Vinara mgogoro wa gesi watajwa...

Vinara mgogoro wa gesi watajwa...

Majina yao
makampuni ya mafuta
mafisadi wanaotaka urais 2015 wakiongozwa na whaite hair
mh. Murji mbunge
mh. Kapenjala ndile dc mtwara
mh.njwayo mbunge tandahimba kwa kutowajibika.
Lengo kumharibia rais wa jamhuri
 
Siku hizi,gazeti kanjanja,mwandishi kanjanja,inakuwa ngumu wakati mwingine kuamini kile tunacholishwa na waandishi wetu,but soon time will talk.
Mkuu, hapo ndio utaona utofauti wa gazeti la MwanaHalisi na haya ya udaku!! Eti "Vinara watajwa," ukisoma ...Majina tunayo..

Makanjanja tupu!
 
Wakishamaliza kutafuta mchawi halafu hawampati inaishiaje?
 
WATANZANIA IZO NI MBUNU ZA WENZETU ASIKUDANGANYE MTU.
Ndugu zangu watanzania wenzangu, kwanza natanguliza shukrani zangu za thati zenye majinzi na masikitiko kwa watanzania wote kwa ujumla kama hatutajitambua kutokana na matukio mbali mbali. Dhumuni lagu ni kuongelea mtizamo na mikakati yetu watanzania kujitambua kuwa kweli sisi ni watanzania araliya katika nchi hii na kutoa mshikamano katika maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla kwa kuinua uchumi wa nchi yetu. Pia ikumbukwe kwamba hatuwezi kuendelea kutokana na mambo yafuatayo kama hatutakuwa tayari kuyatambua haya yafuatayo, kujitambua kifikra/kimawazo, kisiasa na kiuchumi. Pia kwa kujua tunatoka wapi, tuko wapi, na tunaelekea wapi?

