Viongozi wa CHADEMA kutokumtambua Rais ni Kosa?

Asilete VITISHO VYA AJABU KWANZA HIZO PESA ZA MAENDELEO NA HUDUMA ZA JAMII HAZITOKI KWA RAIS WALA CCM BALI NI KODI ZA WANANCHI WOTE KWA MAANA HIYO AKIKWEPESHA MAENDELEO KWENYE MAJIMBO YA WAPINZANI ATAKIWEKA CHAMA CHAKE MAHALI PAGUMU ZAIDI. AACHE VITISHO VISIVYO NA TIJA.
 
Amejitahidi sana ku control mood yake na ujasiri, lakini hili la leo ni pigo kubwa kwake....
Hana ubavu wa kuzuia maendeleo kwa majimbo muhimu kama hayo waliyochukua Chadema...
 
Katika hali iliyokuwa ya kubeza Kikwete awaambia Wapinzani kwamba hata wasipomtambua wasisahau kwamba watahitaji ushirikiano wa Serikali iliyopo madarakani ili kuweza kuleta maendeleo katika Majimbo yao na kusisitiza kuwa na Serikali hiyo yeye ndio Rais wake.

Maana yake ni kwamba itabidi wamtambue ndio wataweza kupata ushirikiano. Sounds like a blackmail!!

Yaani mara nyingine tunataka kusikia tunachotaka kusikia tu. Mtu anakwambia "karibu" wewe unasema kakwambia "toka hapa"

Alichosema Kikwete, kwa mujibu wako hapo juu, na tafsiri yako, ni vitu viwili tofauti.

Kikwete anawaambia tu kwamba yeye ndiye de facto na de jure president, na watahitaji ushirikiano wa serikali yake. Hizi protests zao haziwezi kumu unseat legally. Sijaona tishio hapo, ana knock some common sense into their quixotic zeal tu.

Hata kama wameibiwa kura kweli, wanachofanya ni utoto, wana half step. Kama wameibiwa waitishe maandamano nchi nzima ya wanachama na supporters wao, hata kama hawana legal means. Waitishe muswada wa dharura bungeni kubadilisha sheria za uchaguzi kabla ya kitu kingine chochote, waitishe mkutano wa katiba kwa mgomo wa nchi nzima, hapo nitawaona wako serious.

Hizi habari za kutoka bungeni nusunusu, mara wanapigia kura chaguo la Kikwete PM, mara wanasusia kusikiliza hotuba yake, nawaona wanacheza.
 
Chadema ni kizazi kipya na kipo kwa maslahi ya wengi -ataipata huu ni mwanzo big up chadema -message sent keep going
 
Mi ninachokiona ni kubagua watu. Anajipinga mwenyewe kwa kusema atashughulikia mpasuko halafu....Lakini kuna kitu watanzania tuna sahau nacho ni serikali za mtaa na serikali kuu ni vitu viliwi tofauti. Yeye yuko serikali kuu. Atawezaje kuziamrisha serikali za mtaa na hasa mikoa mikubwa ambako sisiem imeangushwa. Langu jicho

Wenye mamlaka kwenye serikali za mitaa na ambao ndio wenye mafungu ni wakurungezi (DED) na hao huchaguliwa na Rais na huwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, upo hapooooooo?
 
Ha ha aaaa, adui yako muombee njaa, ndio msemo wako hapo juu unavyo maanisha. Kuvunjwa bunge inategemea na wingi wa wabunge ili ile 2/3 ipatikane, je CHADEMA wabunge hao wanao ? Jibu hakuna. Na KWA KAWAIDA MTU HUWA HASUSI KWANI UKISUSA WENZIO WALA, NA CHADEMA WAMESUSA WENZAO WALA WAKIJA KUSHTUKA CHAKULA MEZANI HAKUNA.

u didnt think twice lol...
hivi unajua wale wageni wameshtuka sana na wataanza kumuangalia KIKWETE kwa jicho hivi inawezekana eeh???
ngoja uone misaada anayoitegemea itakavyopigwa Panga ...
sijui atakimbilia wapi....
wewe usiombe ugombane na mumeo halafu waingie wageni mumeo aondoke bila kuaga.....
haitakaa iondoke...
mbaya hawezi kuwafanya kitu.... ni POWER....
 
