Vijana wa Arusha: Ukiisaliti CHADEMA utapigwa tu!

Vijana wa Arusha: Ukiisaliti CHADEMA utapigwa tu!

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Kwenye pita pita yangu nilikutana na vijana wa jiji la Arusha mmoja akasema...
"Ukikisaliti CHADEMA utapigwa tu, na mimi nasema wapigwe tu maana sasa tumechoka"

Kauli hii ilinifanya nicheke maana ina fanana na ile aliyo wahi kutoa Mtoto wa mkulima kwenda WAKULIMA MASKINI.

Niliitafakari sana kauli ya vijana wale na nikajikuta nachambua mantiki ya kauli ile kwa kuangalia hatua ambayo wanachama, mashabiki na wapenzi wa CHADEMA wamekuwa wakipitia mara kadhaa kwenye harakati za chama chao kwa kuangalia uhalisia wa mambo yafuatayo.

1. Kuna watu wameuwawa kwa sababu ya kupigania mabadiliko kupitia chadema. Hawa wamekutwa na mauti kwenye harakati za chama. Makaburi yao yamejikuta hayaoti hata nyasi za matumaini.

2. Kuna watu wamekuwa vilema kwa sababu ya kuipigania chadema. Hawakuwa vilema kwa kupenda ila wanao ogopa mabadiliko ndio wamesababisha vilema hivyo. Hawa hawawezi tena hata kukimbizana na maisha ili wajitoe kwenye umaskini kama walikuwa na ndoto hiyo.

3. Kuna kina mama wamekuwa wajane kwa sababu waume zao wamesimama daima kupigania mabadiliko kupitia chadema. Waume zao wakauwawa aidha kwa mabomu au risasi. Baadhi huenda wameamua kufanya ukahaba au kufanya biashara nyinge haramu.

4. Kuna watoto ambao sasa niyatima kwa sababu wazazi/mzazi wake amepigania mabadiliko kupitia chadema. Akaishia kuuwawa. Mwisho wake anaweza kuwa chokoraa au mtoto wa mtaani asiye na ndoto tena zinazo anzia kwa mzazi.

5. Kuna wazazi wamepoteza watoto kwa sababu watoto hao walipenda kuhudhuria na kusikia maneno ya ukombozi ya viongozi wa chadema lakini mwisho wao ukawa kupigwa mabomu na rasisi. Huenda moja ya wazazi hawa walipata mtoto kwa maumivu makubwa au hawana kizazi tena!

6. Kuna watu wamefilisika kwa kuwa mfumo haukupenda kuona watu hao wanasaidia harakati za mabadiliko kupitia upinzani. Biashara zao zikafungwa au kuwekewa mizengwe. Zikafa! Hawa huenda hawamudu kuwasomesha watoto au kumudu angalau kuhudumia familia zao.

7. Kuna watu wameathiliwa na mfumo wa wizi, rushwa na ufisadi. Tumaini lao ni chadema kuona mfumo huo una unaondoka. Kukisaliti chadema ni kusaliti matumaini yao, ni kuuwa ndoto zao.

8. Kwa kuwa mabadiliko ni mpango wa Mungu, kuna watu tumaini kuwa CHADEMA kinakuja kuleta mabadiliko makubwa katika nchi hii. Tunao amini kuwa mabadiliko ni mpango wa Mungu na si shetani tunaamini kuwa ukisaliti harakati za mabadiliko una saliti mpango wa Mungu. Kwa maana hiyo uko kinyume na mapenzi ya Mungu, Unapingana na Mungu!

9. Dhambi kubwa kwenye mapambano ya haki na ukombozi ni usaliti! Ni heri msaliti mmoja afe kuliko kusaliti na kuuwa ndoto na matumaini ya mamilioni ya watu kwa kile wanacho kitumaini tena kilicho piganiwa na kujengwa kwa jasho na damu kwa miaka mingi.

10. Kumuadhibu msaliti kwa kipigo ni kupeleka ujumbe wenye mwangwi mkali kwa wasaliti wengine wanao panga kurudisha nyuma harakati za kumng'oa mkoloni mweusi. CHADEMA ilipofikia leo ikidhoofishwa na wasaliti. Itachukua zaidi ya miaka mingine 20 kupatikana chama kingine kitakacho kuwa na nguvu ya kukua na kuimarika kama kilivyo CHADEMA leo.

Kila mpenda mabadiliko ambaye kimsingi atakuwa anatimiza mapenzi ya Mungu, ni wakati wake kuhakikisha kuwa harakati za ukombozi na maendeleo kwenye nchi yetu hazirudishwi nyuma na wasaliti. Kuruhusu msaliti akwaze harakati za ukombozi na mabadiliko ni kuenenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Ni kutenda dhambi ya kuua ndoto na matumaini.

