Vijana wa kisasa wa Kiafrika!

Vijana wa kisasa wa Kiafrika!

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,038
Katika jamii ya sasa, vijana wengi wanakosa mwelekeo na thamani, na hili linaweza kuathiri jamii nzima. Kama kizazi hiki hakitapewa uangalizi na mwongozo, tunaweza kujikuta na kizazi kilichopoteza mwelekeo, hata kabla ya kufika kaburini.

Vijana wanavua ndoto kwa kubeti, wakitegemea bahati badala ya juhudi na uvumilivu.Wafanyabiashara wanajua mbinu za kuhamasisha, wanajua vijana wanapenda mafanikio ya haraka, na hivyo wanakuza biashara ya kubeti kwa njia ambazo haziweki wazi hatari zinazohusiana nazo.
  • Vijana wanabugia visungura baada ya kubeti, wakitafuta faraja kwa pombe, lakini wanajua fika kuwa wanajenga majeraha kwa afya zao.
  • Vijana wanavuta shisha wakifikiri wanajifurahisha, lakini wanashindwa kuona athari zinazozidi kutengeneza vidonda kwenye mapafu yao.
  • Mademu wanajikuta kwenye mtindo wa umalaya, wakiona njia rahisi ya kujipatia mali au upendo, lakini wanajenga vidonda vya kiroho na kimwili kwa kila hatua wanayochukua.

Vijana hawajali chochote, na kama kizazi hiki kisiposimamiwa vizuri, tutajikuta na kizazi bora zaidi kaburini kuliko kizazi cha sasa kinachoishi.
 
Usilaumu sana Vijana.
Sera pia za serikali zinatuangamiza.

Zuia bettings sites kama ilivyofanya kwa Porn.
Zuia Vinywaj hivi vya spirit vinavyouzwa bei rahisi rahisi.
Au weka tozo kubwa ya kodi kwenye hizo spirit.

Tengeneza mazingira rafik kwa wajasiriamali.
Futa kodi kwa viwanda vipya vya wazawa atleast kwa miaka 5.
Watoe ruzuku zaidi kwenye pembejeo za Kilimo.
Watoe ujuzi kwa wafugaji wakubwa na wadogo.
Huduma za afya kwa watoto na wazee itokewe bure kupunguza gharama ya hawa wategemezi.

Matokeo yanaweza yasionekane mapema ila in a long run tutaishinda vita umasikini huu wa mtu mmoja mmoja.
 
Una hoja ya msingi ,natamani usikilizwe ,jamii hii yetu sote
 
Kusema kweli watu wamekata tamaa, kuna Lundo la vijana lukuki 30+ hawawazi hata kuoa maana uchumi hauruhusu (sio kisingizio ndio uhalisia)
Waliooa nao very miserable, maana hustling wanayofanya kumaintain maisha hapa mjini ni ngumu sana kuliko hata wazee wao waliyopitia, on top of that wengi wao wake zao wamekengeuka na utandawazi hivyo stress za vijana ni kama vile "zimewapakia mkongo"
Asilimia kubwa ya vijana hili Jiji hawana hata matumaini ya kujenga na kumiliki makazi yao wenyewe
 
Ndio Mtaji Wao Haswa Ni Hao Vijana Wajinga,,,Maskini Na Wenye Maradhi Yatokanayo Na Matumizi Ya Hivyo Vilevi Hovyo/Mavi,,,Ikiambatana Na Matendo Hovyo Katika Jamii Wengi Wamekwisha Jikatia Tamaa Na Hakuna Anaejali Maangamizo Hayo Wanawatumia Kama Toileti Kujinufaisha Alafu Wanatupwa,,Kujitambua Kifikra Ni Jambo La Msingi Lakini Nadhani Wengi Wao Either Ni Bendera Fuataupepo,,Or Njaa Ikihamia Kichwani Ni Hatari Zaidi Ustawi Wa Kifikra Au Wengi Wao Wana Uovyo Wa Mazingira,,,Marithisho Na Kimakuzi,,Mabadiliko Yaanzie Ngazi Za Familia Lakini Ukiangalia Kwa Sasa Mambo Shaghalabagala Kwa Familia Nyingi Lazima Tupate Kizazi Cha Nyakati Na Chakushangaza.
 
Kusema kweli watu wamekata tamaa, kuna Lundo la vijana lukuki 30+ hawawazi hata kuoa maana uchumi hauruhusu (sio kisingizio ndio uhalisia)
Waliooa nao very miserable, maana hustling wanayofanya kumaintain maisha hapa mjini ni ngumu sana kuliko hata wazee wao waliyopitia, on top of that wengi wao wake zao wamekengeuka na utandawazi hivyo stress za vijana ni kama vile "zimewapakia mkongo"
Asilimia kubwa ya vijana hili Jiji hawana hata matumaini ya kujenga na kumiliki makazi yao wenyewe
Ni kweli kabisa,linahitaji discussion ya kitaifa
 
Back
Top Bottom