Ha aha aaaaaa, yeye ndio Rais kweli, na nyenzo zote za kifedha za maendeleo ziko serikalini kwake. Na kodi hata yale majimbo waliyoshinda wapinzani atakusanya kwa mujibu wa sheria na kuitumia serikalini. Na ndipo hapo aliposema hawana wa kumlilia zaidi ya yeye , kwani hayo yote waliyo yaahidi wapinzani, ni yeye ndio wakuyatekeleza na serikali yake na si mwingine.

Mtasoma namba tu !

wewe hata utu wako nadhani utakuwa umeuuza ama lah! hukutoka nao wakati wa kuzaliwa ulikwama sehemu
sidhani kama uko sawasawa
 
ThinkTwice
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
  • email.png
    Send Email
user-online.png
Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

Join DateThu Nov 2010Posts12Thanks0Thanked 0 Times in 0 PostsNaona mwisho wa mwaka unataka ufike post 1000 nini regardless kwamba ni pumba au point
 
Kule anakopenda kukipilia wale watu wanatabia ya kufanyia kila kitu utafiti sio kama ccm kutaka kuzima kwa manufaa ya chama...
Hapo walipo tayari wameshatuma maujumbe kwa nchi zao kilichotokea na wataanza kuchunguza safari zitapungua tuuuuuuuu

i am in love with chadema lol
 
Ningekuwa Kikwete...kwanza nisingekubali kuapishwa kama watu wamechakachua kura. Pili nikielewa maana halisi ya HAKI mshindani wangu ambae ni Dr Slaa ningekaa nae na kuteua kamati maalum ya kupitia kura zote. Ikibainika kuwa kuna mtu au kikundi kimechezea kura ningetumia sheria zilizopo kukishughulikia. Nikitambua kwamba amani haijengwi kwa vitisho na majigambo. Tatu, ningehakikisha kuwa wakurugenzi wote waliohusika na kuharibu matokeo halisi wanaenda jela. Nne, kama mkuu wa nchi ningewaomba msamaha wananchi kwa serikali kuchakachua na ningewajibika ipaswavyo. Tano, ningeitisha uchaguzi mwingine bila mimi kugombea.
 
umewaona wapi? walipokuwa wanaangalia tv wewe ulikuwa unafanya nini?
kama ni wewe na umeumbwa na haya bila kukosa soni, na uwe shekhe/immamu wa msikiti wa mwembechai
uko msikitini na unashika maiki kuanza kuongoza swala waamini wako wanakula nduki
ungefanyaje... kama si aibu

Ukweli uko pale pale, BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA !
 
Wapinzani sasa hivi wameshika majimbo makubwa kama Mwanza, Ubungo, Arusha Mjini, Mbeya, Moshi Mjini, Kawe n.k . CCM wanaweza kuyaignore hayo majimbo at their own peril.

CCM na serelikali yao waliyojipa madaraka bila ya ridhaa ya wananchi wathubutu ku'ignore majimbo ambayo sisi wananchi tumewasimamisha wagombea wachadema,,,,,, hapo ndipo ndio watajua hasira zetu zipo wapi, na ataweka historia ya kuwa raisi wa kwanza duniani atakayeomba aachie nchi hauwezi uraisi,,,,,,,,

na huo umatonya wake anaoupanga kuufanya afikirie upya kwanza maana it wont be that easy,,,, he better not try ku'ignore our majimbos
 
