Viongozi wa Dini kualikwa kwenye uapisho wa viongozi wa kisiasa siyo kuchanganya Siasa na Dini?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Hivi Karibuni kumetokea malumbano makubwa baada ya Waraka wa TEC kutolewa na KANISA KATOLIKI wa Kupinga MKATABA wa BANDARI
Baadhi ya Watu wanaoutetea MKATABA huo wakaja na HOJA ya UDINI badala ya Kuujibu WARAKA kuwa ETI Viongozi wa Dini Wanachanganya SIASA NA DINI.

Kauli hiyo ilipingwa vikali sana na Wananchi kwani VIONGOZI wa DINI ni Wananchi kama Wananchi wengine, Wana HAKI ya KUTETEA RASLIMALI za NCHI kama WANANCHI wengine.

Najiuliza kwanini Hao WANASIASA wakati Wanaapishwa ktk UONGOZI wao wa KISIASA kwanini Wanawataka VIONGOZI wa DINI washiriki na Kushika VITABU vya DINI?

Wakati wa kutafuta UONGOZI ktk CHAGUZI kwanini hao WANASIASA wanatumia NYUMBA za IBADA na Viongozi wa Dini Kuwaombea KURA kwa Waumini?

WANASIASA tuache unafiki DINI ndio kila kitu ili WANASIASA watawale kwa AMANI ni lazima kwanza Viongozi wa Dini wawahubirie Waumini wao umuhimu wa Amani ktk NCHI.

Kauli ya WANASIASA kwa VIONGOZI wa DINI kuwa Wanachanganya DINI na SIASA ni ya KUPUUZWA. VIONGOZI wa Dini WANASTAHIKI HESHIMA.
 
Mkwele ndio atupe majibu kuhusu hili

Maana kipind Cha uongozi wake alishawaita sana viongozi wa dini ikulu Leo ndio anaona dini na siasa havishabiani

Hii imekaaje?
 
Hii ni sawa na wasukuma kulima shamba kama familia kwa shangwe na vigelegele ila mazao yakikomaa yanakuwa ya baba anaenda kuhonga na kuoa mke wa pili.
 
Back
Top Bottom