Vijana Tanzania Amka Tupambane na Umaskini

Paul Makonda

Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
97
Reaction score
186
VIJANA TANZANIA!

Kwa Asilimia ndio wengi (65% ya Watu Milioni 49) Na watoto ni wengi zaidi (44% Ya watu Milion 49). Taifa bado ni changa na Uchumi wake bado ni Mdogo mno. Kwa watu Milioni 49, Asilimia 91.8% karibu watu Milioni 44 ni Wategemezi Yaani Wazalishaji na Wanaotegemeza Taifa Ni Milion 5 Tu.

Tangu Kuvunjika kwa Azimio la Arusha, Uchumi wa Soko umethibitisha kuwa haukuwa Muafaka kwa taifa hili ama uliwahi ama haukutakiwa kuwepo. Asilimia 20% ya Watanzania (Wale wazalishaji) Wanashikilia Asilimia 80% ya Raslimali (Ingawa si kwa halali).

Changamoto za Kuendesha Serikali ni kubwa kwa sababu Uwezo wa kimapato ni mdogo kulinganisha na mahitaji halisi. Asilimia kati ya 33 na 40% ya Bajeti ya Serikali huishia katika Mikono ya Mafisadi yaani ni Matumizi hewa. Vijana Hawana Ajira, Tija ya Uzalishaji katika Sekta ya Umma bado iko chini sana na huduma muhimu zinatolewa si kama wajibu wa mtoaji na haki ya mhudumiwa, bali inatolewa kama hisani.

Wanasiasa badala ya kushughulikia masuala ya msingi ya taifa, wamejinngiza katika UNAFIKI, UFISADI, na UFITINISHAJI wa TAIFA hili wenyewe kwa wenyewe. Kitendo cha kujaribu kuzuia Mchakato muhimu wa kupata Katiba kwa madai ya kuteteawananchi ili hali kwa uhalisia wanajua wanatetea Maslahi yao, Hicho hakikubaliki kabisa. Kama Watanzania hatutasimama na kukemea tabia Chafu kama hizi, ipo siku yatasimama mawe kutusemea na hapo kutakuwa na kilio cha kusaga meno.

Tunapopambana na Mafisadi wanaokula 80% ya Raslimali za Taifa wakiacha watoto hawana kwa kusomea, Akina mama hawana huduma za afya ya Uzazi, Wazee wakitaabika bila huduma muhimu na vijana kuranda mitaani kutwa kutafuta ajira bila mafanikio na hata wale wanaotaka kujiajiri wakikosa mitaji kwa sababu ya masharti magumu katika taasisi za fedha, ni vema pia kupambana na wanasiasa WANAFIKI wanaodhani Ujinga na Umaskini wa Watanzania ndio Mtaji wao.

Nikiwa Kijana, SItanyamaza kwa sababu Vijana wenzangu hawaniungi Mkono, Napambana zaidi sababu naiona sababu nyingine ya kupambana ni kuwaelekeza vijana wenzangu kuungana nami katika Mapambano haya. Vita hii si ndogo, wala si lelemama inatupasa kujikana kwanza nafsi zetu kisha tusimamie maslahi ya Taifa na mwisho tutafanikiwa.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda
 
da ni kweli mazee hali ngumu kitaa nina miaka 30 bado namtegemea father,nina elimu ya masters lkn sina wa kunishika mkono wala ndugu ccm sielewi mbele itakuaje
 
We jamaa sikuelewi, ni mtu mjinga pekee anayeweza kitenganisha neno UFISADI na CCM hao ni chanda na pete kamwe hawatengani. Hivyo tambua unapolia juu ya ufisadi unalia juu ya ccm.

Na ndio maana wapinzani wanafanya juu chini kuwaondoa ninyi ukoo wa panya ni kwasababu yote uliyoyaorodhesha hapo juu kama wanafunzi kukosa madawati,vitabu nk mtesi wetu ni ccm ambayo wewe kwa kiburi unakuja hadharani kuwasemea vijana kwa mgongo wa cheo gani sijui ndani ya uvccm huu ni unafki na ushetani uliotukuka.

