Tuhuma za JWTZ kupiga raia huko Kawe: Tunaomba Waziri wa Ulinzi ajitokezee kukemea, kulaani, na kukataza jeshi kujichukulia sheria mkononi

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu wanaJF wenzangu, nafikiri wengi wetu hapa JF tumesikia, tumesoma na wengine kuona kile kinachosemekana kufanywa na jeshi letu, ambalo tumelipa jina la "Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Jeshi hilo tulilipa jina hilo kwa kuamini kwamba, jeshi hilo limeundwa kwa ajili ya kumlinda, na kumpigania mwananchi wa Tanzania.

Lakini pia liliundwa kwa ajili ya kuilinda mipaka ya Tanzania, pamoja na viongozi wa Tanzania akiwemo raisi wa nchi (ambae ni amiri jeshi wao mkuu) mawaziri, wakuu wa mikoa na viongozi wengine mbali mbali. Hilo ndio lilikuwa lengo la kuundwa kwa jeshi hilo, lkn pia kupewa jina hilo (JWTZ)

Sasa inashangaza sana jeshi ambalo lingewalinda na kuwapigania wananchi, ndio linageuka kuwa jeshi la kuwapiga hovyo wananchi, kuwatesa wananchi na hata wengine kuwauwa wananchi bila sababu za msingi.

Yes tunajua kwamba kila binadamu ana mapungufu yake, hivyo wapo wananchi wanaofanya makosa, au mambo mabaya kwa jeshi letu. Lakini kuna sheria na mahakama ambavyo vinaweza kutumika kuwaadhifu wale wanaofanya mambo mabaya kwa jeshi letu, na sio jeshi hilo kukimbilia tu kujichukulia sheria mkononi mpaka kupelekea maafa kama yaliotokea Kawe na kwengineko.

Malalamiko ya wananchi au raia dhidi ya jeshi hayakuanza leo, ila cha kushangaza badala ya kumalizwa kwa njia ya amani, ndio yanazidi kuongezeka kwa njia za kuchochewa na jeshi hilo hilo lililopewa dhamana ya kutulinda.

Kwa kilichotokea juzi huko Kawe, nafikiri viongozi wengi wa kiserikali wanalifahamu, lkn kwa vile pengine sio wahusika wakuu wa maswala ya kiusalama ndio maana hawahitaji kuliingilia swala hili.

Hivyo sisi wananchi tunamuomba waziri husika wa ulinzi mama yetu Stergomena Tax, pamoja na waziri wa mambo ya ndani brother Masauni waingilie kati swala hili kwa kuonya, kulaani na kutolea maelezo swala husika.

Msingoje mpaka raisi aje kulizungumzia mwenyewe, na wakati nyinyi kama mawaziri mmepewa dhamana ya kutulinda.

Kwa niaba ya wananchi wanyonge, ni mimi mpigania haki zao Mr Dudumizi wa somewhere in Kawe.
 
Mwanajeshi anayepiga mwananchi huyo sio mwanajeshi, ni mgambo kama mgambo wengine tu. Ni vizuri wakabainika hao wachache wakachukuliwa hatua ndani ya jeshi ili wasiendelee kulichafua jeshi letu tukufu.
Sio Mgambo,ni Askari wasio na nidhamu Wananchi wanatakiwa wapewe elimu kuwa lazima warekodi namba na Insignia za vikosi hivyo na kambi wanayotoka kisha kuripoti Polisi.
 
Mwanajeshi anayepiga mwananchi huyo sio mwanajeshi, ni mgambo kama mgambo wengine tu. Ni vizuri wakabainika hao wachache wakachukuliwa hatua ndani ya jeshi ili wasiendelee kulichafua jeshi letu tukufu.
Kweli mkuu, kuna vijana wengi tu wazalendo wa kweli na wenye utii mkubwa kwa jeshi letu huko JKT.

Ila kwa bahati mbaya wamekosa connection au vigezo vichache tu vya kuchaguliwa JWTZ.

Hivyo inabidi hao mgambo kama ulivyosema watolewe jeshini na nafasi zao zichukuliwe na hao niliosema hapo juu au sio mkuu..
 
Nasikia wameua afisa mkuu wa jeshi.....classified info jeshi hawatajibu
Afisa ameuwawa baada ya kuleta utemi wa kishamba.

Kaziba barabara, dogo akamuomba kistarab tu afisa huyo apaki gari yake vizuri ili dogo apate njia ya kupita na bajaj yake. Ofisa kuona macho ya watu akaona kadharauliwa na kutembeza makofi kwa dogo.

Dogo nae hakupenda unyonge uendelee, ndo akachomoa cha mkunjo na kulenga sehemu husika iliyomuangusha ofisa na kupelekea kupotez maisha.
 
Kweli mkuu, kuna vijana wengi tu wazalendo wa kweli na wenye utii mkubwa kwa jeshi letu huko JKT.
Ila kwa bahati mbaya wamekosa connection au vigezo vichache tu vya kuchaguliwa JWTZ. Hivyo inabidi hao mgambo kama ulivyosema watolewe jeshini na nafasi zao zichukuliwe na hao niliosema hapo juu au sio mkuu..
Uko sawa kabisa, hao mgambo wachunjwe, Mwanajeshi hajafunzwa kupiga wananchi anaowalinda.
 
Afisa ameuwawa baada ya kuleta utemi wa kishamba.

Kaziba barabara, dogo akamuomba kistarab tu afisa huyo apaki gari yake vizuri ili dogo apate njia ya kupita na bajaj yake. Ofisa kuona macho ya watu akaona kadharauliwa na kutembeza makofi kwa dogo.

Dogo nae hakupenda unyonge uendelee, ndo akachomoa cha mkunjo na kulenga sehemu husika iliyomuangusha ofisa na kupelekea kupotez maisha.
Sasa unataka nini ? Raia wamechokoza geshi? ...tuwe subira yatapita ni upepo mbaya tuuu.......karibu kambini tuyajenge
 
Afisa ameuwawa baada ya kuleta utemi wa kishamba.

Kaziba barabara, dogo akamuomba kistarab tu afisa huyo apaki gari yake vizuri ili dogo apate njia ya kupita na bajaj yake. Ofisa kuona macho ya watu akaona kadharauliwa na kutembeza makofi kwa dogo.

Dogo nae hakupenda unyonge uendelee, ndo akachomoa cha mkunjo na kulenga sehemu husika iliyomuangusha ofisa na kupelekea kupotez maisha.
Duuuuuuu!!! kumbe :mad:
 
Back
Top Bottom