Vijana wazalendo kutembea kwa miguu kutoka Dar hadi Dodoma kumuunga mkono Rais Magufuli

Nawapongeza kwa matembezi hayo ya UZALENDO, UKAKAMAVU, UJASIRI , MSHIKAMANO na UTIMAMU wa MWILI & AKILI

Nitawaunga mkono kwa njia bora kabisa....

Yaboresheni kwa kuhusisha TAASISI Nyingi zaidi ikiwemo Huduma za kiafya na Huduma ya kwanza kwa Watembeaji, Ulinzi wa washiriki n.k

Matembezi yaonyeshe Mengi zaidi yanayoungwa mkono pamoja na kuchambua changamoto zilizopo pamoja na masuluhisho yake

Matembezi yaainishe yanapoanzia na yanapoishia ikiwemo na Huduma za malazi na Chakula kwa watakaojitolea

NAWATAKIA MAANDALIZI MEMA.....
 
DU! TANZANIA HII HAITABADILIKA NG'OO IWAPO WATU WENYE MAWAZO KAMA HAYA BADO MPO!
 
Kati ya wanne mmoja ni kichaa!! Ule utafiti ulikuwa sahihi kabisa
 
Habari wana jamvi, mimi AUGUSTINO CHIWINGA nimeamua kwa pamoja na vijana wenzangu kufanya matembezi ya kizalendo kutoka jijini Dar Es Salaam, hadi mkoani Dodoma yalipo makao makuu ya nchi yetu kwa miguu ikiwa kama ni njia ya kumuunga mkono mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli, kutokana na hatua anazochukua kupambana na mafisadi na wala rushwa.

Tumeona katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameweza kufanya mambo mengi mazuri kama kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya kila mwezi, utoaji wa elimu bure, ufufuaji wa shirika la ndege la Air Tanzania, suala la madawati ununuzi wa vitanda vya wagonjwa muhimbili, utengenezaji wa mashine za CT-Scan na MRI pamoja na mambo mengine mengi.

Matembezi hayo ya kizalendo yanatarajiwa kufanyika mapema mwakani (2017) na kama wewe ni mzalendo unakaribishwa kuungana nasi kwa kuwasiliana kupitia namba 0756810804 au kupitia barua pepe (E-Mail) augustino162@gmail.com.
Karibuni katika matembezi ya kizalendo 2017.
Aludishe Ajira kwanza kwa vijana...
 
Wataalam wakiwatangazia tanzania kuna watu wengi wagonjwa,mnawafukuza kazi,haya shaulizenu.
 
Wapumbavu wakubwa nyie, mnamuunga mkono kwa lipi hasa alilolifanya kunguni nyie, mnaunga mkono wananchi kuteseka?
 
Habari wana jamvi, mimi AUGUSTINO CHIWINGA nimeamua kwa pamoja na vijana wenzangu kufanya matembezi ya kizalendo kutoka jijini Dar Es Salaam, hadi mkoani Dodoma yalipo makao makuu ya nchi yetu kwa miguu ikiwa kama ni njia ya kumuunga mkono mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli, kutokana na hatua anazochukua kupambana na mafisadi na wala rushwa.

Tumeona katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameweza kufanya mambo mengi mazuri kama kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya kila mwezi, utoaji wa elimu bure, ufufuaji wa shirika la ndege la Air Tanzania, suala la madawati ununuzi wa vitanda vya wagonjwa muhimbili, utengenezaji wa mashine za CT-Scan na MRI pamoja na mambo mengine mengi.

Matembezi hayo ya kizalendo yanatarajiwa kufanyika mapema mwakani (2017) na kama wewe ni mzalendo unakaribishwa kuungana nasi kwa kuwasiliana kupitia namba 0756810804 au kupitia barua pepe (E-Mail) augustino162@gmail.com.
Karibuni katika matembezi ya kizalendo 2017.
Hii ni akili au matope? Karne ya 21?! Kwa nini usikimbie tu mgambo, kwa nini muda huo usitumike kufyatua tofali na kusaidia ujenz wa shule,vituo vya watoto yatima, zahanati, kufanya matembez ya kilometa 5 au 10 kwa ajili ya donation kwa watu wenye mahitaji maalum kama tiba ambapo wanatakiwa kwenda Appolo India ila hawana fedha?
 
maandamano ya kumsifu ni ruksa ila ya kumwambia mapungufu yake utawakuta polisi wamebeba zana za kivita waangamize waandamanaji.

Dhambi ya unafiki msipoitubia mngali hai hakika jehanamu ni makazi yenu ya kudumu.

Badilikeni sana kuweni wakweli kwa kila jambo mziponye nafssi zenu

Ole juu yenu

Isaya 5
20 Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!

21 Ole wao walio wenye hekima katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe!
 
Hongeren sana, lkn sidhan kama kuna dalili yeyote ya ukwel wa hayo matembez, ukizingatia tena ni ya miguu..., fanyeni kwanza mpaka Chalinze, halafu mlete feedback hapa, kama nusu yenu hamjaishia kuomba lift
 
Back
Top Bottom