Vinara mgogoro wa gesi watajwa...

Vinara mgogoro wa gesi watajwa...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Jumanne, Februari 05, 2013

Matajiri wakubwa nchini wanaojihusisha na biashara ya mafuta ya petroli, mafuta mazito ya viwandani na kampuni kubwa za kimataifa, ni miongoni mwa wanaochochea mgogoro wa kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam , JAMHURI imethibitishiwa.

Kwenye mgogoro huo, zimo kampuni zinazoingiza nchini gesi ya matumizi ya nyumbani (LPG), pamoja na mataifa makubwa ya Magharibi ambao kwa desturi yamekuwa yakijitahidi kuhakikisha mataifa machanga, ikiwamo Tanzania , yanaendelea kuyanyenyekea kwa misaada.

Pamoja na ukweli huo kujulikana, tatizo jingine kubwa limebainika kuwapo kwa viongozi wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao, ama kwa woga au kwa kutotaka kuwachukiza "wakubwa", wameshindwa kuwapasulia jipu wahusika wakuu kwenye mgogoro huu.
Badala yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Jakaya Kikwete wametajwa kwamba wamekuwa na kauli za kuwalenga wanasiasa wa hapa nchini na viongozi wa kidini kama wachochezi wakuu.Miongoni mwa wanasiasa walio mstari wa mbele kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwa kudai anawatetea wananchi wa Mtwara, ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).

Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki zinasema Serikali inajiandaa kukabiliana na "wakubwa" wanaopinga mradi huo, kwa kuwaandikia barua na wengine kuwaita. Miongoni mwao kuna mabalozi (majina tunayo) ambao wamebainika kuwa nyuma ya mgogoro huo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini pasi na shaka kwamba lipo kundi la wanasiasa linalotumiwa na wafanyabiashara ya mafuta ya petroli na mafuta mazito, ambao wanaamini kuwa mwisho wa biashara yao utatokana na ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara.

Hofu hiyo imewafanya wafanyabiashara hao wahahe huku na kule, lengo likiwa kukwamisha mpango huo ambao kiuchumi unatajwa kama mwarobaini maridhawa.
Habari za uhakika kutoka serikalini zinasema kwamba Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) pamoja na Benki ya Dunia ni miongoni mwa wachochezi wakuu kwenye mgogoro huu. Pamoja nao, ni mataifa ya Magharibi ambayo ndiyo yanayoshikilia na kuongoza taasisi hizo za fedha."Wanahoji iweje mradi huu ujengwe na Tanzania kwa fedha za mkopo kutoka China . Si hivyo tu, wanahoji kwanini usimamizi ufanywe na shirika la umma (Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ).

Walitaka kazi hiyo iangukie kwenye mikataba ya kudumu ya kampuni zao kama walivyofanya kwenye Songas na Pan African," kimesema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimesema hofu nyingine iliyo wazi ni kasi ya ushirikiano wa China na mataifa ya Afrika, hasa Tanzania ; huku mataifa ya Magharibi yakionekana kutopewa kipaumbele katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Wafanyabiashara ya mafuta wahaha
Kundi la wafanyabiashara ya mafuta ya petroli na mafuta mazito ya viwandani, ndilo linaloonekana kuwa kwenye wakati mgumu. Hawa wanashirikiana na kampuni za mafuta za kimataifa ambazo aghalabu huingiza mafuta na kuyauza nchini kupitia ukwepaji kodi.

Kwa upande wa matumizi ya mafuta kwa magari, baada ya ujio wa gesi jijini Dar es Salaam, magari mengi yatatumia nishati hiyo badala ya petroli na dizeli.

"Kwa sasa Serikali inatumia dola za Marekani zaidi ya milioni 200 kuagiza mafuta ya magari kila mwaka. Hizi ni fedha nyingi sana.

Ukisambaza mtandao wa gesi hadi katika magari utaokoa kiasi hiki cha fedha. Ni wazi wafanyabiashara wataathirika, kwa hiyo uamuzi huu wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda katika jiji kubwa lenye viwanda na magari mengi kama Dar es Salaam hawautaki," kimesema chanzo chetu.

Wafanyabiashara hao wanatambua kuwa matumizi ya gesi viwandani yatashusha mapato yao kwa sababu gharama ya matumizi ya gesi ni madogo mno kuliko mafuta.

Mfano halisi ni Kiwanda cha Saruji cha Twiga ambacho baada ya kuanza kutumia gesi, sasa gharama zake za umeme ni Sh bilioni 1.5; ilhali awali wakati wakitumia umeme walikuwa wanalipa Sh bilioni 8 kwa mwezi. Hadi sasa kuna viwanda 37 vinavyotumia gesi Dar es Salaam. Kwa sasa Tanzania inatumia nusu ya mapato yake ya fedha za kigeni kugharimia ununuzi wa mafuta.

Wengine wanaohaha kuhakikisha gesi haifiki Dar es Salaam , ni wafanyabiashara wa gesi ya LPG. Gharama ya mtungi mmoja wa kilogramu 15 inauzwa Sh 54,000 jijini Dar es Salaam.

Mapato ya wenye gesi pamoja na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo yanatarajiwa kushuka hadi robo ya kiasi hicho, yaani mtungi huo huo utauzwa Sh 13,500 kwa ujazo huo endapo gesi itafika Dar es Salaam .

"Wanajua watakosa mapato makubwa, wananchi watapata nafuu kubwa sana . Ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa utapungua sana …Haya mambo wanayajua ndiyo maana hawataki kabisa," kimesema chanzo kingine kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
 
TWIST HIYOOO Nilijua watatenga ISSUE HIYO KUWA ni WESTERN NATIONS AGAINST CHINESE; Muhongo alianza na NILIWEKA HABARI yake IKINUKULIWA na SHIRIKA LA HABARI la CHINA XINHUA...

IT IS A SHAME; BLAME GAME BEGINS...
 
Mh, ngumu kuamini mana siku hizi ni mwendo wa propa
 
Further research deem to be done in order to find the hidden truth because the post seems plausible, does it mean that Pinda and Kikwete do not know that?
 
Wengine wameachwa kwa sababu yumo pia mkuu wa wilaya mtwara ndg. Kapenjama ndile. Naye anahusika na uchochezi huu. Yeye anahusika kupitia tasisi ya kijerumani pamoja na mbunge wa mtwara mjina na wanowania urais 2015: yaani white hair and the co. Ltd
 
Siamini hii habari hata kidogo.. Maana kila nikijaribu kuangalia tatizo la hao wafanyabiashara kama hiyo gesi ikifika dar ni nini sioni.. Huu ni muendelezo wa twists ili kuwachanganya watanzania.. Ninachokiamini mie ni baada wananchi wa mtwara kupata elimu ya uraia wametambua haki zao na namna gani ya kupambana ili nao waweze kunufaika na racilimali inayopatikana kwao.. Kuja na hoja hii ya external force kuchochea ni sawa na kuwadharau wananchi wa Mtwara wote..
 
Jumanne, Februari 05, 2013

Matajiri wakubwa nchini wanaojihusisha na biashara ya mafuta ya petroli, mafuta mazito ya viwandani na kampuni kubwa za kimataifa, ni miongoni mwa wanaochochea mgogoro wa kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam , JAMHURI imethibitishiwa.

Kwenye mgogoro huo, zimo kampuni zinazoingiza nchini gesi ya matumizi ya nyumbani (LPG), pamoja na mataifa makubwa ya Magharibi ambao kwa desturi yamekuwa yakijitahidi kuhakikisha mataifa machanga, ikiwamo Tanzania , yanaendelea kuyanyenyekea kwa misaada.

Pamoja na ukweli huo kujulikana, tatizo jingine kubwa limebainika kuwapo kwa viongozi wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao, ama kwa woga au kwa kutotaka kuwachukiza “wakubwa”, wameshindwa kuwapasulia jipu wahusika wakuu kwenye mgogoro huu.
Badala yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Jakaya Kikwete wametajwa kwamba wamekuwa na kauli za kuwalenga wanasiasa wa hapa nchini na viongozi wa kidini kama wachochezi wakuu.Miongoni mwa wanasiasa walio mstari wa mbele kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwa kudai anawatetea wananchi wa Mtwara, ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).

Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki zinasema Serikali inajiandaa kukabiliana na “wakubwa” wanaopinga mradi huo, kwa kuwaandikia barua na wengine kuwaita. Miongoni mwao kuna mabalozi (majina tunayo) ambao wamebainika kuwa nyuma ya mgogoro huo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini pasi na shaka kwamba lipo kundi la wanasiasa linalotumiwa na wafanyabiashara ya mafuta ya petroli na mafuta mazito, ambao wanaamini kuwa mwisho wa biashara yao utatokana na ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara.