Ndugu zangu ninapoongelea kifikra/kimawazo nina maana ya ali ya utambuzi wa kujitambua na kuelewa tunakotoka, tulipo na tunako elekea. Ili ni jambo la msingi sana kwetu watanzania wapenda amani, na maendeleo kwania ya kuimalisha na kujenga uchumi imala katika nchi yetu. Suala la kisiasa, siasa ni jambo jema na la msingi sana likitumika vizuri katika sakata la kujenga na kuinua uchumi wan chi yetu. Maana siasa uchokonoa yaliyo fichika nyuma ya pazia na kuyaonesha wazi. Pia siasa ni jambo ambalo linaweza kusababisha machafuko ya nchi pale ambapo itatumika vibaya kutokana na watu wasiopenda maendeleo ya nchi yao bali kujinufaisha wao wenyewe na familia zao. Suala la uchumi, Ndugu zangu tunapo ongelea suala la uchumi inamaana kwamba kila mtanzania awe na uchu wa kutaka kuinua uchumi wa nchi. Pia kila mtanzania awe mwangalizi na msimamizi katika rasilimali za nchi kwa kikatiba na kanuni kwa nia ya kuinua na kujenga uchumi wa nchi yetu kwa ujumla. Watanzania ikumbukwe kuwa sisi ni wamoja na taifa moja. Pale tatizo litakapo jitokeza tuwe tayari kuangalia na kugundua au kuangalia chanzo cha tatizo ni nini? pia tuwe wamoja katika kutatua tatizo ilo bila wonga wala upendeleo wa aina yoyote ile kwa maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla. Watanzania nina imani kuwa kila mmoja wetu anajua kuwa nchi yetu Tanzania ina mikoa mingi, tunapoongelea maendeleo na usimamizi wa rasilimali za nchi yetu inamaana ya Wilaya pamoja na mikoa yote iliyomo ndani ya nchi yetu. Katika sakata la gesi kusafirishwa kutoka Mtwara adi Dar es Salaam. Mimi binafsi siungi mkono ingawa waziri mkuu alielezea sababu za kusafirisha gesi adi Dar. Katika sababu alizoziongelea hazina ushawishi wa kulidhisha ili nikubali au tukubaliane nae kuwa gesi isafirishwe kuwenda Dar es Salaam. Tatizo eti Dar es Salaam haina umeme wa kutosha, kwangu mimi haijaniingia akilini inamaana kama Dar es Salaam haina umeme wa kutosha ipelekee kusafilishwa gesi mpaka Dar es Salaam? Kwanini tusizalishe umeme kutoka Mtwara mpaka Dar? Kila mtanzania ajiulize je gesi ingepatikana Marawi kwavile Dar es Salaam haina umeme wakutosha wange safirisha gesi kutoka Marawi ili Umeme uzalishwe Dar? Au Dar ingekaa gizani kwavile hawana umeme wa kutosha na gesi imepatikana Marawi? Kama kutakuwepo uwezekano wa kupata umeme kutoka Marawi yani nche ya nchi, sasa inashindikanaje umeme kuzalishwa Mtwara? Ili ndilo linatupa uelewa wa kujua na kutambua kuwa serikali yetu iko mifukoni mwa watu wachache ambao wanadiriki kumwaga damu kwa njia yeyote ile kwa manufaa yao binafsi na si kwataifa letu. Au Dar es Salaam ni sehemu ambayo ni maalumu kwa kuendesha miundombinu tofauti na sehemu nyingine za Tanzania? Watanzania wenzangu je! Hatuoni kuwa hapa kuna kitu cha ujuma? Watanzania tuwe macho hapa inapoonekana mpaka serikali inaamua kumwaga damu kwa mambo ya siyo ya msingi, maana kama kuna kitu ambacho kinaweza kufanyika Dar es Salaam alfu kisifanyike sehemu yoyote ya Tanzania tofauti na Dar? Ndugu zangu hapa kuna kitu tukubali tukatae kuna kitu ndani yake, Tanzania ni moja pamoja na wilaya zake na mikoa yote inayo izunguka nchi yetu. Watanzania tuwe na mshikamano wa pamoja kwa kutosapoti serikali katika sakata la usafirishaji wa gesi kutoka Mtwara, maana Mtwara bado ni sehemu ya nchi yetu, kinacho wezekana kuzalisha umeme Dar es Salaam pia inawezekana kuzalishwa Mtwara na kugawia sehemu zenye maitaji ya umeme ndani ya nchi yetu. Pia ikumbukwe kwamba nchi yeyote haiwezi kuendelea bila kuwa na viwanda, lakini sikitiko langu ni juu ya serikali yetu ya chama cha mapinduzi (CCM) ninashidwa kuelewa. Hivi viongozi tulionao kweli wana uwezogani wa kufikiria na mbinu gani za kuendeleza taifa letu la Tanzania? Watanzania tunajua ya kuwa nchi yetu ina madini madini ya Gold, tanzanite na nk. lakini lakushangaza na kusikitisha hatuna makampuni ya tanzanite hapa Tanzania wala hatujulikani kimataifa katika uzalishaji wa madini ya tanzanite. Sasa hivi Makaburu ndio wanao julikana kuwa wazalishaji wakubwa wa tanzanite Africa ya kusini wakati inapatikana hapa nchini. Hapa ukiongelea utaambiwa kuwa wawekezaji ni Makaburu, swali je katika uwekezaji hatuna makubaliano ya mikataba katika madini? Na kama hipo je iyo mukataba ambayo haina kichwa wala miguu ilitungwa na nani? Na nini maana ya mikataba? Pia nijambo la kushangaza kwa nchi yetu hii na watawala wake, maana kwa viongizi/watawala inakuwaje kama kuna mikataba iliyopo inavyunjwa na wawekezaji wao wanakaa kimya? Kuna wawekezaji wa madini wanabeba madini na udongo wake unasafirishwa je! serikali iko wapi au mikataba yao ndivyo inavyo ruhusu? Mambo yote yanafanyika kwa sababu ya serikali na watawala/viongozi wake kuelewa ujinga wa watanzania kutojielewa wala kujitambua kimawazo/kifikra, kimtazamo, kisiasa na kiuchumi. Ndugu zangu watanzania ninaamini kuwa watanzania wa juzi si waleo uelewa tunao, sasa ni wakati wetu wa kupigania haki na kusimamia mali za taifa letu kwa masilai ya wanachi kwa ujumla. Najua tukiwa na mshikamano wa pamoja na kupigia kelele shwala ili kitaeleweka na haki itatendeka daima na amani itatawala. Suala la mabadiliko, watanzania tunapo ongelea suala la mabadiliko, Kwanza tubadilike sisi wenyewe tuwe na nia thabiti ya upendo na utashi wa mabadiriko tusiwategemee watu ambao hawataki mabadiliko tuwabadirishe sisi wenyewe. Hapo ndipo tutakuwa na mabadiliko ya kweli pia ndipo tutakapo wapata viongozi waadilifu wenye nia malengo na makusudi ya kuinua uchumi wa nchi yetu kwa masilai ya wananchi kwa ujumla. Watanzania ikumbukwe kuwa bila kuiondoa CCM madarakani tusitegemee maendeleo ya aina yoyote ile katika nchi hii. Kwa sababu adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu ni CCM na serikali yake. Jambo la kushangaza na bila woga wowote utashangaa watawala/viongozi wa CCM wanapoingia majukwaani bado wanatoa ahadi zao zisizo na misingi wala mishiko kwa wananchi, sababu mtu hajatimiza ahadi alizoziahidi tangu CCM kuingia kwenye uongozi hadi leo bado ni ahadi tupu, watwambie ahadi zao zitakamilika lini hatutaki ahadi zao tena kwanza wakamilishe walizoziahidi. Kwaiyo wanapo ingia majukwaani tunataka watwambie zitakamilika lini sio ahadi tena sisi si watoto wa kudanganywa. Watanzania tuwe makini kwa hawa watu wa CCM. Lakini suruhisho la haya yote ni mabadiliko ya kuiondoa CCM madarakani tu.
Remember that “when a man going down the hill every one will give him a push”
 
