Vijana tusio na ajira japo tumesoma, kura zetu tumpe nani?

Uzi wangu huu ni kwa wale vijana ambao tulipata nafasi ya kusoma hadi level kubwa kidogo. Hapa nazungumzia watu wenye certificate, diploma, bachelor, masters n.k. Kwa mtazamo wako na hali halisi ya maisha hapo ulipo unadhani ni kiongozi gani anaweza kukukufaa na kubadilisha maisha yako?

Mimi ni kijana mpambanaji tena nirudie kusema kuwa mimi ni "Mpambanaji". Maana ya upambanaji ni hali ya kujitoa kufanya kazi yoyote ile regardless ni ya taaluma yako au nje ya taaluma yako. Pamoja na kusoma kidogo hadi nikapata degree ni kwa sababu ya juhudi za wazazi wangu na kidogo juhudi za serikali.

Kwa sasa nipo mtaani bila ajira, nafanya kazi za uvuvi na kusaidia mafundi ujenzi. Serikali haikusema kuwa ukisomeshwa lazima uajiriwe. Watumishi wa serikali wanasema tujiajiri. Mama yangu kama mlezi wangu mkuu aliwahi kuuza ng'ombe wawili kwa thamani ya laki 3 ili nisome. Kibaya zaidi "Mama yangu hajawahi kula matunda yangu tofauti na pesa kidogo ya boom niliyokuwa nikimtumia sometimes".

Usuniulize kuhusu baba maana tunaweza kukosana. Pamoja na juhudi zote nifanyazo katika maisha kitu nilichofanikiwa kumiliki ni uwanja/kiwanja cha kujenga ambacho nacho nilikipata kwa mbinde hadi leo sina hakimiliki yake japo ni kiwanja changu.

CV YANGU KWA UFUPI:

Bachelor of Education in Arts
Best Radio Presenter
Fisher
Comedian
Song writer
Director
Msanifu maandishi
Fighter

Kura yetu tunampa nani?
Mpeni Magufuli
 
Mm nae ni Muhanga wa Ajira huu ni mwaka wetu tunatajwa na vyama vya upinzani chama tawala hakijatugusa basi wale wanao tutaja tutawachagua haswaa
 
Hakuna mtu atakayebadili maisha yako. Sio kiongozi, sio baba ako, sio mama ako wala sio nani ...wewe mwenyewe ni jukumu la maisha yako, amka Simama angalia fursa ingia field.

Thank me later

Kama ni hivyo wasitudanganye kwamba tutawaletea maisha mazuri...full stop
 
Mpe tena Magufuli, mwaka huu atajenga tena viwanda 8000 na ajira zitatoka milioni 6, sawa eeeeeeh
 
Back
Top Bottom