Viongozi wa CHADEMA Bunda, wasimamishwa na kuondolewa kwenye madaraka

Ila watu kama wasira ni wakuondoa kwenye system, na watu waliochoka ningetamani hata kama ni ccm nione damu changa type ya kina mwigulu..huko bunda embu fanyeni mambo mtoondolew wazee kama hawa..

Wasira amechoka sana,yeye kazi yake ni kulala usingizi bungeni amechoka akili na umri
 
Hata kama n kuhujumu lakn kumbuka mkuu CHADEMA hawajafanya haki kabisa kumpitsha esta bulaya na kumwacha yule jamaa wa kwanza hawakutumia akili hapa. Kuna shda gan kumuacha aliyeshnda akagombea? Kwasababu esta alikua tayar ana nafas ya viti maalum inakuaje tena aletwe kugombea huu n uonevu. Nimesikia clouds sasahv uko bunda karbu viongoz karbun wote wanaondoka ni vzr wangewaacha wenyej ndio waamue, haya hata sengerema CHADEMA wamefanya ujinga ulele wakumuacha kijana makin sana aliyekua tayar anakubalika wakamuweka kibaraka wa ngereja yan nina mashaka makubwa na mwenyekit wa CHADEMA kama kwel wanataka mabadiliko waache kuvuruga wananchi na kama walitumia intelligencia kuwapima wagombea kukublika kwao, bas inteligencia yao imefeli kwa kiwango kikubwa sana na ninashaur n vzr waiangalie upya hyo intelligencia
uliyo yaandika ni kweli lakini kumbuka kuwa kushika nafasi ya kwanza si hoja... hoja ni kwamba unamtaji gani wa watu?
 
Hata kama n kuhujumu lakn kumbuka mkuu CHADEMA hawajafanya haki kabisa kumpitsha esta bulaya na kumwacha yule jamaa wa kwanza hawakutumia akili hapa. Kuna shda gan kumuacha aliyeshnda akagombea? Kwasababu esta alikua tayar ana nafas ya viti maalum inakuaje tena aletwe kugombea huu n uonevu. Nimesikia clouds sasahv uko bunda karbu viongoz karbun wote wanaondoka ni vzr wangewaacha wenyej ndio waamue, haya hata sengerema CHADEMA wamefanya ujinga ulele wakumuacha kijana makin sana aliyekua tayar anakubalika wakamuweka kibaraka wa ngereja yan nina mashaka makubwa na mwenyekit wa CHADEMA kama kwel wanataka mabadiliko waache kuvuruga wananchi na kama walitumia intelligencia kuwapima wagombea kukublika kwao, bas inteligencia yao imefeli kwa kiwango kikubwa sana na ninashaur n vzr waiangalie upya hyo intelligencia

Wacha kuweweseka wewe segamneke,cdm wana akili kuliko wewe unaye kuja kumbwelambwela hapa jukwaani.nenda kale mihogo ukunje mbavu
 
Hata kama n kuhujumu lakn kumbuka mkuu CHADEMA hawajafanya haki kabisa kumpitsha esta bulaya na kumwacha yule jamaa wa kwanza hawakutumia akili hapa. Kuna shda gan kumuacha aliyeshnda akagombea? Kwasababu esta alikua tayar ana nafas ya viti maalum inakuaje tena aletwe kugombea huu n uonevu. Nimesikia clouds sasahv uko bunda karbu viongoz karbun wote wanaondoka ni vzr wangewaacha wenyej ndio waamue, haya hata sengerema CHADEMA wamefanya ujinga ulele wakumuacha kijana makin sana aliyekua tayar anakubalika wakamuweka kibaraka wa ngereja yan nina mashaka makubwa na mwenyekit wa CHADEMA kama kwel wanataka mabadiliko waache kuvuruga wananchi na kama walitumia intelligencia kuwapima wagombea kukublika kwao, bas inteligencia yao imefeli kwa kiwango kikubwa sana na ninashaur n vzr waiangalie upya hyo intelligencia

Jamaa wa kwanza alihujumu chama 2010 kwa Wassira
 
Wamevuliwa wamejivua wenyewe tena wameapa kufanya kampeni za kumpinga ester bulaya..watu wamekitumikia chama wewe leo unakuja na kupewa nafasi...hawa ndio viongozi wanaojielewa hongereni KATIBU WA WILAYA WA CHADEMA na KATIBU MWENEZI WAKO

waache wajivue..kwani ukiwa katibu wa chama ni lazima wewe ndio uwe mgombea wa ubunge? walikuwa na mawasiliano na wassira na hilo linajulikana..Ester bulaa ni bora kuliko hao waliokuwa wamenunuliwa na Wassira..
 
