Vilio vya wafanyakazi wa Mount Meru Hotel - Arusha

Yaonekana huijui Biashara ya Hoteli ndio maana unaona Mwajiri wao amejitahidi sana kuwalipa. Labda useme amejitahidi ukimlinganisha na mwajiri mwengine lakini hakuna uungwana wowote.

Waambie waoneshe their financial statements hadharani mujionee ni kiasi gani wanaingiza kwa Mwezi tu mjionee. Unafikiri hoteli yenye gharama ya milioni 100 kwenye mshahara wa wafanyakazi wao wanaingiza kiasi gani kwa mwezi?.

Hio Milioni 100 kwa mwaka net profit nimekutolea mfano tena ni wa hoteli mbuzi tu ata 3 star haifiki vizuri!

Halafu kitu kingine utambue kuwe, katika mwaka kuna kuwa na low season, kipindi ichi hoteli inaweza ikafungwa kabisa, maana yake ata mia haingizi na siku ya kufungua basi wanatumia gharama nyingi katika ufunguzi au huwa wanafanya renovation miezi miwili hadi mitatu, na huwa wanalipa wafanyakazi hela ya likizo full kipindi chote ambacho hawapo kazini.

Sasa swali langu, kwanini wameshindwa kuwalipa hela ya likizo full mara hii na kusingizia corona wakati miaka ya nyuma wakifunga hoteli wanalipa watu?
Milioni 100 mbona hiyo ni hotel ya zero star kaka. Unajua tunazungumza hapa tukiwa na facts nyingi tu.
 
Hakika mwajiri huyu ni muungwana sana! ila mleta mada hakuwa muungwana kuleta mada hii angefaa kumshukuru sana mwajiri wake.
 
Tatizo lako unalinganisha kati ya mjsi na mamba. Huwezi linganisha hizi hotel ulizozitaja na Mount Meru hata kidogo maana hazilingani na hazitalingana hata siku moja
Ok mount meru ni kubwa . So kwanini unazungumzia upande mmoja wa wafanyakazi kuadhirika je kwajili wako hajaadhirika kwa chochote? Na unafikiri flow yake ya mapato ni kama zamani na anatakiwa kukupa wewe kila kitu
 
Huyu ni mwekezaji mpya tena mtanzania mwenzetu aliyeingia mwaka jana mwezi wa nane. Kabla hotel ilikuwa chini ya shirika la wamarekani
Ulichokiandika hapo ☝️ na mimi hapa 👇kinatofautisha nini?

Hii ni kati ya zile hotel zinazomilikiwa na serikali nchini ila baada ya marehemu mkapa kuingia madarakani ndipo ubinafsishaji ulizipeleka kwa wawekezaji na serikali kuwa mdau wa 49% kama sijakosea.
 
Mtoa mada kuwa muungwana..corona imeharib biashara...hapo hapo TRA wanatembeza bakuli bila kujali.kama mwenye hotel alipangisha mwenye jengo hajali hyo yeye anataka kodi yake ...

Alichowafanyia ni cha kiungwana na bado unalia...jiajir mkuu
 
Milioni 100 mbona hiyo ni hotel ya zero star kaka. Unajua tunazungumza hapa tukiwa na facts nyingi tu.
Yaani hapo nimewatolea mfano tu. Halafu wakae kitako waoneshe huo uungwana wa mwajiri uko wapi? Wanashindwa kutofautisha kati ya kufanya uungwana na kutimiza wajibu wa mkataba.

Pia hawatambui kuwa Mwajiri hawezi kumpa mfanyakazi likizo bila malipo ikiwa hakukaa na kushauriana nae.
 
Asante sana kwa maoni yako.
Lakini unaposema kajitahidi tena sana unalinganisha na nani? unapima kwa mizania ipi?
Hivi unafikiri wafanyakazi tu wajinga kulalamika pasipo sababu? Hivi unajua nini kilichotokea hadi tunasema hiki anachokifanya mwajiri sio sawa? Hivi unajua kuwa hadi sasa mwajiri hajapoteza chochote kwa upande wake ila tu wafanyakazi ndio wanaoumia?
Hivi unapojaribu kusema mwajiri kajitahidi, unazijua haki za mfanyakazi kweli wewe?
kwa hiyo hoteli haijapoteza wateja kutokana na corona? hivi hujui Naura Spring hoteli imekufa kabisa mpaka umeme/ maji hamna? hujui wafanyakazi wake hawajalipwa chochote? mvumilieni huyo mwajiri anawapenda
 
Kajitahidi kwa lipi? Ulipoteza ajira ndiyo lakini si ulilipwa stahiki zako zote? Hivi unajua kuwa huwezi sema una ajira wakati huna ujira? penye ajira lazima kuwe na ujira, right? Halafu tuambie hiyo hotel ya 5 star ambayo imepunguza wafanyakazi kwa ajili ya COVID-19 ni ipi?
Naura Spring hapo sanawari sio kupunguza wafanyakazi tu, bali imekufa kabisa mpaka umeme/ maji wameshindwa kulipa sababu ya corona
 
Asante sana kwa maoni yako.
Lakini unaposema kajitahidi tena sana unalinganisha na nani? unapima kwa mizania ipi?
Hivi unafikiri wafanyakazi tu wajinga kulalamika pasipo sababu? Hivi unajua nini kilichotokea hadi tunasema hiki anachokifanya mwajiri sio sawa? Hivi unajua kuwa hadi sasa mwajiri hajapoteza chochote kwa upande wake ila tu wafanyakazi ndio wanaoumia?
Hivi unapojaribu kusema mwajiri kajitahidi, unazijua haki za mfanyakazi kweli wewe?
kwa hiyo hoteli haijapoteza wateja kutokana na corona? hivi hujui Naura Spring hoteli imekufa kabisa mpaka umeme/ maji hamna? hujui wafanyakazi wake hawajalipwa chochote? mvumilieni huyo mwajiri anawapenda
 
Tatizo watu wanaongea lakini hawajui biashara ya hoteli inavoingiza hela. Kwanza ukitizama bei ya chakula tu. unakuta mtu breakfast na dinner analipa dola 30, sasa kitizame anachokula, slice, yai, bacon chai ausubuhi, cha usiku anakula wali labda ambao mimi na wewe ni tonge moja tu na vipande vya samaki ama kuku. soda unaweza kuta inauzwa dola 3 bia dola 5, hio ni hoteli ya kwaida tu uku zenji, ukija izo za 5 star bei ya milo utaenda mbio. Sasa kwenye makazi kwenye za 5 start unakuta bei ya chumba tu $500 kwenda juu. Kipindi cha high season hotel zinajaza, halafu unashindwa kuwalipa wafanyakazi wako hela yao ya likizo? huu ni unyonyaji tu
Kuna bosi mto wa mbu ana lodge sitaitaja jina iyo lodge bana mwenye nayo akiona booking ni chache anawalipa nusu mshahara kuanzia kwa manager hakuna mtu anafikisha. Lakin mbili na nusu yaani ni unyonyaji mtupu kwa mabosi wa hoteli jaman
 
Duh

Ova
 
Back
Top Bottom