Tatizo si kwamba gasi isifike Dar. Ila tunataka kiwanda kijengwe Mtwara na gasi isafirishwe kwenda sehemu nyinhine r:
 
Watajenga mabomba mangapi ya gesi kutoka kusini kuja Dar? kila kampuni ikichimba gesi wanasafirisha kuja Dar walianza songas sasa hao wa mtwara nao wanajenga bomba kuja Dar huko ardhini kutakua na mabomba mangap? Hizi ndio story za mazao wakulima wakivuna wanaleta mjini baadae wanakumbwa na njaa wanaanza kuomba misaada!
 
Wataje kwa majina na makampuni yao wala usiogope..hapa ni JF we dare to talk. Unapoteza maana ya post yako bila kuwataja hao.
 
Ina maana mi ndiye zuzu sielewi?kwani hiyo gesi ikifanyiwa kila kitu Dar haitouzwa? na matumizi ya gesi katika magari nifahamishwe vizuri huo mfumo wake!hivyo viwanda na umeme...-inamaana gesi ikiwa mtwara ndio watakuwa hawaipati?msinizodoe nifahamisheni mie zuzu!
 
Kwendeni zenu. Tafuten mwingine wa kumpiga porojo hizi.
Na mue makini mataifa ya magharibi mnayo yasingizia yakianza uchunguzi wa kujiepusha na mizigo isio yao mtavuka misuli hadharani.
 
----!

Hapa serikali inataka kuingiza propaganda kukwepa kujibu maswali ya msingi ya wana Mtwara na watanzania kwa ujumla.

Sijasikia mahali popote wakieleza kuwa gesi hii ikitumika kufua umeme huko mtwara (badala ya Kinyerezi) na kuusafirisha kuja Dar kutakuwa na hasara gani kwa taifa, au lile swali kwamba kwa nini serikali ina ng'ang'ania mradi wa bandari Bagamoyo badala ya kuboresha miundombinu kwenye bandari ya Mtwara na kusaidia usafirishaji wa mizigo ya nchi jirani kama Malawi, Zambia, DRC, na Msumbiji! Kwa nini Bagamoyo na si Tanga au Mtwara????
 
uchochezi,madai ya kunufaika na rasilimali yao?

wamechafuka, na kutafuta wa kumtupia lawama watanuka

serikali ya ajabu hii
 
TWIST HIYOOO Nilijua watatenga ISSUE HIYO KUWA ni WESTERN NATIONS AGAINST CHINESE; Muhongo alianza na NILIWEKA HABARI yake IKINUKULIWA na SHIRIKA LA HABARI la CHINA XINHUA...

