Vijana kutanguliza maslahi binafsi kuliko maslahi ya taifa ni zao la jamii iliyo walea na kuwakuza

ndegemzungu

Member
Mar 10, 2019
92
240
Habari za zenu,bilia kupoteza muda naomba niende kwenye mada moja kwa moja
Kumekuwa na utaratibu wa kuwalaumu vijana kuwa wameweka mbele maslahi binafsi kuliko maslahi ya taifa.

Mimi ninaona tatzo hili linaanzia katika ngazi ya famili mtoto anasisitizwa aende shule asome kwa bidii ili maisha yake yaje kuwa mazuri yani tunamuandaa mtoto kiwa mbinafsi hatusemi aende akasome ili aje kuikomboa jamii yake

Anapofika shule mtoto huyu walimu pia humsisitiza kusoma kwa bidii ili maisha yake yaje kuwa mazuri hafundishwi kuhusu nchi yake muda mwingi anasisitizwa asome ili tu maisha yake yaje kuwa mazuri.

Naona ni vzuri kuwafundisha vijana kuanzia ngazi ya familia juu ya kuithamini na kuipenda nchi yao tena ni muhimu zaidi kuwakumbu ustawi na hatma ya nchi yao inawategemea zaidi wao.

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom