Ninaanza rasmi mgomo wa kulipa kodi

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Ndio, Kuna watu watakuja hapa na story zao za uzalendo wakijifanya wanaipenda Sana hii nchi huku wakiwa wamejificha kwenye kivuli Cha kutetea matumbo yao, Binafsi naanza mgomo rasmi wa kulipa Kodi maana sioni namna inavyonifaidisha Mimi na watanzania tulio wengi pamoja na kuwa na rasilimali nyingi hapa nchini.

Kuanzia leo nikikamatwa na traffic natoa pesa tu sitaki risiti, nikipanda mwendo kasi nitataka wanipe ticket used ifanikishe tu kunifikisha ninakoenda, nikienda ubungo nikilipa 300 sitaki ticket na nikinunua kitu chochote sitaki risiti ya aina yeyote ama nikifanya manunuzi kariakoo hata ya mamillion ya pesa nitawaambia wanipe risiti yenye gharama pungufu na niliyonunulia,nikienda shell najaza mafuta kwenye gari siombi risiti( ni bora hii pesa iliwe na wavuja jasho wenzangu, kuliko kuliwa na manyang'au wachache serikalini).

Sijaona Sera na watawala wenye uchungu na nchi hii wa kunifanya niwe mzalendo, hawa wapo kwa ajili ya matumbo yao na familia zao huku wakiimba pambio za uzalendo, Ukiwaona utadhani wanamaanisha wanachokiongea lakini kiuhalisia wanalinda maslahi yao.

KWA NINI NASEMA HIVI?

Nimejaribu kufuatilia maisha ya watanzania walio wengi hayafurahishi hata kidogo, wamechoka, wamekata tamaa hawaijui hata kesho yao.., maisha ni magumu kuzidi maelezo na hamna Sera nzuri za kibiashara na kiuchumi dhidi yao, wakiwa bado wanahangaika kutafta pesa angalau ya kula wanakutana na migambo wa jiji na tume ya mkurugenzi na mkuu inapita kukagua usafi, Hawa jamaa wanachojali ni rushwa tu wao wakikuta hata vikaratasi havijachomwa au majivu umemwaga pembeni wanataka elfu50 papo hapo au uwape rushwa kidogo wakuache na Kama huna wanakupeleka polisi ambapo wanaweza kukuambia uyachome au kuyasogeza na hali ikawa ya kawaida kabisa.

Angalia wakulima wa mahindi, kahawa, mbaazi, na Sasa korosho wameshafungwa mdomo hurusiwi kusema hujalipwa Tena, ukisema hujalipwa unapelekwa ndani.., huko mahospitalini watoto wwtu wa chini ya miaka5 na mababu zetu wanatakiwa watibiwe bure.. kaangalieni kinachoendelea huko, Huko bungeni Bunge linapanga bajeti ya Billioni 8 kwenda kulipa madeni ya mikopo ya wabunge wa kuteuliwa waliofukuzwa na CUF lipumba, bunge ( spika) anakubali ( anainjinia) wabunge wafukuzwe halafu anatumia pesa za walipa kodi kuwalipia madeni yao bank..... Kwa style hii kwa nini nilipe Kodi?

Shule za serikali zimeshakuwa vituko, watoto wetu wanachokipata humo sio elimu tena na ndo maana hata hawa wanaotutungia mitaala na Sera hizi za elimu hawaruhusu watoto wao wakasoma hizi shule, wenzetu wa Kagera walipata maafa, Kila mtu ni shahidi kwa majibu ya serikali dhidi yao na walienda mbali zaidi mpaka michango iliyotolewa na wanyonge wenzao ikaenda kufanya shughuli zingine za serikali, watawala hawakujali Kama watu wao..., Kwa nini nilipe Kodi?