IT IS A SHAME; BLAME GAME BEGINS...

Nilikuwa namheshimu sana huyo Prof. Mhongo lakini amenisikitisha sana..Nimeona kwenye one of the networks akizungusha scholarship za kwenda kusoma China sikumbuki kwingine huku akihimiza elimu tu ndiyo itakayo wakomboa watanzania that looks fine lakini reading between the lines unagundua intents zake kwani akaweka statement kuwa bila direct quotation, .........tuwapinge wanaotaka kutugawa kwa sera za majimbo na maendeleo.

How can a person like him kuwa na such cheap arguments za kuwa entice vijana wa Tanzania kwa nafasi za kusoma huku aki attach kiakili statements ambazo zita create biasness katika judgement zao kwa mambo muhimu ya kitaifa? He has to stop this, nchi yetu haitaweza kuendelea bila rushwa hizi za cheap promisses kukomeshwa. Watu wajifunze kuwa objective na kuacha tabia za ku attach vitu ama favours ku influence innovations na critical discussions za kitaifa ambazo zitasaidia kila mtu na siyo individual interest kama zake. I was real provoked by his attitude na kwasababu hiyo na doubt credibility yake kama msomi na mtu ambaye amekuwa exposed to the world. He could do better than this!
 
Mwandishi ametoa mambo ya kufikirika ambayo ni ya ukweli lakini si halisi kwa suala hili. Mosi, umeme unaweza kuzalishwa Mtwara bila kusafirishwa hadi Dar na umeme ukaungwa kwenye gridi ya taifa. Kwa hiyo sioni uhusiano na hofu ya wafayabiashara wa mafuta mazito yanayotumika kwa kazi hiyo kwani umeme ukizalishwa Mtwara au Dar tutaachana nayo! Pili matumizi ya gasi kwenye magari bado ni nadharia. Huwezi kubadilisha gari kutumia gesi wakati mtandao wa gesi yenyewe ni finyo katika maeneo na pengine vituo vichache tu. Tatu mikataba ya songas na Pan Africa ni ujinga wetu na hata tuyliposhautiwa kuwa tunaibiwa hakuna tulivjokifaya, tunawachekea tu. Msiwafanye watanzania kwamba hawawezo kufikiria wao mpaka watumiwe na watu wengine wenye maslahi Yao! Leo iweje kuwa haya hayajajirudia na Wachina? Pengine ukweli mdogo katika makala hii ni vita vya kibiashara Kati ya magharibi na Wachina.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Eti gesi ya kupikia ikifika dar itauzwa Tsh 13.000 badala ya sh54.000. Magamba kweli mzidi uongo ,mbona hicho kiwanda cha cement hakija shusha bei ya cement pamoja na kutumia gas ya songa' s
 
Jumanne, Februari 05, 2013

Matajiri wakubwa nchini wanaojihusisha na biashara ya mafuta ya petroli, mafuta mazito ya viwandani na kampuni kubwa za kimataifa, ni miongoni mwa wanaochochea mgogoro wa kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam , JAMHURI imethibitishiwa.

Kwenye mgogoro huo, zimo kampuni zinazoingiza nchini gesi ya matumizi ya nyumbani (LPG), pamoja na mataifa makubwa ya Magharibi ambao kwa desturi yamekuwa yakijitahidi kuhakikisha mataifa machanga, ikiwamo Tanzania , yanaendelea kuyanyenyekea kwa misaada.

Pamoja na ukweli huo kujulikana, tatizo jingine kubwa limebainika kuwapo kwa viongozi wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao, ama kwa woga au kwa kutotaka kuwachukiza “wakubwa”, wameshindwa kuwapasulia jipu wahusika wakuu kwenye mgogoro huu.
Badala yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Jakaya Kikwete wametajwa kwamba wamekuwa na kauli za kuwalenga wanasiasa wa hapa nchini na viongozi wa kidini kama wachochezi wakuu.Miongoni mwa wanasiasa walio mstari wa mbele kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwa kudai anawatetea wananchi wa Mtwara, ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).

Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki zinasema Serikali inajiandaa kukabiliana na “wakubwa” wanaopinga mradi huo, kwa kuwaandikia barua na wengine kuwaita. Miongoni mwao kuna mabalozi (majina tunayo) ambao wamebainika kuwa nyuma ya mgogoro huo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini pasi na shaka kwamba lipo kundi la wanasiasa linalotumiwa na wafanyabiashara ya mafuta ya petroli na mafuta mazito, ambao wanaamini kuwa mwisho wa biashara yao utatokana na ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara.

Hofu hiyo imewafanya wafanyabiashara hao wahahe huku na kule, lengo likiwa kukwamisha mpango huo ambao kiuchumi unatajwa kama mwarobaini maridhawa.
Habari za uhakika kutoka serikalini zinasema kwamba Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) pamoja na Benki ya Dunia ni miongoni mwa wachochezi wakuu kwenye mgogoro huu. Pamoja nao, ni mataifa ya Magharibi ambayo ndiyo yanayoshikilia na kuongoza taasisi hizo za fedha.“Wanahoji iweje mradi huu ujengwe na Tanzania kwa fedha za mkopo kutoka China . Si hivyo tu, wanahoji kwanini usimamizi ufanywe na shirika la umma (Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ).

Walitaka kazi hiyo iangukie kwenye mikataba ya kudumu ya kampuni zao kama walivyofanya kwenye Songas na Pan African,” kimesema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimesema hofu nyingine iliyo wazi ni kasi ya ushirikiano wa China na mataifa ya Afrika, hasa Tanzania ; huku mataifa ya Magharibi yakionekana kutopewa kipaumbele katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Wafanyabiashara ya mafuta wahaha
Kundi la wafanyabiashara ya mafuta ya petroli na mafuta mazito ya viwandani, ndilo linaloonekana kuwa kwenye wakati mgumu. Hawa wanashirikiana na kampuni za mafuta za kimataifa ambazo aghalabu huingiza mafuta na kuyauza nchini kupitia ukwepaji kodi.

Kwa upande wa matumizi ya mafuta kwa magari, baada ya ujio wa gesi jijini Dar es Salaam, magari mengi yatatumia nishati hiyo badala ya petroli na dizeli.

“Kwa sasa Serikali inatumia dola za Marekani zaidi ya milioni 200 kuagiza mafuta ya magari kila mwaka. Hizi ni fedha nyingi sana.

Ukisambaza mtandao wa gesi hadi katika magari utaokoa kiasi hiki cha fedha. Ni wazi wafanyabiashara wataathirika, kwa hiyo uamuzi huu wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda katika jiji kubwa lenye viwanda na magari mengi kama Dar es Salaam hawautaki,” kimesema chanzo chetu.

Wafanyabiashara hao wanatambua kuwa matumizi ya gesi viwandani yatashusha mapato yao kwa sababu gharama ya matumizi ya gesi ni madogo mno kuliko mafuta.

Mfano halisi ni Kiwanda cha Saruji cha Twiga ambacho baada ya kuanza kutumia gesi, sasa gharama zake za umeme ni Sh bilioni 1.5; ilhali awali wakati wakitumia umeme walikuwa wanalipa Sh bilioni 8 kwa mwezi. Hadi sasa kuna viwanda 37 vinavyotumia gesi Dar es Salaam. Kwa sasa Tanzania inatumia nusu ya mapato yake ya fedha za kigeni kugharimia ununuzi wa mafuta.

Wengine wanaohaha kuhakikisha gesi haifiki Dar es Salaam , ni wafanyabiashara wa gesi ya LPG. Gharama ya mtungi mmoja wa kilogramu 15 inauzwa Sh 54,000 jijini Dar es Salaam.