Udhaifu wa Wassira
Kauli za vitisho na zinazoashiria udikteta. Moja ya udhaifu mkubwa wa Wasira ni kupenda kudharau haki, hoja na hata madai ya watu wengine. Mathalani, zilipotokea vurugu kadhaa katika mikutano ya vyama vya siasa zikihusisha polisi kuzuia shughuli za vyama hivyo na baadaye mapambano ya polisi na raia na labda raia kuuawa, Wasira alijitokeza hadharani na kushangaa kwa nini Msajili wa Vyama vya Siasa hajavifuta, ilhali akijua kwamba waliozuia mikutano ya vyama kinyume na sheria inavyotaka ni Polisi na walioua Raia ni polisi. Kauli hizi zinaashiria kuwa Wasira ni mtu anayeamini katika dola zaidi kuliko haki na mustakabali wa wananchi.
Jambo jingine ni "ubishi na ujuaji". Ukimsikiliza Wasira katika vyombo vya habari, bungeni na kwingineko, unaona kabisa kuwa kauli zake mara zote hazitolewi kujibu maswali yaliyoulizwa au kutatua matatizo yaliyopo, bali maswali hayo huishia kuuliza maswali mengine kwa kejeli na weledi mkubwa wa kiuzungumzaji.
Kwa mfano, alipoulizwa na mwandishi mmoja wa habari juu ya kuteswa na kuumizwa kwa Absalom Kibanda, Wasira alijibu: "…Kibanda ni nani katika siasa za vyama vingi Tanzania hadi Serikali imsake na kumtesa? Yeye siyo Mbowe, Slaa au Lipumba. Hata kama Serikali ingeamua kupambana na maadui zake Kibanda bado hawezi kufuzu kwa sababu yeye hayuko chama cha upinzani."
Unaweza kuona kuwa mwandishi amemuuliza swali muhimu ambalo lilihitaji ufafanuzi mkubwa wa Serikali, badala ya kulijibu, anaanza kumshusha Kibanda na kuonyesha kuwa si lolote wala chochote katika ulingo wa raia muhimu katika nchi.
Wangapi tunajua mchango wa Kibanda katika kusimamia ukuaji wa haki za vyombo vya habari na waandishi wa habari Tanzania? Kwa nini waziri mwenye hadhi ya Wasira haanzi hata kusema alivyosikitishwa kutokana na kuumizwa vibaya kwa mhariri huyo mwandamizi na badala yake anaanza kuonyesha kuwa "Kibanda si lolote". Kauli hizi zisidharauliwe hata kidogo, ndizo zinapaswa kuwagutusha wananchi kujua aina ya viongozi wao wanaohitaji kuongoza dola.
Nilikuwa najiuliza, Kama kesho Wasira akiwa Rais wa nchi hii halafu mwandishi mwingine ameuawa au kuumizwa, atajibu nini? Unaposhindwa kuwa mwaminifu na mlinzi wa maisha na haki za watu unapokuwa mdogo, huwezi kujifunza kufanya hivyo utakapokuwa mkubwa.

Tuwe makini na waroho wa madaraka kama huyu kiumbe
 
Wamevuliwa wamejivua wenyewe tena wameapa kufanya kampeni za kumpinga ester bulaya..watu wamekitumikia chama wewe leo unakuja na kupewa nafasi...hawa ndio viongozi wanaojielewa hongereni KATIBU WA WILAYA WA CHADEMA na KATIBU MWENEZI WAKO

Cdm ni zaidi ya kiongozi,siyo ccm inayokumbatia viongozi
 
Soma biblia Yesu alitoa mfano kuwa kuna watu waliajiliwa asubuhi wakapatana mshahara wengine wakaja SAA 11 asubuhi wakapatana bei sasa unakuja kugoma kupokea mshahara
 
Viongozi wa CHADEMA jimbo la BUNDA akiwemo Katibu Mwenezi wameamua kuachia ngazi katika nafasi zao zote wakipinga kuteuliwa kwa Ester Bulaya kuwa mgombea wa CHADEMA katika jimbo hilo...

