Viongozi wa kidini wanaondoa dhambi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
915
4,270
Kwa mujibu wa vitabu vitakatifu hakuna ondoleo la dhambi linalotokana na kiongozi wa dini; vitabu vitakatifu vyote vimekabidhi mamlaka yakuondoa dhambi kwa Mungu siyo kwa wanadamu.

Kwanini watanzania tumekuwa wepesi kuamini maaskofu na masheikh wanaweza kutuondolea dhambi? Hawa ni viongozi wa taasisi wanapiga kampeni kuchukua madaraka kwenye taasisi zao; hawa ni binadamu kama sisi ila wao wamechagua ofisi zao ziwe nyumba za ibada lakini haina maana kwamba wao ni watakatifu.

Tukilitambua ilo tutarejea kwenye dini ya kweli ambayo ni kutenda yaliyo mema. Ukisimama na wema hata usipoenda nyumba ya ibada wanaokuzunguka watabarikiwa na maisha yako na hii ndiyo ibada ya kweli.

Kuna viongozi wa dini ambao wanawaabudu wanasiasa kuliko Mungu; wapo tayari kutamka adharani kwamba mwanasiasa anayekatili watu ni mtu mwema. Huyu kiongozi anawezaje kuondolea dhambi? Anawezaje kupeleka maombi yako kwa Mungu?

Viongozi wa dini ambao wanaona wanachofanyiwa Wamasai Arusha ni jambo wanalostahili si viongozi wa dini bali ni wachumia familia zao.
 
Mbaya zaidi ni ile ya kwenda kwa Padri kuungama dhambi kwa kumtajia madhambi yote uliyoyafanya bila kumficha kisha yeye ndio akutangazie msamaha wa dhambi

Ilihali yeye akitoka hapo anaenda zake kwa manzi ake na kupiga pombe za kutosha
 
Mbaya zaidi ni ile ya kwenda kwa Padri kuungama dhambi kwa kumtajia madhambi yote uliyoyafanya bila kumficha kisha yeye ndio akutangazie msamaha wa dhambi

Ilihali yeye akitoka hapo anaenda zake kwa manzi ake na kupiga pombe za kutosha
Dah.! Noma sana ila kuyaelezea madhambi yako kwa mtu husaidia utulivu wa moyo. Siri inatesa asikwambie mtu. so nawaza tuu labda kwa vile mapadri ni watu wakiimani wanatumika kama watunza siri.
 
Back
Top Bottom