Viongozi na Hotuba zao nane nane 2023

Thegreatcardina

JF-Expert Member
Mar 29, 2009
406
178
1. Naombeni kujuzwa, hivi kwenye Hotuba za viongozi wa nchi hii ni lazima kutaja majina ya wakuu wote waliohudhuria??

2. Hivi Hotuba si zinapaswa kuendana na tukio lililokusanya hadhira? Leo ni sikukuu ya wakulima, why mtu anachukua muda mwingi kuongea yaliyo nje ya sherehe?

3. Na mwisho, hivi mtoa Hotuba hawezi kuwa na mada mbili au tatu hivi akaziongea kwa kina? kuliko ambavyo tunaona watoa Hotuba wanavyoimba maneno mengi na mwisho wa Hotuba hatuelewi alikuwa anafikisha ujumbe upi.

Naombeni mnifunze mnaojua..
 
Lazima unapohutubia ujue unamuhutubia nani yaani hicho ndicho kipaumbele cha kwanza na uwe unamtajataja sana mhudhuriaji mkuu ili kumjengea usikivu yaan muhemiwa 'Rais' ziwe nyingi nyingi hata km hotuba yako Ina maneno 200 basi hakikisha unamtaja mgeni mualikwa Mara 120 ndani ya hotuba
 
Lazima unapohutubia ujue unamuhutubia nani yaani hicho ndicho kipaumbele cha kwanza na uwe unamtajataja sana mhudhuriaji mkuu ili kumjengea usikivu yaan muhemiwa 'Rais' ziwe nyingi nyingi hata km hotuba yako Ina maneno 200 basi hakikisha unamtaja mgeni mualikwa Mara 120 ndani ya hotuba
Hahahahahaha
Hii kali...
Sio hadhara tena ndio walengwa
 
Mlengwa mkuu sio hadhara mlengwa mkuu wa hotuba ni Mgeni Rasmi ndio maana unatakiwa umtaje sana tena na tena na tena shukurani mpe ongeza maombi humo humo mtaje tena na tena na tena ili kumjengea usikivu
Usikivu gani unaomjengea wakati 5 days before "Hotuba" yako muandaa tukio inatakiwa iwe imeshafika mezani kwa mgeni rasmi ili aje na majawabu??!!
 
Anatakiwa awataje yule mtu wa kwanza. Wengine wote wanatakiwa wataje kwa majina au nyadhifa watu watatu hadi watano kisha warifae kama walivyotajwa na mtangulizi.
Mfano fanani anaweza kusema, mh mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, viongozi wa dini na wageni wengine wote mlioalikwa kama ambavyo mlivyo orodheshwa/ tambulishwa na katibu tawala, itifaki imezingatiwa...
Nipende tena kuwashukuru kwa kushiriki nasi katika tukio hili...
 
Back
Top Bottom