Vigogo 'wavamia' maliasili za watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo 'wavamia' maliasili za watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mafinga kwetu, Dec 11, 2010.

 1. m

  mafinga kwetu Member

  #1
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vigogo 'wavamia' msitu wa Sao Hill Send to a friend Saturday, 11 December 2010 08:12 0diggsdigg

  [​IMG]Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Uratibu na Bunge, William Likuvi.

  Mussa Mkama
  WAKATI biashara ya magogo ikiendelea kutikisa vichwa vya viongozi wa serikali, imebainika kuwa mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, kada wa CCM, wakuu wa polisi na maafisa wa Takukuru ndio wanaomiliki vibali vya kuvuna magogo katika msitu wa serikali wa Sao Hill ulio wilayani Mufindi.Biashara ya magogo ambayo ilishamiri mwaka 2005/06 ilipigwa marufu baada ya kuonekana kasoro kwa wasafirishaji magogo nje ya nchi ambao walionekana kukiuka masharti ya leseni zao na wiki iliyopita Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alisema marufuku hiyo inaendelea kwa kuwa ni kinyume cha sheria za nchi.
  Lakini msimamo huo wa Waziri Maige utakuwa mgumu kuutekeleza baada ya Mwananchi kubaini kuwa wanaomiliki vibali vya kuvuna magogo ni baadhi ya viongozi wa serikali ambao badala ya kuvitumia kwa malengo waliyoombea, wamekuwa wakivikodisha kwa wafanyabiashara.

  Baadhi ya vigogo mbao majina ambayo yamo kwenye orodha watu wanaomiliki vibali hivyo ni pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Cyril Chami, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Uratibu na Bunge-, William Likuvi, mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evalista Kalalu, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita na wengine waliotumia majina ya jamaa zao.

  Wengine ni Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene na kampuni ya Rombo Green View inayomilikiwa na mmoja wa mawaziri wa zamani katika serikali za awamu tofauti.
  Katika orodha hiyo pia yamo majina ambayo ubini wake unafanana na baadhi ya viongozi kama vile Selemani Kikwete, Aneth P. Msekwa na Juma Abdallah Zombe.

  Hata hivyo, haikufahamika mara moja kama watu hao wana uhusiano wa moja kwa moja na watu ambao majina yao ya ubini yanafanana na ya viongozi wa serikali.
  Vyanzo vyetu vya habari vimebainisha kuwa vigogo walioficha majina yao wanafahamika na kwamba itakapohitajika watatajwa hadharani na raia wema walioapa kuwa tayari kufanya hivyo.
  Habari za kiuchunguzi zimebaini kuwa kuwepo kwa watumishi hao wa serikali katika biashara ya magogo kumezua mgogoro mkubwa wa kimaslahi kati yao na wavunaji wadogo wanaolalamika kupunjwa kwenye mgao wa vitalu vya uvunaji.

  Uchunguzi umebaini kuwa mgao wa kitaifa unaelekeza meneja mradi wa Sao Hill kugawa magogo yasiyozidi mita za ujazo (cubic metre) milioni moja kwa mwaka.
  Hata hivyo, katika hali inayoweka mashaka, mgao huo unaonekana kuwapendelea zaidi vigogo hao wanaotumia nyadhifa zao kupata vibali bila kuwa na sifa za kupata mgao huo, huku wengine wanaonufaika wakitajwa kuwa ni baadhi ya wawekezaji wakubwa.
  Imeelezwa kuwa masharti yaliyowekwa na serikali kwa kila kibali ni kwamba lazima muombaji awe na vifaa kama malori makubwa ya kukokota magogo (break down), mashine zenye uwezo mkubwa wa kuchana magogo na lazima muomba kibali awe ameajiri wataalamu toka chuo cha misitu kinachotambuliwa na serikali, masharti ambayo Mwananchi imedokezwa kuwa hayajatekelezwa na vigogo hao.

