Pole sana mkuu. Haikuwa bahati yako. Mimi nimebahatisha kimoja tu though niliwajazia fomu na wanangu wote. Ayway, usiwe na wasiwasi hop kwenye waiting list na jina lako litakuwepo.Hawa jamaa wa manispaa hovyo kabisa. Wanatuuzia form tena unapanga foleni kuanzia saa kumi usiku lakini kiwanja hupati. Huu ni wizi wa mchana kweuupe. Sipendi
Pole sana mkuu. Haikuwa bahati yako. Mimi nimebahatisha kimoja tu though niliwajazia fomu na wanangu wote. Ayway, usiwe na wasiwasi hop kwenye waiting list na jina lako litakuwepo.
Jamani viwanja 1800, viwanja vya wanaolalamikiwa ni viwanja havizidi 50 inamana 1750 wamepewa walalahoi sasa malalamiko ya nini? mbona tumegeuka kama wale jamaa wanaolalamikia kilakitu? mi ningekuwa mojawapo ya wanaolalamika kama wangechukua viwanja 500.
Viwanja 1800 vimeuzwa kwa wananchi. Kati yao, kuna viongozi wa kada mbali mbali, na kuna ndugu zao ama watoto wao. Majina yaliyoorodheshwa ya "wanene" hao ni kama 50.
1800-50= 1750. Tufikirie tu kwamba "walala hoi" 1,750 au hata 1500 wamepata viwanja, na vigogo 300 wamepata pia. Tunalalamika vigogo wamegawana viwanja!
Katika vigogo hao, wana watoto wakubwa tu...namfahamu Juanita Mramba, anafanya kazi benki moja jijini. Naye amenunua kiwanja. Tunalalamika mtoto wa kigogo kauziwa kiwanja? Hivi, wao hawapaswi kuwa na kiwanja simply because baba yake (tu assume tu) ni kigogo na ana viwanja vingine? Kweli hili ni taifa la walalamishi tu...hata tufanyeje.
Ninadhani pengine kama wamekiuka sheria, kwamba vigogo hawakustahili kuuziwa hata mmoja, na kwamba iwe ni kinyume cha sheria kumiliki kiwanja zaidi ya kimoja Tanzania, basi hawa wangekuwa wana makosa. Wengi wetu tumekuwa tunawekeza mno kwenye kulalamika kuliko kutoa maoni ya namna bora ya kuendesha mambo.
mwabakuki you've said it all, Godbless yougo back to school ujifunze kufikiri...hata kwa umri huu bado huwezi kutambua hata jambo dogo kama hili....kaa soma kati kati ya mistari ili ugundue malalamiko ya wananchi ni nn, je malalamiko yao yanajikita kulalamikia idadi yao hao wanaolalamikiwa au tabia yao? wewe unakomaa na idadi yao tunaofikiri nje ya box tunaichambua tabia na hulka za hawa wanaolalamikiwa..........
Viwanja 1800 vimeuzwa kwa wananchi. Kati yao, kuna viongozi wa kada mbali mbali, na kuna ndugu zao ama watoto wao. Majina yaliyoorodheshwa ya "wanene" hao ni kama 50.
1800-50= 1750. Tufikirie tu kwamba "walala hoi" 1,750 au hata 1500 wamepata viwanja, na vigogo 300 wamepata pia. Tunalalamika vigogo wamegawana viwanja!
Katika vigogo hao, wana watoto wakubwa tu...namfahamu Juanita Mramba, anafanya kazi benki moja jijini. Naye amenunua kiwanja. Tunalalamika mtoto wa kigogo kauziwa kiwanja? Hivi, wao hawapaswi kuwa na kiwanja simply because baba yake (tu assume tu) ni kigogo na ana viwanja vingine? Kweli hili ni taifa la walalamishi tu...hata tufanyeje.
Ninadhani pengine kama wamekiuka sheria, kwamba vigogo hawakustahili kuuziwa hata mmoja, na kwamba iwe ni kinyume cha sheria kumiliki kiwanja zaidi ya kimoja Tanzania, basi hawa wangekuwa wana makosa. Wengi wetu tumekuwa tunawekeza mno kwenye kulalamika kuliko kutoa maoni ya namna bora ya kuendesha mambo.
