Viongozi wa dini msipende kusikiliza makutano, mkisikiliza makutano mtaishia kumsulubisha Yesu kama Ponsio Pilato alivyofanya. Msikilizeni Mungu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Baadhi ya viongozi wa dini wameanza kujitumbukiza kwenye kusikiliza makutano wanasema nini yaani watu wengi wanasema nini ili kutafuta sifa kwa makutano.Hii kitu imepelekea wao kutelekeza wito wa Mungu walioitiwa kwenye kazi zao za kichungaji na kiaskofu nk

Ponsio Pilato alikuwa msomi na mwanasaheria na mwenye vitabu vya sheria lakini Yesu alipoletwa na makutano akajaa mihemko akatelekeza vitabu vyake vya sheria akawauliza makutano mnataka nimfanyie nini huyu Yesu makutano wakapiga kelele asulubishwe asulubishwe! Akaamua asublubishwe bila hata ku quote kifungu chochote cha kitabu chake cha sheria.

Sasa kuna ma Ponsio Pilato wengi ambao wamegeuka kazi yao kuongelea makutano wanataka nini na kuacha kuongelea Mungu anataka nini.

Wachungaji na maaskofu Yesu aliwatuma akisema enendeni ulimwenguni kote mkaihubiri injili.Baadhi yao wamegeuka wasikiliza makutano wanataka nini wamegeuka wahubiri katiba mpya na tume huru za uchaguzi ili kutafuta sifa za makutano na kuitelekeza Injili waliyotumwa na Yesu. Wanasulubisha Yesu.

Niseme wazi Yesu alikuwa yuko sahihi kusema ufalme wangu si wa ulimwengu huu! Hii trend ya wachungaji na maaskofu kutafuta ufalme wa ulimwengu huu iwe kutaka kukubalika kwa makutano, kugombea vyeo vya kisiasa na kuwa upande wa vyama fulani kiwe tawala au upinzani ni kumsulubisha Yesu.

Viongozi wa kidini wana waumini wa vyama vyote na wasio na vyama ni vyema wakabaki kwenye wito wao tu na nashauri hata wasiwe na kadi ya chama chochote cha siasa na mwegemeo wa chama chochote.

Wabaki tu watangaza injili ya Kristo ya tubuni na kuiamini injili .Ulaya viongozi wa dini walijitia wapenda sifa za makutano kwa kushabikia siasa makanisa Ulaya yamekufa.
 
kwenye mikutano yenu nyie wanasiasa mnawatumia haohao kwenye maombi. wakitoa maoni yao mnasema watulie.
Martin Luther wa Marekani ,harakati zake zilisaidia sana kuondoa ubaguzi marekani
Waache waseme
 
kwenye mikutano yenu nyie wanasiasa mnawatumia haohao kwenye maombi. wakitoa maoni yao mnasema watulie.
Martin Luther wa Marekani ,harakati zake zilisaidia sana kuondoa ubaguzi marekani
Waache waseme
Aliyekwambia ubaguzi wa rangi marekani umeisha nani? Martin Luther king alipoteza tu maisha yake bure

Pili kuna huyu kibaraka mwingine aliyeacha kanisa na kukimbilia sijui kupinga ubaguzi wa rangi anaitwa Desmund Tutu.Ubaguzi Africa ya kusini umeisha? Umeaona waafrika wa nchi zingine wanavyobaguliwa na kuuawa na maduka yao kuchomwa moto na waafrika weusi wenzao wa Afrika ya kusini?

Ulishawahi ona mzungu wa Afrika ya kusini akichoma duka la mwafrika mweusi toka nchi nyingine ya kiafrika? Wachomaji maduka ni waafrika kusini ndugu zake Askofu Desmond Tutu.Heri angebaki tu kanisani kazi aliyofanya ni hopeless hakumaliza ubaguzi wowote wa maana kama alichopigania ndicho hicho cha kufanya waafrika weusi wa Africa ya kusini wabague waafrika wenzao weusi
 
Back
Top Bottom