pistmshai
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,313
- 3,683
Kwa lengo la kuwekana sawa, unaweza ukawa unatabia mbaya, ila hujui kama ni mbaya mbele za watu.
Mimi katika kuishi na watu mbalimbali, nimeshuhudia watu wenye tabia tofauti tofauti ila tunavumiliana tu, wakati mwingine tunarekebishana..!
Hizi hapa ni zile chache miongoni mwa nyingi ninazozikumbuka toka kwa watu niliwahi kuishi nao..
Mimi katika kuishi na watu mbalimbali, nimeshuhudia watu wenye tabia tofauti tofauti ila tunavumiliana tu, wakati mwingine tunarekebishana..!
Hizi hapa ni zile chache miongoni mwa nyingi ninazozikumbuka toka kwa watu niliwahi kuishi nao..
- Kutumia simu wakati wa kula. Hii nimeiweka ya kwanza kabisa kwa sababu ilikuwa tabia yangu, mama yangu kila alipokuwa akinikemea niliona kama anazingua tu! ila siku nilipokemewa ugenini ndio nikaamini kweli hii ni tabia mbaya, na nikaacha mara moja.
- Kutawala mazungumzo. Huyu alikuwa rafiki yangu, classmate, alikuwa anapenda aongee yeye muda wote, hata kama mada haijui vizuri hakupenda kuwa msikilizaji kabisa.
- Kutotambua muda wa utani. Hii niliiona kwa watu wengi sana, ila tamzungumzia jamaa yangu mmoja hivi, Rashid (R.I.P), huyu mshikaji alikuwa hawezi kuwa serious, alikuwa hajali mood ya mtu, hajali watu waliokuzunguka muda huo, yeye atakachoona kinafaa kukutania anakisema tu popote wakati wowote.
- Kutumia viwakilishi badala ya jina la mtu. Hii nayo niliiona kwa wengi, unakuta mtu analijua jina lako kabisa, lakini anakuita, wewe, huyu, yule.
- Kukosoa ovyo ovyo. Sikatai mtu kukosolewa anapokosea, ila unapokosoa hakikisha una lengo la kumuelimisha mkosolewa na sio kumuaibisha au kwa lengo la kujikweza mbele za watu, jambo la kuzingatia zaidi, lugha ya ukarimu itumike.
- Kucheka hadi kwenye serious moments. Wengine sijui huwa ni makusudi au sijui ndo hawezi kuzuia kicheko, yaani mtu hatambui nyakati za kuwa serious, kicheko kikija, yeye anacheka tu! ni kweli kuna jambo linaweza kukufurahisha peke yako na ukajikuta umeshindwa kuzuia kicheko, basi ukacheka. Huenda watu wakakuvumilia wakajua ni bahati mbaya tu! ajabu inakujua pale inapoonekana kuwa wewe sasa umekuwa ni mtu wa kuchekacheka kila muda ni wewe tu!