Vijana popote Tz hatuhitaji midomo ya vijana mafisadi na walamba viatu kama ninyi kwaajili ya kutusemea vua kwanza koti la unafki unaokukabiri ndipo uje hadharani kutusemea vijana

Mwenyewe hapa unakiri kuwa changamoto za kuendesha serikali ni kubwa kwa kuwa nyingi ya pesa zinazokusanywa zinaishia mikononi mwa MAFISADI na kwa kutoelewa kwako unataka kutuaminisha hao mafisadi wanatoka upinzani!. Huku ni kujidanganya, Ni lini wanasiasa especially wa CCM mtaishi ktk ukweli??

BACK TANGANYIKA
 
VIJANA TANZANIA!

Nikiwa Kijana, SItanyamaza kwa sababu Vijana wenzangu hawaniungi Mkono, Napambana zaidi sababu naiona sababu nyingine ya kupambana ni kuwaelekeza vijana wenzangu kuungana nami katika Mapambano haya. Vita hii si ndogo, wala si lelemama inatupasa kujikana kwanza nafsi zetu kisha tusimamie maslahi ya Taifa na mwisho tutafanikiwa.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda

Wangeweza kukusupport kama ungekuwa kweli unatetea hao vijana.Hebu mdogo rudi siku tano au sita nyuma,unadhani ulijadili hoja iliyoko mbele yako ya Katiba?Au uliwajadili watu mpaka kuwaita binadamu wenzako mashetani?

Kama kijana unadhani kwenye uso wa binadamu wengine ambao unadhani unawasemea wamejisikiaje pale hata ulipoombwa uyatoe maneno yako kwa kiburi kabisa ukasema hapana,je,kwenye katiba kuna sura inapaswa kuweka matusi,mipasho na kejeli?Je hauoni utatundea haki watanzania tuliokusikia kama utatuomba radhi kwa kupokea posho kwa kujadili matusi na mipasho?

Jitazame upya,bado haujachelewa,kuwa upinzani siyo uadui au kuwa na mitazamo tofauti hautufanyi tutukanane ,Taifa/Tanzania yetu sote haijali hata umetokea nchi gani ardhi inachukua kila mmoja,Muhindi,msomali,mchina,mchagga ,mnyakyusa nk nk.Kwa nini mnatubagua kwa sababu ya itikadi zetu,au mitazamo yetu?

Je kuna nchi ilijengwa kwa kuwa na mtazamo mmoja? Mimi ni Mtanzania tu ambaye kwenye UJANA siko wala kwenye UZEE siko!
 
VIJANA TANZANIA!

Kwa Asilimia ndio wengi (65% ya Watu Milioni 49) Na watoto ni wengi zaidi (44% Ya watu Milion 49). Taifa bado ni changa na Uchumi wake bado ni Mdogo mno. Kwa watu Milioni 49, Asilimia 91.8% karibu watu Milioni 44 ni Wategemezi Yaani Wazalishaji na Wanaotegemeza Taifa Ni Milion 5 Tu.

Tangu Kuvunjika kwa Azimio la Arusha, Uchumi wa Soko umethibitisha kuwa haukuwa Muafaka kwa taifa hili ama uliwahi ama haukutakiwa kuwepo. Asilimia 20% ya Watanzania (Wale wazalishaji) Wanashikilia Asilimia 80% ya Raslimali (Ingawa si kwa halali).

Changamoto za Kuendesha Serikali ni kubwa kwa sababu Uwezo wa kimapato ni mdogo kulinganisha na mahitaji halisi. Asilimia kati ya 33 na 40% ya Bajeti ya Serikali huishia katika Mikono ya Mafisadi yaani ni Matumizi hewa. Vijana Hawana Ajira, Tija ya Uzalishaji katika Sekta ya Umma bado iko chini sana na huduma muhimu zinatolewa si kama wajibu wa mtoaji na haki ya mhudumiwa, bali inatolewa kama hisani.

