Vijana waliopo CCM wanalo la kujifunza hapa

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,801
71,222
Ujumbe huu nimeutoa mahali lakini author hafahamiki ila utawasaidia sana vijana hawa kujitambua na kujua kuwa ubaguzi wao na dharau kwa wengine hauna manufaa kwao;

Matokeo ya Kisiasa yanataka Moyo Sana vijana wa CCM tutulieni nchi ni yetu sote, tupunguze kuchukiana na kuumizana kimwili!

Moses Machali, DC
David Kafulila, RC
Mwita Waitara, Naibu Waziri
Joshua Nassari, DC
Fakii Lulandala, DC
Julius Mtatiro, DC
Albert Msando, DC
David Silinde, Naibu Waziri,
Vincent Mashinji, DC
Mwambe, MB
Gekuli, Naibu Waziri
Juliana Shonza, MB
Patrobasi Katambi, N/W
Lijua Likali, DC

UVCCM tunajifunza nini toka kwa Vijana waliojengwa na CHADEMA wakaiponda CCM, Wamechukuliwa kuisaidia CCM

NCHI YETU SOTE tufanye siasa za hoja na siyo vioja na kuumizana.
 
Hao ulowataja tayari ni wanachama watiifu wa CCM... Nilitarajia unitajie hata mmoja alotoka direct upinzani
Wametokea wapi? Wote hao hawajamaliza walau mwaka wakiwa bench, wametoka Chadema straight wakapata vyeo serikalini, yaani serikali ya ccm; tafsiri yake ni kwamba, vijana wa ccm hawana uwezo wa kujenga hoja, wanajua kupayuka with no points, wateuaji wanaona, wanasikia and then wana act.
 
Hao wote ndio waliokuwa wanaelezea kushindwa kuleta maendeleo kwa CCM na nyie mkawaita nyumbu.
Lakini CCM ikaona wana akili na kuamua kuwanunua kama wachezaji bora wanunuliwavyo Ulaya na kuwaacha UVCCM wanaendelea kulipiga vuvuzela.
 
Maana yake ni kwamba, hao in ccm kabla hawajajijunga hadema, waliwekwa cdm kwa shughuli maalum wakisimamiwa na mwenyekiti.
 
Ujumbe huu nimeutoa mahali lakini author hafahamiki ila utawasaidia sana vijana hawa kujitambua na kujua kuwa ubaguzi wao na dharau kwa wengine hauna manufaa kwao;

Matokeo ya Kisiasa yanataka Moyo Sana vijana wa CCM tutulieni nchi ni yetu sote, tupunguze kuchukiana na kuumizana kimwili!

Moses Machali, DC
David Kafulila, RC
Mwita Waitara, Naibu Waziri
Joshua Nassari, DC
Fakii Lulandala, DC
Julius Mtatiro, DC
Albert Msando, DC
David Silinde, Naibu Waziri,
Vincent Mashinji, DC
Mwambe, MB
Gekuli, Naibu Waziri
Juliana Shonza, MB
Patrobasi Katambi, N/W
Lijua Likali, DC

UVCCM tunajifunza nini toka kwa Vijana waliojengwa na CHADEMA wakaiponda CCM, Wamechukuliwa kuisaidia CCM

NCHI YETU SOTE tufanye siasa za hoja na siyo vioja na kuumizana.
Ongeza kwenye list wale Covid-19, Lusinde, Makongoro
 
ELewa kwamba CCM aijawahi mtupa kada mwenye uwezo aliejitokeza mbele.

Ukiwa CCM na una uwezo uwezi achwa kamwe mbele ya mtu mwingine.

Kwa CCM makada kwanza kabla ya yeyote.

Kuna teuzi zingine ni unless kwa sababu ya kisiasa; lakini kama wewe ni kada CCM na una uwezo awawezi kukuacha miaka 800.

CCM chama.
 
Hao wote ndio waliokuwa wanaelezea kushindwa kuleta maendeleo kwa CCM na nyie mkawaita nyumbu.
Lakini CCM ikaona wana akili na kuamua kuwanunua kama wachezaji bora wanunuliwavyo Ulaya na kuwaacha UVCCM wanaendelea kulipiga vuvuzela.
CCM kuna mbumbumbu tu. Hata watafiti wanajua hilo
 
Naona huyu kada wa CCM na kijana mwenzao ameamua naye kuwapa soma hilo hapo chini;

Na Thadei Ole Mushi.

1. Kuwa Mwigizaji au Msanii Hakukunyimi kuwa na sifa za kuwa Kiongozi. Tena Mwigizaji anaweza kuwa Kiongozi mzuri. Kinachoangalia ni uwezo wake katika kufanya vitu. Nilisema wiki Chache hapa zilizopita ni vigumu Sana kufanya vetting kwa vijana wanaosifia tu kuanzia January hadi December. Watu wanahoji why Nick wa Pili lakini niwaambie Nick ni msomi mzuri Sana na ameshaonyesha kuwa ana kitu Cha Ziada.... Niliwahi kuandika kuhusu Chine's Meritocracy kuwa ili uwe Kiongozi angalau lazima uwe una kitu ulishakifanya Nick na Mchopanga kawapita wengi katika Hili tuwaacha tuwapime katika Majukumu. Hata Joket alivyoteuliwa mara ya kwanza watu walimtafsiri ndivyo sivyo...