Kisheria ni lazima wamtambue Rais kwani amechaguliwa kwa njia ambayo pia imewaweka hao wabunge madarakani. Yaani wamechaguliawa na wananchi na tume ya uchaguzi ikathibitisha matokeo. Watanzania tunapiga hatua na kusonga mblele na demokrasia. Uchaguzi wa safari hii unaonyesha kuwa CCM itapata taabu sana uchaguzi ujao. Kitu kikubwa cha kuangalia ni kuchagua watu wenye fikira za kuleta maendeleo na kuondoa umasikini na kuimarisha umoja. Mie kama raia wa kawaida sina chama utakapo fika uchaguzi ujao nitangalia nini CCM imefanya muhula huu na nini CCM na vyama vinginevyo wanasema watatekeleza ikiwa watapewa ushindi na wananchi. Tusikubali siasa za utengamano na machafuzi. Tunaomba Mola ije siku ambayo baada ya uchaguzi wale walioshindwa wanawapongeza walioshinda na kuahidi kushirikiana kwa bidii moja kwa maslahi ya taifa. Na wale walioshinda wanachukua ushindi waliopewa kama dhamana na wasianze kuwasaka walioshindwa na kulipiza kisasi kwa mambo yaliopita - hiyo ni kazi ya vyombo vya sheria na haki. Mungu ibariki TZ
 
Ha aha aaaaaa, yeye ndio Rais kweli, na nyenzo zote za kifedha za maendeleo ziko serikalini kwake. Na kodi hata yale majimbo waliyoshinda wapinzani atakusanya kwa mujibu wa sheria na kuitumia serikalini. Na ndipo hapo aliposema hawana wa kumlilia zaidi ya yeye , kwani hayo yote waliyo yaahidi wapinzani, ni yeye ndio wakuyatekeleza na serikali yake na si mwingine.

Mtasoma namba tu ![/QUOTE

Hayo majimbo yasipopata huduma ya kuridhisha, uchaguzi ujao ccm wategemee kutupwa nje kabisaaa, na wataisoma namba tu ccm.
 
Woooow sasa naanza kuipenda siasa ya Tanzania, kwani kwa hili walilolifanya CHADEMA limedhihirisha namna gani tulivyo na Rais mwenye upeo wa k.....k..... ktk kutazama mambo kwa mapana na marefu yake. Sasa ni maana ya kugeuza bunge kuwa baraza la vijembe, majigambo, ubabe badala ya kuwa mstaarabu na kuwaita wapinzani mezani kwa mazungumzo, it's real sad but He is the president, i feel like crying and laughing at the same time, how do you see Tanzania five years from now?????????
 
Wabunge wa CHADEMA wametoka kwenye ukumbi wa Bunge ila wameonekana wakitazama TV (Runinga) hotuba ya JK , sasa hapo haumtambui kivipi ili hali unamsikiliza ? si ni bora ungekaa tu ukumbini ukamsikiliza vizuri Mh. Rais
you ====>:caked: too much==> :blabla: No Evidence===> :lie:
 
Kisheria ni lazima wamtambue Rais kwani amechaguliwa kwa njia ambayo pia imewaweka hao wabunge madarakani. Yaani wamechaguliawa na wananchi na tume ya uchaguzi ikathibitisha matokeo. Watanzania tunapiga hatua na kusonga mblele na demokrasia. Uchaguzi wa safari hii unaonyesha kuwa CCM itapata taabu sana uchaguzi ujao. Kitu kikubwa cha kuangalia ni kuchagua watu wenye fikira za kuleta maendeleo na kuondoa umasikini na kuimarisha umoja. Mie kama raia wa kawaida sina chama utakapo fika uchaguzi ujao nitangalia nini CCM imefanya muhula huu na nini CCM na vyama vinginevyo wanasema watatekeleza ikiwa watapewa ushindi na wananchi. Tusikubali siasa za utengamano na machafuzi. Tunaomba Mola ije siku ambayo baada ya uchaguzi wale walioshindwa wanawapongeza walioshinda na kuahidi kushirikiana kwa bidii moja kwa maslahi ya taifa. Na wale walioshinda wanachukua ushindi waliopewa kama dhamana na wasianze kuwasaka walioshindwa na kulipiza kisasi kwa mambo yaliopita - hiyo ni kazi ya vyombo vya sheria na haki. Mungu ibariki TZ