Wanasiasa badala ya kushughulikia masuala ya msingi ya taifa, wamejinngiza katika UNAFIKI, UFISADI, na UFITINISHAJI wa TAIFA hili wenyewe kwa wenyewe. Kitendo cha kujaribu kuzuia Mchakato muhimu wa kupata Katiba kwa madai ya kuteteawananchi ili hali kwa uhalisia wanajua wanatetea Maslahi yao, Hicho hakikubaliki kabisa. Kama Watanzania hatutasimama na kukemea tabia Chafu kama hizi, ipo siku yatasimama mawe kutusemea na hapo kutakuwa na kilio cha kusaga meno.

Tunapopambana na Mafisadi wanaokula 80% ya Raslimali za Taifa wakiacha watoto hawana kwa kusomea, Akina mama hawana huduma za afya ya Uzazi, Wazee wakitaabika bila huduma muhimu na vijana kuranda mitaani kutwa kutafuta ajira bila mafanikio na hata wale wanaotaka kujiajiri wakikosa mitaji kwa sababu ya masharti magumu katika taasisi za fedha, ni vema pia kupambana na wanasiasa WANAFIKI wanaodhani Ujinga na Umaskini wa Watanzania ndio Mtaji wao.

Nikiwa Kijana, SItanyamaza kwa sababu Vijana wenzangu hawaniungi Mkono, Napambana zaidi sababu naiona sababu nyingine ya kupambana ni kuwaelekeza vijana wenzangu kuungana nami katika Mapambano haya. Vita hii si ndogo, wala si lelemama inatupasa kujikana kwanza nafsi zetu kisha tusimamie maslahi ya Taifa na mwisho tutafanikiwa.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda

Dogo kama umeamua kula na vipofu usiwashike mkono. Kitendo cha kuanza kusema mafisadi, Azimio la Arusha lilivunjika nani alilivunja, naanza kuwa na wasiwasi na CV yako. Du hivi kweli kwa umri wako unataka kutuaminisha kwamba hujui kinachoendela hapa Duniani.

Wala usiwachokoze watu wewe endelea kula bata tu ndani ya CCM, tena laiti kama ungejua hasira za wananchi nakuomba uache kabisa hizo mbwembwe zako. Fanya utafiti mdogo tu kila mara unapo post andika hapa wananchi wana react kwa namna gani dhi ya maandiko yako? Tulizeni akili kabisa watu wamechoka na utawala wenu. Kama unaweza tumia tu mtandao kuuliza kuhusu maoni ya Rasimu ya Waryoba inaungwa Mkono kwa kiasi gani na wananchi ndio utagundua mnachokitetea ni kwa maslahi yetu ccm na watoto wenu mnaowarithisha madaraka.
"AMA KWELI CCM INA WENYEWE NA WENYEWE NDIO NINYI "
 
Hivi huyu makonda elimu yake ni darasa la saba au form 1v ? nataka kupata jibu kwanza. ukiangalia uandishi wake hapo juu takwimu amejikanyaga kweli, niambie kwanza kwa sasa Tanzania kutokana na sensa ya 2012 linakadiriwa kuwa na watu wangapi ? Kwa kukusadia ni karibu mil. 45. Sasa mbona hapo mara unaeleza habari za milioni 44 alafu tena unatueleza habari za mil. 49. Kijana tuliza kichwa siasa itakufanya uwe kama kasuku .
 
kama uwezo wa kimapato ni mdogo mbona mkweree kila siku anapaa angani???kwikwikwiiiiii, watu wenye background za hovyo wanakuwa na mawazo ya hovyo hovyo
 
da ni kweli mazee hali ngumu kitaa nina miaka 30 bado namtegemea father,nina elimu ya masters lkn sina wa kunishika mkono wala ndugu ccm sielewi mbele itakuaje

Masterz yako hiyo umeikota au?
Unashindwaje kujiajiri unasema ccm huwaelewi!!! Changamka
 
:embarassed2:ningeweza kukusanya vijana wote wenye akili kama yako ndani ya tanzania kwenye ukumbi mmoja bendera ingepepea nusu mlingoti kwa siku 3:embarassed2:
 
