Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Nimesoma andiko la rafiki yangu na mwanachama mwenzangu Ndugu Malisa GJ juu ya kile alichokiita:
"Pamoja na madhaifu mengi ya CCM na serikali yake lakini yapo machache ya kujifunza "
Kwa mujibu wa andiko la Ndugu Malisa, kati ya machache ya kujifunza ni pamoja na "utaratibu mzuri wa CCM kuandaa vijana". Pamoja na maswali mengi aliyoibua Malisa kwenye andiko lake swali lake kubwa ni Je, kwa sasa vyama vya upinzani vimewaandaa vijana gani kuchukua nafasi za viongozi waliopo? Kuanzia CHADEMA ,CUF ,ACT na NCCR-Mageuzi?
Kwa hiyo msingi mkuu wa andiko la Malisa kuhusu dhana ya kuwaandaa vijana kuwa viongozi wakubwa ndani ya chama ni wao kupata nafasi za uongozi sasa.
Nianze kwa kukubaliana naye kwa baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba, chama chochote cha siasa au taasisi yoyote ili iweze kukuza uwezo wake na muendelezo wa falsafa yake ni lazima iwe na mpango maalum wa kupokezana vijiti au majukumu kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Malisa anasema;
Kwamba chama kikongwe hapa nchini CCM kimewaandaa vizuri vijana wake akina Emmanuel Nchimbi, Antony Mtaka, Elibariki Kingu (mwanachama wa CHADEMA wa zamani), Antony Mavunde, Martin Shigela n.k.
Sijui kwa nini hakuwataja vijana kama Paul Makonda, Mrisho Gambo, Halima Bulembo, Zainabu Katimba, Asenga Abubakari (mwanachama wa zamani wa CHADEMA), Ally Salum Happy (ambaye amewahi kuwa CUF, CHADEMA na leo ni CCM), Humprey Polepole n.k.
Kwanza naomba kumfahamisha rafiki yangu Malisa yafuatayo;
1. Mwenyekiti wa sasa Wa CHADEMA Mh. Mbowe alikuwa Kiongozi wa Vijana CHADEMA. Amekulia na kulelewa kwenye chama.
2. Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr. Vincent Mashinji ni zao la kuandaa vijana tangu akiwa chuo kikuu. Amekulia kwenye chama na kulelewa katika harakati za mapambano ya mabadiliko. Hakuibuliwa tu kutokea hewani leo kuwa katika nafasi hiyo ya utendaji mkuu akingali umri wa ujana pia.
3. Manaibu Katibu Mkuu wote wawili, Salum Mwalim na John Mnyika ni vijana waliokulia ndani ya chama.
4. Kamati Kuu cha CHADEMA ni kamati kuu pekee iliyosheheni vijana kuliko chama chochote. Tazama composition yake Mwenyekiti wa BAVICHA, Wenyeviti wa Kanda za Chama, Wawakilishi 6 wa wabunge, wawakilishi 3 wa madiwani. Wote hao ni vijana ambao wamekulia na kulelewa ndani ya chama.
5. Secretariat ya CHADEMA inayoongozwa na Katibu Mkuu, robo tatu yao ni vijana tena wenye umri chini ya miaka 35. Wanaongoza kurugenzi za chama makao makuu.
Wengine wanaongoza idara nyeti japo bado ni vijana wadogo Mf; Tumaini Makene ambaye ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ally Hemed, Mkuu wa Idara ya Uenezi, wakiwa chini ya Mkurugenzi wao kijana John Mrema .
Ukienda Ofisi ya Katibu Mkuu wasaidizi wake wote wanne na wakuu wa Idara zilizoko ndani ya ofisi yake, ni vijana.
6. Waratibu /Makatibu wa kanda 10 za chama, 8 kati yao ni vijana , wahitimu wa vyuo vikuu wanaotokana na zao la CHASO ambayo iko chini ya BAVICHA.
Nao ni; Kanda ya Kusini- Frank Ngatunga, Kanda ya Nyasa -Emmanuel Masonga, Kanda ya Magharibi - General Kaduma, Kanda ya Victoria -Meshack Micus, Kanda ya Serengeti -Renatus Nzemo ambaye ameanzia kwenye uongozi wa BAVICHA nk.
Bila kusahau karibu ofisi zote za kanda maafisa wa kanda ni vijana na kila kanda ina maafisa wasiopungua wanne (04) .