Hofu hiyo imewafanya wafanyabiashara hao wahahe huku na kule, lengo likiwa kukwamisha mpango huo ambao kiuchumi unatajwa kama mwarobaini maridhawa.
Habari za uhakika kutoka serikalini zinasema kwamba Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) pamoja na Benki ya Dunia ni miongoni mwa wachochezi wakuu kwenye mgogoro huu. Pamoja nao, ni mataifa ya Magharibi ambayo ndiyo yanayoshikilia na kuongoza taasisi hizo za fedha.“Wanahoji iweje mradi huu ujengwe na Tanzania kwa fedha za mkopo kutoka China . Si hivyo tu, wanahoji kwanini usimamizi ufanywe na shirika la umma (Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ).

Walitaka kazi hiyo iangukie kwenye mikataba ya kudumu ya kampuni zao kama walivyofanya kwenye Songas na Pan African,” kimesema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimesema hofu nyingine iliyo wazi ni kasi ya ushirikiano wa China na mataifa ya Afrika, hasa Tanzania ; huku mataifa ya Magharibi yakionekana kutopewa kipaumbele katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Wafanyabiashara ya mafuta wahaha
Kundi la wafanyabiashara ya mafuta ya petroli na mafuta mazito ya viwandani, ndilo linaloonekana kuwa kwenye wakati mgumu. Hawa wanashirikiana na kampuni za mafuta za kimataifa ambazo aghalabu huingiza mafuta na kuyauza nchini kupitia ukwepaji kodi.

Kwa upande wa matumizi ya mafuta kwa magari, baada ya ujio wa gesi jijini Dar es Salaam, magari mengi yatatumia nishati hiyo badala ya petroli na dizeli.

“Kwa sasa Serikali inatumia dola za Marekani zaidi ya milioni 200 kuagiza mafuta ya magari kila mwaka. Hizi ni fedha nyingi sana.

Ukisambaza mtandao wa gesi hadi katika magari utaokoa kiasi hiki cha fedha. Ni wazi wafanyabiashara wataathirika, kwa hiyo uamuzi huu wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda katika jiji kubwa lenye viwanda na magari mengi kama Dar es Salaam hawautaki,” kimesema chanzo chetu.

Wafanyabiashara hao wanatambua kuwa matumizi ya gesi viwandani yatashusha mapato yao kwa sababu gharama ya matumizi ya gesi ni madogo mno kuliko mafuta.

Mfano halisi ni Kiwanda cha Saruji cha Twiga ambacho baada ya kuanza kutumia gesi, sasa gharama zake za umeme ni Sh bilioni 1.5; ilhali awali wakati wakitumia umeme walikuwa wanalipa Sh bilioni 8 kwa mwezi. Hadi sasa kuna viwanda 37 vinavyotumia gesi Dar es Salaam. Kwa sasa Tanzania inatumia nusu ya mapato yake ya fedha za kigeni kugharimia ununuzi wa mafuta.

Wengine wanaohaha kuhakikisha gesi haifiki Dar es Salaam , ni wafanyabiashara wa gesi ya LPG. Gharama ya mtungi mmoja wa kilogramu 15 inauzwa Sh 54,000 jijini Dar es Salaam.

Mapato ya wenye gesi pamoja na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo yanatarajiwa kushuka hadi robo ya kiasi hicho, yaani mtungi huo huo utauzwa Sh 13,500 kwa ujazo huo endapo gesi itafika Dar es Salaam .

“Wanajua watakosa mapato makubwa, wananchi watapata nafuu kubwa sana . Ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa utapungua sana …Haya mambo wanayajua ndiyo maana hawataki kabisa,” kimesema chanzo kingine kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Mkuu safi sana ila kwenye list umemsahau yule mbunge muhindi anaitwa Murji
 
gesi ya songosongo iliambata na ongezeko la bei ya gwsi inayotumika majumbani na kauli zao zilikuwa tamu sana,wanadhani sisi ni vilaza kutaminisha kwamba hiyo gesi ya jk na ridhiwan itashusha bei ya gesi ya majumbani..nyambaf zao,gesi haitoki ntwara
 
Siku hizi,gazeti kanjanja,mwandishi kanjanja,inakuwa ngumu wakati mwingine kuamini kile tunacholishwa na waandishi wetu,but soon time will talk.
 
sioni tofauti gesi ikbaki mtwara na ikija dar yote ni Tanzania na mtumiaji ni mtanzania,serikali fanyeni kazi acheni kusaka mchawi.
 
