Vijana wasomi wa Tanzania

OHA

Member
Aug 20, 2013
34
42
Kuna haja kubwa ya kutaka kufanya uchunguzi ili kubaini katika elimu ya vijana wanayo pata hapa nchini inawasaidia kitu gani?

Kwakuwa swala la katiba ni swala ambalo vijana kama vijana wangekuwa na ari kubwa kulipigania ili kukomboa nchi na kujenga katiba isiyo na ubagudhi kwa mustakabali wa Taifa letu la Tanzania.

Hatuwezi kuwa na mazingira rafiki aidha kujiajiri au kuajiriwa kama nchi haitakuwa na katiba ambayo tunaweza muwajibisha yoyote kisheria ni kwamba nchi hii itaendelea kuongozwa na baadhi ya watu ambao wataendelea kuidumaza.

Kwa miaka ambayo nchi imepata uhuru na rasilimali tulizo nazo ingetosha kuleta mabadiliko mqkubwa sana bila kutegemea matamko ya rais. Tukiwa na katiba imara kutakuwa kutoingiliana kwa mamlaka ambayo ingeleta tija katika kuongoza nchi.

Tufike mahali hata kuwakuza vijana wetu tuwakuze kwa namna ambayo watakuja kulisaidia Taifa letu na kuleta mabadiliko ambayo nchi yetu itafika mahali tuondokane na umasikini kulingana na rasilimali tulizo nazo.

Itoshe kusema vijana wajitambue na watambue majukumu yao katika kuleta mabadiliko katika kuchochea demokrasia haki na kuitaka katiba kwa njia zilizo sahihi bila kuathiri maendeleo ya nchi.
 
Wengi wanaitumia elimu yao kulima karoti
5i6siedr6ocz.jpg
 
Tuache kuwa watumwa wa wanasiasa, kuna nchi hazina katiba iliyoandikwa na zinamaendeleo kutupita. ishu sio katiba ishu ni Uadilifu na Uaminifu katika kutekeleza majukumu ya kujenga nchi (Uzalendo)
 
Back
Top Bottom