasa kwenye mji wa Mimba ambao umekuwa Kaburi ni rahisi kuchomoka,
Ingawaje zipo sababu za kisayansi kama uwepo wa makovu katika Kuta za kizazi, na vivimbe au uteute usiosapoti Kijusi kujipachika katika Kuta za Uzazi, lakini Kiroho ni ngumu Kwa roho hai kuishi Kaburini.
Taikon hashauri mtu kujaribu kutoa mimba ingawaje pia hatahukumu ikiwa kuna aliyefanya hivyo.

Ni muhimu na lazima ikiwa MTU alitoa mimba, kufanya ibada ya kujitakasa na kuliondoa hilo Kaburi lililopo katika mji WA mimba ili kuruhusu ujio wa watoto wengine. Vinginevyo ni Jambo la kawaida Kwa MTU aliyetoa mimba, kukutwa na mambo ya Miscarriage (mimba kuchomoka au mtoto kufia tumboni). Hata hivyo miscarriage nyingine hutokana na mazingira au Ulaji wa vyakula Fulani ambacho huchochea homoni za Uzazi kupanda au kushuka Sana Hali inayoathiri ukuaji WA mimba.

Pia sio vizuri Kutumia vidonge vya Uzazi au Kutumia Tembe kama P2 Kwa lengo la kudhibiti mimba. Ingefaa hayo yatumike Baada ya MTU kumaliza Kupata watoto.

"Taikon unaongea Sana, umetoka nje ya mada"
Sawa, ngoja turudi.

Kumloga mtoto ni Jambo rahisi Mno Kwa sababu Watoto Imani zao zinatokana na Wazazi wao.
Mzazi akiwa na kinga ndogo ya Kiroho hupelekea na mtoto kuwa na kinga ndogo,
Na kinachoondoa Imani ya mtu ni Matendo yake. Halikadhalika kinachoongeza Imani ya mtu ni Matendo yake.
Kadiri unavyokuwa Mwema ndivyo Imani yako inavyoimarika. Kadiri unavyokuwa mwovu ndivyo Imani yako inavyodhoofika.
Matendo mara nyingi huathiriwa na kile MTU asikiacho na aonacho.
Ni ngumu kutenda Jambo ambalo hujawahi kuliona au kulisikia.

Ili Imani Ife kabisa yapo Makosa lazima uyafanye, mfano Kufanya Mauaji ya Makusudi hasa Kwa MTU asiye na hatia, kuwa mchawi au mshirikina WA namna yoyote Ile. Kufanya uzinzi hovyohovyo hasa na Watu uliokatazwa mfano, Ndugu yako, baba au Mama yako, Binti au kijana wako au MKE wa MTU.
Wachawi na waganga wote wanajua kuwa ni rahisi kumloga mtu mwenye Matendo ya hivyo. Yaani hauhitaji nguvu kubwa kumloga mtu mshirikina.

Mtoto wako anaweza kudhuriwa na Uchawi Kwa sababu yako kama mzazi au mlezi. Ni kweli mtoto Hana kosa lakini pia kumbuka pia Hana kinga hivyo Njia rahisi ya kukuumiza wewe ni kumloga yeye ili uumie wewe.
Mtu anaweza kumloga au kumdhuru mtoto wako Kwa sababu nyingi lakini kubwa zaidi ni Kisasi Fulani, lakini kuna kitu inaitwa Karma.

Unapotenda Jambo lolote Baya, Jambo Hilo linasajiliwa katika Ulimwengu wa Ubaya, hivyo linakuwa pending kama Akiba yako ambayo itatumika baadaye.
Mtu akitaka kukufanyia ubaya mara nyingi hutumia Akiba yako ya ubaya kukulipa mabaya iwe Kwa kujua au kwakutokujua.

Halikadhalika MTU akifanya Mema, Wema wake unasajiliwa katika Ulimwengu wa Mema. Hivyo Wema huo utabaki kuwa pending kama Akiba yake ambayo itatumika baadaye.

Kama tunavyojua kila kitu kina riba.
Kadiri malipo ya mtu yanapochelewa iwe ni Wema au Ubaya, ndivyo riba yake itakavyokuwa kubwa,

Mtoto anapokutwa na tatizo lolote basi Jambo la Kwanza ni kuangalia mzizi WA tatizo Hilo.
Mfano mtoto anaumwa malaria, basi chanzo cha tatizo Hilo ni kumuacha mtoto sehemu isiyosalama yenye Mbu.
Mtoto kuharisha basi hapo utajua aidha anaota Meno, au Kala chakula chenye uchafu,

Mtoto ili alogwe au apigwe juu basi hapo wakuangalia ni wazazi wake au Walezi wake, full stop.

Tutaendelea na kinga zingine, Mimi ngoja nipumzike.

Ni Yule Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili zenye nguvu na utukufu,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Umesema vyema sana brother Robert
 
Back
Top Bottom