Mapato ya wenye gesi pamoja na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo yanatarajiwa kushuka hadi robo ya kiasi hicho, yaani mtungi huo huo utauzwa Sh 13,500 kwa ujazo huo endapo gesi itafika Dar es Salaam .

“Wanajua watakosa mapato makubwa, wananchi watapata nafuu kubwa sana . Ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa utapungua sana …Haya mambo wanayajua ndiyo maana hawataki kabisa,” kimesema chanzo kingine kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
hzo no propaganda haswaaaaaaa kinachozuiliwa cyo uchimbaji wa gesi bali ni usafirishaji wa gesi kwahyo ukiniambia external influence znatumika kwa wanamtwara kutaka wadai processing plants zjengwe kwao na huku dar ije finished products basi washukuriwe maana nia syo kupinga uzalishwaj wa gesi Tanzania bali wanawatakia mema wnamtwara mimi naamini kuna kubwa lililonyuma ya mambo haya tusiwadanganye wa Tanzania kwa propaganda znazojionyesha kabisa kwa hili hakuna cha kuficha wanamtwara sasa wameamua kujitafutia maendeleo kwanguvu zao wenyewe maana baada ya bandari kutowanufaisha ajali ya maendeleo iliyojitokeza ni gesi mungu awape nini? huu ndo muda wa kujikwamua kimaendeleo go go go,,,,,wanamtwara suluhisho nisera za majimbo ilimjiamulie na kuwa wanufaikaji wa kwanza katika hiki.
 
Hii ni propaganda kutoka ikulu, imeletwa humu jf ili watu waisapoti mbona wewe mleta mada hatujaliskia hili kwenye media yoyote hapa nchini?
Munaogopa nini jitokezeni muwalaani ha wazungu basi musituletee sisi utumbo wenu huu mukatafuta sapot hapa jf. Iweje?
 
Jumanne, Februari 05, 2013

Matajiri wakubwa nchini wanaojihusisha na biashara ya mafuta ya petroli, mafuta mazito ya viwandani na kampuni kubwa za kimataifa, ni miongoni mwa wanaochochea mgogoro wa kupinga ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam , JAMHURI imethibitishiwa.

Kwenye mgogoro huo, zimo kampuni zinazoingiza nchini gesi ya matumizi ya nyumbani (LPG), pamoja na mataifa makubwa ya Magharibi ambao kwa desturi yamekuwa yakijitahidi kuhakikisha mataifa machanga, ikiwamo Tanzania , yanaendelea kuyanyenyekea kwa misaada.

Pamoja na ukweli huo kujulikana, tatizo jingine kubwa limebainika kuwapo kwa viongozi wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao, ama kwa woga au kwa kutotaka kuwachukiza “wakubwa”, wameshindwa kuwapasulia jipu wahusika wakuu kwenye mgogoro huu.
Badala yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Jakaya Kikwete wametajwa kwamba wamekuwa na kauli za kuwalenga wanasiasa wa hapa nchini na viongozi wa kidini kama wachochezi wakuu.Miongoni mwa wanasiasa walio mstari wa mbele kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwa kudai anawatetea wananchi wa Mtwara, ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).

Habari zilizopatikana mwishoni mwa wiki zinasema Serikali inajiandaa kukabiliana na “wakubwa” wanaopinga mradi huo, kwa kuwaandikia barua na wengine kuwaita. Miongoni mwao kuna mabalozi (majina tunayo) ambao wamebainika kuwa nyuma ya mgogoro huo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini pasi na shaka kwamba lipo kundi la wanasiasa linalotumiwa na wafanyabiashara ya mafuta ya petroli na mafuta mazito, ambao wanaamini kuwa mwisho wa biashara yao utatokana na ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara.

Hofu hiyo imewafanya wafanyabiashara hao wahahe huku na kule, lengo likiwa kukwamisha mpango huo ambao kiuchumi unatajwa kama mwarobaini maridhawa.
Habari za uhakika kutoka serikalini zinasema kwamba Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) pamoja na Benki ya Dunia ni miongoni mwa wachochezi wakuu kwenye mgogoro huu. Pamoja nao, ni mataifa ya Magharibi ambayo ndiyo yanayoshikilia na kuongoza taasisi hizo za fedha.“Wanahoji iweje mradi huu ujengwe na Tanzania kwa fedha za mkopo kutoka China . Si hivyo tu, wanahoji kwanini usimamizi ufanywe na shirika la umma (Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ).

