Wana Jamii
Member
- Sep 10, 2020
- 16
- 3
Mhe. Mkuu wa Mkoa - Arusha,
Sisi wafanyakazi wa Mount Meru Hotel, tunaleta malalamiko yetu kwa ujumla kutokana na adha tunayoipata kutoka kwa mwajiri wetu.
Adha hii tunayoipata ilianza mnamo mwezi wa Aprili 2, 2020 pale tulipolazimishwa wafanyakazi 163 kuchukuwa likizo isiyo na malipo kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Uamuzi huu haukuwa umewashirikisha wafanya kazi wenyewe bali yalikuwa ni maagizo ya uongozi wa hoteli ikiwa ni pamoja na kulazimishwa kusaini barua.
Kutokana na hatua hii, wafanyakazi tulilazimika kuondoka na kurejea majumbani kwetu tukiwa hatujui nini hatma mstakabali wetu kutokana na barua hiyo kueleza kuwa wafanyakazi watatakiwa kurejea kazini kuanzaia Julai 1, 2020.
Mnamo mwishoni mwa mwezi wa tano ikiwa ni miezi miwili tangu tuanze kutumikia likizo isiyo na malipo, tulipokea wito wa kikao kilichofanyika mnamo tarehe 26 Mei 2020. Wafanyakazi tulifika katika kikao hicho kilichokuwa kikiongozwa na Mkurugenzi mwenyewe.
Baada ya majadiliano ya muda mrefu, Mkurugenzi aliagiza tume ya wafanyakazi ikae na uongozi wa hoteli ili kupata mapendekezo ya wafanyakazi.
Baada ya kamati teule kukaa, mnamo tarehe 9 Juni 2020 kulikuwa na kikao na mkurugenzi ili kupata mrejesho wa mapendekezo ya kamati. Maamuzi yalikuwa kama ifuatavyo:-
Miezi mitatu baada ya maamuzi ya tarehe 9 Juni 2020, wafanyakazi tulipokea wito wa kikao ambacho kilifanyika mnamo tarehe 29 Agosti 2020. Wafanyakazi tuliitikia wito huo. Katika kikao hiki maamuzi yalikuwa kama ifuatavyo:-
Hali ya kibiashara inazidi kutengemaa siku hadi siku hasa ukizingatia kipindi hiki cha miezi mitatu iliyopita ( Juni – Agosti)
Sisi wafanyakazi wa Mount Meru Hotel tunaomba msaada wako hasa tukizingatia kuwa serikali yetu imekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi yetu sisi wananchi wa hali ya chini.
Mwisho kabisa tukutakie utendaji kazi wako mzuri na tunategemea utalitatua suala hili.
Wako,
Wafanyakazi wa Mount Meru Hotel.

- Kwa kuwa maamuzi ya awali yalionekana ni batili, mkurugenzi aliazimia kuwalipa fedha taslim shilingi Laki tano (500,000) kila mmoja kwa wafanyakazi wote waliokuwa likizo pasipo malipo kwa mwezi Aprili na Mei. Malipo haya yalifanyika siku hiyo hiyo na wafanyakazi tulipewa pesa taslim mkononi.
- Malipo ya asilimia 50% kwa wafanyakazi wa ngazi ya chini, asilimia 40% kwa wafanyakazi wa ngazi ya kati, asilimia 30% kwa wafanyakazi wa ngazi ya juu na kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) kwa wafanyakazi wote watakao kuwa nyumbani kwa miezi mitatu yaani Juni, Julai na Agosti.
Miezi mitatu baada ya maamuzi ya tarehe 9 Juni 2020, wafanyakazi tulipokea wito wa kikao ambacho kilifanyika mnamo tarehe 29 Agosti 2020. Wafanyakazi tuliitikia wito huo. Katika kikao hiki maamuzi yalikuwa kama ifuatavyo:-
- Mzunguko wa wafanyakazi kuingia kazini kila mwezi kuanzia Septemba 2020 hadi Aprili 2021 kuruhusu kila mfanyakazi kupata nafasi ya kupata angalau kipato kidogo kwa asilimia kama ifuatavyo:
- Asilimia 50% kwa wafanyakazi wenye mshahara wa ngazi ya chini
- Asilimia 40% kwa wafanyakazi wenye mshahara wa ngazi ya kati na
- Asilimia 30% kwa wafanyakazi wenye mshahara wa ngazi ya juu
- Wafanyakazi watakaokuwa kwenye mzunguko wa kuwa nyumbani hawatalipwa mshahara bali kampuni itawachangia kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kwa ajili ya kujikimu kuanzia mwezi septemba 2020 hadi Aprili 2021. Kiwango hiki kitaambatana na mchango wa asilimia 20% itakayo kwenda kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF). Kiwango hiki cha asilimia 20% kitatokana na makato ya asilimia 10% kutoka kwa mwajiri na asilimia nyingine 10% ni mchango kutoka kwa mwajiri kwenda kwa mwajiriwa. Hivyo Mfanyakazi atapata shs. 90,000?=