Vigogo wengine kutimkia chadema

Napenda sana mipango ya CHADEMA hasa vikikaa kikao vile vichwa vitano, yaani Kamanda Mbowe, Dr Slaa, Zitto Kabwe (nadhani nae yupo mbioni kuitwa Dr, nasikia anamalizia PHD yake huko German) Mzee/Sheikh Arfi na Prof. Mwesiga, wakitoka tu kweney hicho kikao lazima kieleweke tu, si mnakumbuka Operation Sangara? ilianzia kule Tarime 2008, ccm ilitetemeshwa kweli kweli, kwa mara ya kwanza mawaziri na wabunge wa magamba walianza kuzomewa hadhani na rais kurushiwa mawe, sasa kuna M4C, hapo magamba hayapati usingizi kabisa, kweli anayechukia CDM lazima atakuwa mchawi tu, CDM ni noumer!
 
Mbona wapo viongozi kibao wanaokuja cdm,hapa nlipo enyewe mabalozi watatu wa ccm nimewapa bendera za cdm wamehama kwa kuchukizwa na dhulma alofanyiwa lema kortini.mtaani siisikii ccm,na wala cwaoni,naisikia TBC1 na kwa nape.cjui wanamwongoza nani.
 
Kazi nzuri John Heche (M/Kiti BAVICHA TAIFA)
BIG-UP MKUU
Sasa kazi yako inaonekana mkuu.

Vijana wote wa Taifa hili wako nyuma yako.
 
Ole Milya ndo kiongozi wa mtandao wa Lowasa kanda ya Arusha yote. Sasa kama ameipiga chini ujue lazima aondoke na theluthi yake. Safi sana imenikumbusha jinsi shetani alicyokokota theluthi ya malaika alipoasi mbinguni
 
uko lazima ni kaskazini,maana ndio chama chao wachaga...ila nafikiri walishaambiwa urais watauskia kwenye bomba tu..
 
Tanga nani kawaroga? mbona amjifunzi kwa wenzenu wa Arusha? amkeni vijana wa Tanga mlete mabadiliko ya kweli kwa Mkoa wenu, acheni mazowea yasio na tija.
 
Nilishasema haya yanayotokea sasa hivi ni manyunyu tu, mvua za mafuriko ziko around the corner. Ahsante Mungu kwa kunipa uhai huu ili nishuhudie kifo cha CCM.
 
Huyo hana kashfa iliyosikika juu yake, labda kupingana na vijana wa pwani waliosema rais ajaye hatatoka ksakazini na kwamba tayari yupo mifukoni mwa Mkuu wa kaya ndio kashfa kwa CCM cause ni wagumu kuheshimu mawazo ya mtu.CHADEMA haiwezi na haitaweza kusambaratishwa na mamluki toka ccm cause mipango ya chama ni madhubuti na kuna njia za kufuata ili uwe kiongozi wa chama.Milya karibu sana kwenye jeshi la ukombozi na tunategemea kuwa soon utakuwa na vazi la gwanda kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya mkoloni mweusi yaani CHAMA CHA MAGAMBA.
 
Back
Top Bottom