Rugemeleza
JF-Expert Member
- Oct 26, 2009
- 668
- 136
- Mkuu heshima sana, lakini huu ni mtizamo wako tu na sio kwamba ni standard ya elimu ya uraia Tanzania kama ulivyobainisha mwanzoni, umeandika maneno mengi mazuri ya kimapinduzi lakini tatizo ni ushahidi kwamba Dr. slaa ndiye aliyeshinda urais tungependa kuuona upo wapi? Kama watu kama wewe mnao tuwekeeni hapa tuuchambue tuone ukweli ulipo maana hapa si unajua ni uwanja wa werevu. Halafu umeharibu sana kumuingiza Mwalimu on this kwa sababu at the ehart hapa ni sheria za chama kimoja kutumuika kwenye system ya vyama vingi, na pia Rais wa sasa hakuhusika na kuiba kura unless unao ushahidi kwamba aliiba na kuwaamuru NEC pia kuiba, au aliiba nao!
- Wagiriki hawakusema Demokrasia ni lazima kushinda Wapinzani tu, wakishindwa basi sio Demokrasia na sidhani kama walisema kwamba Wapinzani wakitoka kwenye kikao cha bunge basi chama chenye majority kinakuwa hakina mandate ya wananchi kuongoza taifa. Cha muhimu ni kwamba CCM kama chama cha siasa wana kila sababu ya kusikiliza kilio cha Chadema na kutafakari wanacholilia ni nini hasa, maana huwezi kuwa-ignore wananchi Millioni 2.2 waliompigia kura za U-Rais Dr. Slaa as of official matokeo yaliyopo tayari, otherwise ni muhimu sana tukaonyeshwa ushaidi mzito kwamba Dr. Slaa ndiye aliyeshinda huu uchaguzi. Hiii protest ni simply political protest na ni kawaida katika very Demokraisa ya Wagirki unayoisema, kwa sababu hata CCM pia inaweza kutoka nje wabunge wa Chadema wanapochangia hoja inaweza kufanyika both ways, lakini muhimu ni isitugawe taifa kwamba kwa sababu chadema wanasusia Rais, basi wana haki sana na hili taifa kuliko wasiosusia yatakwua ni mawazo mufilisi sana!
William.
Ninachosema ni kuwa kukiuka utashi wa Watanzania ni kukiuka maadili ya Kitanzania kwani tunaamini katika na kujenga utamaduni wenye maadili ya kuheshimu matakwa ya watu. Sasa Kikwete na CCM wanataka tuamini katika utamaduni wa Stalin kuwa mtu wa maana si mpiga kura bali muhesabu kura. Na kwa kweli wamekwenda mbele zaidi na kuamini ule wa Kibaki na Kivuitu kuwa mtu wa maana katika uchaguzi si mpiga kura, msimamizi wala muhesabu kura bali mtangaza matokeo. Hii ni hatari. Ushahidi ni wazi kwamba matokeo yaliyotangazwa na Tume ni tofauti na yale yaliyopatkana katika vituo.
Nimemtumia Mwalimu kwani msemo ule wa mwaka 1962 ni wa muhimu kuwa katika nchi yetu wananchi wana haki ya kumpinga kiongozi yoyote yule anayekiuka maadili na sheria za nchi. Upingaji huu hautaishia kwa Kikwete bali kwa kiongozi yeyote yule awe wa Chadema, CUF, TLP, UDP na wengine wote. Ni kwamba katika kulinda maslahi, heshima ya nchi wananchi wana haki na jukumu la kuwapinga na kuwakosoa viongozi wao. Nasimama katika maelezo yangu nadhani yanahitaji kutiliwa maanani na wote wenye kuitakia nchi yetu mema. Ni lazima tuhakikishe kwamba chaguzi zetu si tu zinakuwa ni huru na haki bali pia zinaonekana kuwa ni huru na haki kwani taswira hushinda uhalisia (perception trumps reality). Na kwa bahati mbaya katika hili ukweli ni kuwa muonekano na ukweli vilifanana kwamba uchaguzi umechakachuliwa.