Mgombea akiyeshika nafasi ya kwanza na kupigwa chini ameanza kampeni ya kumpindua ESTER..

Naye katibu wa wilaya wa jimbo hilo ameamua kuachia ngazi katika nafasi hiyo kwa madai ya kutoridhishwa na namna chama hicho kinavyoendeshwa na kutothaminiwa kama kiongozi....

Niahasema toka mda sana chama cha chadema ni chama kinachoongozwa na fikra za wachache wenye maslahi yao binafsi
ukitizama ujio wa lowasa ni mawazo ya mtu mmoja kwa manufaa yake pia wote waliofukuzwa ccm wameenda na kupewa madaraka sasa iko wapi kasi yao ya kupambana na mafisadi zaidi wameanza kuwapokea hao hao waliowaita mafisadi hii inajionesha wazi hawa ni WASAKA TONGE TU #HAPAKAZITU NDIO HABARI YA MJINI
 
Nimecheka sana. Yaani, dawa ya mamluki ni rahisi sana. Yaani baada ya kukatwa jina asigombee CHADEMA, mamluki katimkia CCM na hapo hapo kawa mpiga debe wa Wassira!
Kuna kila dalili kuwa, Bulaya atashinda kirahisi kabisa.
 
Hata kama n kuhujumu lakn kumbuka mkuu CHADEMA hawajafanya haki kabisa kumpitsha esta bulaya na kumwacha yule jamaa wa kwanza hawakutumia akili hapa. Kuna shda gan kumuacha aliyeshnda akagombea? Kwasababu esta alikua tayar ana nafas ya viti maalum inakuaje tena aletwe kugombea huu n uonevu. Nimesikia clouds sasahv uko bunda karbu viongoz karbun wote wanaondoka ni vzr wangewaacha wenyej ndio waamue, haya hata sengerema CHADEMA wamefanya ujinga ulele wakumuacha kijana makin sana aliyekua tayar anakubalika wakamuweka kibaraka wa ngereja yan nina mashaka makubwa na mwenyekit wa CHADEMA kama kwel wanataka mabadiliko waache kuvuruga wananchi na kama walitumia intelligencia kuwapima wagombea kukublika kwao, bas inteligencia yao imefeli kwa kiwango kikubwa sana na ninashaur n vzr waiangalie upya hyo intelligencia

Kama mpenzi wa chadema, naona hapa wamekosea sana. Uchaguzi wa kura za maoni umefanyika, mtu kashinda, unamkataje jina, tunaanza kufanya makosa yale yale ya ccm. Esther yeye hata kwa viti maalumu ataingia bungeni. Tatizo liko wapi? Kwa mfano Esther akishindwa uchaguzi ndo itakuwaje? Atakaa nje ya bunge?
 
image.jpg Chadema Bunda yabomoka vibaya
-Robo tatu ya viongozi wa kamati tendaji wajihudhuru nyadhifa zao
-Wasema chanzo ni Esther Bulaya kubebwa na viongozi wa juu wa chama hicho
-Wasema wamekitumikia chama hicho na kuwekwa ndani lakini sasa hawathaminiwi

Agosti 21, 2015;

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) katika Wilaya ya Bunda, kimepata mpasuko mkubwa kutokana na jana karibu robo tatu ya viongozi wake kujihudhuru nafasi zao, akiwemo katibu mwenezi wa Chadema jimbo la Bunda Emmanuel Malibwa, mwenyekiti wa jimbo hilo Samwel Alfred na katibu wa Chadema Wilaya Rita Itandilo.

Baadhi ya viongozi hao pamoja na baadhi ya wanachama wa chama hicho walisema kuwa sasa hivi watamuunga mkono mgombea wa CCM katika jimbo la Bunda Stephen Wassira, kwa sababu viongozi wao wamejichanganya sana, kwa kuwafanyia maamuzi ambayo siyo sahihi.