  Katika kipindi ambacho Rais Jakaya Kikwete amewataka mawaziri na wasaidizi wao kuwa tayari kutoa habari kwa wananchi, katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Ladslaus Komba hakuweza kuzungumzia suala hilo kila mara Mwananchi ilipowasiliana naye kuanzia Jumatano iliyopita.
  Badala yake, katika simu zote sita alizopigiwa kati ya Jumatano na jana jioni, Dk Komba alipokea lakini baada ya mwandishi kujitambulisha na kueleza kile anachotaka kufahamu kutoka kwake, alijibu:
  "Kwa sasa niko kwenye kikao nitakutafuta baadaye."
  Hata hivyo, hakutekeleza ahadi hiyo hata mara moja.

  Katika moja ya simu hizo, Dk Komba alisema: “Kuna kitu hapa nakinukuu, naomba unipe muda nitakujulisha.”
  Hata hivyo alipotafutwa baadaye simu yake ilikuwa haipatikani.
  Hata alipofuatwa ofisini kwake, katibu muhtasi wake alieleza kuwa Dk Komba alikuwa ameenda kikazi nje ya ofisi na kumtaka mwandishi amsubiri.
  Mmoja wa vigogo waliotajwa kwenye orodha ya mgao wa magogo, WaziriLukuvi alikiri kupokea mgao huo, lakini akasema aliomba kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari zilizo jimboni kwake Isimani na si kwa nia ya biashara.

  Kwenye mgao huo, Lukuvi amepewa kibali cha kuvuna magogo yenye mita za ujazo 1,000, kulingana na orodha iliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo wa Sao Hill Mufindi. Katika orodha hiyo Lukuvi ni mtu wa 564.
  “Ni kweli niliomba na nikapewa kibali cha kuvuna magogo. Lakini, si kwa nia ya biashara bali kwa ajili ya kupata mbao za ujenzi wa sekonda zilizopo jimboni kwangu, ikiwemo ile iliyoungua moto ya Idodi,” alisema.

  Mbunge wa jimbo la Kibakwe, George Simbachawene alipoulizwa kuhusu suala hilo alikiri kuomba mgao wa uvunaji magogo katika msitu huo, lakini akasema lengo lake si kwa ajili ya kufanya biashara bali ni ujenzi wa madarasa.
  "Ni kweli niliomba wala sibishi, lakini si kwa ajili ya kufanya biashara. Ilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule zetu zilizo katika halmasahauri yetu, kwa sababu kununua mbao zikiwa zimeshaandaliwa ni gharama kuliko kuomba kuvuna magogo na kuchana mwenyewe," alisema Simbachawene.

  Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni jitihada za kumpata Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Cyril Chami na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita zilishindikana.

  Taarifa zinasema kuwa licha ya kujipatia vibali vinavyotolewa bure na Wizara ya Maliasili na Utalii, wamekuwa hawavitumii kwa uvunaji bali huvikodisha kwa wavunaji wadogo kwa gharama ya Sh5 milioni hadi Sh7 milioni kwa kibali kimoja huku ikielezwa kuwa wapo wanaomiliki vibali zaidi ya 10 na wanavitumia kwa majina tofauti.
  Hali hiyo imefanya wavunaji wadogo kupunjwa mgao wa uvunaji magogo tofauti na ilivyokuwa kabla ya watumishi hao wa umma na vigogo kuvamia sekta hiyo.

