Haiwezekani kuwatenga viongozi wa kanisa na siasa za nchi yao

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,606
93,326
HAIWEZEKANI KUWATENGA VIONGOZI WA KANISA NA SIASA ZA NCHI YAO!

Wapendwa Watanzania!

Limekuwa ni jambo la kawaida kwa watawala au watu walio karibu na watawala wa Tanzania wakibanwa na viongozi wa dini hasa maaskofu huanza kutoa maneno ya propaganda dhidi ya viongozi wa dini wakiwaambia 'wasichanganye dini na siasa'. Msemo huu wanautumia kama kichaka cha kujifichia wasiguswe na viongozi wa dini!

Kauli hizo zimeibuka tena kwa kishindo zaidi kuanzia mwezi Juni 2023 baada ya maaskofu kuingilia sakata la Mkataba wa Bandari. Hivi karibuni tuliikemea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilipoitisha mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili hoja ya viongozi wa dini kuonekana wakiwa na viongozi wa vyama vya siasa.

Tumeona ni wajibu wetu ili kuwaelimisha watu kuhusu suala hili kusudi wasije wakapotoshwa na wanasiasa katika suala zima la kudai haki katika taifa lao. Wanasiasa ni wajanja sana na wanajua nafasi na nguvu ya viongozi wa dini katika jamii ndio maana wanatumia nguvu ili kupotosha ukweli kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika ukombozi wa kifikra katika taifa.

Tunapenda kukiri kuwa hili tunaloliandika ndilo eneo ambalo sisi tuna ubobezi nalo, kwa hiyo hatubahatishi bali tunakiandika tunachokijua, tulichokisomea na kukifundisha katika ngazi za Chuo Kikuu.

Kwa upande wa Wakristo, chimbuko la dini hiyo ni mji wa Yerusalemu, Israeli ya Kale. Lakini, ni vizuri watu wakaelewa kuwa Ukristo una mizizi yake miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hivyo, msingi mkubwa wa mafundisho ya Ukristo ni Biblia Takatifu yenye sehemu kuu mbili - Agano Jipya na Agano la Kale.

Dini haifanywi kwa wanyama na wala siasa pia haifanywi kwa ndege. Dini ni mfumo mzima wa maisha ambao ndani yake kuna mambo mengi. Tunaposoma au kufundisha kuhusu dini lazima tusome maisha ya jamii nzima ambayo kwanza dini ilifika kwayo. Kwa upande wa Wakristo, sisi tunasoma kuhusu jamii mbalimbali kama Misri, Syria, Ukaldayo (Babeli), Rumi, Wagiriki, Jordan, Waisraeli, Waajemi, Waarabu, Lebanon, nk.

Katika kusoma na kujifunza dini tunafundisha waumini kuishi kwa mifano ya jamii hizo ikiwa ni pamoja na kuiga mema na kuyaacha mabaya na hayo yanawezekana tu kwa kusoma kuhusu maisha yao kupitia viongozi au manabii wao.

Tunaposoma na kujifunza Biblia tunakutana na mambo yafuatayo:
1. Familia (family institutions): familia, ndoa, watoto, wajane, urithi, kifo, maziko, nafasi ya wanawake katika jamii, nk

2. Taasisi za Kiraia (Civili institutions): idadi ya watu, utumwa, taasisi ya kifalme, familia za kifalme, utawala, ajira na uchumi, kilimo, Afya na tiba, sheria na haki, mgawanyo wa muda, vipimo vya uzito, mahakama, nk.

3. Taasisi za Kijeshi (military institutions): majeshi ya Israeli, ngome za kijeshi, mbinu za kivita, siraha za kivita, vita, vita vitakatifu, nk

4. Taasisi za dini (Religious institutions): ibada, madhabahu, nyumba za ibada, uongozi wa taasisi za dini, Ofisi ya Ukuhani, Ofisi ya Walawi, sadaka, imani potofu, uchawi, utaratibu wa ibada, siku za ibada, sherehe na siku za sikukuu, nk.

Watu waliokuwa juu ya yote hayo ni viongozi wa dini na ndio waliopewa majukumu ya kuifundisha na kuionya jamii. Taasisi hizo ziliwekwa kwa ajili ya watu na kilichotofautisha ni ratiba. Wakati wa vita walipigana na wakati wa amani watu hao walifanya sherehe. Wakati wa mambo mazito ikiwemo kujua mustakabari wa nchi walikwenda kutafuta ushauri kwa viongozi wa dini. Alipotokea kiongozi mkorofi au jeuri alikemewa na viongozi wa dini au hata kutangaziwa kuondolewa madarakani na hao viongozi wa dini.

