Viongozi wa CHADEMA Arusha warudisha kadi

Viongozi wa CHADEMA Arusha warudisha kadi

Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha wameanza kurudisha kadi za chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mara tu baada ya uteuzi wa Katibu Mkuu mpya wa Chama.

Viongozi hao wa CHADEMA Arusha wametoa madai kadhaa ambayo yamewafanya kufikia uamuzi huo kwa nyakati tofauti.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Olumuriaki Ndugu Godfrey Kitomari na wanachama wanachama wa chadema 97 wa Kata ya Sombetini wamerudi CCM kwa sababu zifuatazo;-

1. Kuridhishwa na kasi ya Mhe Dkt Magufuli.

2. Kuchukizwa na Mbowe kukiuza chama na kuiacha agenda ya kukemea ufisadi kama ilivyokuwa mwanzo na badala yake kuwatetea.

3. Uteuzi wa Katibu Mkuu asiye na uwezo lakini mwenye rekodi mbaya kwenye jamii.

CdkkXfVWAAA2dsb.jpg

Pichani: Ndugu Kitomari akiveshwa Kofia ya CCM kwenye Mkutano wa hadhara wa kukaribishwa CCM.

CdkkZoeWIAAhLtg.jpg

Wananchi wa Kata ya Sombetini wakishuhudia tukio la Mwenyekiti huyo wa Mtaa kujiunga na CCM.

CdkkdP0XIAAuS6a.jpg

WanaCCM wakimlaki Ndugu Kitomari mara baada ya kujiunga na Chama hicho.


Katika tukio jingine;
Mwenyekiti wa BAVICHA Kata ya Mjini Kati Ndugu Ally Kaole (pichani) naye amejiuzulu nafasi yake hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi - CCM.

Kaole ametoa sababu za uamuzi wake huo kuwa ni;-

1. Uteuzi wa Katibu asiyekijua Chama lakini asiyejua falsafa za Uongozi na Utawala, amesema uteuzi huo unalenga kuua Chama hicho. Ndugu Ally amedai kuwa Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA na yule aliyestaafu hawafanani hata chembe, ni sawa na kufananisha Kifo na Usingizi.

2. Amesikitishwa na Mwenyekiti wa Chama kutetea majipu tena hadharani, akisema hatua hiyo imeondoa uhalali wa yeye kuwepo katika chama hicho ambacho aliamini kuwa kinachukizwa na majipu na kwamba kilikuwa kinaomba ridhaa ili kuyashughulikia.

944864_715173401958985_6697346186317879331_n.jpg

Pichani: Ndugu Ally Kaole (aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Arusha.
huko arusha walimtaka nani awe katibu? warudishe tuu tutazalisha wengine mwenyekiti mbowe namuaminia kwa kujua kutengeneza mambo
 
Ila ki ukweli ukitaka upate katibu mwingine kama Dr Slaa kwa Chadema huwezi kupata labda kidogo angekuwepo Zitto . Tukubali huo ukweli kwamba Mbowe ameshampoteza mtu muhimu lazima aanze kujenga upya.
Kama Zitto kabwe wangekuwepo chadema huu ndo ulkua mud a Wa kumpa ukatibu mkuu tatzo CHADEMA wanafeli katika jambo la kuhandle matatzo yao mana hawana uvumilivu km wenzao Wa ccm hua wanavumilia sana name laiti km CHADEMA ingepewa uvumilivu wa kisiasa mpaka Leo ingekua tishio maana kuna wengi walifukuzwa CHADEMA kwa tuhuma kama vile kina Kitilya Mkumbo.

Samson mwigamba, Zitto kabwe name wengneo ndo mana hadi Leo CDM imepoteza watu muhimu ktk chama chao.
 
Hao watoto wa kiswahili hapo bondeni tunawajua watoto wa mama hao...hot port family.
Wakati mko nao ni makomando Sasa wameondoka ooo watoto wa Kiswahili
Vizuri umewaita watoto wa mama badala ya watoto wa mjini
 
Muliotoka CHADEMA na mutakaotoka ni haki yenu.Muhimu tuendelee kupeana heshima.
 
Siasa za propaganda zinawapeleka wapi acheni uwongo ..mimi nipo Arusha ..cjaona haya mnayopost wala hizo picha cjui mmetoa wapi?
 
Duh hao walikuwa CCM siku nyingi sana.Pili kwani kuna ubaya mtu akihama chama??Mie sioni shida,nawatakia hao wawili kila la heri.Mie nilidhani Arusha wamehamia CCM kumbe hao UVCCM wa siku nyingi....................
 
Umaarufu wa Zitto ulimpatia jimbo moja katika uchaguzi uliopita. Uzembe wa Chadema wa kumwondoa Zitto umewapa majimbo mangapi?
 
Arusha hata lema akihamia ccm bado chadema itakua strong hold ya chadema.but kwa ujumla chadema in a hali mbaya sana kitaifa ,kwa kuondokewa na mjenga hoja slaa.na kwa kasi hii ya magufuli! I don't see chadema wakipa hata 30 percent ya votes 2020!
 
Kwa faida ya jamvi hao wote unaowaona wanatokea kata ya Kati ambayo CCM walishinda kati ya kata kumi na tisa.Sifa ya kata ya kati ni kama ifuatavyo.
1.Vijana wengi hawataki kufanyakazi muda mwingi wapo kwenye vibaraza wanapiga story za Yanga na Simba wakichoka wanaazisha story za Manchester na Chelsea.Mwisho wanahamia siasa za CCM na CDM.

2.Vijana wengi wa kata ya kati ni watumiaji wa Mirungi.Mchana wanalala usiku wanaamka na kuanzisha zoezi la kutafuna mirungi.

3.Vijana wengi wa Kata ya Kati wanategemea kodi ya nyumba za urithi.Mfano Ally Kaole Marehemu Baba aliwakuwa diwani wa kata hiyo kwa miaka mingi.Kazi kubwa ilikuwa kuwatoa wauza mirungi na wala mirungi kila wanapokamatwa.

4.Vijana wengi wanategemea mgao wa mauzo ya viwanja na kupelkea kubweteka.
 
Back
Top Bottom