Vikomo vya nauli vinachangia kusababisha ajali?

Kikojozi

JF-Expert Member
Mar 24, 2009
331
1
Nilikua najiuliza kama vikomo vya nauli vinavyopangwa na serikali vinawafanya wamiliki wa magari kushindwa kumudu gharama za uendeshaji na hivyo kupendelea kuajiri madereva wasio na sifa bila mikataba kwa ujira duni, kutumia magari mabovu na yaliyochoka na kuwakatisha tamaa wajasiriamali/wawekezaji wanaotaka kununua na kuendesha magari/mabasi mapya na ya kisasa.

Kama kwa mabasi yaendayo mikoani mfano Arusha kikomo cha nauli ni shs 50,000/- kwa full luxury. Ina maana serikali inanikataza mimi kama mwekezaji kununua full luxury mpya ya mwaka 2010 yenye "airbags" kwa kila abiria na kila aina ya kifaa kuhakikisha usalama kwa abiria ambayo gharama yake ya uendeshaji kwa kila abiria huenda ikawa 80,000/-? Kama kuna watu wako radhi kulipa shs100,000/- nauli ya Arusha kusafiri na basi jipya na la kisasa kabisa kuna tatizo?

Kwa kifupi, vikomo vya nauli za daladala na mabasi yaendayo mikoani vinatulazimu kusafiri kwa kutumia mikweche/vimeo vinavyoendeshwa na vihiyo na hivyo kusababisha ajali nyingi?

Is cheap expensive?
 
serilkali si imeangalia hali halisi ya kipato cha raia wake kama wanaweza kumudu, hivi kwa maisha ya walio wengi na ndio wahangaikaji unategemea mtu alipe nauli ya dar mpk arusha laki moja,kwenda na kurudi ni laki mbili.!
we kama ni mjasilia mali ukitaka kuleta hayo ma luxury coach leta usubiri watalii wakija bongo uwakodishe, lakini kwa tulio wengi hatuwezi ku-afford hiyo kitu japo cheap is expensive , hata expensive nayo ni expensive tu.! Mungu atatushikia sie tusioweza kwenda na luxury coach maana hata kwa Fuso tutafika tu.
mwenda kwao sio mtoro.
ni maoni tu nawakilisha.
 
Back
Top Bottom