Vijana wote wa morogoro wasio na kazi njooni

KICHWA BOGA

Member
Apr 27, 2014
51
15
HABARI wana JF, tunawahitaji vijana wote wasio na kazi yoyote. wafike chuoni kwetu cha MICTES kilichopo kihonda maghorofani jirani na shule ya msingi kihonda maghorofani. LENGO KUU;
Kupeana mawazo, elimu na miongozo juu ya nini twaweza kufanya ili kujikwamua kimaisha.
ADA
Ni huduma ya BURE ili kuimarisha jamii yetu yenye ustawi kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Wasiliana na
DEAN
0752-698691 na
0658-698691
 
Andika tarehe na muda wa tukio tafadhari, asiye na kazi hawezi kuwa na hela ya vocha....toa taarifa iliyokamilika kuepusha upigaji wa simu.
 
Wewe ni KICHWA BOGA mie nlijua unaenda kuwapa deal ya kazi kumbe unaenda kuwachanganya na theories zenu kwanini nyie hamzitumii hizo theory? Au mnapenda kula vumbi la chaki miaka yote?
 
Last edited by a moderator:
Andika tarehe na muda wa tukio tafadhari, asiye na kazi hawezi kuwa na hela ya vocha....toa taarifa iliyokamilika kuepusha upigaji wa simu.

MKUU, Tunachokifanya ni kukaa chini na vijana, awe amesoma au hajasoma, tunamskiliza mawazo yake, malengo yake, nini kinamtatiza, tunamuwezesha kadri atakavyotaka na wenye mawazo yanayofanana, wanaweza kufanya kitu kwa pamoja kama kundi kwa mentorship ya chuo. Haina muda maalum wa tukio kwani tutaendelea kuwa nao muda wowote tarehe yoyote.

Mwenye mchango wa mawazo anaweza kuchangia ili kuwawezesha wenzetu. Tutashukuru kwa mchango wa mawazo utakaoutoa.
 
KWELI hujitambui wewe! miaka hii unajua kumsaidia mtu ni kumpatia ajira!!! pole sana, wengine tushatoka enzi hizo, achana na mawazo ya kitumwa hayo, tulia uelekezwe, umeshajua chuo chetu kina deal na nini hadi uropoke kwa hoja za kukaririshwa.. eti theory, njoo uone tunachofanya na c kujaza ----- kichwani mwako.

Unajua tuna miradi gani hadi useme tunaishi kwa chaki? Kumbe ndo maana mnalialia ajira hazpo kumbe mnadhani kushika chaki unakuwa na dhiki, POLE kwa dharau.

Usiwakatishe tamaa vijana kwa mawazo yako mgando, we mwenyewe unafanya kazi gani kama c ushabiki wa kipuuzi?

kweli ualimu ulikuwa wito!
 
kweli ualimu ulikuwa wito!

Umeona eeh! Bila wito, utakimbia wanazoziita vumbi za chaki na kusahau kuwa siku hizi kuna projectors.
Kwa akili ya baadhi ya watz, tena wanaojiita wenye digrii wanabaki na digrii vichwani na kusahau ujuzi walionao na wengine kujineemesha wao na kuwasahau wenzao walio mtaani hawajui wafanye nini.
 
Ingekuwa mitaji mngepeana na ndugu zenu...
Mbona kazi nzuri hamtangazi acha wizi wewe..unataka utokee kwa migongo ya watanzania wnzako,
Bogas wewe, hiyo mitaji wape nduguzo maskin
 
Ni wazo zuri sana

Dar es Salaam napo nafikiri mtuandalie program kama hii

Ahsante mkuu, kwa uelewa wako na ninadhani watu kama nyie mna mchango mkubwa sana ktk jamii. Dar tutafika, tuombeane. Sio hao maroboti wa kucomment upuuzi kukatisha tamaa vijana walio ktk dilemma, tusipowashika mkono tunasubiri wajiue tuilaani serikali.
 
Kaka vp tena mbona umetoa tangazo then unaanza kujibizana na watu maneno machafu

MKUU, cjaona ubaya wa post hii but nashangaa maneno ya ovyo ovyo yanayotoka akilini mwa watu, kuonesha kukereka kwangu, naona niwajibu kama wanavyotaka.

Any way, sorry kwa niliyemkwaza bt tabia hii tuliyonayo ya kubeza ideas za watu ipo siku mtu ataumbuka maana unaweza kujikuta tunakuwa wote baada ya kuona idea ni productive kwa jamii.
 
'..no free lunch in london...' sijui huu msemo huwa bado hupo? labda niulize swali : nyinyi wawezeshaji mnapataje faida katika hili? au ndo wale wale waliokunywa uji wa mgonjwa?
 
'..no free lunch in london...' sijui huu msemo huwa bado hupo? labda niulize swali : nyinyi wawezeshaji mnapataje faida katika hili? au ndo wale wale waliokunywa uji wa mgonjwa?

Unapomsaidia mtu kupata kile anachotaka kupata, automatically nawe utapata kile ukitakacho, kumsaidia mtu ni kuwekeza, hatuangalii faida ya leo, furaha kubwa ni kuona mtu uliyemsaidia anafanikiwa.
 
Kutokana na idadi ya vijana kuzidi kuongezeka ktk mpango, awamu ya kwanza itafungwa tar 15 JUNE 2014. Na wengne watasubiri awamu ya pili hapo mwezi OCTOBER mwaka huu.
 
MKUU, Tunachokifanya ni kukaa chini na vijana, awe amesoma au hajasoma, tunamskiliza mawazo yake, malengo yake, nini kinamtatiza, tunamuwezesha kadri atakavyotaka na wenye mawazo yanayofanana, wanaweza kufanya kitu kwa pamoja kama kundi kwa mentorship ya chuo. Haina muda maalum wa tukio kwani tutaendelea kuwa nao muda wowote tarehe yoyote.

Mwenye mchango wa mawazo anaweza kuchangia ili kuwawezesha wenzetu. Tutashukuru kwa mchango wa mawazo utakaoutoa.

Kichwa Boga hebu jisikilize mwenyewe, hapo nilipo bold na ku-underline pananipa mashaka. Sema ukweli, au kuna hela za mradi fulani ambao unataka kuonyesha ni idadi gani ya watu wamefika hapo chuoni kwenu?
 
Hakuna kitu kama hicho mkuu, tunajiwezesha wenyewe nikimaanisha tunajitegemea. ninachomaanisha hapo ni kuwa atawezeshwa kulinganba na wazo na ndoto alizonazo maana si wote wasio na kazi wana malengo na ndoto japo wana elimu. wenye ndoto na malengo tunawapa support na wasiojitambua kabisa, tuna kazi za kuwapa na kuwasaidia waweze kujitambua na kusimama kimaisha.
 
Back
Top Bottom