Vijitabia vidogo vidogo vinavyokera..!

Vijitabia vidogo vidogo vinavyokera..!

Kwa lengo la kuwekana sawa, unaweza ukawa unatabia mbaya, ila hujui kama ni mbaya mbele za watu.
Mimi katika kuishi na watu mbalimbali, nimeshuhudia watu wenye tabia tofauti tofauti ila tunavumiliana tu, wakati mwingine tunarekebishana..!

Hizi hapa ni zile chache miongoni mwa nyingi ninazozikumbuka toka kwa watu niliwahi kuishi nao..

  1. Kutumia simu wakati wa kula. Hii nimeiweka ya kwanza kabisa kwa sababu ilikuwa tabia yangu, mama yangu kila alipokuwa akinikemea niliona kama anazingua tu! ila siku nilipokemewa ugenini ndio nikaamini kweli hii ni tabia mbaya, na nikaacha mara moja.
  2. Kutawala mazungumzo. Huyu alikuwa rafiki yangu, classmate, alikuwa anapenda aongee yeye muda wote, hata kama mada haijui vizuri hakupenda kuwa msikilizaji kabisa.
  3. Kutotambua muda wa utani. Hii niliiona kwa watu wengi sana, ila tamzungumzia jamaa yangu mmoja hivi, Rashid (R.I.P), huyu mshikaji alikuwa hawezi kuwa serious, alikuwa hajali mood ya mtu, hajali watu waliokuzunguka muda huo, yeye atakachoona kinafaa kukutania anakisema tu popote wakati wowote.
  4. Kutumia viwakilishi badala ya jina la mtu. Hii nayo niliiona kwa wengi, unakuta mtu analijua jina lako kabisa, lakini anakuita, wewe, huyu, yule.
  5. Kukosoa ovyo ovyo. Sikatai mtu kukosolewa anapokosea, ila unapokosoa hakikisha una lengo la kumuelimisha mkosolewa na sio kumuaibisha au kwa lengo la kujikweza mbele za watu, jambo la kuzingatia zaidi, lugha ya ukarimu itumike.
  6. Kucheka hadi kwenye serious moments. Wengine sijui huwa ni makusudi au sijui ndo hawezi kuzuia kicheko, yaani mtu hatambui nyakati za kuwa serious, kicheko kikija, yeye anacheka tu! ni kweli kuna jambo linaweza kukufurahisha peke yako na ukajikuta umeshindwa kuzuia kicheko, basi ukacheka. Huenda watu wakakuvumilia wakajua ni bahati mbaya tu! ajabu inakujua pale inapoonekana kuwa wewe sasa umekuwa ni mtu wa kuchekacheka kila muda ni wewe tu!

Tabia ya kutema mate ovyo.

Kupiga chafya tena inayonuka na huombi msamaha.

Puuu.

Kuongea huku unatafuna chakula.
 
Dah kuna watu wanapenda sana kupiga mizinga (kuomba hela), yaani hata kama ni mshkaji au ndugu unaogopa hata kumpigia umsalimie maana lazima tu atakupiga mzinga. Ukiona simu yake roho inakwenda mbio hata kupokea unaogopa.
Punguza uchoyo
 
Siku ya kwanza unamuita msichana aje muonane sehemu na umejiandaa kwa bajeti ya watu wawili tu...unakuta limsichana badala ya kuja yy peke yake linakuja na committee mfano(rafiki zake wawil na dada ake)

Nyie wasichana muache hii tabia.
 
Kwa lengo la kuwekana sawa, unaweza ukawa unatabia mbaya, ila hujui kama ni mbaya mbele za watu.
Mimi katika kuishi na watu mbalimbali, nimeshuhudia watu wenye tabia tofauti tofauti ila tunavumiliana tu, wakati mwingine tunarekebishana..!

Hizi hapa ni zile chache miongoni mwa nyingi ninazozikumbuka toka kwa watu niliwahi kuishi nao..