Walitaka kazi hiyo iangukie kwenye mikataba ya kudumu ya kampuni zao kama walivyofanya kwenye Songas na Pan African,” kimesema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimesema hofu nyingine iliyo wazi ni kasi ya ushirikiano wa China na mataifa ya Afrika, hasa Tanzania ; huku mataifa ya Magharibi yakionekana kutopewa kipaumbele katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Wafanyabiashara ya mafuta wahaha
Kundi la wafanyabiashara ya mafuta ya petroli na mafuta mazito ya viwandani, ndilo linaloonekana kuwa kwenye wakati mgumu. Hawa wanashirikiana na kampuni za mafuta za kimataifa ambazo aghalabu huingiza mafuta na kuyauza nchini kupitia ukwepaji kodi.

Kwa upande wa matumizi ya mafuta kwa magari, baada ya ujio wa gesi jijini Dar es Salaam, magari mengi yatatumia nishati hiyo badala ya petroli na dizeli.

“Kwa sasa Serikali inatumia dola za Marekani zaidi ya milioni 200 kuagiza mafuta ya magari kila mwaka. Hizi ni fedha nyingi sana.

Ukisambaza mtandao wa gesi hadi katika magari utaokoa kiasi hiki cha fedha. Ni wazi wafanyabiashara wataathirika, kwa hiyo uamuzi huu wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda katika jiji kubwa lenye viwanda na magari mengi kama Dar es Salaam hawautaki,” kimesema chanzo chetu.

Wafanyabiashara hao wanatambua kuwa matumizi ya gesi viwandani yatashusha mapato yao kwa sababu gharama ya matumizi ya gesi ni madogo mno kuliko mafuta.

Mfano halisi ni Kiwanda cha Saruji cha Twiga ambacho baada ya kuanza kutumia gesi, sasa gharama zake za umeme ni Sh bilioni 1.5; ilhali awali wakati wakitumia umeme walikuwa wanalipa Sh bilioni 8 kwa mwezi. Hadi sasa kuna viwanda 37 vinavyotumia gesi Dar es Salaam. Kwa sasa Tanzania inatumia nusu ya mapato yake ya fedha za kigeni kugharimia ununuzi wa mafuta.

Wengine wanaohaha kuhakikisha gesi haifiki Dar es Salaam , ni wafanyabiashara wa gesi ya LPG. Gharama ya mtungi mmoja wa kilogramu 15 inauzwa Sh 54,000 jijini Dar es Salaam.

Mapato ya wenye gesi pamoja na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo yanatarajiwa kushuka hadi robo ya kiasi hicho, yaani mtungi huo huo utauzwa Sh 13,500 kwa ujazo huo endapo gesi itafika Dar es Salaam .

“Wanajua watakosa mapato makubwa, wananchi watapata nafuu kubwa sana . Ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa utapungua sana …Haya mambo wanayajua ndiyo maana hawataki kabisa,” kimesema chanzo kingine kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Propoganda hizo ili huruma itumike gas ije dar,hata wakati wa uzinduzi wa matumizi ya gas kiwandani wazo rais alidanganywa kuwa bei ya cement itashuka sana lakini cha ajabu ikatoka sh 6500 mpaka leo ni 15000,inapunguzwa bei kwa sasa kwa sababu ya cement ya nje toka pakistani ambayo ni imara sana kwa tofali na bei ipo sh 14000.Wao wameshavuta zao zipo uswisi wewe wanakudanganya uwaoe support!!!tunataka maendeleo kwanza mtwara lindi
 
Kwani Mitungi ya Gesi Haiwezi kusafirishwa tokea mtwara hadi bomba lijengwe/? tusidanganyane waachie gesi yao harafu muinunue tokea mtwara viwanda vijengwe mtwara wawekezaji wawekeze mtwara maendeleo yasambae nchi nzima si DAR tu.
 
Back
Top Bottom