Vijue vyeo, Majina na Alama za Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ)

nyongeza:
1. gari la mkuu wa majeshi(CDF) lina nyota nne kama plate namba
2. vyeo-kuanzia nyota moja hadi tatu wanaitwa Junior officers na juu ya hapo wanaitwa Senior officers. waliosalia wanaitwa askari.
masahihisho yanakaribishwa
 
silaha nyingi nzito jeshi linanunua nje hasa China, Marekani, Uingereza, Ukraine, India n.k sare zinatengenezwa bongo na silaha chache.
Poa nimekusoma, hivi hawawezi kujijengea majumba yao wenyewe kiasi cha kutosha mahitaji yao kutokana na vyanzo vyao vya mapato ???? ( maana najua kuna mainjinia wa majengo na wataalamu kibao wa masuala ya ujenzi.)
 
nyumba nyingi mbona wanajenga wao wenyewe.
 
Nasahihisha kidogo
13. Ngao na nyota tatu ni Brigedia General
14.X na ngao ni Major General
15.X na nyota moja na ngao ni luten general
16.X na nyota mbili na ngao ni general
mambo yamebadilika siku hizi mtiririko hauko hivyo. Jamaa hapo juu yuko sahii
 
1. Asiye na cheo-Private
2. V moja- Koplo usu
3. V mbili-Koplo
4. V tatu- Sajenti
5. V tatu na mwenge- sajinitaji
6. Mwenge(mkononi)-Afisa mteule daraja la pili, na ngao(mkononi)afisa mteule daraja la kwanza
7. Nyota moja-luteni usu
8. nyota mbili-luteni
9. nyota tatu-kapteni
10. ngao-meja
11. ngao & nyota moja-luteni kanali
12. ngao & nyota mbili-kanali
13. X & nyota moja na ngao-brigedia jenerali
14. X & nyota mbili na ngao-meja jenerali
15. X & nyota tatu na ngao-luteni jenerali
16. X & nyota nne na ngao-jenerali
N.B: Mwenye masahihisho anakaribishwa
Mkuu je mwenye bibi na bwana na nyota tatu zilizokaa kwenye mtindo wa triangle anaitwaje?#
 
Mkuu namba 1 usiseme asiye na cheo, hamna askari asiye na cheo, bali tungesema askari/mwanajeshi aliyeajiriwa cheo cha kwanza/cha chini kabisa ni Private. Pia namba 11 na 12 ungeanza na nyota badala ya ngao, maana tafsiri itakuwa tofauti. Pia hongera kwa kuweka vizuri hizo ranks kama ilivyo sasa maana wengi wanajua ranks za zamani. Pia kuwajibu wanaochanganya, JKT ni sehemu ya JWTZ na hata askari wanaweza toka upande mmoja na kuhamia upande mwingine.
 
Na vyeo vya Polisi, Magereza, uhamiaji na zimamoto vinatofauti gani na hivi vya Wanajeshi? Mwanajeshi mwenye nyota tatu yuko sawa na polisi mwenye nyota tatu pia? Au vinatofautianaje?
Kuna tofauti kubwa mno....Ukiona mwanajeshi ana nyota basi ujue nyota hiyo inamtambulishs kama Commisioned Officer anayopewa na Rais peke yake...

Polisi na hao wengine zile nyota zao sio commissioned na Rais...Ila wanaitwa gazetted officer wanapeana wenyewe huko.....

Kuachilia Kamishna wa Polis anayeteuliwa na Rais wengine wote hata kama ana nyota 10 na mabibi na mabwana na mangao mabegani ni mdogo kwa Afisa wa jeshi mwenye nyota moja na akikuta na Luten usu wa JWTZ lazima ampe saluti..
 
Nashukuru sana kwa maelezo hayo hakika umenifuta ujinga.
Na hawa MP, wanamamlaka ya kufanya kazi kwa raia kama alivyo polisi wa kawaida? Maana kuna sehemu kama Makongo huwa wanakaa mpaka barabarani.
 
MP maana yake ni Millitary Police(polisi jeshi)...Anafanya shughuli zake za kipolis jeshi within Millitary premises only (maeneo ya jeshi tu)

Makongo ipo Within Lugalo Millitary Base kwa hiyo wanafanya kazi zao eneo la jeshi....Eneo hilo huwezi kuta Polisi wa kawaida..
 
Back
Top Bottom