Wewe kijana lazima utakuwa mwehu una akili timamu hao mafisadi unao wasema wanakula asilimia 80 ya pato la Taifa ni chini ya utawala wa chama kipi ? Je sio CCM na kama ndo hivyo mbona wewe ni mwanachama wa ccm . Unataka kuwambia watanzania nini hapo ? kama kweli mafisadi ndani ya serikali ya ccm wanawaibia wananchi asilimia 80 ya pato la taifa je kuna haja tena ccm iendelee kuwepo madarakani ?
VIJANA TANZANIA!

Kwa Asilimia ndio wengi (65% ya Watu Milioni 49) Na watoto ni wengi zaidi (44% Ya watu Milion 49). Taifa bado ni changa na Uchumi wake bado ni Mdogo mno. Kwa watu Milioni 49, Asilimia 91.8% karibu watu Milioni 44 ni Wategemezi Yaani Wazalishaji na Wanaotegemeza Taifa Ni Milion 5 Tu.

Tangu Kuvunjika kwa Azimio la Arusha, Uchumi wa Soko umethibitisha kuwa haukuwa Muafaka kwa taifa hili ama uliwahi ama haukutakiwa kuwepo. Asilimia 20% ya Watanzania (Wale wazalishaji) Wanashikilia Asilimia 80% ya Raslimali (Ingawa si kwa halali).

Changamoto za Kuendesha Serikali ni kubwa kwa sababu Uwezo wa kimapato ni mdogo kulinganisha na mahitaji halisi. Asilimia kati ya 33 na 40% ya Bajeti ya Serikali huishia katika Mikono ya Mafisadi yaani ni Matumizi hewa. Vijana Hawana Ajira, Tija ya Uzalishaji katika Sekta ya Umma bado iko chini sana na huduma muhimu zinatolewa si kama wajibu wa mtoaji na haki ya mhudumiwa, bali inatolewa kama hisani.

Wanasiasa badala ya kushughulikia masuala ya msingi ya taifa, wamejinngiza katika UNAFIKI, UFISADI, na UFITINISHAJI wa TAIFA hili wenyewe kwa wenyewe. Kitendo cha kujaribu kuzuia Mchakato muhimu wa kupata Katiba kwa madai ya kuteteawananchi ili hali kwa uhalisia wanajua wanatetea Maslahi yao, Hicho hakikubaliki kabisa. Kama Watanzania hatutasimama na kukemea tabia Chafu kama hizi, ipo siku yatasimama mawe kutusemea na hapo kutakuwa na kilio cha kusaga meno.

Tunapopambana na Mafisadi wanaokula 80% ya Raslimali za Taifa wakiacha watoto hawana kwa kusomea, Akina mama hawana huduma za afya ya Uzazi, Wazee wakitaabika bila huduma muhimu na vijana kuranda mitaani kutwa kutafuta ajira bila mafanikio na hata wale wanaotaka kujiajiri wakikosa mitaji kwa sababu ya masharti magumu katika taasisi za fedha, ni vema pia kupambana na wanasiasa WANAFIKI wanaodhani Ujinga na Umaskini wa Watanzania ndio Mtaji wao.

Nikiwa Kijana, SItanyamaza kwa sababu Vijana wenzangu hawaniungi Mkono, Napambana zaidi sababu naiona sababu nyingine ya kupambana ni kuwaelekeza vijana wenzangu kuungana nami katika Mapambano haya. Vita hii si ndogo, wala si lelemama inatupasa kujikana kwanza nafsi zetu kisha tusimamie maslahi ya Taifa na mwisho tutafanikiwa.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda
 
Wale vijana mnaowafundisha kwenye makambi yenu wakati wa chaguzi ndogo ni vijana gani? Yaani na wewe unaona umeshafikia kiwango cha Ustates man kuwaalika watu mpambane. Mnataka kupambana na nani?Mnataka kuapmbana kwa nini? Mnataka kupambana kwa lini? Mnataka kupambana kwa muda gani?Mnataka kupambana ili mpate nini? Mnataka kupambana kwa kutumia nini? Mnataka kupambana kwa kufurahisha nani? Mnataka kupambana kwa kuwatumia vijana gani? Mnataka kupambana kwa kuwalipa nini? Mnataka kupambana kwa kulenga nini?
 