Kwa watumishi wa umma huko ndo Hali iko mbaya sana mpka Leo Kuna watumishi wa umma wanalipwa 260,000/= kwa mwezi kabla ya makato, wamewabagua kwa makundi watoto wa masikini utawakuta kwenye taasisi sizizolipa vizuri hizi za 260k, 300k,340k,400k,450k,650k,700k, na 820k na hawana allowance zozote zingine tofauti na mshahara, huku watoto na Hawa vigogo wakiwekwa kwenye taasisi za umma zinazolipa vizuri ambazo utakuta security guard tu anaanzia 1.5m na allowance Kama housing na transport wanapata, kwa Hali hii kwa nini niwe mzalendo?

Ndgu zangu vijijini wanachangia bwawa moja la maji ya kunywa na mifugo na huku budget ya waziri kutembelea zinduzi mbalimbali zisizokuwa na tija zinatosha kujenga visima zaidi ya10 vijijini, mshahara wa mkurungenzi na marupurupu yake kwa mwezi yanatosha kulipa mishahara ya kima chini Cha miaka 30 ya mtumishi wa taasisi hiyohiyo moja huku akiwa analipiwa kila kitu na huyu wa kima Cha chini hana Cha ziada zaidi ya mshahara, kwa nini nilipe Kodi?

Yanayoendelea huko PSSSF/NSSF yananiongezea hasira zaidi ya kutokulipa Kodi... Hapa namba one alicheza mchezo wa kuagiza akijua kabisa alichosema hakitekelezeki, ukienda kwenye hizi ofisi utawahurumia vijana na wazee wanaosubiria mafao Yao, wastaafu wanalipwa kwa kikotoo Cha asilimia 25 na vijana wanaambiwa waje baada ya kufikisha miaka55 kuchukua pesa isiyozidi mill5:D:cool:, Cha kusikitisha zaidi wengine hawakuwa wanachangia kisheria kwenye mifuko hii, walikuwa wanachangia kwa hiari Cha ajabu nao wanapata usumbufu mkubwa mno kupata pesa zao

Binafsi, sitaki kuwa mnafiki na mzalendo kwa watawala wanaofuja rasilimali zetu, na hata nikikuta mtumishi wa umma anakula rushwa ama anaihujumu serikali kwa vyovyote vile nitamsapoti, nina sababu nyingi za kufanya hivi kuliko kuwa mzalendo.

Angalia bunge la ndugai na CAG, wanamnyonga Assad ili wafisadi vizuri wakijifichicha kwenye koti la uzalendo, wanatetekeza mabillion ya pesa kwa kununua madiwani na wabunge na kugharamia chaguzi zisizo na tija.. kwa nini nilipe Kodi ikatumike namna hii?

Viongozi wakubwa ambao wanagharamiwa kila kitu na serikali ambao hawajui hata gharama ya kujinunulia chumvi ikoje wakilipwa mishahara minono isiyokatwa PAYE anatunga na kupitisha Sera za kukatwa Kodi kwa mtumishi anaelipwa 260k per month na asiye na allowance yeyote na akistaafu alipwe kwa kikokotoo Cha asilimia25, huku yeye akichukua pesa zake zote za kustaafu kwa mkipuo.. kwa Hali hii kwa nini nihamasike kulipa Kodi?

Watawala wasiojali usalama wa raia wao,Wala hawastushwi na Hali za maisha yao unawezaje Kusema ni wazalendo, wametengeneza mazingira gani ya kuwaajiri vijana? Ukiwauliza swali hili Wana majibu rahisi tu eti hakuna serikali yeyote duniani iliyoajiri raia wake wote, sawa hatukatai lakini mmetengeneza Sera na mazingira mazuri ya Hawa vijana kujiajiri? Au hii sio kazi yenu?...kwa nini tulipe Kodi kama hamjui Cha kufanya?

Kuanzia leo nawasapoti watumishi Wala rushwa na mafisadi na wasiolipa Kodi kuliko mafisadi mapapa wanaojificha kwenye koti la uzalendo, wanajoiita watetezi wa wanyonge huku wakiwanyonga bila huruma, wanaoimba pambio za maskini huku wao wakiwa matajiri wa kutupwa.

