Vijana tuacheni kubeti, kindege (aviator) kimenimaliza milioni 7 yote ya mtaji

Achana na mawazo ya kujiua sio solution ya matatizo yako, ukipitia changamoto yeyote acha kabisa kuwaza kifo kama suluhu, huo ni udhaifu uliotukuka.

Kama mimi nilipitia hayo na nikavuka licha ya maumivu makali kwanini wewe ushindwe?

Uza simu anza upya tafuta cha kufanya kadri muda unavyoenda mambo yatakuwa sawa.

Epuka kuazima hela kwa watu na kuahidi kurejesha ukiwa na hiyo simu yenye uwezo wa kukufanya ucheze aviator, kwa sasa hata ukipewa hela utakimbilia kucheza tena(najua hili wengi watakataa/utakataa) ila nimepitia na ninajua kwa kuyaona kwa wengi. Jijenge mwenyewe taratibu taratibu na usifosi uazime hela usiomudu kurudisha, utajivunjia uaminifu na upo kwenye kipindi kigumu cha kusimama upya kuna muda utahitaji msaada na wakukusaidia ndio hao wanaokuamini, usiwapoteze.

Nakuandikia magazeti kwa sababu nimeyapitia haya na sipendi kuona mtu anayapitia naelewa maumivu yake.
Duuh...brother unanielewa sana.

Hii simu kweli kuendelea kuwa nayo nikipata pesa nitacheza tu, bora nisiwe nayo kwa sasa.
 
Najua nakosea Ila ndivyo ninavyo waona watu wanao beti

Huwa nawaona Kama hawako timamu na wavivu
Kwa mtazamo wako huenda ukawa sahihi.

Maana nakumbuka fainali ya world cup mwaka 2022 kati ARGENTINA na UFARANSA.

Msanii drake wa marekani alibeti dau la dolar milion moja (Tsh 2.3 bilion) na kumpa argentina ashinde.

Lakini kilichofata mechi ilitoka draw kwenye 90 minutes hivyo akapoteza tsh 2.3 bilion.

Ila kwake haikuwa shida maana ni sawa na alichukua 1000 katika laki akabetia.
 
Ninachoshukuru sijui kuendesha kindege, sijui kuzungusha lile tairi na wala sijui kucheza dubwi la mchina.

Ila kuna siku nimewahi kupoteza laki 2 kizembe sana ilikuwa 2020 kama sikosei.

Ni kupitia 1xbet nilikuwa nimebet football nikala.
Sasa ukatokea ujumbe kuwa naweza kudouble my winning, nikakubali.
Ukaja mchezo wa kupiga penalt halafu kuna goalkeeper anadaka.

Ninachokumbuka nilikula kama mara 2 tu, nyingine goalkeeper alikuwa anadaka na kutema hadi nikakauka kau.
 
Kama vile unaniona.

Ni aviator ya huko huko sportybet ndiyo iliyo nikausha.

Na kwenye mshahara kama vile wewe ndiyo ulikuwa mhasibu maana ni kule kule kwenye 400k.

Alafu kilichotokea sasa ni kwamba, nilipukutwa kutoka 7.5 milion ikabaki 2 milion.

Kindege kikaja kuachia nikarudisha pesa angu mpaka nikafika 5 milion, nikajisemea moyoni Mungu nisaidie nirudishe pesa yangu yote niliyoliwa bado 2.5 milion tu.

Kilichotokea baada ya hapo ni kwamba nilitoka kwenye 5 milion nikarudi kwenye zero milion.

Yaani shetani huyu mbwa ningekuwa na uwezo wa kumkamata namla mbichi mbichi bila kumchoma.

Future yangu naiona kabisa ndiyo nimeizikia hapa
Wenzako wanacheza kuondoa arosto tu, wewe unafanya kuwa ni kazi
 
Nashindwa kuwaambia jinsi nilivyojikatia tamaa kiasi cha kuwa kichaa.

Ila ninachoweza kuwaambia tu vijana wenzangu tuacheni kubeti kwa malengo kwamba tunapata pesa huko haraka haraka.

Fikiria nimefanya kazi ya kuajiriwa kwa miaka 8, nikafukuzwa kazi nikaenda NSSF nikachukua milion 7.5 niliyokuwa nakatwa alafu yote nimeimaliza kwenye kindege cha aviator ndani ya siku 5 tu.