Mh, ngumu kuamini mana siku hizi ni mwendo wa propa

Ni upumbavu wa hali ya juu, wakati unapata tatizo unakimbilia kumtafuta mchawi kwa majirani badala ya kuangalia udhaifu wako na kuchukua hatua stahili.

Kwa mwendo huu wa kukimbilia nje kutafuta wachawi waliotuletea mabaaa, tuna safari ndefu sana kufikia maendeleo ya kweli.

Matatizo yatusaidie kuangalia udhaifu wetu na kurekebisha badala ya kuyakimbia na kuwatafuta wachawi, yamkini wachawi ni sisi wenyewe.
 
Haya mataifa ya magharibi kwa kutumia organs zao IMF & WB na baadhi ya wanasiasa wetu walioandaliwa na CIA kama Economic Hit Men ndiyo yaliyowawekea makuwadi wa CCM mabilioni ya Dola kule USWIS... Ukweli usiopingika ni kuwa CCM walichemsha sana kufungua milango na kuruhusu kutungiwa sera za Madini 1998, Walichemsha zaidi pale ambapo waliruhusu sera ya Ubinafsishaji kufanyika bila ya kufanya utafiti wa kina...Wazungu wamegundua kuwa CCM hawana exposure na niwapenda anasa sana...kama kawaida yao wamecapitalise kwenye weakness ya CCM na sasa wanafanya wanachokitaka...Prof Muhongo, Benno Ndullu et al, Hawa ni EHT waliokubuhu! Ole wetu Watanzania....
 
This is Trash!!! Itafika siku hii serikali watakosa wa kumsingizia watatuambia wamegundua anayefanya wananchi wa Mtwara wagome kumbe ni Shetani! Wameshahishiwa hoja sasa wanatapatapa tu hawa. Na kwa kutaka kuliongozea Uzito hilo, watamchukua Mzee wa Upako (Na full kujipendekeza kwake kwa Magamba) aje eti atushawishi kwamba amepata maono hayo.
 
kwa mini Hoja ya ukweli inapindishwa? hoja ya wanamtwara ni kichakata gesi ghafi mtwara ili wapate maendelleo kutokana na viwanda muambata vitakavyojengwa!!! Japo huwezi kutenga hoja ya kukopwa korosho na barabara zilizosahaulika na uduni wa maendeleo ya kanda hiyo. kwa hiyo Hata kama gesi safi yote ikibidi iende Dar kama hiyo ndio shida iende tu. Hata rais kakubali kuwa hii ndio ilikuwa plan ila haikuelezwa fasaha na watendaji. so why keep twisting the truth. utekelezaji uanze hakuna mchawi.
wanamtwara wanahitaji Maendeleo yaliyochelewa kwa njia nyingine kwa kutumia hiki kutoka kwao, wasikilizeni na muwaelewe .....
 
Makala ya kipuuzi ambayo imeandaliwa na mtu mjinga kutetea watawala wala rushwa kwa kuonyesha eti wananchi wa Mtwara walikua hawajui wanapigania kitu gani. Ni makala ya inayowadhalilisha wananchi wa Mtwara.
 
Mkuu safi sana ila kwenye list umemsahau yule mbunge muhindi anaitwa Murji

Magamba kwa kushabikia U-FIRAUNI,hata mpindue maneno vipi....! sakata la MTWARA lita watafuna tu,nyie MAFISADI wa chama cha magamba ndio mpo mstali wa mbele kuiba mali za umma na kuwajengea mazingira ya UMASIKINI.
 
TWIST HIYOOO Nilijua watatenga ISSUE HIYO KUWA ni WESTERN NATIONS AGAINST CHINESE; Muhongo alianza na NILIWEKA HABARI yake IKINUKULIWA na SHIRIKA LA HABARI la CHINA XINHUA...

IT IS A SHAME; BLAME GAME BEGINS...

Umeona eeh...mie mwenyewe I shitukad.
 
Back
Top Bottom