Ninadhani kuwa wengi wetu humu tunahitaji elimu ya uraia ili tuweze kuwa na mijadala chanya. Nchi yetu ni Jamhuri maana yake ni nchi ambayo viongozi wanapatikana kwa kuchaguliwa na watu. Wagiriki walitumia maneno demos (watu) na kratos (nguvu) yalipounganishwa ndipo tukapaa neno demokrasia (democracy) yaani utawala wa watu. Warumi wao walieleza dhana hiyo kwa maneno mawili res publica ambayo inamaanisha mambo ya watu. Maneno haya yalipounganishwa ndipo tukapata neno (republic) ambayo ina maana nchi ambayo utawala wake si wa kifalme na ambao madaraka na chanzo kamili hubaki kwa wananchi. Ni kwa mintaarafu hiyo basi kiongozi wa nchi ya kidemokrasia anahesabiwa kuwa mtumishi na ni lazima awe ametokana na utashi wa kweli wa watu wa nchi ile.

Kingine ni kuwa watu katika nchi wana haki ya kupinga na kutoa mawazo tofauti jinsi nchi yao inavyotawaliwa au wanavyotaka kutawaliwa. Kumpinga kiongozi kunafanyika popote pale iwe bungeni, barabarani, kwenye karamu na kadhalika na kadhalika. Katika sehemu ambapo upingaji wa serikali au viongozi wake kunaruhusiwa kwa nguvu zote bunge ndiyo sehemu kubwa. Kwani hapa wawakilishi wa wananchi wana haki ya kuonyesha kwa uwazi kabisa juu ya kutoridhishwa na vitendo vya serikali au kupinga hatua za serikali. Mbinu za kupinga ni nyingi wengine wanaweza kutoa hoja za maneno na wengine za vitendo.

Kwa Chadema mbinu waliyoitumia leo ni sahihi na wao si wa kwanza na hawatakuwa wa mwisho. Kule Kenya baada ya Kibaki kuiba kura wabunge wa ODM walikuwa hata hawasimami alipokuwa akiingia bungeni. Kule Kenya Raisi ni mbunge pia. CUF huko Zanzibar walisusia baraza hata kufikia hatua ya Wawakilishi wa CCM kutumia kanuni za kuwafungia. CUF hawakuyumbishwa na hilo kitu kilichosababisha muafaka wa kwanza. Katika mazingira ya sasa nani anategemea kuwa CCM wana hamu ya kuwapa Chadema nafasi katika bunge hili kwani CCM, CUF, NCCR-Mageuzi(nasikia siku hizi ni "NCCR-manunuzi"), TLP na UDP wamejiunga pamoja dhidi ya Chadema. Hapo ndio Chadema ilikuwa ni lazima watumie mbinu nyakaji (headline grapping tactic) ili kuweza kutuma ujumbe. Leo macho ya wengi yalielekezwa bungeni, mabalozi wa nje walikuwepo na hiyo ilikuwa fursa nzuri sana kwa Chadema kutoa na kutuma ujumbe si tu kwa Kikwete bali pia kwa jumuia ya kimataifa kuwa uchaguzi uliomuweka madarakani Kikwete haukuwa huru wala wa haki. Na ndicho kitu kimemuuma sana Kikwete na CCM. Wahenga walisema "Mtenda akitendewa ujihisI kaonewa" na vilevile "Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu." Wakati wanafanya hujuma za uchaguzi wao waliona ni sawa kwani "ushindi ni lazima." Sasa ulazima huo umeonekana kuwa ulikuwa ni wizi wanaona haya lakini wanataka kulazimisha kuwa tufunike kombe mwanaharamu apite na kuwa yaliyopita yamepita tugange yajayo. Katu kamwe.