  1. Kutumia simu wakati wa kula. Hii nimeiweka ya kwanza kabisa kwa sababu ilikuwa tabia yangu, mama yangu kila alipokuwa akinikemea niliona kama anazingua tu! ila siku nilipokemewa ugenini ndio nikaamini kweli hii ni tabia mbaya, na nikaacha mara moja.
  2. Kutawala mazungumzo. Huyu alikuwa rafiki yangu, classmate, alikuwa anapenda aongee yeye muda wote, hata kama mada haijui vizuri hakupenda kuwa msikilizaji kabisa.
  3. Kutotambua muda wa utani. Hii niliiona kwa watu wengi sana, ila tamzungumzia jamaa yangu mmoja hivi, Rashid (R.I.P), huyu mshikaji alikuwa hawezi kuwa serious, alikuwa hajali mood ya mtu, hajali watu waliokuzunguka muda huo, yeye atakachoona kinafaa kukutania anakisema tu popote wakati wowote.
  4. Kutumia viwakilishi badala ya jina la mtu. Hii nayo niliiona kwa wengi, unakuta mtu analijua jina lako kabisa, lakini anakuita, wewe, huyu, yule.
  5. Kukosoa ovyo ovyo. Sikatai mtu kukosolewa anapokosea, ila unapokosoa hakikisha una lengo la kumuelimisha mkosolewa na sio kumuaibisha au kwa lengo la kujikweza mbele za watu, jambo la kuzingatia zaidi, lugha ya ukarimu itumike.
  6. Kucheka hadi kwenye serious moments. Wengine sijui huwa ni makusudi au sijui ndo hawezi kuzuia kicheko, yaani mtu hatambui nyakati za kuwa serious, kicheko kikija, yeye anacheka tu! ni kweli kuna jambo linaweza kukufurahisha peke yako na ukajikuta umeshindwa kuzuia kicheko, basi ukacheka. Huenda watu wakakuvumilia wakajua ni bahati mbaya tu! ajabu inakujua pale inapoonekana kuwa wewe sasa umekuwa ni mtu wa kuchekacheka kila muda ni wewe tu!
Mkuu umesahau kale katabia kako ka kunuka sox vepee umesahau kukaodhesha au labda hujakasanukia!
 
Tabia ya kutema mate ovyo.

Kupiga chafya tena inayonuka na huombi msamaha.

Puuu.

Kuongea huku unatafuna chakula.
Kutema tema vitu hovyo tena huangalii ni wapi.Mfano mnakula samaki,basi mtu miba anatemea hata chipi ya sakafu au hata kwenye kapeti....
 
Kukatisha maongezi ya watu.
Mpo mnaongea na mnasikilizana vizuri mara mmoja anaibua mada nyingine tofauti kabisa nje ya mlichokuwa mnaongea.
Au anatokea mtu kama anamsalimia mmoja wenu na ndio anaendeleza mazungumzo tofauti huku nyie mkiwa mme-pause. Ina kera sana.
Anyway, ubinadamu ni kuvumiliana tu.
 
Kupishana kwenye barabara nyembamba usiku halafu mtu amewasha full.
 
Unajadili na mtu mada muhimu yuko bize na lisimu lake tena ma sms ya watsap yanaingia kwa milio inayokera mbaya zaidi anaanza kukuonyesha ma clip aliyotumiwa kumbe wewe uazijua hizo clip siku nyingi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]una kibamia mkuu??
Hata hii nayo inakera. Nani alichagua maumbile ya jinsi alivyo? Wengine warefu, wengine wafupi, wengine wembamba, kuna weusi na weupe wewe ni nani hata uwacheke watu kwa maumbile yao?
 
Tabia ya kwenda bar hauna ela unaanzia kuomba bia " broo nA Mimi moja " umeagiza nyama Au mchemsho yeye ndiye wa kwanza kunawa bila hata kukaribishwa inakera Sana na nikuharibiana bajeti
 
Back
Top Bottom