9. Sehemu kubwa ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vijana ni kutoka vyama vya upinzani, tofauti kabisa na CCM.
10. Ktk chaguzi zote zilizopita, CHADEMA imeweza kusimamisha wagombea wengi vijana ktk uchaguzi mkuu. Maeneo mengi vijana wengi wazuri walikuwa wagombea wa CHADEMA/upinzani dhidi wa wazee kutoka chama tawala/CCM.
11. Lakini pia nadhani sio watu wengi wanajua Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Mh. Said Issa Mohamed alichaguliwa kwa mara ya kwanza kwenye nafasi hiyo mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 27 akiwa yuko mwaka wa pili Chuo Kikuu na hadi leo bado anahudumu nafasi hiyo kubwa kabisa kwenye chama akiwa bado kijana.
12. Hivi rafiki yangu Malisa anajua kuwa wale viongozi wote wa JUVCUF iliyokuwa inaongozwa na Katani Ahamed Katani 90% ni wabunge Mh. Katani akiwa Mbunge wa Tandahimba na aliyekuwa Makamu wake Mh. Kaiza Yusuph akiwa Mbunge wa CHAKE CHAKE na aliyekuwa Naibu Katibu wa JUVCUF bara ndio Mbunge wa Kinondoni leo? Na pia, Mwenyekiti wa sasa wa JUVCUF rafiki yangu Hamidu Bobal ni Mbunge wa Mchinga na kiongozi wa wabunge wa CUF bungeni .
13. Rafiki yangu Malisa anajua CHADEMA imeendelea kuwapa nafasi vijana kuongoza Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji mbalimbali kuwa wenyeviti au makamu wenyeviti ama mameya pamoja na ukweli kuwa wengine hawajawahi hata kuwa madiwani kabla lakini wameaminika na wamepewa nafasi na chama kuongoza. Nitatoa Mifano michache;
Wenyekiti wa Halmashauri za Tarime Mjini na Vijijini, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Serengeti, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rombo (pia hawa ni viongozi ktk chama/Bavicha katika maeneo yao). Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Charles ni kijana, Boniphace Jacob Meya wa Ubungo na Katibu wa Madiwani wa CHADEMA nchi nzima ni kijana, Meya wa Bukoba Chief Kalumna ni kijana, bila kusahau Naibu Meya wa Iringa Mjini (Mwenyekiti wa zamani wa BAVICHA Mkoa) na kule Moshi vijijini (Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa hadi sasa).
Wako wengi lakini hii ni mifano michache ya viongozi vijana wanaoaminiwa na chama na kupewa nafasi kubwa na nyeti ikiwa ni mwendelezo wa kuwakuza na kuwalea vijana kuwa viongozi na kupanda ngazi za uongozi, ingawa si kwa kigezo cha umri au ujana wao, bali uwezo wao na namna wanavyoweza kuaminiwa kuwa viongozi.
Ni vyema pia ikafahamika kuwa kwa CHADEMA hizo nafasi vijana hawa wamepewa kwa sababu ya uwezo wao na nia njema ya kuwajenga na kuwalea kiuongozi.
14 .Jambo lingine kubwa ni kwamba watanzania wanajua CHADEMA walianza kutambua na kuthamini mchango na uwezo wa vijana na kuwaamini kabla hata CCM hawajaanza kufanya hivyo. Ukiacha huko nyuma wakati wa chama kimoja tukianzia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995, rekodi zinaonyesha CHADEMA ilianza kuwapa fursa vijana toka zamani, kama akina Zitto Kabwe aliyeingia bungeni akiwa mbunge kijana zaidi mwenye umri mdogo, akina Halima Mdee, John Mnyika.
Leo hii wameongezeka bungeni tuna akina David Silinde, Joshua Nassary, Paschal Haonga, Susanne Maselle Makene, Yosepha Komba, Rhoda Kunchela, Upendo Peneza, Aida Khenani, Anatropia Theonesty, Julius Kalanga, Frank Mwakajoka, Peter Lijualikali, John Heche n.k ni mifano ya wabunge vijana kupitia CHADEMA.
Kwa hiyo ni wazi bado tunaendeleza utamaduni wa kulea vijana na kuwaandaa kuwa viongozi wa chama na ktk nafasi mabalimbali ndani ya Serikali.
