Vigogo wengine kutimkia chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wengine kutimkia chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurunzi, Apr 17, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Kuna habari kwamba baadhi ya wenyeviti wa UVCCM kutoka baadhi ya wilaya za mkoa wa Arusha nao wanatarajiwa kuhamia CHADEMA pamoja na Millya siku chache zijazo.

  Makundi ya vijana mjini hapa walizipokea kwa shangwe taarifa hizo, huku wakiwataka vijana wengine ndani ya CCM kuondoka na kujiunga na CHADEMA kwa kile walichoeleza kuwa itawawezesha kujenga nguvu ya pamoja kuiondoa madarakani CCM ambayo imekuwa ikiwathamini na kuwajali watoto wa vigogo hasa katika suala zima la uongozi .

  "Vijana wa CCM watoke wote waende CHADEMA. Kule vijana wanapewa fursa ya kuongoza na mawazo yao yanasikilizwa; hivyo ni rahisi kupanga mipango ya maendeleo inayotekelezeka hasa wakifanikiwa kuing'oa madarakani serikali ya CCM 2015 ambayo imabaki kuwalundikia vyeo wazee wastaafu huku vijana wakiambiwa wao bado hawana uzoefu" alisema Jackob Mollel, mkazi wa Arusha mjini.

  Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alisema chama kinamkaribisha Millya na wanasiasa wengine walio safi kujiunga nacho ili kuongeza nguvu ya mabadiliko kinayopigania.

  Baadhi ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema hatua iliyochukuliwa na Millya ni mwendelezo wa mmeguko ndani ya CCM na ishara kwamba chama hicho tawala kinazidi kumong'onyoka.

  Source. Tanzania Daima.
   
 2. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,
   
 3. Chillipo

  Chillipo Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuwachukue hao vijana wa Magamba kwa taadhari sana isje kuwa matatizo kwan waweza kuwa mapandikizi katika chama
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  "Not all glitters are gold".
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  But gold glitters, isn't it?
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mkuu Jogi, kwani msimamo wako ni upi ktk hili suala la wana magamba kukimbilia CDM?
   
 7. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ccm ni dume la mbegu wachukueni tu hayo makapi!
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Tutakapoikomboa nchi Usitarajie kuwawekea vikwazo vya kuijenga nchi wananchi waliokuwa na mafungamano na ccm, ama la sivyo hatuijui falsafa ya mzee Nelson Rolilohlo Mandela kuhusu Afrika kisini. Cha msingi ni kuwa watu wabadili mindset kwa nchi yetu. wasiichukulie kimagamba magamba!!!!
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Mkuu, mimi naunga mkono mwana mpotevu kurudi nyumbani. ulinzi wa nyumbani kwangu ni mzuri kum-acomodate naye pia. NAUNGA MKONO. Kwa hawa viongozi kunafaida kubwa imejificha ndani yake, ikiwa ni pamoja na kuwaongezea ujasiri vijana au wazee wenye woga kule vijijini ambako ushindi tunategemea uataanzia huko.
   
 10. kiagata

  kiagata Senior Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wasije toka ccm pekee yake,bali toka vyama mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza mchakato wa mageuzi ya kweli na maendeleo ya Taifa hili.
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nimekuelewa vizuri. Hata mimi sina kinyongo na wageni, cha msingi wanatakiwa kufuata kanuni na maadili ya CDM. Ni furaha iliyoje kwa mzazi kumpata mwana mpotevu!
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  ungemalizia hv ccm ni dume la mbegu chafu za ufisadi! acha waende kwenye demokrsasia na maendeleo kama ni makapi mbona hamkuwafukuza kabla wanapojiengua ndio mnaona makapi!! vipi yale magamba sugu matatu nayo mnasubiri yajivue yenyewe?? CCM jiandaeni tu kutumbukia kwenye shimo walimo rafiki zenu KANU!!!
   
 13. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  yes we can, ccm is like KANU is going to die soon completely
   
 14. U

  Ubhumara Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Chama cha CDM kiwe makini. Ngoma ikivuma sana mwisho hupasuka. Naogopa sana Millya asiwe ni Mrema mwingine aliyetumwa kuja kukithoofisha chama hasa wakati wa uchaguzi mdogo wa Arusha. Anaweza kuwakomalia ateuliwe yeye badala ya Lema na endapo watakataa akakigawa chama ukizingatia Arusha ni IKULU ya CDM inatakiwa ilindwe kama mboni ya jicho. Yangu ni hayo tu. Nilikuwa napita tu.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Wale wanaccm wanaojiona ni wasafi, na sisi tumewathibitisha ni wasafi tunawakaribisha chadema, waje tukaijenge nchi yetu!
   
 16. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kauli za viongozi mbali mbali wa CCM zinaonyesha swala hilo la Milya kuhama limewavuruga sana, isipokuwa nampongeza mwenyekiti wa CCM mkoa kwa busara alizotumia kutokurupuka kutoa shutuma mbele ya waandishi wa habari.
   
 17. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mweeeeeeeeeeeeeeeee.ccm.kuanzia k.njaro,arusha,bbti..chadema.moto.kule tanga,na pwani mtwara lindi .cuf wanawapa joto la kubambua magamba.eti mkama anasema chama chake hakinina mchoko wa akili wala wakimwili.kipo imara.du.mpaka 2015.meng twashuhudia.
   
 18. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  katika msafara wa mamba hata chura wamo. unangalifu kwanza
   
 19. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja sana.
   
 20. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Mzee Mukama hatusikii kuhutubia mkutano wa hadhara zaidi ya kwenye kampeni, unadhani anao mvuto wa kuwakusanya watu awahutubie, iwe mvuto wa chama au wake binafsi!
   
Loading...