Pale mtawala katika nchi ya kidemokrasia anapokiuka matakwa au utashi wa wananchi na wananchi wakajua hivyo wana kila haki ya kumpinga na kumsuta. Kwa wenzetu Wazungu humtupia mayai viza. Eti sisi wanataka tumwache atanue. Hiyo haikubaliki kwani wananchi waelewa wana kila haki ya kumwonyesha kuwa hawatakubali kugeuzwa mazezeta. Mwaka 1962 Mwalimu Nyerere alisema kuwa kama tuna Raisi anafanya kitu ambacho si cha Kitanganyika kwa kukiuka maadili ya Kitanganyika Wananchi wana haki ya kuamuka na kusema "We won't have this either from the President or President Squared" yaani hatutakubali iwe kutoka kwa Raisi au Raisi kipeuo cha pili.

Nilirudia kauli hii pale Channel Ten kwenye moja ya vipindi vya Pambanua lakini sijui kama wengi walinielewa. Kitendo cha leo cha Chadema ni kutimiza maneno ya Mwalimu kuwa kitendo cha Kikwete, Tume ya Uchaguzi, Usalawa wa Taifa, CCM na washirika wao wote kuchakachua uchaguzi hakikubaliki kwani kimekiuka maadili ya Kitanzania na hivyo wamesema WE WON'T HAVE IT EITHER FROM THE PRESIDENT OR PRESIDENT SQUARED!
 
Ha aha aaaaaa, yeye ndio Rais kweli, na nyenzo zote za kifedha za maendeleo ziko serikalini kwake. Na kodi hata yale majimbo waliyoshinda wapinzani atakusanya kwa mujibu wa sheria na kuitumia serikalini. Na ndipo hapo aliposema hawana wa kumlilia zaidi ya yeye , kwani hayo yote waliyo yaahidi wapinzani, ni yeye ndio wakuyatekeleza na serikali yake na si mwingine.

Mtasoma namba tu !
Endelea kujipumbaza....
Huijui impact ya kukataliwa mbele ya Mabalozi unaowapelekea mabakuli ya misaada kila siku.
Hujui political impact kwa CCM na kwa JK mara baada ya wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi.
Kitakachomwokoa (ambacho najua ni kigumu sana) ni perfomance ya serikali yake. Iki-meet expectations za wadanganyika atawin lakini kama ita perfom mashuzi kama serikali iliyoisha, ategemee machungu na fedheha zaidi
 
Ninadhani kuwa wengi wetu humu tunahitaji elimu ya uraia ili tuweze kuwa na mijadala chanya. Nchi yetu ni Jamhuri maana yake ni nchi ambayo viongozi wanapatikana kwa kuchaguliwa na watu. Wagiriki walitumia maneno demos (watu) na kratos (nguvu) yalipounganishwa ndipo tukapaa neno demokrasia (democracy) yaani utawala wa watu. Warumi wao walieleza dhana hiyo kwa maneno mawili res publica ambayo inamaanisha mambo ya watu. Maneno haya yalipounganishwa ndipo tukapata neno (republic) ambayo ina maana nchi ambayo utawala wake si wa kifalme na ambao madaraka na chanzo kamili hubaki kwa wananchi. Ni kwa mintaarafu hiyo basi kiongozi wa nchi ya kidemokrasia anahesabiwa kuwa mtumishi na ni lazima awe ametokana na utashi wa kweli wa watu wa nchi ile.

Kingine ni kuwa watu katika nchi wana haki ya kupinga na kutoa mawazo tofauti jinsi nchi yao inavyotawaliwa au wanavyotaka kutawaliwa. Kumpinga kiongozi kunafanyika popote pale iwe bungeni, barabarani, kwenye karamu na kadhalika na kadhalika. Katika sehemu ambapo upingaji wa serikali au viongozi wake kunaruhusiwa kwa nguvu zote bunge ndiyo sehemu kubwa. Kwani hapa wawakilishi wa wananchi wana haki ya kuonyesha kwa uwazi kabisa juu ya kutoridhishwa na vitendo vya serikali au kupinga hatua za serikali. Mbinu za kupinga ni nyingi wengine wanaweza kutoa hoja za maneno na wengine za vitendo.