" Nchi inajengwa na wenye moyo, Inaliwa na wenye meno"

Mungu wabariki wakwepa Kodi wote
 
Ndio, Kuna watu watakuja hapa na story zao za uzalendo wakijifanya wanaipenda Sana hii nchi huku wakiwa wamejificha kwenye kivuli Cha kutetea matumbo yao, Binafsi naanza mgomo rasmi wa kulipa Kodi maana sioni namna inavyonifaidisha Mimi na watanzania tulio wengi pamoja na kuwa na rasilimali nyingi hapa nchini.

Kuanzia leo nikikamatwa na traffic natoa pesa tu sitaki risiti, nikipanda mwendo kasi nitataka wanipe ticket used ifanikishe tu kunifikisha ninakoenda, nikienda ubungo nikilipa 300 sitaki ticket na nikinunua kitu chochote sitaki risiti ya aina yeyote ama nikifanya manunuzi kariakoo hata ya mamillion ya pesa nitawaambia wanipe risiti yenye gharama pungufu na niliyonunulia( ni bora hii pesa iliwe na wavuja jasho wenzangu, kuliko kuliwa na manyang'au wachache serikalini).

Sijaona Sera na watawala wenye uchungu na nchi hii wa kunifanya niwe mzalendo, hawa wapo kwa ajili ya matumbo yao na familia zao huku wakiimba pambio za uzalendo, Ukiwaona utadhani wanamaanisha wanachokiongea lakini kiuhalisia wanalinda maslahi yao.

KWA NINI NASEMA HIVI?

Nimejaribu kufuatilia maisha ya watanzania walio wengi hayafurahishi hata kidogo, wamechoka, wamekata tamaa hawaijui hata kesho yao.., maisha ni magumu kuzidi maelezo na hamna Sera nzuri za kibiashara na kiuchumi dhidi yao, wakiwa bado wanahangaika kutafta pesa angalau ya kula wanakutana na migambo wa jiji na tume ya mkurugenzi na mkuu inapita kukagua usafi, Hawa jamaa wanachojali ni rushwa tu wao wakikuta hata vikaratasi havijachomwa au majivu umemwaga pembeni wanataka elfu50 papo hapo au uwape rushwa kidogo wakuache na Kama huna wanakupeleka polisi ambapo wanaweza kukuambia uyachome au kuyasogeza na hali ikawa ya kawaida kabisa.

Angalia wakulima wa mahindi, kahawa, mbaazi, na Sasa korosho wameshafungwa mdomo hurusiwi kusema hujalipwa Tena, ukisema hujalipwa unapelekwa ndani.., huko mahospitalini watoto wwtu wa chini ya miaka5 na mababu zetu wanatakiwa watibiwe bure.. kaangalieni kinachoendelea huko.

Shule za serikali zimeshakuwa vituko, watoto wetu wanachokipata humo sio elimu tena na ndo maana hata hawa wanaotutungia mitaala na Sera hizi za elimu hawaruhusu watoto wao wakasoma hizi shule,

Kwa watumishi wa umma huko ndo Hali iko mbaya sana mpka Leo Kuna watumishi wa umma wanalipwa 260,000/= kwa mwezi kabla ya makato, wamewabagua kwa makundi watoto wa masikini utawakuta kwenye taasisi sizizolipa vizuri hizi za 260k, 300k,340k,400k,450k,650k,700k, na 820k na hawana allowance zozote zingine tofauti na mshahara, huku watoto na Hawa vigogo wakiwekwa kwenye taasisi za umma zinazolipa vizuri ambazo utakuta security guard tu anaanzia 1.5m na allowance Kama housing na transport wanapata, kwa Hali hii kwa nini niwe mzalendo?