2. Issue ya Uteuzi wa Rais ni kwamba Rais huangalia yupo comfortable kufanya Kazi na nani. Kumbukeni hawa ni wawakilishi wake..... Ukiachana na masuala ya Vetting Rais hupenda kufanya Kazi na watu anaoona kuwa hawa wanamfaa katika mazingira anayoyataka yeye. Hapa Kuna Utashi binafsi wa Rais....

3. Kuhusu Vijana wa Upinzani kuteuliwa ni jambo Zuri. Ni Kweli kwamba kwa siku za karibuni nimekuwa nikisema kuwa hawa vijana wanaotokea upande wa Pili wanapimika na Mara nyingi wapo Smart sana kuliko huku kwenye Jembe na Nyundo. Kitalu Chao kipo vizuri Sana na hapa ndipo HUWA nasema screening ya Vijana wa CCM Izingatie weledi sio Uchawa. Niliwahi kushauri kuwa CCM ianze kuchukua vijana walio machachari Kutoka vyuoni kama wanavyofanya Chadema badala ya kuwachukia na kuwaacha wakaangukia kwenye mikono ya Upinzani.

4. Kwa wale ambao BADO Wana matumaini ya kuwinda U DED na U DAS waanze kufikiria Kazi nyingine za kufanya. Ipo hivi Para A1 (21) ya Standing Orders ya 2009 kama kanuni za kudumu za Utumishi wa Umma........inasema "District Administrative Secretary" means a public servant in-charge of administration in a district; Ikimaanisha kuwa ni mtumishi wa umma atakayewajibika na shughuli za kiutawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya.....Kwa kifupi kabisa huyu ni mtumishi wa umma ambaye upatikanaji wa upo wazi kabisa. Mama SAMIA anaonekana kuwa mfuasi mzuri wa kanuni na Sheria za nchi. Hivyo kama haupo kwenye Utumishi wa Umma hadi sasa maana yake U-DAS na U- DED ushakupita..... Anza kutafuta Kazi nyingine ya kufanya kama Polepole anavyosema kwenye video hii

6. Angalau sasa Mwenyekiti na Katibu wa UVCCM wamegraduate toka ngazi Moja kwenda nyingine. Nimekuwa nikisema Sana kuhusu hii jumuiya kutoivisha viongozi watakaograduate kutoka level Moja kwenda nyingine nikifanya Comparison na Chama kikuu Cha Upinzani. Kwa Miaka kadhaa hawa vijana walikuwa baada ya Utumishi wao kwenye jumuiya ya Vijana walikuwa wakipoteza kabisa kwenye Ramani tunao kina Sadifa ambaye baada ya kusota Sana Juzi Juzi kakumbukwa Ila wenzake wa Upinzani aliokuwa nao walishafikia level za uwaziri, Beno Malisa na wengineo hawajulikani wapo wapi huku kina Katambi, Henge na wengineo wakigraduate. Haya ni mafanikio ya UVCCM inaanza angalau kuivisha viongozi wa Kutumika maeneo mengine.

6. Naongea Sana kuhusu Self Actualization kwa vijana. Taifa letu limekumbwa na pepo la kila Mtu kutaka kuitwa Mheshimiwa. Kwa mataifa mengine hasa yaliyoendelea vijana hawana thinking hiyo. Wengi Wana matamanio ya kutimiza Ndoto zao kwenye biashara, Kwenye fani walizosomea nk. Kama vijana wakilielewa Hili wanaweza kulisaidia Taifa vizuri zaidi kuliko kuwaza kuteuliwa. Na hapa ndipo ninapotaka wengi wadondoshe dhana ya UCHAWA wavae uhalisia wao na waonyeshe Wana vitu Gani vya Ziada.

7. Ni makosa makubwa kudhani kigezo Cha kuteuliwa ni Kumtukana Mbowe na Chadema au ni kuimba nyimbo za kampeni Sana, au ni kusifia Tu. Kuna mambo mengine ya msingi ambayo huangaliwa. Ndio maana unaona sura Mpya ambazo hazijawahi kusema hata CCM hoyee mahali.

8. Soon tutaanza kuona Sura halisi za watu, Expectations sasa zimeisha kabisa. Akili zitarudi kwenye fuvu la kichwa. Lilikuwa ni Suala la Muda tu.

Tufundishane Adabu

Ole Mushi
0712702602.
 
Ndio uzuri wa CCM freedom of opinion; jaribu kwenda kinyume cha Mbowe au viongozi wa vyama vingine uone shughuli yako

CCM Chama
 
Back
Top Bottom