Vijana wengi wa Kitanzania hawana tofauti na Wazee wao. Wamezoea shida mpaka shida zimekuwa wao

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Moja ya jambo ambalo huwa linanisikitisha ni kuona kuwa tayari vijana wakitanzania katika Umri wa miaka 25-45 wanawaza kama wazee wenye Miaka 70-90 Nchi nyingine wazee wa miaka 60 wanawaza kama vijana wa miaka 25-45. kuna tofauti kubwa sana. Mtanzania anaweza furahi sana unapomsimulia kuwa Jana hukula ulilala na njaa, gari lako linakusumbua sana, huna pa kulala, una shida n.k hapa atakusikiliza sana utamwona anatikisa hadi kichwa kana kwamba anakuonea huruma. hapo atataka kukusikiliza sana. yaani anafurahia kusikiliza shida ulizo nazo ili mwishoni akuambie tu POLE halafu naye akawasimulie wengine shida ,taabu na mateso uliyo nayo.

Ukitaka mtanzania asikusikilize mwambie mambo ya Maendeleo. mwambie jinsi ambavyo sasa umejikwamua kiuchumi huna shida ndogo ndogo. hapo utaanza kumkwaza. kesho hatotaka tena kukusikiliza ataanza kujitenga na wewe. Yaani watanzania wengi mnaamini katika shida na kuona ni sehemu ya maisha yenu kuliko maisha mazuri. akianzisha Uzi mtu akasema " Wadau ni week sasa sijalakit chochote hata mate tu sijameza maana yamekauka mdomoni" watu hawatahoji huyu jamaa hajala week nzima anaishije? ila watasema aisee...pole sana Mungu akusaidie, Serikali hii haijali watu wake, Acha uvivu wewe mwanaume kapambane" n.k wataamini bila shaka hata kidogo.

Akija mtu mwenye uwezo akasema jamani nina mwaka sasa sijui kupungukiwa. Sijui njaa ikoje, Sijui kukosa kukoje nina maisha niliyokuwa nataka" hapo atashambuliwa sana. kuwa aache uongo. aweke ushahidi, anaota n.k sasa unashangaa hawa watu kwa nini mambo negative wana amini ila positive wanakataa? Ukisema " katika haya maisha nimewahi kutana na shetani... aanambia ABC" watu hawataubishia watasema " haya mambo yapo jamani msibishe. ila akija mtu mwingine akasema "katika haya Maisha nimekutana na Mungu" watu watamshukia kama mwewe. na kumwambi aache kuota, aache kudanganya umma n.k

Haya maisha mara nyingi unapokea unachomini. isipokuwa tu kama kutakuwa na exceptional flan ndani yako. Vijana wanaamini maisha yao yameshagota hawawezi kuendelea tena mbele. na hili ni tatizo ambalo linatokana na urithi mbovu. wanarithi umaskini si mali bali wa akili toka kwa wazazi wao. huwezi mlaumu mzazi wako kwa kuwa maskini. dont do that. wewe sasa onesha tofaut pambana umsaidie yeye. mbadilishe maisha yake kwa kuwaza kitajiri. but kinyume chake unakuta kijana wa miaka 25-45 ana waza kama mzee wa miaka 70. anakwambia " ACHA UONGO WEWE HUWEZI MILIKI RANGE ROVER, HUWEZI MILIKI JEEP, HUWEZI MILIKI MERCEDES BENZ. ukimuuliza kwa nini. anakwambia "hayo magari yana wenyewe , wewe hizo pesa unazipata wapi. unaota tu" unajiuliza hao wenyewe ni akina nani?