Ndgu zangu vijijini wanachangia bwawa moja la maji ya kunywa na mifugo na huku budget ya waziri kutembelea zinduzi mbalimbali zisizokuwa na tija zinatosha kujenga visima zaidi ya10 vijijini, mshahara wa mkurungenzi na marupurupu yake kwa mwezi yanatosha kulipa mishahara ya kima chini Cha miaka 30 ya mtumishi wa taasisi hiyohiyo moja huku akiwa analipiwa kila kitu na huyu wa kima Cha chini hana Cha ziada zaidi ya mshahara, kwa nini nilipe Kodi?

Yanayoendelea huko PSSSF/NSSF yananiongezea hasira zaidi ya kutokulipa Kodi... Hapa namba one alicheza mchezo wa kuagiza akijua kabisa alichosema hakitekelezeki, ukienda kwenye hizi ofisi utawahurumia vijana na wazee wanaosubiria mafao Yao, wastaafu wanalipwa kwa kikotoo Cha asilimia 25 na vijana wanaambiwa waje baada ya kufikisha miaka55 kuchukua pesa isiyozidi mill5:D:cool:, Cha kusikitisha zaidi wengine hawakuwa wanachangia kisheria kwenye mifuko hii, walikuwa wanachangia kwa hiari Cha ajabu nao wanapata usumbufu mkubwa mno kupata pesa zao

Binafsi, sitaki kuwa mnafiki na mzalendo kwa watawala wanaofuja rasilimali zetu, na hata nikikuta mtumishi wa umma anakula rushwa ama anaihujumu serikali kwa vyovyote vile nitamsapoti, nina sababu nyingi za kufanya hivi kuliko kuwa mzalendo.

Angalia bunge la ndugai na CAG, wanamnyonga Assad ili wafisadi vizuri wakijifichicha kwenye koti la uzalendo, wanatetekeza mabillion ya pesa kwa kununua madiwani na wabunge na kugharamia chaguzi zisizo na tija.. kwa nini nilipe Kodi ikatumike namna hii?

Kuanzia leo nawasapoti watumishi Wala rushwa na mafisadi na wasiolipa Kodi kuliko mafisadi mapapa wanaojificha kwenye koti la uzalendo, wanajoiita watetezi wa wanyonge huku wakiwanyonga bila huruma, wanaoimba pambio za maskini huku wao wakiwa matajiri wa kutupwa....

Mungu wabariki wakwepa Kodi wote
Bado Bunge litatenga fedha ya kodi ya Tsh Bilioni moja kwenda kulipa deni la wabunge 8 waliofukuzwa na lipumba.
 
Sasa kwa Hali hii kwa Nini nilipe Kodi?
Ulipaji wa kodi TZ haupo vizuri,nchi za mabeberu kuna kiwango cha kulipa kodi,ukishavuka hicho kiwango fedha inayozidi unarudishiwa,cha kushangaza TZ,viongozi wenye nyadhifa/vyeo vikubwa ndani ya nchi hawalipi kodi kabisa,mie ngumbaru mchoma mkaa nalipa kodi kubwa kumzidi hata waziri wa serikalini.
 
Asante sana mtoa post wewe ni mimi kabisa................ kodi watakayopata ni ile ya kukatwa kwa lazima PAYE 506,000 kila mwezi.... Inaniuma sana na ndio maana nikiona inachezewa hovyo nakasirika.. MUNGU TUPE UJASIRI
Yaani hata Mimi hii PAYE na haya mamifuko ya Hifadhi za kijamii kwa vile ni sheria tu,..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulipaji wa kodi TZ haupo vizuri,nchi za mabeberu kuna kiwango cha kulipa kodi,ukishavuka hicho kiwango fedha inayozidi unarudishiwa,cha kushangaza TZ,viongozi wenye nyadhifa/vyeo vikubwa ndani ya nchi hawalipi kodi kabisa,mie ngumbaru mchoma mkaa nalipa kodi kubwa kumzidi hata waziri wa serikalini.
Hapa ndo tatzo lipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom