Viongozi wa CHADEMA Bunda, wasimamishwa na kuondolewa kwenye madaraka

SCOOBY DOO

Member
Dec 16, 2013
76
69
CHAMA CHA DEMOKRASI NA MAENDELEO MKOA WA MARA KINAWAFAHAMISHA KUWA WAFUATAO WAMESIMAMISHWA NAFASI ZA UTENDAJI WA CHAMA WILAYA YA BUNDA KUANZIA TAREHE 15/08/2015

1. ALFRED SAMWEL IMANANI - MWENYEKITI WA JIMBO BUNDA

2.
RITHA SALVATORY IKANDILO - KATIBU WA WILAYA

3. EMMANUEL MACHUMU MARIBWA - MWENEZI JIMBO

4. DAMAS KUNJU - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO

5. MWITA NG'WENA - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO

6.
DICKSON KUJELWA - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO

7. DAVID ARBOGAST - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO

8. JUMANNE D. MOSSY - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO

9. NOAH LAWRENCE - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO

10. JACTON MUYENGI - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO

11.
MATALA ATHUMANI - KATIBU BAVICHA KATA SAZIRA

SABABU ZA KUSIMAMISHWA KWAO NI:
1. Kumpiga na kumjeruhi sana aliyekuwa mtia nia wa jimbo la Bunda Mjini Ndugu Chacha Nyamhanga ambaye alilazwa kwa muda wa siku tisa katika Hospitali ya Wilaya ya Bunda. Sababu za kumpiga mtia nia huyo ni baada ya kukataa kutoa rushwa na kuhamasisha wenzake wasitoe rushwa kwa viongozi hao.

2.
Kuhujumumatokeo ya kura za maoni kwenye kata zaNyamuswa, Nyamakokoto, Nyasura, Manyamanyama na kufanya vikao vya uteuzi wa madiwani nje ya ofisi bila vikao vya kikatiba ili kuifanya CCM ishinde kata zote za Wilaya ya Bunda, mfano; kwenye kata Nyamakokoto walimteua ndugu EMMANUEL MALIBWA aliyepata kura 5 badala ya ndugu GEORGIES MIYAWA aliyeshinda kwa kura 37, Kata ya Nyasura aliteuliwa Jumanne Mosi aliyepata kura 17 na akaachwa Mwamba Wasira aliyepata kura 47.

3. Kuiba mihuri ya Ofisi kwa lengo la kugushi nyaraka za chama.

4.
Kuwataka wagombea wa nafasi za udiwani kutoa rushwa ya kiasi cha shilingi laki tano ili waweze kuteuliwa na kamati tendaji kama wagombea wa nafasi hizo.

5.
Kuwasiliana na mgombea ubunge wa CCM Ndugu Steven Wasira kwa lengo la kuhujumu Chama ili mgombea huyo kutoka CCM apite bila kupingwa.

6.
Mwenyekiti wa Jimbo na aliyekuwa mtia nia wa ubunge Ndugu Ismail Pius Masululi amekuwa na mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ndugu Mirumbe kwa lengo la kuhujumu chama.

7. Matumizi mabaya ya fedha za chama.


IMETOLEWA NA

KATIBU WA MKOA MARA
 
Maccm wangewahamisha hapa na kuwapeleka kule.

Kazi njema Cdm, Ukiharibu unaharibiwa papohapo.!!

BACK TANGANYIKA
 
TANGAZO


CHAMA CHA DEMOKRASI NA MAENDELEO MKOA WA MARA KINAWAFAHAMISHA KUWA WAFUATAO WAMESIMAMISHWA NAFASI ZA UTENDAJI WA CHAMA WILAYA YA BUNDA KUANZIA TAREHE 15/08/2015

