Vijana wa zamani tukutane hapa - old school

Jul 14, 2008
1,820
1,032
Enzi hizo ukienda Rungwe Oceanic Beach Resort ya Mzee Mwakitwange ulikuwa unakuitana na majina kama vile DJ Ngomely, DJ Pop Juice na wengine. Ukiosea jirani na hapo Rungwe, yaani Silver Sands, unakutana na kina John Peter Pantalakis, Choggy Sly na Kalikali ambaye baadaye alihamia YMCA.

Ukienda Africana ulikuwa huangalii simba aliyekuwa anafugwa hapo, bali pia DJ Mehboob, wakati ukishuka mjini hususan Motel Agip na baadaye New Africa hotel ghorofa ya saba kulikuwa na DJ Emperor (huyu Joseph Kusaga bosi wa Clouds 88.4 fmunaemjuea), Boniface kilosa a.k.a Bonny Love na DJ Jesse Malongo (wa Club Afrique, London).

Baadaye kidogo ikaja Space 1900 iliyoanzia hoteli ya Mbowe na kuhamia YMCA, na kuleta ushindani mkubwa kwenye fani ya muziki ambapo disko lilifunika kabisa muziki wa dansa. Vile vile ikazuka New Vision ambako DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee na Joe Johnson Holela walitengeneza majina sio kawaida, huku wakimpa darasa DJ Young Millionaire ambaye sasa anatamba Star TV ya Mwanza akiwa na jina lake halisi ya Jacob Msungu, kwenye kipindi chake cha TV cha Roving DJ.Baada ya Space 1900 discotheque kuhamia YMCA, disko la RSVP Discotheque likazaliwa Mbowe na Ma DJ wake walikuwa mkongwe Saidi Mknadara a.k.a DJ Seydou, akisaidiana na DJ Yaphet Kotto.

Kwa ufupi, pamoja na kwamba DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis wa hoteli ya Keys mtaa wa Uhuru walikuwa juu kwa vyombo vya kwanza vya kisasa vya disko, lakini ni DJ Seydou na DJ Yaphet Kotto ambao ndio walikuwa vinara pale RSVP Mbowe. Yaani baada ya kuruka majoka kila sehemu uijuayo, lakini vijana wote wa Dar walikuwa wanakwenda Mbowe kumalizia usiku kwa DJ Seydou na DJ Kotto.Kwa ufupi huyu ndiye aliyekuwa baba wa disko Dar, sio pekee kwa uwezo usio wa kawaida wa kupanga muziki tu bali pia ngekewa ya kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote nchini.

Kwa hisani ya: MATUKIO UK: NAWAKILISHA ENZI YA MIAKA YA THEMANINI (OLD SCHOOL)

My take:

Enzi hizo miaka ya 1983-1985 nilikuwa Kibaha High School (Enzi hizo tunakula Kuku na wali). na kisha JKT Ruvu. Tulikuwa kila weekend tunakuja Down Town na akina Ray Bagenda (Nadhani yuko ardhi sasa). Sometimes tunaanza Boogie (Disko la Mchana hadi majogoo.) Mbowe Hotels, YMCA; Rungwe Oceanic; Silversends, Msasani Club nk wanahusika.

Mabingwa wa Kudance wakati huo: Akina Black Moses (RIP) and the likes. Arusha Cave Disco ilikuwa ni hatari kwa kwenda mbele.
  1. Tuambie wewe enzi za ujana wako ulikuwa wapi na unakumbuka nini?
  2. Na Je; sasa hivi ma-DJ wetu hawa waliovuma wako wapi na wanafanya nini?
  3. Rafiki zako wa Ujana wako wapi na wanafanya nini?
  4. Na vipi Madisco ya Darasa la 7 enzi hizo? Secondari? High School? Vyuo? Graduation? Freshers ball? Tiririka . . . .
Karibuni tukumbushane
 
Source: MATUKIO UK: NAWAKILISHA ENZI YA MIAKA YA THEMANINI (OLD SCHOOL)

DJ Seydou alianza shughuli hizi pale Sea View enzi za Sansui miaka ya katikati 70…akipewa muda mfupi sana kwani enzi hizo Afro 70, Safari Trippers walikuwa ndio ngome ya jiji ktk muziki. Maneno yote yalikuwa Princess pale mnazi mmoja.

Nakumbuka mwaka 1980 Dj Seydou akishirikiana na Eddy Sally na Choggy Sly walianzisha disco pale Key’s Hotel hapo mjomba hakuna YMCA wala Msasani isipokuwa Mbowe Dj akiwa Gerry Kotto (sio Yafet Kotto), Africana na Seaview.

Nakumbuka walifanya mashindano ya kucheza na mshindi alikuwa Golden hair (Abdallah) na Mosi Ally yule mkimbiaji wetu wa mita 100.

