Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,458
- 7,837
Dar es Salaam.Viongozi wanne wa CHADEMA wamewasili Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu Dk. Vicenti Mashinji.
Viongozi hao ambao wamewasili Polisi kwa ajili ya kuitikia wito ni pamoja na manaibu katibu John Mnyika na Salum Mwalimu pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti John Heche.
Wakili wao Fredrick Khiwelo amesema wengine wako njiani akiwamo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Aikaeli Mbowe.
Awali Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai kwa Taifa Leo tarehe 22 Machi 2018, ametoa waraka wa kuitwa Polisi yeye na viongozi wenzake.
Katika waraka huo Mbowe amesema kwamba kuna taarifa pia ya kumuunganisha Peter Msigwa, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika shauri hili.
====
UPDATES:
Baadhi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA, wameachiwa na polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar, wametakiwa kuripoti tena Machi 27 kwa mahojiano.
Wakati huo huo viongozi wa chama hicho John Heche na John Mnyika, wanaendelea kushikiliwa kituoni hapo kwa mahojiano.
Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge Halima Mdee na Ester Matiko wa CHADEMA wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
Jeshi la polisi kanda ya maalumu ya Dar es Salaam limewaachia kwa dhamana viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo na kutakiwa kuripoti tena Machi 27 kwa ajili ya kuendelea na mahojiano zaidi.
Habari zaidi....
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa mbili katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kuachiwa, Heche ambaye ni mbunge wa Tarime Vijijini amesema kitendo cha viongozi wa Chadema kuripoti polisi na kukaa kwa saa tano bila kuhojiwa chochote na kutakiwa kuripoti siku nyingine ni sawa na kifungo cha nje.
“Hii ni mara ya tano ninaripoti polisi. Polisi Tanzania ni kama wametuhukumu kifungo cha nje, kila baada ya siku mbili wanataka turipoti kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam bila kujali unaishi wapi, gharama unazotumia kuja na kurudi Dar es Salaam na majukumu yako mengine ya kikazi unayoshindwa kuyatekeleza. Kuna wakati inabidi kukataa uonevu huu,” amesema Heche
Leo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji; naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) pamoja na Heche waliripoti kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano.
Hata hivyo, mbunge huyo wa Tarime Vijijini na Mnyika waliendelea kuhojiwa huku wenzao wakiachiwa kwa dhamana, sababu ya wao kubaki kituoni hapo ikielezwa kuwa ni kitendo chao cha kutoripoti Machi 16, 2018.
Mara baada ya kuachiwa viongozi hao wametakiwa kuripoti tena kituoni hapo Machi 27, 2018.
Heche amesema kitendo wanachofanyiwa si sahihi kwa maelezo kuwa baadhi yao ni wabunge na kwa sasa wanapaswa kushiriki vikao vya kamati za chombo hicho.
“Mimi napaswa kuwa katika vikao vya kamati za Bunge Dodoma. Mbali na hilo nikiwa jimboni kwangu, kutoka huko mpaka Dar es Salaam natumia nauli zaidi ya Sh1milioni. Hivi kwa nini hawalioni hili,” amehoji Heche.
Amesema kwa hali ilivyo ni vyema wakaelezwa hatima yao kwa maelezo kuwa mbali na kupoteza fedha, pia wanashindwa kushiriki shughuli za kibunge.
“Mfano wanataka turejee tena Jumanne ijayo (Machi 27, 2018). Hapa ninaondoka nakwenda Dodoma kushiriki vikao vya kamati, nitalazimika kuondoka jumatatu ili kuwahi. Sasa huu ni usumbufu kwa kweli. Katika hili sitakubali nitafanya kitu,” amesema Heche.
Wakili wa viongozi hao, Frederick kihwelo amesema Mnyika na Heche walizuiwa kuondoka na kutakiwa kuandika maelezo.
"Baada ya kufika, polisi waliwataka Heche na Mnyika ambao hawakufika Machi 16 . Walitaka wabaki baada ya wenzao kuondoka na kuwaagiza kuandika ahadi ya maandishi kuwa Jumanne ijayo watakuwepo,”amesema.