Nchi hii imekwisha hilo ndo jembe kwa mujibu wa rais kwenye hotuba yake
 
VIJANA TANZANIA!

Kwa Asilimia ndio wengi (65% ya Watu Milioni 49) Na watoto ni wengi zaidi (44% Ya watu Milion 49). Taifa bado ni changa na Uchumi wake bado ni Mdogo mno. Kwa watu Milioni 49, Asilimia 91.8% karibu watu Milioni 44 ni Wategemezi Yaani Wazalishaji na Wanaotegemeza Taifa Ni Milion 5 Tu.

Tangu Kuvunjika kwa Azimio la Arusha, Uchumi wa Soko umethibitisha kuwa haukuwa Muafaka kwa taifa hili ama uliwahi ama haukutakiwa kuwepo. Asilimia 20% ya Watanzania (Wale wazalishaji) Wanashikilia Asilimia 80% ya Raslimali (Ingawa si kwa halali).

Changamoto za Kuendesha Serikali ni kubwa kwa sababu Uwezo wa kimapato ni mdogo kulinganisha na mahitaji halisi. Asilimia kati ya 33 na 40% ya Bajeti ya Serikali huishia katika Mikono ya Mafisadi yaani ni Matumizi hewa. Vijana Hawana Ajira, Tija ya Uzalishaji katika Sekta ya Umma bado iko chini sana na huduma muhimu zinatolewa si kama wajibu wa mtoaji na haki ya mhudumiwa, bali inatolewa kama hisani.

Wanasiasa badala ya kushughulikia masuala ya msingi ya taifa, wamejinngiza katika UNAFIKI, UFISADI, na UFITINISHAJI wa TAIFA hili wenyewe kwa wenyewe. Kitendo cha kujaribu kuzuia Mchakato muhimu wa kupata Katiba kwa madai ya kuteteawananchi ili hali kwa uhalisia wanajua wanatetea Maslahi yao, Hicho hakikubaliki kabisa. Kama Watanzania hatutasimama na kukemea tabia Chafu kama hizi, ipo siku yatasimama mawe kutusemea na hapo kutakuwa na kilio cha kusaga meno.

Tunapopambana na Mafisadi wanaokula 80% ya Raslimali za Taifa wakiacha watoto hawana kwa kusomea, Akina mama hawana huduma za afya ya Uzazi, Wazee wakitaabika bila huduma muhimu na vijana kuranda mitaani kutwa kutafuta ajira bila mafanikio na hata wale wanaotaka kujiajiri wakikosa mitaji kwa sababu ya masharti magumu katika taasisi za fedha, ni vema pia kupambana na wanasiasa WANAFIKI wanaodhani Ujinga na Umaskini wa Watanzania ndio Mtaji wao.

Nikiwa Kijana, SItanyamaza kwa sababu Vijana wenzangu hawaniungi Mkono, Napambana zaidi sababu naiona sababu nyingine ya kupambana ni kuwaelekeza vijana wenzangu kuungana nami katika Mapambano haya. Vita hii si ndogo, wala si lelemama inatupasa kujikana kwanza nafsi zetu kisha tusimamie maslahi ya Taifa na mwisho tutafanikiwa.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda

1:Unasema mfumo wa soko hauna tija kwa Taifa.Chama chako kinajiita chama cha kijamaa.Hujawahi kujenga hoja yoyote ndani ya chama chako kuhusu kuvunja azimio la Arusha lililokua bench mark ya Miiko na Maadili ya Uongozi

2:Unaongelea Ufisadi wakati unajua Ufisadi ulishamiri pale ambapo Miiko ya Uongozi ilipotupiliwa mbali na watawala wanaotokana na chama chako

3:Wewe ni sehemu ya waliohusika kukwamisha mjadala wa Katiba

4:Unakuja kulialia kuhusu ufisadi huku JF wakati unajua chama chako kina uwezo wa kujisafisha na pia kusafisha serikali yake ambayo imelea ufisadi.Unataka wanaJF wafanyeje ?

