VILE "visit Rwanda" inanizinguaga

Tukijitangaza zaidi tunaweza ku double idadi ya watalii wanaokuja nchini.

Kuna kipindi kuna tyimu ya EPL iliukuwa inatangaza vivutio vyetu kwenye matangazo uwanjani kwao..vipi ilichangia kuongezeka kwa watalii kiasi gani?.. Huko London pia nasikia kuna madereva taxi wanatangaza vivutio vyetu...nayo imechangia kiasi gani kuongezeka kwa watalii?
 
Ilikua Sunderland na sio Newcastle.

Sasa hivi upigaji umebadilika tu style,jiulize kwanini Atcl imehamishiwa ofisi kuu ili tu CAG asiguse hesabu zake.


Mkuu huko juu awamu hii nasikia Kuna rushwa zinafanyika unaweza kufa kwa presha..kiongozi akiwa Magu..hii nimedokezwa Jana tu..watu wapige tu wakipata chances ..hakuna Cha uzalendo Wala nn..
 
Mkuu anataka na sisi tujitangaze kama Rwanda. So kama unajua platform inayotumika kuitangaza tz kiutalii abroad unaeza mpatia link na sio kumbeza.Ahsante
 
Hela za Matangazo kama hayo si ndio wanafanya wasanii, eti wanaenda kupanda kilimanjaro
 
Mkuu huko juu awamu hii nasikia Kuna rushwa zinafanyika unaweza kufa kwa presha..kiongozi akiwa Magu..hii nimedokezwa Jana tu..watu wapige tu wakipata chances ..hakuna Cha uzalendo Wala nn..

Hahah Mkuu hata siwezi kushangaa maana huu uzalendo wao wa kuibukia ghafla ghafla hata hua siuelewi elewi.

Na huko kwny miradi ndio wanazipiga kishenzi ndio maana wanakomaa tu kila siku miradi miradi.
 
Kila nchi inanjia zake za kutangaza vivutio vyake.Rwanda wao wameona hiyo ndo njia yao bora kujitangaza.
Nakumbuka kipindi Rwanda wamesign deal na Arsenal.Liligharimu kama Β£32 M hivi nahisi.Yaani wabongo mliwaandama sana.Mara Rwanda bado masikini wanajikakamua tu, sijui Rwanda kama CCM tu wananchi masikini ila wanaharibu pesa n.k.Nadhani impact umeanza kuiona sasa wanazidi kupata watalii na kujulikana zaidi.
Naona sisi tumetumia njia nyingine tofauti na hiyo.Niliona wanawasainisha hawa mastaa kama Samatta mikataba.
Yote kwa yote Serengeti pekee au Kilimanjaro ni mtaji tosha hatuwezi spend pesa nyingi hivyo kujitangaza.Idadi ya watalii wa Tz ni zaidi ya mara mbili ya Rwanda.Uchumi wa Tz ni mara saba ya Rwanda.Rwanda ni LDC na Tz ni MIC.Rwanda Air ipo juu kuliko ATCL.
 
Sawa kabisa ulivyojibu. Tusiwabeze Rwanda kwa kujitangaza japo hawana vitu vya kuweza kulinganisha na sisi. Badala yake tujifunze kwao kwa mantiki kwamba kama hata Rwanda wanafanya, vipi sisi?
 
Ila mie naona hii ishu ya kujitangaza ingeanza ngazi za chini pia .! Diaspora nao wangesaidia Sana huko walipo!
Tatizo jamaa wa kule serikalini wakisikia tu neno Diaspora wenyewe wanajua ni zile type za kina Le Mutuz wanaona bora wawapotezee tu,kumbe kuna watu wa maana tu huko wangesaidia kusukuma gurudumu.
 
Kila industry inahitaji wazee wa Fitna ili ku win, Nimekutana na Bango kubwa Arusha pale Taa za tripple A likitangaza RwandAir Niko excited kujua yaliyomo ndani ya Rwandair nime follow page zao zote mitandaoni excitation ni kubwa sana nasubiri wafanye resumption ya flights nifanye booking walau ka trip chochote nipate exposure na experience
 
Tatizo jamaa wa kule serikalini wakisikia tu neno Diaspora wenyewe wanajua ni zile type za kina Le Mutuz wanaona bora wawapotezee tu,kumbe kuna watu wa maana tu huko wangesaidia kusukuma gurudumu.


Hahhaaa...Ila hata dada wa Taifa wangemweka sawa angeweza tangaza poa tu
 
Hahah yule siku akiamka mapepo yamempanda atatoa shit mpk watalii/wageni wanaomfuatilia watasema huyu 'agency wa utalii' wa Tz ni wa aina yake kwa kweli hahah.

🀣🀣🀣🀣🀸🀸🀸🀸🀸πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ™ŒπŸ™Œ! Kile kichwa kiboko ya Bashite
 
Juzi nasikitika eti hua waziri anaomba apate namba za mastaa kama willsmith ili wapost japo insta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…