Vijana wa Afrika waipa somo Marekani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
微信图片_20220628112635.png

Inawezekana kuwa wengi wanakumbuka kuwa Oktoba mwaka jana, vyombo vya habari vya Zimbabwe vilifichua kwamba ubalozi wa Marekani nchini humo uliwalipa waandishi wa habari wa nchi hiyo kuchapisha ripoti za kuchafua sura ya China kwa bei ya dola za Marekani 1,000 kwa kila makala, jambo ambalo lilizua taharuki kubwa. Huku hisia ya uwepo wa Marekani barani Afrika ikipungua zaidi katika miaka ya hivi karibuni, shughuli za kuupaka matope uhusiano kati ya China na Afrika kwa kiasi kidogo cha fedha kama hatua hii zimekuwa moja ya njia zenye gharama nafuu. Hata hivyo, hali halisi ni kuwa mbinu chafu za Marekani zimetambuliwa ipasavyo. Hivi majuzi, matokeo ya utafiti mpya uliofanywa na taasisi ya Ichikowitz Family Foundation yenye makao makuu mjini Johannesburg, Afrika Kusini yanaonyesha kwamba katika macho ya vijana wa Afrika, China imeipita Marekani na kuwa nchi yenye ushawishi chanya zaidi barani humo.

Utafiti huo uliwashirikisha vijana 4,507 wenye umri wa miaka 18 hadi 24 katika nchi 15 za Afrika, ambapo 76% yao wanaona China ni nchi ya nje ya Afrika inayoonesha athari nzuri zaidi katika maisha yao, wakati ushawishi huu wa Marekani ukishuka kutoka 83 % ya mwaka 2020 hadi 72% ya leo. Mwenyekiti wa taasisi hiyo Ivor Ichikowitz alisema, "Marekani imekuwa ikitoa kauli za kuikashfu China kwa kuzuia ukuaji na maendeleo ya Afrika, lakini maoni ya vijana wa Afrika ni kinyume kabisa." Matokeo haya si yasiyotarajiwa, na yanaendana na mambo mawili halisi: kile ambacho China inafanya barani Afrika kinatambuliwa vizuri na wenyeji, hasa vijana; waafrika wamechoshwa na sera ya mambo ya nje ya Marekani ya "umwamba" na "ahadi hewa" inazotoa mara kwa mara kwa Afrika.

Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa sababu kuu zinazowafanya vijana wa Afrika waliohojiwa kuamini kuwa China ina ushawishi chanya zaidi katika bara la Afrika ni hizi zifuatazo: China imejenga miundombinu mingi barani Afrika, China imesafirisha bidhaa zenye ubora wa juu na bei nafuu barani Afrika, na China imetengeneza nafasi nyingi za ajira kwa watu wa Afrika. Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, China imekuwa mdau muhimu katika ujenzi wa miundombinu barani Afrika. Jengo refu zaidi barani Afrika, kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha umeme kwa maji barani Afrika, reli ya kwanza ya kisasa inayotumia umeme barani Afrika.

Miradi mingi maarufu ya kiujenzi katika nchi nyingi za Afrika imejengwa na China. Wakati huo huo, kutoka simu za mikononi hadi paneli za jua na vitu vinavyotumiwa kila siku, "Made in China" imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya kila Mwafrika. Wakati nchi za Magharibi zikiiona Afrika kama ghala la rasilimali za madini, China inawawezesha watu wa Afrika kuwa watumiaji. Vilevile utafiti huru umeonesha kuwa 89% ya wafanyakazi wa kawaida na 44% ya wasimamizi katika makampuni ya China barani Afrika ni wafanyakazi wazawa.

Hata hivyo, baadhi ya watu nchini Marekani wanahusisha kudorora kwa ushawishi chanya wa Marekani barani Afrika na hali kwamba Marekani imepuuza ongezeko la nguvu za taifa la China kutokana na operesheni za kijeshi katika Mashariki ya Kati katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, na kuiruhusu China kutumia fursa hizo za kimkakati kupanua ushawishi wake barani Afrika. Hebu tujiulize, hata kama Marekani haijachochea mfululizo wa vita huko Mashariki ya Kati katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, je, inaweza kujihusisha katika uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kisasa ya Afrika? Kuleta Iraq au Afghanistan nyingine barani Afrika ni jambo linalowezekana. Zaidi ya hayo, kutoka mpango wa Obama wa "Power Africa", hadi mpango wa Trump wa "Prosper Africa" na kisha mpango wa Biden wa " Build Back Better World (B3W) ", inachokosea Marekani kwa Afrika sio mpango, bali ni utekelezaji.?

Katika suala la maendeleo ya Afrika, China imefanya kazi kubwa za kiujenzi, na hivyo kupata uungaji mkono wa watu wa Afrika, lakini Marekani haikufanya hivyo. Kama tovuti ya Capital FM ya Kenya inavyosema, “tofauti na kukandamizwa na mchezo wa ‘zero-sum’ unaoendeshwa na Marekani na washirika wake, mtazamo thabiti wa China wa kujitahidi kujenga dunia yenye haki na usawa zaidi unakaribishwa zaidi. Kauli mbiu ya China ya 'kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja na kuleta mafanikio kwa pamoja’ ni ‘injili’ mpya ya karne ya 21.”
 
Back
Top Bottom