1. ALFRED SAMWEL IMANANI - MWENYEKITI WA JIMBO BUNDA 2. RITHA SALVATORY IKANDILO - KATIBU WA WILAYA 3. EMMANUEL MACHUMU MARIBWA - MWENEZI JIMBO 4. DAMAS KUNJU - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 5. MWITA NG’WENA - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 6. DICKSON KUJELWA - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 7. DAVID ARBOGAST - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 8. JUMANNE D. MOSSY - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 9. NOAH LAWRENCE - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 10. JACTON MUYENGI - MJUMBE WA KAMATI TENDAJI JIMBO 11. MATALA ATHUMANI - KATIBU BAVICHA KATA SAZIRA
SABABU ZA KUSIMAMISHWA KWAO NI:
1. Kumpiga na kumjeruhi sana aliyekuwa mtia nia wa jimbo la Bunda Mjini Ndugu Chacha Nyamhanga ambaye alilazwa kwa muda wa siku tisa katika Hospitali ya Wilaya ya Bunda. Sababu za kumpiga mtia nia huyo ni baada ya kukataa kutoa rushwa na kuhamasisha wenzake wasitoe rushwa kwa viongozi hao. 2. Kuhujumu matokeo ya kura za maoni kwenye kata za Nyamuswa, Nyamakokoto, Nyasura, Manyamanyama na kufanya vikao vya uteuzi wa madiwani nje ya ofisi bila vikao vya kikatiba ili kuifanya CCM ishinde kata zote za Wilaya ya Bunda, mfano; kwenye kata Nyamakokoto walimteua ndugu EMMANUEL MALIBWA aliyepata kura 5 badala ya ndugu GEORGIES MIYAWA aliyeshinda kwa kura 37, Kata ya Nyasura aliteuliwa Jumanne Mosi aliyepata kura 17 na akaachwa Mwamba Wasira aliyepata kura 47. 3. Kuiba mihuri ya Ofisi kwa lengo la kugushi nyaraka za chama. 4. Kuwataka wagombea wa nafasi za udiwani kutoa rushwa ya kiasi cha shilingi laki tano ili waweze kuteuliwa na kamati tendaji kama wagombea wa nafasi hizo. 5. Kuwasiliana na mgombea ubunge wa CCM Ndugu Steven Wasira kwa lengo la kuhujumu Chama ili mgombea huyo kutoka CCM apite bila kupingwa. 6. Mwenyekiti wa Jimbo na aliyekuwa mtia nia wa ubunge Ndugu Ismail Pius Masululi amekuwa na mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ndugu Mirumbe kwa lengo la kuhujumu chama. 7. Matumizi mabaya ya fedha za chama.


IMETOLEWA NA

KATIBU WA MKOA
MARA



Ujio wa Esther Bulaya chadema una kishindo kikuu.
Kukatwa kwenda mbele
 
Mtoa mada sijamwelewa vizuri yeye alitaka chama kisichukue hatua kwa faida ipi kwa viongozi wapuuzi kama hao hayo tuwaachie ccm ndiyo wenye mfumo wa kulindana siyo CDM
 
Salaam,

Leo nimeamua kuwapigia salute CHADEMA kwa upande wa Bunda na hii inadhihirisha ni jinsi gani wako imara kiintelligence na kipekee nipongeze uimara wa uongozi wa mkoa kwa kufanya kazi bila kutazama sura ya MTU wa pesa alizonazo hasa pale upuuzi unapojitokeza.

Ndugu,wasira ameshajitahidi kwa kadri awezavyo hili jimbo aweze kulichukua kilaini bila hata kupiga kampeni,kwa kutumia pesa kuwaonga wagombea hili wamrahisishie ushindi lakini njia zake zote zimedhibitiwa kwa kiwango cha hali ya juu (na kitengo cha ujasusi cha Chadema).

Wasira hakufurahia kupitishwa kwa bi.ester bulaya kuwa mgombea wa ubunge alitegemea apitishwe Pius hili amuwekee pingamizi kwenye hile scandal yake ya (MD/OP).Ndio maana walimzuia bi.ester kuchukua form kwa masaa kadhaa lakini walikubali kutoa form baada ya mabishano makali.mpango huo ni moja kati ya njama ovu ambayo Chadema waliipangua kitaamu.
 
Back
Top Bottom