Sisi Askofu Mwamakula tunaitoa kwenu elimu hii ili msiyumbishwe ili muelewe kuwa viongozi wa dini kuingilia kati mtafaruku wa kisiasa au kiutawala ni ishara kuwa jamii yenu iko na afya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 20 Agosti 2023; 12:35 jioni.
 
JamiiForums1572050030.jpg
 
Tukubaliane kuwa watu wa dini wasiingie kabisa kwenye siasa za nchi hii. Wasisifie wala kukemea maswala yoyote ya wanasiasa. Wachungaji na masheikh wasigombee vyeo vya kisiasa. Wimbo wetu wa taifa tutoe ile sala. Viongozi wa serikali wasipewe vipaza sauti kwenye nyumba za ibada. Mikutano yao viongozi wa dini wasipande. Kama tunataka kutenganisha dini na siasa tufanye hayo. Pungufu na hayo, tutulie na kuacha unafiki.
 
Wakitaka kutenganisha siasa na dini. Waache pia kuita viongozi wa dini kwenye zindunzi na sherehe zao za kitaifa.

Ccm ni wale wanafunzi wanataka siku zote kuonekana namba moja. Msuli tembo matokeo sisimizi. Wakisikia unga unga ana wakosoa na kuwa challenges wanakuja juu
 
Wanaosema Dini isihusihwe na siasa hawajui hata wanachoongea, mahali pekee tunapaswa kuweka mipaka ni viongozi wa kanisa kuwa na upande wakati wa uchaguzi na kutopanda majikwaani kuwapigia kampeni wanasiasa.

Huwezi kutumia kauli ya kutohusisha dini na siasa kama sindano ya kushona midomo ya viongozi wa kiroho wakalie kimya mambo yanayoendelea katika uongozaji wa nchi.

Inashangaza zaidi maana kelele za dini isichanganywe na siasa huwa zinaibuka mara tu viongozi wa kiroho wanapoanza kuwanyoonya watawala.
 
Mmi najiuliza kwanini watu wa dini wakisifia watu wa siasa ...... hufurahi na hawasemi mambo ya udini ...lakini linapokuja swala la kukosolewa ndo idini huanzia hapo ..... nahisi neno udini ni kichaka cha watu kufivha maovu yao yasi semwe
 
Yani serikali inatamani viongozi wa dini wasiwe na uelewa hata kidogo wa siasa, wawe Kama mazwazwa hivi. Bila kujua viongozi wa dini wameingia darasani wamesoma Tena elimu kubwa tu. Rubbish .
 
Shekhe ponda alipokuwa anapambania haki za waislamu mpaka kupigwa risasi wakristo wengi walisema shekhe ponda anachanganya dini na siasa hivyo ni haki yake kupigwa.

Leo TEC wanapambana wao na serikali wanasema dini na siasa havitengamani.

Wakipambana waislamu kuomba haki zao kina kina Lukuvi wanasimama kusema zanzibar ni waislamu wasiachwe wajitawale watawakaribisha warabu wenzao walete ugaidi bara.

Wakati huo TEC wanakwambia tuna mizizi mirefu na tunaweza pata msaada kutoka ROMA.

Wakristo wa Tanzania unafki umewajaa damuni.

Acheni unafki na ubinafsi hili mapambano yoyoye na CCM yalete maana.

Kwenye hili sakata wakatoliki kazi yao kubwa ni kuwashambulia waislamu na serikali.
 
HAIWEZEKANI KUWATENGA VIONGOZI WA KANISA NA SIASA ZA NCHI YAO!

Wapendwa Watanzania!

Limekuwa ni jambo la kawaida kwa watawala au watu walio karibu na watawala wa Tanzania wakibanwa na viongozi wa dini hasa maaskofu huanza kutoa maneno ya propaganda dhidi ya viongozi wa dini wakiwaambia 'wasichanganye dini na siasa'. Msemo huu wanautumia kama kichaka cha kujifichia wasiguswe na viongozi wa dini!

Kauli hizo zimeibuka tena kwa kishindo zaidi kuanzia mwezi Juni 2023 baada ya maaskofu kuingilia sakata la Mkataba wa Bandari. Hivi karibuni tuliikemea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilipoitisha mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili hoja ya viongozi wa dini kuonekana wakiwa na viongozi wa vyama vya siasa.