Kijana anashindwa kutafuta muda kuwasikiliza watu wenye akili ila anapata muda wa kwenda msikiliza mtu mmoja anasema ana date msanii flani. mimi huwa naangalia tu hata watu ambao mtu ame wafollow insta,twitter au fb.unaweza gundua akili ya huyu mtu ikoje kutokana na hao alio wa follow. unaacha kuwafollow watu wenye akili unawafollow watu wa hovyo hovyo. unafollow watu ambao hawana mchango positive katika maisha yako. wewe ndo tatizo. halafu sisi wengine tukizungumzia maisha yetu mnaona ndoto... ni sababu mmezaliwa katika shida, mkasoma katika shida, mkakua katika shida,mkaishi katika shida mpaka ninyi wenye mkawa ndo shida zenyewe.

Mtu anakuwa mpumbavuh (ashakum si matusi/pardon my language ) mpaka upumbavuh unakuwa yeye. hujawahi sikia watu wanasema "na wewe usiwe kama chande" unauliza huyo chande ndo nani.... unaambia aaargh bwege mmoja teja flani maarufu" au mtu anaaambiwa huyu jamaa ni kama juma lokone" unauliza huyo juma lokone ni nani. unaambiwa ni shoga flani maarufu. yaaani jamaa amekuwa shoga mpaka ushoga umekuwa yeye.

Mwaka fulani nilikuwa namsikia sana ombaomba mmoja anaitwa matonia. siku hiyo nakumbuka nilikuwa na Mercedes Benz nikamwambia dereva aniepeleke anakopatikana Matonia. mimi nilikuwa mgeni nilifika toka Sweden nikawa nimefikia nyumba yetu iliyoko upanga. sasa nikaangalia nitumie gari gani kati ya Range Rover, BMW na Benz nikamwambia Dereva tuendeshe Benz anipeleke alipo huyo Ombaomba maarufu. nikiwa mdogo tu miaka hiyo. mimi mitaa siifahamu. akaendesha mpaka sehemu hiyo tukamkuta huyo omba omba. nakumbuka nilikuwa na tu hela kidogo tu mfukoni Usd 2000 nikampa yule Ombaomba. kuwa akapumzike kwake angalau kwa siku mbili tatu naye aenjoy maisha ili next time nikija nije muuliza anawea fanya nini. unajua kuomba si jambo baya . omba ufundishwe namna ya kutengeneza mtumbwi ukavue au omba usaidiwe pesa ya kununulia ndoano au jembe. siyo unaomba omba pesa za kula tu. hapo unakosea sana.

After two days nikarudi nikamkuta pale nikamkumbusha ndo mimi nilimoa vijicent kidogo siku kadhaa ago. nikamuuliza ulienda pumzika akanambia hapana.leo hii namkuta kama alivyokuwa siku ile ambayo nimempa Usd 2000 siyo hata amevaa nguo mpya au safi. nothing has changed.the same person,the same man the same everything.nilikwazika sana nikagundua jamaa hasaidiki. amekuwa ombaomba mpaka kuomba omba kumekuwa yeye. nikaja sikia mtu anamwambie mwenzie usiwe kama Matonia. nikaelewa maana yake.

Vijana hatupaswi chukia wanaofanikiwa tunapaswa kuwa nao karibu na kuuliza "mwenzetu ulifanyaje una friji kama sebule yangu. una kabati kama vyumba vyangu viwili."mimi nakumbuka nilimkaribisha jamaa mmoja home hapa hapa Obay. akaomba Tour.. nikamwingiza kabatini akaanza sema "aargh Bill una Boutique humu ndani sasa wateja watakuwa wanakujaje huku chumbani kwako?" nlimwambia hapana ni kabati languo... akasema "ooooohh haya". nikampeleka kwenye friji akasema "hiki chumba kina baridi sana aiseee.unaweza ganda.utadhani mochwari" nikamwambia hapa tupo ndani ya friji. akasema "oooh haya". yaani akajifanya kama alikuwa anafaham before. unampeleka mtu kwenye dressing table anauliza "unataka fanya biashara ya vipodozi?" nikamuuliza why? anasema "naona umejaza hapa ma lotion,cream,perfumes n.k" nikabonyeza remote yakafunguka mapazia nikamwonesha kioo mbele yake na kumwambia hii ni dressing counter. maana si dressing table tena.