Moyo unao ishi bila ndoto na matumaini mahali pake ni makaburini. Ni afadhari msaliti apigwe kuliko aachwe auwe ndoto na matumaini ya mamilioni ya watanzania kwa kile wanacho kiamini, na mimi nasema "WAPIGWE TU"
 
Kwa Tanzania usaliti kwa sehemu nyingine inaonekana kama 'fashion' tu na ndio maana hata wengine wanajitangaza hadharani kwa kuufanya. Nimeangali mdahalo wa jana (Jumapili 26/10/2013) Serena Hotel juu ya Katiba, mzee mmoja anasema Watanganyika tumekuwa hivi kwa sababu tulipata uhuru wetu bila kuupigania kikamilifu hivi wengi hawajui maana ya kuwa huru au kutokuwa huru.
Kama hawa vijana kweli wameamua kuja na hii njia, basi hii inaweza kurudisha heshima ya chama na nchi kwa ujumla wake kwa maana hakuna anayelazimishwa kujiunga na chama ili baadae alazimishe usaliti.
 
Mkuu na kubaliana na wewe kimsingi kwamba wasaliti waadhibiwe ila ninapendekeza kwa heshma ya CHAMA ambacho kimsingi kwa sasa ndiyo chama halali cha Kisiasa kwani kingine nadhani mmesikia hata mwenyekiti wake amewagombeza na kuwaasa waache kucheza na kuimbaimba jukwaani (NYIMBO ZA AKINA WALETE TUWACHANECHANE TU WATUPE) bali waende chini vijijini wakakutane na wananchi na kujua matatizo yanayowasibu (KAMA AMBAVYO CHADEMA INAFANYA) kwani kwasasa watanzania wanachaguo lingine (AMINI USIAMINI HAPA ALIMAANISHA CHADEMA) japo hakusema wazi .Tuna shauri Uongozi kuhakikisha kwamba wakosaji wachunguzwe na kuadhibiwa kwamujibu wa Katiba ya Chama ili kuwaonesha watanzania tofauti ya ( akina wapigwe tu BUNGENI ) na nguvu ya UMA.

UWEKWE UTARATIBU MAKINI WAKICHAMA WAKUWASHUGHULIKIA WAHUSIKA WAMAKOSA HAYA NA KUWAVUA UANACHAMA SIYO UONGOPZI TU NA KUWATANGAZA KUWA MAADUI WA MAGEUZI NA WASALITI WA JITIHADA ZA UKOMBOZI WA WATANZANIA.

CHADEMA ni chama bora kabisa cha upinzani Afrika kwa hiyo lazima katika kushughulikia matatizo yake basi hatua zake zilingane na sifa za kichama na ionekana siyo tu kwamba haki inatendeka bali ikitendeka kwa mujibu na uzito wa kosa husika
 
naona jahazi la cdm linazama, cdm ni chama pekee ambacho ukijifanya kuuliza maswali ya msingi unaitwa msaliti, ukitaka kufanikiwa chadema, wewe kuwa msukule tu, hakuna haki ya kuulizana, walioko juu ndio Miungu watu wengine kazi yao ni kuandamana...
 
nyie toaneni ngeu wenzenu wakizidi kujenga mahekalu na makasri huko ulaya.............
nonsense.
ptuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!
 
Na wapigwe tu, jitu zima kiongoz la chama lenye uwezo wa kusema hoja zake ndani ya vikao halali linanaleta usnitch kwenye mitandao then tulionee haya?!! Chadema ipo katika point of no return, kama unaona huwezani na kasi yetu ruka nje ukafie mbele usitutie majaribun tukakuangamiza, HII NI CHADEMA SIO CHAMA CHA MASHOGA........NA WAPIGWE TU
 
Ipo wapi demokrasia ndani ya Chadema.

Demokrasia yao ni ya kupiga wenzao kisa wanahoji mambo yahusuyo chama.
hawa mashua yao imeshazama tayari.......................

tuwaache wazikane wenyewe sie tuendeleze juhudi za kuhakikisha kwamba LOWASSA anachukua nchi mwaka 2015.
 
Tofautisha kupinga na kusaliti! Kuna tofauti kubwa kati ya kupinga na kusaliti. Mtoto wa darasa la kwanza shule ya kata anaweza kukusaidia hili.
Huyo mtoto hapa JF hayupo mkuu embu tusaidie tafsiri yenu ya kupinga na usaliti maana tunayoifahamu sisi siyo mnayokuja nayo sasa, please by using chadema's dictionary tufafanulie mkuu
 
Mkuu kupiga watu ndiyo uchambuzi makini? Siku mkichukuwa dola wale wote ambao watakawapinga si mtawauwa wote.
Ok, kwa sasa ni wazi suluhisho la wengi wetu ni kupigwa tu, ...'na wapigwe' -PM
Lakini kipi ni bora, kumpiga mwananchi anayedai kujua rasilimali za umma zimetumikaje au mnafiki aliyehama chama baada ya kupewa 'mtaji wa duka' alafu akaanza kusimama majukwaani akisema hicho chama ni magaidi huku akijua anazusha!?
 
Back
Top Bottom