Thursday, 26 July 2012 20:36 |
Patricia Kimelemeta Mwananchi MLOLONGO mrefu zaidi wa majina ya vigogo umebainika kugawiwa viwanja katika eneo la Gezaulole, jijini Dar es Salaam, ambapo safari hii imo familia ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassani Mwinyi. Jana, gazeti hili lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari iliyoonyesha baadhi ya majina ya vigogo waliogawiwa viwanja na kufanya wananchi wa kawaida kulalamika. Katika uchunguzi zaidi, imebainika kuna orodha ndefu ya majina ya vigogo waliopewa viwanja katika mradi huo wa Gezaulole ambayo inahusisha mawaziri, wabunge, wakuu wa taasisi za Serikali na familia za baadhi ya watu maarufu. Kwa upande wa familia maarufu, imo ya mzee Mwinyi ambaye pia amegawiwa eneo, wengine wana majina ya ukoo yanayofana na ya kwake ambao ni, Asina Mwinyi, Maimuna Mwinyi, Salama Mwinyi na Steven Ali Mwinyi, huku kutoka katika familia yenye jina la Kikwete yumo Ali J. Kikwete. Viongozi wengine maarufu waliogawiwa viwanja hivyo ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emanuel Nchimbi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima. Kwa upande wa watendaji wa taasisi za dola, yumo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, Balozi wa Tanzani nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, SACP Hamdan Makame, ACP John Gudaba, ACP Saada Juma Haji na ACP Mohamed Usi. Mlolongo huo pia unaonyesha majina ya baadhi ya wabunge ambao ni Murtaza Mangungu wa Kilwa Kaskazini (CCM), Mohamed Misanga, (Singida Kusini CCM), Jenister Mhagama (Peramiho CCM), Kheri Ameir (Matemwe, CCM), Kaika Telele (Ngorongoro, CCM), Amina Clement (Koani, CCM) na Ali Hamis Seif (Mkoani, CUF) Pia kuna orodha ya wabunge wa Viti Maalum CCM ambao ni Subira Mgalu, Alshaiymaa Kweygir, Elizabeth Batenga, Josephine Genzabuke, Betty Machangu, Lediana Mngongo na Mwanakhamis Kassim Said. Wabunge wengine wa Viti Maalum CCM ni Mariam Mfaki, Mariam Kasembe, Agnes Hokororo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa pamoja na Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Viti Maalum, Chadema na Ania Said Chaurembo ambaye ni mbunge mstaafu. Majina mengine ambayo koo zake ni za watu maarufu ni pamoja na Ahmed Dau, David Kandoro, Asila Ditopile, Alice Koka, Gemini Suchak, Fidelis Owenya, Filoteus Msigwa, Evelyne Manumba, Fatma Ismail Rage, Jamhuri Kihwelo, Issack Mwangonda, Hijjal Makamba, Joseph Nyambibo, Mbwana Samata, Mohamed Mzimba na Mohamed Mtonga. Wengine ni pamoja na Masanja Manumba, Mariam Mkama, Mansour Al-Maamry, Onesmo Mtasiwa, Musa Chagonja, Omary Shein, Shimbo Shimbo, Sikitu Kijazi, Solomon Kivuyo, Thomas Nyalile na Aisha Sululu (diwani Jangwani, CCM). Pia wamo maofisa watatu wa Bunge ambao ni Herman Berege, Anslem Mrema na Theonest Ruhilabake pamoja na mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Boniface Njombe. Wananchi waja juu Baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke walisema fomu zilizochukuliwa ni zaidi ya 20,000 na kwamba kila fomu ilikuwa ikiuzwa Sh30,000, hivyo kufanya fedha zilizokusanywa kuwa zaidi ya Sh600 milioni. Tayari mlolongo huo wa majina ya vigogo umesababisha baadhi ya wananchi waliokuwa wakisoma majina hayo kulalamikia mchakato wa utoaji viwanja hivyo, huku wengine wakidai kuwa, warejeshewe fedha zao. Tumelipa Sh20,000 kila fomu ya kuombea kiwanja na wananchi tuliojitokeza ni karibu 30,000, lakini majina yanaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waliopata ni vigogo ambao tunaamini wana viwanja mahali pengine, alisema mwananchi mmoja(jina limehifadhiwa). Mwananchi huyo alisema kuwa, hakukuwa na umuhimu wa kutangaza zabuni hiyo kwa sababu tayari walikuwa na majina yao, hivyo walitakiwa kuwakabidhi viwanja vyao badala ya kuwasumbua na kuwatoza fedha. Hali hii inaonyesha kuwa Serikali ipo kwa ajili ya watu wachache, wenye fedha na si wananchi wa kawaida, aliongeza. Mwananchi mwingine (jina tunalo), alisema idadi kubwa ya watu waliokabidhiwa viwanja hivyo ni watoto wa vigogo na wabunge. Aliongeza kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa, hakuna kiongozi atakayewatetea wananchi, kwa vile kila mmoja wao yupo kwa ajili ya kupigania maslahi yake. Wabunge ambao tuliwategemea kutetea maslahi ya wananchi ndio wanaoongoza kwenye orodha ya kujichukulia viwanja, hii inaonyesha wazi kuwa hakuna kiongozi atakayeacha shughuli zake ili kutetea maslahi ya wananchi, alisema. Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Manispaa hiyo vinaonyesha kuwa, halmashauri hiyo imeingiza zaidi ya Sh600 milioni kutokana na uuzaji wa viwanja hivyo. |
Wananchi Tumeanza tambua haki zetu, lakini bado hatujaanza kupambana,
Mjenzi mkuu wa Kigamboni, ni Serikali ya Marekani,
Atajenga Kituo kukubwa, cha Kijeshi chenye, Bandari kubwa, Uwaja mkubwa wa ndege,
Hospitali kubwa, na nyumba za kuishi askari zaidi ya 200,000.