Na ifahamike kwamba huko nyuma CCM walitumia bunge na vyombo vingine vya uwakilishi wa nchi kama taasisi ya watumishi wa umma waliostaafu na kufanya bunge kutawaliwa na wazee sehemu kubwa, kabla ya upinzani kufanya mapinduzi kwa kuwapa fursa vijana, ambao ndio wamekuwa chachu mkubwa ya mabadiliko ktk vyombo hivi.
Baada ya kukumbushana hayo, Malisa anisaidie haya;
Je kuandaa viongozi kunakofanywa na CCM, anakosema ni pamoja na;
1. Vijana wake kutumwa kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi wengine ndani ya chama chao kama walivyokuwa wakifanya akina Makonda, kwa Lowassa na hata kutumwa kumfanyia fujo Mzee Warioba. Na baadae kupewa madaraka makubwa? Au akina Mwampamba, Abubakari Asenga na Kimeta wa Mpui waliokuwa wanakesha kuwatukana matusi ya nguoni viongozi wa upinzani ambao ni sawa na wazazi wao? Ili wapewe zawadi ya vyeo walivyonavyo sasa?
2. Kutumia rushwa kwenye uchaguzi za ndani ili kupata madaraka ktk chama kama tulivyoshudia uchaguzi wao wa UVCCM uliopita?
3. Kuteuliwa kwa vijana wengi kuingia serikalini, kutoka CCM, nafasi ambazo vijana wa upinzani wanastahili lakini hawapati kwa sababu tu wako CHADEMA.
NB: Ni vyema pia ikafahamika, dhana ya kuandaa vijana kuwa viongozi wa baadae haiwezi kupimwa kwa vyeo na nafasi za juu serikalini walizonazo/wanazopewa tu bali twende zaidi ktk ushirikishwaji wao, mipango ya ndani ya kuwajengea uwezo, nk.
CHADEMA hatuwezi kujifunza CCM kugroom vijana, siku zote CCM wako nyuma yetu kwenye hili na wataendelea kuwa nyuma yetu kwa namna vijana tunavyoendelea kuaminiwa. Na Inawezekana kabisa kama Mh. Mbowe alikuwa kiongozi wa vijana na sasa ni Mwenyekiti wa Chama Taifa, haishindikani John Heche aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana na sasa ni Mbunge wa Tarime Vijijini na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti kuwa Mwenyekiti wa Chama hapo badae ama Deo Munishi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vijana baadae akawa Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje Hq, kabla ya kuteuliwa kuwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa chama, kuwa Katibu Mkuu hapo badae au kwa kijana kama Makene kuwa Mkurugenzi au Wakili John Mallya aliyeanza kama Mwanasheria wa BAVICHA na sasa Wakili wa Chama kushindwa kuwa Mkurugenzi wa Sheria wa chama hapo baadae.
Kwangu mimi, leo Chadema haiwezi eti kuanza kulinganishwa au kuwa ijifunze CCM kwa sababu tu ya uteuzi wa wagombea ubunge wa EALA ambao hata hivyo relatively walioteuliwa bado wanawakilisha umri wa ujana.
Lakini jambo la muhimu ni lazima vijana tukubali kuwa kuna ngazi ya kupanda katika kufikia ndoto kubwa za uongozi ndani ya chama na hadi serikali ambayo inahitaji uoneshe uwezo wako, dhamira yako isiyotiliwa shaka, imani yako kwa taasisi na zaidi kuzingatia misingi inayowaweka pamoja kwa sababu hatimaye mgawanyo wa majukumu unazingatia matabaka yote ya ujana, jinsi na masuala mengine muhimu.
Vile vile japo sijui exactly vigezo vilivyotumika kuwapata wabunge wa EALA bado naamini mchakato ulikuwa shirikishi kwa maana ya kilichoamuliwa kilikuwa na ushiriki wa Vijana ,Wanawake na wazee kupita Secretariet ya chama na kamati kuu kwasababu makatibu wao na Wenyeviti wa mabaraza ni wajumbe wa vikao hivyo muhimu kabisa vya chama.
NB:Nimeamua kutoa maoni yangu juu ya andiko la rafiki yangu Malisa japo kwa kuchelewa kwasababu nimeona mjadala huu bado unaendelea so nimeona sio mbaya nikatoa maoni yangu binafsi pia na haya ni maoni binafsi. Ahsante.