  Hivi sasa wavunaji wadogo zaidi ya 400 wanaambulia mgao kiduchu na wengine kukosa kabisa, hivyo wengi wamelazimika kufunga viwanda vyao kutokana na kukosa malighafi.
  “Kama watoa vibali ndio wahusika katika biashara hii je, haki itatendeka kwa wavunaji wadogo?,” kilihoji chanzo kimoja.
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,682
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Yaani nimechoka kabisa jinsi inji hii inavyolambwa... Yaani Vigogo wameamia kwenye Magogo....
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndo Tz zaidi ya uijuavyo! Conflict of interest isn't a taboo, only shielding a public servant/leader cum administrator from the ire of the wananchi but buffing his image. In Africa, accountability moves offshore! Unfortunately, they (leaders cum ...) have had to confront the evidence that they can't justify doing what they do.
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mi sioni kosa lao kuomba kibali na kupewa kama wengine. Shida ni pale tu taratibu zinapokiukwa. Hapo nitapiga kelele. Lakini kama ataomba kama watu wengine na kupewa kibali sioni ubaya wowote maana ni haki yao.
  Nimefurahia wale ambao waliomba kwa ajili ya maendeleo ya kujenga shule. Lakini ifuatiliwe ili kujua hakika ndivyo ilivyokuwa wasije wakawa wanasema magogo hayo yalitumika mashuleni kumbe badala yake waliuziwa wauza mbao.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  me siwezi kushangaa ndo maana wanagoma kutoka madarakani hata km wameshindwa!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Halafu sio kila mganga njaa aliyepo madarakani ni kigogo. Tunawapa sifa hata wale wsiostahili kupewa sifa hizo.
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo (tuchukulie investigative journalism imekamilika)......ni wazi kuwa njia nyingine zibuniwe na kutumika.
  Hawa hayawani (huge majority are) hawana haya wala chembe ya huruma. Kuipora wanaipora Tz, kuifilisi, kuingamiza (God forbid), ikiwezekana wagawane (exlusive ownership) na kuacha urithi kwa vinasaba wao. Walitajwa Mwembeyanga ...name and shame. Unfortunately they're shameless monsters.

  Si hili yapo mengi zaidi yalotokea na yanakuja. Ndo maana mbinu za upambanaji lazima nazo zibadilike kuendana na kasi na mahitaji ya wakati. Kusubiri uchaguzi 2015 ni kama kusubiri kaburi au handaki. Muda wa kutenda ni sasa.....Kwani wao si wanaiba na kufisadi sasa? Mbona sisi tunataka kuwapa pumzi kwa kuahirisha vitendo?
   
 8. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Watu walishavamia wamemaliza leo ndio tunasema wamevamia! Hiyo Ndio Tanzania nchi ya AMANI
   
 9. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wote waliotajwa ni CCM.....the muungwana anaulizwa " WHY ARE U STILL POOR???? ANAJIBU "I DONT KNOW" sijui huwa hasomi hata magazeti???? na ndo imetoka hiyo...hakuna changes wala hatua zitakazochukuliwa.........
   
 10. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani si kila kitu tunamlaumu JK wa watu, sasa si unaona yeye angejuaje kwamba hawa jamaa wangepora msitu. Na yeye ana kazi zake pia he can not always be the policeman watching big fishes.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  wewe umelijuwa leo hili?

  Nchi ina wenyewe!! na wenyewe ni wavaa nguo za kijani kwa manjano.

  siyo wale wanaohongwa hizo kofia na fukana za kijani, manjano...wale wanaowagaia hao.

  Nchi hii ni ya viongozi wajasiri mali ,mkuu, kama unataka salama yako na ya nchi, washauri walirejeshe azimio la Arusha.
  Wameshaonja asali, sijui kama watakukubalia!

  na wamesema watafanya kila kitu kwa kasi zaidi na kwa ari zaidi na kwa nguvu zaidi... sijui tulie au tucheke!

  kwa mwendo wetu huu wa jongoo, watatuacha kwa mbali. ndege yao ya uchumi imeshapaa!
   
 12. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2010
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani hawa jamaa wanakera sana. Nyerere aliweka nguvu kuipanda hiyo misitu na kutumia Waswidi, wao badala ya kuendeleza kupanda sehemu nyingine wameanza kuvuna kitu ambacho hawakupanda. Yaani Nyerere angekuwa mroho kama hawa jamaa sijui tungekuwa wapi sasa hivi. Kitu kingine cha kuchekesha mtu anasema aliomba kibali kwa ajili ya kupanda mbao za ujenzi wa shule, si wangeorodhesha majina ya hizo shule na siyo jina la mtu binafsi. Maana hapo inakuwa ngumu kuhakikisha kama kweli mzigo aliouchukua ulifika shuleni.