Nahisi kuna roho flani iliniongoza kwa sababu kwa akili ya kawaida najiona siyo mimi.

Lengo ilikuwa kubetia elfu 50 kama mtaji wa kubetia lakini kilichofata ni kupoteza milion 7.5 zote bila kubaki hata mia ndani ya siku 5 tu.

Hapa nilipo I wish hata nijitoe roho tu maana sijui ni wapi naanzia maisha tena pesa yote nishaipoteza kwenye uraibu wa kamari.

Kila nikiwaza nna miaka 30, sijaoa, sina biashara yoyote niliyoisimamisha kunilinda, sina maisha, kwa kifupi hiyo milion 7.5 nilitegemea ndiyo niingie nayo mtaani inilinde.

Lakini shetani kanikamata na kunikanda kisawa sawa.

Najiona mjinga wa kiwango cha Phd ndiyo maana nimejiita Zero Brainer, sina wa kumlaumu ila tujiepushe sana na uraibu hasa wa kubeti.

Mimi naweza nikafa leo ila sitaki vijana wenzangu yaje yawakute yaliyonikuta mimi sasahivi.

Mimi hali nnayopitia sasa kwa sababu ya kubeti nakosa maneno ya kuwaelezea ila siku nikifa mjua KINDEGE cha AVIATOR kwenye kampuni ya kubeti ya SPORTYBET kimesababisha kifo changu .
weka ushahidi otherwise tutaita...

CHAI
 
Ninachoshukuru sijui kuendesha kindege, sijui kuzungusha lile tairi na wala sijui kucheza dubwi la mchina.

Ila kuna siku nimewahi kupoteza laki 2 kizembe sana ilikuwa 2020 kama sikosei.

Ni kupitia 1xbet nilikuwa nimebet football nikala.
Sasa ukatokea ujumbe kuwa naweza kudouble my winning, nikakubali.
Ukaja mchezo wa kupiga penalt halafu kuna goalkeeper anadaka.

Ninachokumbuka nilikula kama mara 2 tu, nyingine goalkeeper alikuwa anadaka na kutema hadi nikakauka kau.
FB_IMG_1709182982732.jpg
FB_IMG_1709182967949.jpg
 
Nashindwa kuwaambia jinsi nilivyojikatia tamaa kiasi cha kuwa kichaa.

Ila ninachoweza kuwaambia tu vijana wenzangu tuacheni kubeti kwa malengo kwamba tunapata pesa huko haraka haraka.

Fikiria nimefanya kazi ya kuajiriwa kwa miaka 8, nikafukuzwa kazi nikaenda NSSF nikachukua milion 7.5 niliyokuwa nakatwa alafu yote nimeimaliza kwenye kindege cha aviator ndani ya siku 5 tu.

Nahisi kuna roho flani iliniongoza kwa sababu kwa akili ya kawaida najiona siyo mimi.

Lengo ilikuwa kubetia elfu 50 kama mtaji wa kubetia lakini kilichofata ni kupoteza milion 7.5 zote bila kubaki hata mia ndani ya siku 5 tu.

Hapa nilipo I wish hata nijitoe roho tu maana sijui ni wapi naanzia maisha tena pesa yote nishaipoteza kwenye uraibu wa kamari.

Kila nikiwaza nna miaka 30, sijaoa, sina biashara yoyote niliyoisimamisha kunilinda, sina maisha, kwa kifupi hiyo milion 7.5 nilitegemea ndiyo niingie nayo mtaani inilinde.

Lakini shetani kanikamata na kunikanda kisawa sawa.

Najiona mjinga wa kiwango cha Phd ndiyo maana nimejiita Zero Brainer, sina wa kumlaumu ila tujiepushe sana na uraibu hasa wa kubeti.

Mimi naweza nikafa leo ila sitaki vijana wenzangu yaje yawakute yaliyonikuta mimi sasahivi.