Trilion 16?!! Serikali ya CCM itazinya wapi?? Ili safari ya Mzee Kichaka rais wa Marekani, na zawadi ya vyandarua sijui vya $ M5,
faida yake ni kumegewa kipande cha ardhi, mtakoma na bakuli lenu la umataonya.
Lakini kuna mshiko mkubwa wa karibu $1000,000,000.00 kila mwaka, zitalipwa kama ada ya kunajisi ardhi yetu,
Kuna watu account zao USWIZI zitafura kishenzi.
Mmepigwa sementi ya macho safari hii si changa tena.
Hapo nilipoweka red colour, tumuulize nani atuhakikishie kama masuala hayo ni kweli ndivyo yalivyo??? Wabunge wetu basi wajaribu kuuliza huko bungeni wakati huu wa bunge la bajeti, au kiongozi mkuu wa upinzani amuulize Mhe Waziri Mkuu wakati wa maswali ya papo kwa papo
nooo agyeman ni namna ulivoleta taarifa mwanzo ila sasa nimekuelewa kwamba bei ya 12m ilikuwa ni kwa low density plots. Pole mkuu i didnt mean to say u a liar
hii hapa
Kimbunga, Naona siku hizi kuuza form za viwanja imekuwa ni njia moja wapo ya source ya revenue kwa manispaa zetu. Wanashindwa kubuni njia mbadala za kujipatia kipato. Nakumbuka vya Kinyerezi mpaka leo sijui kinachoendelea. najutia kwanini niliapply. Kuhusu idadi ya fomu, kumbuka pia kama zingetolewa form chache watu wangelalamika. Cha muhimu hao wagawaji wawe fair kwenye ugawaji.Mkuu Rejao hii ni mara ya tatu naliwa vihela vyangu; ilala mara moja na temeke mara mbili. Nilikuwa nikiamka usiku na kwenda kupanga foleni lakini wapi wanakuja kupata watu ambao hawakuwepo kwenye foleni! Mkuu hapa kuna wizi wa mchana. Kama wanajua viwanja ni vichache kwa nini wauze maform lukuki? Viwanja havitakiwa kuwa issue ila.wao wanafanya supply iwe scarce ili demand iwe juu na wao kujipatia chochote.
Hakuna wakumwuliza,
Zaidi ya Kikwete,
Kama huamini,
Subiri mpaka wajenge.
Mama wa Liberia aliomba wajenge kwake,
Wakamwambia wana interest na Indian Ocean siyo Atlantic.
One thing hwa jamaa wakisha ingia hawatoki.