Kwa Chadema mbinu waliyoitumia leo ni sahihi na wao si wa kwanza na hawatakuwa wa mwisho. Kule Kenya baada ya Kibaki kuiba kura wabunge wa ODM walikuwa hata hawasimami alipokuwa akiingia bungeni. Kule Kenya Raisi ni mbunge pia. CUF huko Zanzibar walisusia baraza hata kufikia hatua ya Wawakilishi wa CCM kutumia kanuni za kuwafungia. CUF hawakuyumbishwa na hilo kitu kilichosababisha muafaka wa kwanza. Katika mazingira ya sasa nani anategemea kuwa CCM wana hamu ya kuwapa Chadema nafasi katika bunge hili kwani CCM, CUF, NCCR-Mageuzi(nasikia siku hizi ni "NCCR-manunuzi"), TLP na UDP wamejiunga pamoja dhidi ya Chadema. Hapo ndio Chadema ilikuwa ni lazima watumie mbinu nyakaji (headline grapping tactic) ili kuweza kutuma ujumbe. Leo macho ya wengi yalielekezwa bungeni, mabalozi wa nje walikuwepo na hiyo ilikuwa fursa nzuri sana kwa Chadema kutoa na kutuma ujumbe si tu kwa Kikwete bali pia kwa jumuia ya kimataifa kuwa uchaguzi uliomuweka madarakani Kikwete haukuwa huru wala wa haki. Na ndicho kitu kimemuuma sana Kikwete na CCM. Wahenga walisema "Mtenda akitendewa ujihisI kaonewa" na vilevile "Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu." Wakati wanafanya hujuma za uchaguzi wao waliona ni sawa kwani "ushindi ni lazima." Sasa ulazima huo umeonekana kuwa ulikuwa ni wizi wanaona haya lakini wanataka kulazimisha kuwa tufunike kombe mwanaharamu apite na kuwa yaliyopita yamepita tugange yajayo. Katu kamwe.

Pale mtawala katika nchi ya kidemokrasia anapokiuka matakwa au utashi wa wananchi na wananchi wakajua hivyo wana kila haki ya kumpinga na kumsuta. Kwa wenzetu Wazungu humtupia mayai viza. Eti sisi wanataka tumwache atanue. Hiyo haikubaliki kwani wananchi waelewa wana kila haki ya kumwonyesha kuwa hawatakubali kugeuzwa mazezeta. Mwaka 1962 Mwalimu Nyerere alisema kuwa kama tuna Raisi anafanya kitu ambacho si cha Kitanganyika kwa kukiuka maadili ya Kitanganyika Wananchi wana haki ya kuamuka na kusema "We won't have this either from the President or President Squared" yaani hatutakubali iwe kutoka kwa Raisi au Raisi kipeuo cha pili.

Nilirudia kauli hii pale Channel Ten kwenye moja ya vipindi vya Pambanua lakini sijui kama wengi walinielewa. Kitendo cha leo cha Chadema ni kutimiza maneno ya Mwalimu kuwa kitendo cha Kikwete, Tume ya Uchaguzi, Usalawa wa Taifa, CCM na washirika wao wote kuchakachua uchaguzi hakikubaliki kwani kimekiuka maadili ya Kitanzania na hivyo wamesema WE WON'T HAVE IT EITHER FROM THE PRESIDENT OR PRESIDENT SQUARED!

Ahsante kwa somo zuri la uraia

Sisemi kwamba Kikwete hajaiba kura, lakini naona CHADEMA wanachanganya watu, walipopiga kura kuhakiki pendekezo la Kikwete kwa nafasi ya Waziri Mkuu, walipiga kura kupigia pendekezo la nani ?
 
Back
Top Bottom