Mwkaa mmoja tu walisambaratika! Choggy na Eddy Sally walikwenda Silversand na Seydou pamoja na Gerry Kotto waliungana kuunda kikundio kipya cha Space 1900 pale YMCA. Hapo ndipo Joe Janson na Kalikali walikuja ibuka hata ilipofika mwaka 1982, Space 1900 walihamia Mbowe. Kule YMCA wakawa wanapiga disco la mchana kwa vijana wadogo. Space wakafungua tena sehemu mbili New Africa na huko Moshi pale YMCA ama Moshi Hotel..

Mwaka 1982 kweli madisco yalifunika kabisa miziki ya magita!.Msasani, Rungwe, Slversand,Italian club (clouds), Keys Hotel, Motel Agip, New Africa, Twiga Hotel, Dar Institute na sehemu nyingine kibao ambazo siwezi kuzimaliza.

Seydou alikuwepo Mbowe hadi 1985 wakati Freeman alipoamua kufungua RSVP kuwaondoa Space 1900 ambao walihamishia makazi yao sewhemu mbili New Africa Hotel na Pale Maggot.

Toka wakati huo Seydou hakuwa na mahala maalum kwani Space 1900 ilivunjika kutokana na matatizo ya ndani. Hata hivyo jina Space 1900 liliendelea kutumika na ndio vijana wengine akina Super Deo,Young Millionea wakaibuka.
 
Fidelis Tungaraza:

Mlionitangulia asanteni kwa michango yenu. Nami naomba nichangie kwa sababu disco era ndiyo ulikuwa wakati wa ujana wangu. Na ndiyo kilikuwa kipindi cha disco haswa kuanzia New York (Saturday Night Fever). Kati ya mwaka 1978 na 1985 baada ya hapo Break Dance baada ya Break Dance sijui la kusema…Safu ya Madj wa wakati huo kwa ninaowakumbuka miye walikuwa kina Justin Kussaga (SANSUI hadi BIRIBI/CLOUDS toka Sea View mpaka Italian Club).

Eddy Sally(FM Disco), Gerald-Gerry Kotto- (Mbowe au kwa jina la utani wa wakati huo CHOONI), John Bure(Rungwe), Mehboo na Clemency/t?(Gogo Disco na Floating Bar, Africana), Abby Sykes(Blowout Disco, YMCA), Ebonite WooJack(Uptown, Disco YMCA)baada ya haya madisco mawili ndipo Sudi Mwarabu akaleta Space 1900 YMCA, Madj Gerry Kotto na Seydou.

Madj hawa wawili walikuja na staili mpya kabisa ya kupiga chapati (santuri) na dawa za mbu (kanda) huku wakidansi behind the Dj desk. Kwa mtakao kuwa mnakumbuka mtakumbuka ndiyo waliokuwa madj wliokuwa wanachoreography dansi zao na wanaovaa sare ya kazi maovaroli. Jamaa walikuwa watamu sana.Ok Tuendelee, Msasani Beach lilikuwepo disco la Marehemu? Nassoro Born City (Nasikia alifariki mwaka jana sina uhakika).

Hapa ndiyo walipoingia kina Choggy na John Peter na baadaye Nigger J na Kalikali. Au siyo?Kama sijakosea mwaka 1982 au 83 likavuma JeSet Disco na Dj Rusual na Baadaye Young Omar, Msasani Beach Club. Ninaweza kusema mpaka sasa hivi katika historia ya burudani ya muziki hakuna disko wala bendi lililowahi kutengeneza matangazo makali kama JetSet Disco. Kwa mnaokumbuka mtaweza kukubaliana nami. Nadhani kazi ile ya matangazo ilikuwa ni ubunifu wa Mzee Fred Jimmy Mdoe na mwenziye Bwana Bakari Omari.

Jet Set hawakuwa na miziki mizuri lakini walijua kutengeneza aina ya wateja na mashabiki.Wakati wote huo Princess hotel kulikuwa na Parliament Disco la kina Joe na Eddo. Nilichokuwa nakizimia Parliament Disco ni mafunk beat waliyokuwa wanayabaruza. Halafu lilikuwa disko la watoto wa mjini sina maana mbaya katika hili lakini lilikuwa ni disco la watoto wa mjini kwa maana ya watoto wa mjini kweli.Bila kusahau Pango Disco, Rex Hotel Clock Tower na lile la Continental Hotel, Nkrumah Street.

Zama ninayoizungumzia hapa mahoteli ya ukanda wa pwani ulikuwa bado umeshikwa na mabendi isipokuwa Rungwe Oceanic kwa Dj John Bure.Yakaja madisko ya maghorofani Motel Agip na New Africa Hotel. Madisko haya ndiyo yaliyokuwa ya mwisho mwisho na wateja wake zaidi walikuwa vijana wapya wapya, sina maana mbaya kwa kuwaita wapya wapya. Walikuwa wapya kwa sababu hawakuwa maaluatani wa jiji wengi wao walitokea mitaa ya ushuani na attitude za kiushuani.