Source; Very Skinny BioMosquito
Acha mambo ya kizamani unatupa orodha ya zamani wakati watu wako serioushii hapa
Vigogo waliopata mgawo Viwanja Dar waongezeka | |
Thursday, 26 July 2012 |
MLOLONGO mrefu zaidi wa majina ya vigogo umebainika kugawiwa viwanja katika eneo la Gezaulole, jijini Dar es Salaam, ambapo safari hii imo familia ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassani Mwinyi. Jana, gazeti hili lilichapisha katika ukurasa wa mbele habari iliyoonyesha baadhi ya majina ya vigogo waliogawiwa viwanja na kufanya wananchi wa kawaida kulalamika. Katika uchunguzi zaidi, imebainika kuna orodha ndefu ya majina ya vigogo waliopewa viwanja katika mradi huo wa Gezaulole ambayo inahusisha mawaziri, wabunge, wakuu wa taasisi za Serikali na familia za baadhi ya watu maarufu. Kwa upande wa familia maarufu, imo ya mzee Mwinyi ambaye pia amegawiwa eneo, wengine wana majina ya ukoo yanayofana na ya kwake ambao ni, Asina Mwinyi, Maimuna Mwinyi, Salama Mwinyi na Steven Ali Mwinyi, huku kutoka katika familia yenye jina la Kikwete yumo Ali J. Kikwete. Viongozi wengine maarufu waliogawiwa viwanja hivyo ni Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emanuel Nchimbi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Manejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima. Kwa upande wa watendaji wa taasisi za dola, yumo Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Polisi, Clodwig Mtweve, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, Balozi wa Tanzani nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, SACP Hamdan Makame, ACP John Gudaba, ACP Saada Juma Haji na ACP Mohamed Usi. Mlolongo huo pia unaonyesha majina ya baadhi ya wabunge ambao ni Murtaza Mangungu wa Kilwa Kaskazini (CCM), Mohamed Misanga, (Singida Kusini CCM), Jenister Mhagama (Peramiho CCM), Kheri Ameir (Matemwe, CCM), Kaika Telele (Ngorongoro, CCM), Amina Clement (Koani, CCM) na Ali Hamis Seif (Mkoani, CUF) Pia kuna orodha ya wabunge wa Viti Maalum CCM ambao ni Subira Mgalu, Alshaiymaa Kweygir, Elizabeth Batenga, Josephine Genzabuke, Betty Machangu, Lediana Mngongo na Mwanakhamis Kassim Said. Wabunge wengine wa Viti Maalum CCM ni Mariam Mfaki, Mariam Kasembe, Agnes Hokororo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa pamoja na Suzan Kiwanga ambaye ni mbunge wa Viti Maalum, Chadema na Ania Said Chaurembo ambaye ni mbunge mstaafu. Majina mengine ambayo koo zake ni za watu maarufu ni pamoja na Ahmed Dau, David Kandoro, Asila Ditopile, Alice Koka, Gemini Suchak, Fidelis Owenya, Filoteus Msigwa, Evelyne Manumba, Fatma Ismail Rage, Jamhuri Kihwelo, Issack Mwangonda, Hijjal Makamba, Joseph Nyambibo, Mbwana Samata, Mohamed Mzimba na Mohamed Mtonga. Wengine ni pamoja na Masanja Manumba, Mariam Mkama, Mansour Al-Maamry, Onesmo Mtasiwa, Musa Chagonja, Omary Shein, Shimbo Shimbo, Sikitu Kijazi, Solomon Kivuyo, Thomas Nyalile na Aisha Sululu (diwani Jangwani, CCM). Pia wamo maofisa watatu wa Bunge ambao ni Herman Berege, Anslem Mrema na Theonest Ruhilabake pamoja na mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Boniface Njombe. Wananchi waja juu Baadhi ya maofisa wa Manispaa ya Temeke walisema fomu zilizochukuliwa ni zaidi ya 20,000 na kwamba kila fomu ilikuwa ikiuzwa Sh30,000, hivyo kufanya fedha zilizokusanywa kuwa zaidi ya Sh600 milioni. Tayari mlolongo huo wa majina ya vigogo umesababisha baadhi ya wananchi waliokuwa wakisoma majina hayo kulalamikia mchakato wa utoaji viwanja hivyo, huku wengine wakidai kuwa, warejeshewe fedha zao. Tumelipa Sh20,000 kila fomu ya kuombea kiwanja na wananchi tuliojitokeza ni karibu 30,000, lakini majina yanaonyesha kuwa asilimia kubwa ya waliopata ni vigogo ambao tunaamini wana viwanja mahali pengine, alisema mwananchi mmoja(jina limehifadhiwa). Mwananchi huyo alisema kuwa, hakukuwa na umuhimu wa kutangaza zabuni hiyo kwa sababu tayari walikuwa na majina yao, hivyo walitakiwa kuwakabidhi viwanja vyao badala ya kuwasumbua na kuwatoza fedha. Hali hii inaonyesha kuwa Serikali ipo kwa ajili ya watu wachache, wenye fedha na si wananchi wa kawaida, aliongeza. Mwananchi mwingine (jina tunalo), alisema idadi kubwa ya watu waliokabidhiwa viwanja hivyo ni watoto wa vigogo na wabunge. Aliongeza kuwa hali hiyo inaonyesha wazi kuwa, hakuna kiongozi atakayewatetea wananchi, kwa vile kila mmoja wao yupo kwa ajili ya kupigania maslahi yake. Wabunge ambao tuliwategemea kutetea maslahi ya wananchi ndio wanaoongoza kwenye orodha ya kujichukulia viwanja, hii inaonyesha wazi kuwa hakuna kiongozi atakayeacha shughuli zake ili kutetea maslahi ya wananchi, alisema. Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Manispaa hiyo vinaonyesha kuwa, halmashauri hiyo imeingiza zaidi ya Sh600 milioni kutokana na uuzaji wa viwanja hivyo. |