  Tafadhali viongozi wa Tanzania acheni tamaa
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  I beg to differ mkuu..... Kama kiongozi ataonyesha mfano na kila mmoja atakayeshikwa anakiuka maadili angekuwa anafatiliwa na kuwajibishwa watu tusingefika hapa... the problem is kila mtu anaona you can get away with it kwahiyo anafanya ufisadi.... siku hizi hata messenger ukimtuma sehemu inabidi kwanza umpe rushwa..... nchi imeoza from top to bottom and the problem lies at the top
   
 14. N

  Nonda JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mafinga kwetu,

  Pia rekebisha title yako.... kwani viongozi wetu ni nani? sio watanzania?

  tena wao ndio wametuzidi kwa utanzania, tumewachaguwa kuwa viongozi, vigogo...whatever!
  Ni kuwa wametuzidi kwa utanzania bwana... huwezi kuwa kigogo kama si mtanzania.. waache wavune shamba la bibi.. Kuna mwana JF anasema "if you cant beat them..........."
  Ushauri huo umeshapewa, just polish utanzania wako and join the exclusive club. Bongo hapa!! ndugu yangu.
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,798
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  na
  Sijui orodha ina watu wangapi?
   
 16. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi walijenga shule ngapi na hizo shule zinahitaji magogo kiasi gani hadi wapewe vibali? Hivi hiyo shule ya kutumia magogo ya mita za ujazo 1000 inafananaje?
   
 17. N

  Nonda JF-Expert Member

  #17
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  mkuu,

  Kumbe unawalaumu bure, Miti walipandiwa na baba yao wa taifa, sasa kuvuna urithi waliochiwa kuna kosa gani?

  Au umesoma waraka wa urithi ukakuta majina yao hayamo?

  Pia kama miti imekomaa kuvunwa, ivunwe, ili "nchi" ipate maendeleo!

  Nchi ni watu, na kwa katiba ya Tanzania, huwi mtu mpaka uwe CCM... Unanielewa, ninakuona unatikisa kichwa kumaanisha unanielewa.

  Kama huna Kadi ya kijani, pitia maskani moja ya CCM hapo..halafu piga shati yako ya kijani na kofia manjano, nenda kaombe kibali na wewe ukavune..

  Kufa kufaana , ndio huko. Mwalimu kaipanda wahitimu wake wanavuna.

  This is BOngoland, Mkuu.
   
 18. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #18
  Dec 12, 2010
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwi kwi kwi nimekuelewa mkuu
  Sasa hata kama shamba alipanda baba yao wao wanavuna tu, si inabidi wakumbuke kupanda maana mazao huwa yanaisha shambani
   
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,


  Ile document inayoweka miiko na maadili ndio wameigaia ile mashine inayapenda kuchezana karatasi (wazungu wanasema nini vile?...nimesahau kidogo, mkuu...ninajiuma ulimi..sikumbuki ,mkuu ahh, paper shredder) lakini matokeo yake huwa ikitoka humo huwa vipande vipande viduuchu.. kadogo kweli, hata uwe mtaalamu wa kuunga unga huambulii kitu.

  document imechanwa ile, na kila mtu hakumbuki muliandikwa nini mule...hata hivyo, Mkuu wetu ametengeneza nyengine, mtu achague, siasa, uongozi au/na biashara..
  wengi wameamua kuendelea na uongozi, na kwa kujificha wanafanya biashara.


  At least kwa hili walikuwa wakweli, watutupa jalalani azimio la Arusha, wanafanya vitu vyao...lakini la katiba limewashinda,,wanasema nchi yetu ina mfumo wa kijaamaa,,, sasa hapa wametuweza..wakati wao wameamuwa kuwa mabepari sisi bado wanataka tuamini nchi ni yetu sote... any way, wanakula kwa niaba yetu..


  Uwakumbushie kitu kinachoitwa miiko na maadili ya uongozi...pia uwafundishe maana ya kuwajibika na kuwajibishwa.


  Tuko pamoja , Mkuu.
   
 20. N

  Nonda JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Nilikufahamu vibaya, nilifikiri ni miti ya kiswideni. ya kule huwa inadondosha mbegu yenyewe,unataka ya kuanzia tu halafu iko kwenye auto pilot..mbegu zikipea zinadondoka, inaota mengine.

  kama hiyo miti sio mbegu ya kiswideni,
  hapo itabidi tuwaambie wavune na kupanda. au watatutengenezea jangwa!
   
Loading...