Kweli si kweli?Bendi zilizotamba wakati huo: Brass Construction, Con Funk Shun, Earth, Wind, and Fire, The Isley Brothers, The Jacksons, Osibisa, Ross Royce, Soul Brothers, Lakeside, Kool and the Gang, Commodores, Orchestre Veve, Super Mazembe, Le Mangelepa, TP Ok Jazz, The Parliament, Fela Ransome Kuti and Afro 70, Simba Wanyika, The Wagadugu, Bunny Mack, Third World, Zappow. Jamani, nisaidieni nimezeeka kumbukumbu inavia.

Madisko ya wakati huo miziki ilikuwa mchanganyiko lakini miziki ya Kimarekani ilikuwa ndiyo inatawala.Mziki iliyotamba You can do it, Kulukuni, Moni afinda, Shakala, Sina makosa, Let me love you, Sweet mother, Easy dance, Ladies night, Sail on, Why you wanna try me, You give me fever(Love to love you darling), What you waiting for, Shake your body down to the ground, Lift up the roof, Holding on, Love’s got me dancing on the floor,This is reggae music, Night fever, Staying alive, na mingineyo mingi.

Kwa kifupi kamaliza yote, “BC” mnatukumbusha mbali sana, kumbukumbu zenye kuleta furaha, na zile za majonzi kwa wakati ule “nilivyokuwa natoroka nyumbani kwenda Disko, mfukoni nikiwa na pesa ya kiingilio tu, sina pesa ya soda na wala sijui nitarudi vipi nyumbani” na nikifanikiwa kurudi nyumbani kwa kudandia lifti za washikaji, najitayarisha kupokea viboko kutoka kwa wazazi.
Keep it up BC Mnafanya kazi ya Pongezi.JL
 
Bado katiba tu ili nchi hata akiondoka aiache pazuri la sivyo kitakuwa kama hao tu!
 
Kama Sikosei mwaka 1985 kuna mashindano ya disko kitaifa yalifanyika jijini Dar es Salaam na aliyeibuka mshindi alikuwa ni dada mmoja hivi mwanafunzi wa sekondari ambaye baba yake alikuwa ni baharia. Baada ya ushindi huo walimu wake shuleni na wanafunzi wenzie wakawa wanamzonga kila mara hali iliyomfedhehesha sana na hatimaye akaamua kujiua. Mwenye kumbukumbu nzuri kuhusu tukio hilo atujuze.
 
Kama Sikosei mwaka 1985 kuna mashindano ya disko kitaifa yalifanyika jijini Dar es Salaam na aliyeibuka mshindi alikuwa ni dada mmoja hivi mwanafunzi wa sekondari ambaye baba yake alikuwa ni baharia. Baada ya ushindi huo walimu wake shuleni na wanafunzi wenzie wakawa wanamzonga kila mara hali iliyomfedhehesha sana na hatimaye akaamua kujiua. Mwenye kumbukumbu nzuri kuhusu tukio hilo atujuze.

Duuh wakati huo mimi niko JKT. Bila shaka Vijana wa zamani wa Kitaa watatukumbusha zaidi . . .
 
Dah......enzi hizo nikiwa relwe Tabora.......jamaa yangu Filipo akaniacha akahamia RTC Kagera.......kipindi ndio ule wimbo wa Sisily umetoka......acha kabisa......
Sisili mama yeye x 2, Sisili monamu mamaa, mpenzi wangu ninakupenda mimi na wee pamoja nayo motema...... umshikeshike!....fafashimoya mama!..Sisili....umkamate, fafashimoya mamaa! Sisili...(Moni Mambo akiwa na Orchestra Shikashika). Aaaah aah.
 
mimi wa shamba unanikumbusha kanda za utumbo nilipokuja kwa mjomba miaka hiyo, disko tulienda donbosko (tuliita hivyo) dj alikuwa marlon, na kibonde sijui alikuwa anahusika nn alikuwa anaharibu tu mziki na uniform zake za kino muslim!
disko lilikuwa la kufana nashangaa hujakutaja huko!
 
mimi wa shamba unanikumbusha kanda za utumbo nilipokuja kwa mjomba miaka hiyo, disko tulienda donbosko (tuliita hivyo) dj alikuwa marlon, na kibonde sijui alikuwa anahusika nn alikuwa anaharibu tu mziki na uniform zake za kino muslim!
disko lilikuwa la kufana nashangaa hujakutaja huko!


Haaaaa haaaaa umenifanya nicheke sana.

Mkuu, sikuwa mtu wa Kiwanja kihivyooo . . . .

Wapi Le-Mutuz . . . W. J. Malecela ?
 
Back
Top Bottom