Tumeona ni wajibu wetu ili kuwaelimisha watu kuhusu suala hili kusudi wasije wakapotoshwa na wanasiasa katika suala zima la kudai haki katika taifa lao. Wanasiasa ni wajanja sana na wanajua nafasi na nguvu ya viongozi wa dini katika jamii ndio maana wanatumia nguvu ili kupotosha ukweli kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika ukombozi wa kifikra katika taifa.

Tunapenda kukiri kuwa hili tunaloliandika ndilo eneo ambalo sisi tuna ubobezi nalo, kwa hiyo hatubahatishi bali tunakiandika tunachokijua, tulichokisomea na kukifundisha katika ngazi za Chuo Kikuu.

Kwa upande wa Wakristo, chimbuko la dini hiyo ni mji wa Yerusalemu, Israeli ya Kale. Lakini, ni vizuri watu wakaelewa kuwa Ukristo una mizizi yake miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hivyo, msingi mkubwa wa mafundisho ya Ukristo ni Biblia Takatifu yenye sehemu kuu mbili - Agano Jipya na Agano la Kale.

Dini haifanywi kwa wanyama na wala siasa pia haifanywi kwa ndege. Dini ni mfumo mzima wa maisha ambao ndani yake kuna mambo mengi. Tunaposoma au kufundisha kuhusu dini lazima tusome maisha ya jamii nzima ambayo kwanza dini ilifika kwayo. Kwa upande wa Wakristo, sisi tunasoma kuhusu jamii mbalimbali kama Misri, Syria, Ukaldayo (Babeli), Rumi, Wagiriki, Jordan, Waisraeli, Waajemi, Waarabu, Lebanon, nk.

Katika kusoma na kujifunza dini tunafundisha waumini kuishi kwa mifano ya jamii hizo ikiwa ni pamoja na kuiga mema na kuyaacha mabaya na hayo yanawezekana tu kwa kusoma kuhusu maisha yao kupitia viongozi au manabii wao.

Tunaposoma na kujifunza Biblia tunakutana na mambo yafuatayo:
1. Familia (family institutions): familia, ndoa, watoto, wajane, urithi, kifo, maziko, nafasi ya wanawake katika jamii, nk

2. Taasisi za Kiraia (Civili institutions): idadi ya watu, utumwa, taasisi ya kifalme, familia za kifalme, utawala, ajira na uchumi, kilimo, Afya na tiba, sheria na haki, mgawanyo wa muda, vipimo vya uzito, mahakama, nk.

3. Taasisi za Kijeshi (military institutions): majeshi ya Israeli, ngome za kijeshi, mbinu za kivita, siraha za kivita, vita, vita vitakatifu, nk

4. Taasisi za dini (Religious institutions): ibada, madhabahu, nyumba za ibada, uongozi wa taasisi za dini, Ofisi ya Ukuhani, Ofisi ya Walawi, sadaka, imani potofu, uchawi, utaratibu wa ibada, siku za ibada, sherehe na siku za sikukuu, nk.

Watu waliokuwa juu ya yote hayo ni viongozi wa dini na ndio waliopewa majukumu ya kuifundisha na kuionya jamii. Taasisi hizo ziliwekwa kwa ajili ya watu na kilichotofautisha ni ratiba. Wakati wa vita walipigana na wakati wa amani watu hao walifanya sherehe. Wakati wa mambo mazito ikiwemo kujua mustakabari wa nchi walikwenda kutafuta ushauri kwa viongozi wa dini. Alipotokea kiongozi mkorofi au jeuri alikemewa na viongozi wa dini au hata kutangaziwa kuondolewa madarakani na hao viongozi wa dini.

Sisi Askofu Mwamakula tunaitoa kwenu elimu hii ili msiyumbishwe ili muelewe kuwa viongozi wa dini kuingilia kati mtafaruku wa kisiasa au kiutawala ni ishara kuwa jamii yenu iko na afya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 20 Agosti 2023; 12:35 jioni.
Je kanisa la kilumi linahuruma na sisi?au masilahi yao yako hatarini
 
Awe padre, askofu ,sister, mkulima ,mfanyakazi au raia yoyote linapokuja Suala la nchi yetu, rasilimari zetu na urithi wetu lazima kila mtu ahoji walio na elimu lazima wahoji kwa elimu zao na wasiokuwa na elimu lazima pia waelimishwe juu huo mkataba kwa uwazi, mbona serikali wao huwa Kuna wakati hutumia viongozi wa dini pia kwenye mambo Yao? Jibun hoja kwa hoja zama za kufanya watu ni wajinga zinaenda zinaisha
 
Back
Top Bottom