Anyway. vijana msizoee maisha ya shida kiasi kwamba mkaona shida ni sehemu yenu ya maisha. ni stahii yenu na watu wote wanaishi kama ninyi kiasi mtu akisema ana maisha kinyume nanyi mnaanza mchukia na kumwona adui. msizoee shida mpaka shida zikawa ninyi. haya maisha ni kupambana bila kuchoka. usiku na mchana. badala ya kumendea kula tunda kimasikhara ili nawe ukaandike kitu kwenye ule uzi, hebu mendea fursa sehemu. ni ngumu kukuta vijana wanabishana kwa facts kuhusiana na shughuli za kiuchumi. kuwa kipi bora, kulima au kufanya biashara ya mazao. ila utakuta wanabishana hadi mishipa kuwatoka kuwa Simba au Yanga ni bora kuliko nyenzie. au Ronaldo ni bora kuliko Messi. Ok akiwa ni bora then what?

Tujifunze kwa walioweza lakini pia tusikubali kushindwa ikiwa hatujafa. kama hukufa katika mapambano yoyoteni vile kuwa uliachwa hai ukajipange this time ukiwa umashayagundua makosa. na kurudi nyuma kujipanga upya si dhambi. ili mradi mission inabaki kuwa ni ile ile. you may lose the battle but not the war. kumbuka he who fights and run away will live to fight another day. ingawa pia usiingie vitani kabla hujajifunza kuhusiana na pambano au mchezo wenyewe. huwa nawaambia wengi. kabla hujaamua kufanya biashara hebu fanya utafiti kwanza. jifunze kwa waliofanikiwa. then rudi now ukiwa unafahamu changamoto za hiyo biashara na nini na utazikabili vipi. then ingia kupambana. na usiingie kwenye vita ukiwa umetanguliza silaha zako zote za gharani. no acha nyingine for back up. usitumie mtaji wote kwenye biashara moja mpya. anza kidogo kidogo kwanza.

Tuanze kuishi maisha mazuri katika akili halafu tuya transform katika viteno tukifanya kile tunachoamini na si kile wanachoamini wengine. ukifahamu kuwa kila mtu ana kusudi lake hapa duniani hutaishi ukitaka kuwa kama X utaishi ukitaka kuwa kama wewe.
 
Kwahiyo ili uwe na maisha mazuri utakiwi kuzungumzia wala kutaniana mambo ya Simba na Yanga au Messi na Ronaldo. Kakojoe ukalale unaonekana hauna furaha na maisha yako ndo maana unapata mda wa kujilinganishia na maisha ya watu wengine.
 
Hatari
Screenshot_20200216-164959~2.jpeg
 
Nikampeleka kwenye friji akasema "hiki chumba kina baridi sana aiseee.unaweza ganda.utadhani mochwari" nikamwambia hapa tupo ndani ya friji. akasema "oooh haya". yaani akajifanya kama alikuwa anafaham before.🤣🤣🤣 daaaaah sio poa unakamba sijui huwa unazisikia wapi".
 
Umeandika kweli tupu, umaskini ukizidi unapofusha akili, uwezo wa kufikiria unapungua au kwisha kabisa, unakuwa na mawazo hasi kila wakati, kwako story za shida ndio unazipenda kwasababu unatafuta watu wa kufanana nao, badala ya kutafuta tofauti na wewe ujiongeze kwao, matokeo yake tunageuka kizazi cha kurithishana shida/ chuki/ hasira miaka yote, akitokea aliefanikiwa kidogo anaonekana adui, utachukiwa bila sababu mpaka ujiulize umewakosea nini usipate majibu, kumbe sababu ya kuchukiwa wewe ni tofauti nao kiuchumi, ukitaka wakupende simply kuwa mchovu kama wao.
 
Back
Top Bottom