Habari zinasema kuwa chanzo cha viongozi hao kujihudhuru nafasi zao ni aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kundi la vijana kutoka mkoani Mara, kupitia tiketi ya CCM Esther Bulaya, aliyejiunga na chama hicho hivi karibuni na kuteuliwa kuwa mgombea wa ubunge katika jimbo la Bunda mjini kupitia tiketi ya Chadema, huku aliyeshinda kura za maoni Pius Masururi akikatwa jina lake.

Viongozi hao walisema kuwa kwa mjibu wa katiba uteuzi wa mbunge huko kwenye kamati kuu, lakini walivyowaletea Esther Bulaya yeye alikuja na uongozi wake bila ya kuwashirikisha viongozi waliokuwepo na kwamba kwa jinsi hiyo wameamua kujihudhuru nafasi zao na kumwachia viongozi aliokuja nao.

Viongozi hao pamoja na wa kamati tendaji na baadhi ya walinzi, wakifuatana na wananchama wa kawaida zaidi ya 70, wamejihudhuru nafasi zao kwa kile walichodai kuwa viongozi wa chama hicho wakiwemo wa ngazi ya juu wameivunja katiba ya chama hicho kwa makusudi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika hoteli ya Green Guden, mjini Bunda viongozi hao walisema kuwa wameamua kujihudhuru nafasi zao na kubakia wanachama wa kawaida kwa sababu viongozi wao wa Mkoa, kanda na Taifa wamekiuka katiba ya chama hicho.

“Kwa kile kilichotokea kupitia uongozi wetu wa mkoa, kupitia katibu wetu wa Chama Mkoa Chacha Heche na mwenyekiti wetu wa Mkoa wameshindwa kujua jimbo la Bunda msemaji wa chama au Mkoa ni nani wao badala ya kufuata katiba wameshindwa kujua katiba inasemaje kuhusu malalamiko yoyote.

“Wao badala ya kuona katiba inasemaje na kanuni za chama zinasemaje na taratibu zinasemaje kuhusu malalamiko yoyote kama yalikuweo ili waweze kuyafanyia kazi, lakini kilichofanyika ni udhalilishaji na maamuzi ambayo kamati tendaji ina mamlka ya kuyafanyia kazi, kupitia viongozi hawa ambao leo wanatoa matamko, mimi huwa sikubali kutokuonyesha msimamo.

“Mimi siku zote huwa napenda kuwa muwazi leo nafikia kuchukuwa maamuzi haya magumu, mimi ni mwanchama mwaminifu wa Chadema nimekitumikia chama kwa kipindi cha miaka zaidi ya kumi, lakini leo Bunda imekuwa shamba la bibi, maamuzi ya mtu ndiyo yanayokuja kulitengeneza jimbo la Bunda, kamati tendaji ya jimbo la Bunda ilifanya uteuzi wake wa awali kupitia kura za maoni.

“Walimaliza kura za maoni wakaenda kwenye kamati tendaj,i mimi kama katibu wa Wilaya naletewa mapendekezo ya kamati tendaji ndiyo ninayAfanyia maamuzi, nilichukuwa majina ya wsagombea nikayapeleka kwenye tume kwenda kuyawatambulisha, lakini kilichotokea Mkoa na Kanda na Naibu Katibu mkuu wakatoa maelekezo mengine mbadala, akaletwa mtu ndani ya ofisi yangu bila kunishirikisha wala hata kupewa barua ya kunitambuliusha.

“Lakini kilichofanyika huyo aliyeletwa akaanza kunielekeza lakini mimi kama katibu wa Wilaya ninayejua utaratibu nilikataa, lakini kilichotokea nikiingia ofisini kwangu pale naonekana kama mimi ni mgeni au mtuanayehitaji huduma pale, na kilichotokea wakachonga mhuri mwingine wakatengeneza mhuri ndani ya mhuri mwingine.

“Ndicho kilichopelekea leo hii nimeamua kuchukuwa maamuzi magumu kama mwanamke na nimeamua kujihudhuru nafasi hii ya katibu wa wilaya Chadema nitabaki kama mwanachama wa kawaida isije ikaonekana mimi ndiye nimesababisha chama kushindwa”alisema.