Mimi hali nnayopitia sasa kwa sababu ya kubeti nakosa maneno ya kuwaelezea ila siku nikifa mjua KINDEGE cha AVIATOR kwenye kampuni ya kubeti ya SPORTYBET kimesababisha kifo changu .
Nachokushauri siku yoyote ukapitia changamoto usiwaze kujitoa uhai!hilo ni moja kingine katika maisha kuna kujaribu hivyo na wewe ulikuwa unajaribu sema aikutick sasa basi fikiria kingine chakufanya hiyo pesa uliyoipoteza itakuja kwa njia nyingine ila siyo kwakubweteka hapo lazima uchezeshe ubongo utapasua maana hilo nifunzo kwako!! Kwa maneno haya kula hii ngoma hapa
 
Mnyama Aviator ndani ya Sportybet, miezi 3 iliyopita kuna mwana nilikuwa namdai kwa muda mrefu sana akanitumia 50000 kwa hasira nikaona hii hela haina issue tena nikaona niitumie kama mtaji kwenye kubeti

nika deposit Sportybet kama mtaji kwakuwa ilikuwa asubui hakuna game za football nikaona nijitupe kwenye Aviator, Mungu sio Baraka maviatu nikampiga muhindi hadi 1.5M, kwakuwa kampuni ya Sportybet ukitoa zaidi ya 1M hela inachukua muda mrefu kukufikia nikaona nitoe Kwanza 1M nikaacha 500000

Tamaa kama kawaida nikasema ngoja niendelee kuizalisha hiyo 500k, haikuchukua ata lisaa limoja laki 5 yote ikawa imeteketea, kwahiyo kwa upande wangu nakuelewa vizuri sana kuchoma 7.5M ndani ya siku 5 ni kawaida sana

Anyway, Pole mkuu, Hilo pigo limekuja wakati sahihi sana maana itakufanya ukumbuke maisha yako yote kuwa hakunaga hela ndogo wala kubwa, inategemea na matumizi yako

7.5M imeisha ndani ya siku 5 ilhali unakuta ulikuwa una survive siku 30 Kwa Mshahara wa laki 4, hapo sasa ndio unakuwa Sugu na maumivu na ilikuwa ni lazima upitie hii ili ubadirike

Kufa huwezi kufa ila ukweli ni kwamba hakuna Rangi utaacha kuona kwa sababu kipindi cha matatizo, matatizo huwa yanaitana kwa pamoja, hadi inafikia hatua wewe unakaa pembeni unayaacha yagombane yenyewe maana wewe umeshindwa

Litatoka hilo la kupigwa 7M, litakuja la Mpenzi wako kukupiga chini,Kodi itaisha ulipopanga na kutakiwa kusepa, washkaji waliokuwa wana survive kwa uwepo wako haitakuwa the same wewe u-survive kwa uwepo wao bali watakukwepa

Kila deal ambayo utakuwa unaseti inaishia njiani,kama wakati ukiwa kazini kulikuwa na job opportunity zingine saizi huwezi ata kuziskia, ndugu wataanza kukuona ni mzigo na huna msaada,

Kwahiyo kuna uwezekano mkubwa sana ukapitia at least 6-24 Months ya mikausho mikali, ila usishangae wala kukata Tamaa na kufikia kufanya maamuzi ya kijinga kwa sababu kawaida ya maisha, kipindi cha magumu unakuwa full surrounded with negative energy na kipindi cha mazuri kila unachogusa kinaenda na beat
kubwa sana hiii
 
kukosea kupo tu kwenye haya maisha , hata siku moja huwezi fanya yalio sahihi tu, jua kuna siku utakosea na unapokosea ndio kuna kujifunza ,kifo hakijawai kuwa solution kwenye matatizo pesa uliopoteza kama uliitafuta wewe amini unaweza kuipata zaidi ya mara mia kama ukiamua kuanzia upya , mimi naekuandikia hapa nilikwa mrahibu wa kamali na hakuna kamali sijawai cheza kuanzia dubu karata paka kasino ila 2020 niliamua kuacha na kuanza maisha mapya hakuna linaloshindikana maamuzi yote unayo wewe futa account au waombe wao betting company wakurestrict hutoona ujumbe wowote ule wala hutoweza kuingia kwenye io account ya kidenge kikubwa Muombe sana Mungu betting ni spirit muda mwingine ndio maana vitabu vya dini vyote vimekataza.
 
Wiki Moja nyuma hapo nimemtwanga mhindi laki 7 Kwa buku2
Laki saba kwa buku mbili...; Hizo ni odds zaidi ya 350 to 1 yaani usishangae ukajaribu tena kucheza hio na katika mara 1400 ukashinda mara mbili sasa hapo ukipa hesabu; utakuwa umemtwanga muhindi 1.4m kwa mtaji wa 2.8m; Na hapo sijaweka mkono wa Serikali kula 10% kila unaposhinda....

In the end the House always wins (Hesabu zinawalinda)
 
Back
Top Bottom