5:Uliposhindwa uchaguzi wa vijana ulisema ulishindwa kwa sababu ya Rushwa.Baadae waliotoa Rushwa kukushinda kwenye uchaguzi wakakupa cheo kisha ukakubali kuwa katibu wa hamasa na Chipukizi ndani ya UVCCM.Principle ziko wapi hapa?Consistency ya kile unachoamini iko wapi hapa? Kama ni maslahi binafsi hakuna mtu ambaye ni bad example zaidi yako hapa.

Acha unafiki kaka.Huwa sipendi kujibu Thread za aina hii lakini nimeona nianike unafiki huu tu
 
Tunapopambana na Mafisadi wanaokula 80% ya Raslimali za Taifa wakiacha watoto hawana kwa kusomea, Akina mama hawana huduma za afya ya Uzazi, Wazee wakitaabika bila huduma muhimu na vijana kuranda mitaani kutwa kutafuta ajira bila mafanikio na hata wale wanaotaka kujiajiri wakikosa mitaji kwa sababu ya masharti magumu katika taasisi za fedha, ni vema pia kupambana na wanasiasa WANAFIKI wanaodhani Ujinga na Umaskini wa Watanzania ndio Mtaji wao.

Nikiwa Kijana, SItanyamaza kwa sababu Vijana wenzangu hawaniungi Mkono, Napambana zaidi sababu naiona sababu nyingine ya kupambana ni kuwaelekeza vijana wenzangu kuungana nami katika Mapambano haya. Vita hii si ndogo, wala si lelemama inatupasa kujikana kwanza nafsi zetu kisha tusimamie maslahi ya Taifa na mwisho tutafanikiwa.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda[/QUOTE]

Ebu fungua hii kitu halafu kama kweli unajua unataka kupambana kwa ajili ya Taifa hili nitakuonyesha Jamaa ambaye ametengeneza filamu fupifupi za aina hii utwambie chama na serikali yenu inafanyaje kuwaokoa hawa walala hoi ambao sasa ziaidi ya kuwaibia hizo raslimali sasa mnawaua na makemikali ya migodini. Ushahidi nenda Ocean Road na Bugando uliza wale wagonjwa wanatokea mikoa gani na ujuilize kuna shughuli gani za Kiuchumi na uwekezaji.

Ebu fungua hii kitu http://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=zxkKLJXXB4c
angalia kwa makini halafu unambie wenye dhamana kwa nini wasipelekwe "The Hague"
 
Huyu ni mnafiki wa wiki!Ndo hawa hawa wametumiwa kuharibu mjadala wa katiba.CCM wanatumia shughuli za kiserikali kama za chama,halafu jitu linataka kuunganisha vijana
 
Hao wanasiasa unaosema wamejiingiza kwenye ufisadi,unafiki mbona ndo hao unawaowatetea?

Sindio hapo!mkuu watu wa namna hii ni lazima tuwaogope kama ukoma anakiri kwamba kuna ufisadi na mafisadi ila hataki kubainisha fisadi ni nani na anafanya huo ufisadi kwa mgongo wa nani

Kunamahali nimesema tatizo kubwa linalosababisha nchi yetu kuendelea kudorola. kiuchumi kila uchao, ni NJAA ni kutokana na njaa mtu hawezi kufanya kile anachokiamini kwa hofu ya kumuudhi yule anayemlisha na hili tunaliona wazi kwa huyu jamaa.

BACK TANGANYIKA
 
Huyu ni mnafiki wa wiki!Ndo hawa hawa wametumiwa kuharibu mjadala wa katiba.CCM wanatumia shughuli za kiserikali kama za chama,halafu jitu linataka kuunganisha vijana.
 
Back
Top Bottom