Naye mwenyekiti wa jimbo la Bunda, Samwel Alfred, alisema kuwa “mimi kama mwenyekiti wa Chadema jimbo nimeamua kujihuduhuru uenyekiti wangu wa jimbo la Bunda na nimeamua kujihudhuru uenyekiti wangu wa mtaa, kwa sababu kuna vitu vilivyonikera baada ya kuona kuna watu wanavunja katiba.
“Cha kwanza tulipiga kura za maoni wakapatikana washindi watatu wakiwemo wawili ambao waamekitumikia chama, lakini cha ajabu wakarudisha jina la mshindi wa tatu (Esther Bulaya), hawakuvunja katiba, lakini cha ajabu aliyerudishwa hakuonyesha ushrikiano na viongozi waliokuwepo, kwa kuhofia kuwa walikuwa kambi nyingine kwamba watasababisha ashindwe.” Alisema.

Aliongeza kuwa pia kwa upande wa wagombea udiwani wagombea waliopendezwa na kamati tendaji pia majina yao yalibadilishwa na viongozi wa mkoa, kanda pamoja na Naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, ambapo yaliletwa majina ya wagombea wengine na kuondolewa wale waliokuwa wameshinda na kupitishwa na kamati tendaji ya jimbo.

“Mimi kama kiongozi niliyepigania chama hiki niliyepata kesi nyingi nimekaa magereza, nimenyanyaswa nimepigwa na nimedhalishwasana, leo hii nimeamua kujihudhuru lakini siyo kwamba naondoka peke yangu naondoka na makamanda wakiwemo wajumbe wa kamati tendaji na katibu wa Bavicha, kwa hiyo robo tatu ya kamati tendeji yote tumejihudhuru.

“Hata wenyeviti wa kata, viongozi wa vijiji, vitongoji wote wameamua kujihuduhuru, najua makamanda wataumia sana maana wanakitaka sana Chadema, lakini kiongozi aliyeletwa kugombea ameshindwa kutambua mchango wa viongozi hawa waliokipigania chama na kufikia hatua hii sisi tumeamua tumpishe ili ashinde salama’ alisema.

Katibu mwenezi wa Chadema jimbo la Bunda, Malibwa alisema “ Mimi kama katibu mwenezi wa Chadema jimbo la Bunda natangaza rasmi kuwa nimejihuduru nafasi yangu hiyo ya uenezi, na wafuasi wangu wote ambao niliwashawishi wakaingia Chadema leo watambuwe kuwa nimejihudhuru nafasi hiyo nitabaki kuwa mwanachama wakawaida tu.

“’Na sijaondoka peke yangu kama mnavyoona hapa ndugu waandishi wa habari tunao viongozi wote wa kata 20 za jimbo la Bunda, wakiwemo wenyeviti wa kata, makatibu wa kata, kwa ujumla kamati tendaji ya watu 17, mimi mwenezi, mwenyekiti wangu na wajumbe wengine tumeondoka imebaki na watu watatu tu” alisema.

Alisema kuwa yeye pia alikuwa ni mgombea udiwani wa kata ya Nyamakokoto na alikuwa tayari amechukuwa fomu katika ofisi ya Tume, lakini sasa hatarudisha fomu hizo na kwamba kutokana na utaratibu huo kuvunjwa na viongozi wao kwenye baadhi ya kata kuna wagombea wawili wa Chadema ambao tayari wameshachukuwa fomu za Tume kuwania nafasi hiyo.
Viongozi hao walisema kuwa pamoja na kujihudhuru watapiga kura zao katika uchaguzi mkuu ujao.

Wakati viongozi hao wakisema wamejihudhuru nyadhifa zao viongozi wa Chadema, akiwemo mmoja kwa niaba ya katibu mkuu wa Wilaya Kaunya Yohana, alisema kuwa viongozi hao wapatao kumi na moja hawajajihudhuru kama walivyodai bali wamesimamishwa uongozi kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kupandikiza wagombea bila taratibu, rushwa na kukiuka maadili na kanuni za chama hicho.
 
Wamevuliwa wamejivua wenyewe tena wameapa kufanya kampeni za kumpinga ester bulaya..watu wamekitumikia chama wewe leo unakuja na kupewa nafasi...hawa ndio viongozi wanaojielewa hongereni KATIBU WA WILAYA WA CHADEMA na KATIBU MWENEZI WAKO
Kama Zitto kashindwa katibu wa wilaya ataweza? wafanye wanachotaka UKAWA imejipanga.
 
Back
Top Bottom