Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,296
- 9,928
Kuna habari kwamba baadhi ya wenyeviti wa UVCCM kutoka baadhi ya wilaya za mkoa wa Arusha nao wanatarajiwa kuhamia CHADEMA pamoja na Millya siku chache zijazo.
Makundi ya vijana mjini hapa walizipokea kwa shangwe taarifa hizo, huku wakiwataka vijana wengine ndani ya CCM kuondoka na kujiunga na CHADEMA kwa kile walichoeleza kuwa itawawezesha kujenga nguvu ya pamoja kuiondoa madarakani CCM ambayo imekuwa ikiwathamini na kuwajali watoto wa vigogo hasa katika suala zima la uongozi .
"Vijana wa CCM watoke wote waende CHADEMA. Kule vijana wanapewa fursa ya kuongoza na mawazo yao yanasikilizwa; hivyo ni rahisi kupanga mipango ya maendeleo inayotekelezeka hasa wakifanikiwa kuing'oa madarakani serikali ya CCM 2015 ambayo imabaki kuwalundikia vyeo wazee wastaafu huku vijana wakiambiwa wao bado hawana uzoefu" alisema Jackob Mollel, mkazi wa Arusha mjini.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alisema chama kinamkaribisha Millya na wanasiasa wengine walio safi kujiunga nacho ili kuongeza nguvu ya mabadiliko kinayopigania.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema hatua iliyochukuliwa na Millya ni mwendelezo wa mmeguko ndani ya CCM na ishara kwamba chama hicho tawala kinazidi kumong'onyoka.
Source. Tanzania Daima.