BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Date::12/3/2008
Vigogo wa Benki Kuu wanyang'anywa mabenzi
WAKATI uchunguzi wa ufisadi katika ujenzi wa majengo pacha (Twin Towers) ukifanyika, Gavana wa Benki Kuu (BoT) amezuia matumizi ya magari manne ya kifahari aina ya Mercedese Benz yaliyokuwa yakitumiwa na baadhi ya wakurugenzi na gavana huko nyuma.
Hatua ya kuzuia mabenzi hayo ambayo yanagharimu takriban Sh1 bilioni, imekuja wakati BoT katika siku za karibuni imekumbwa na tuhuma za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Duru za uchunguzi kutoka ndani ya BoT ambazo zimethibitishwa na Gavana Profesa Benno Ndulu, zinaonyesha magari hayo ya kifahari kwa sasa yapo katika yadi ya benki hiyo kwa ajili ya matumizi maalumu.
Hivi sasa wakurugenzi wa BoT pamoja na Gavana Ndulu wanatumia gari aina ya Toyota Land Cruiser VX ili kubana matumizi.
Kwa mujibu duru hizo za uchunguzi wa Mwananchi, mabenzi hayo yalikuwa yakitumika zaidi na vigogo wa BoT wakiongozwa na aliyekuwa Gavana marehemu Daud Ballali.
Gazeti hili limebaini zaidi kwamba, marehemu Ballali alikuwa akibadili matumizi ya mabenzi kila mara pamoja na vigogo wengine.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, taarifa za kitaalamu zinasema VX inaingizwa nchini kwa thamani ya Sh100 milioni huku Mercedese Benz ikigharimu takriban Sh250 milioni.
Uchunguzi umebaini pia kuwa gharama za matumizi ya benzi kwa mafuta ni kubwa karibu mara mbili ikilinganishwa na gari aina ya Vx.
Wakati Benzi ikitumia lita moja kwa kati ya kilomita sita hadi saba, Vx hutumia lita moja kwa kati ya kilomita 6 hadi tisa, wakati gharama za vipuri vyake, kwa mfano taa ya nyuma ya benzi ni Sh 1 milioni wakati Vx ni Sh 400,000 hadi 500,00, ikiwa ni mara mbili ya benzi.
Uchunguzi huo wa kitalaamu unaonyesha kwamba wakati benzi hufanyiwa matengenezo (Service) makubwa kwa kila kilomita 10,000, Vx linahitaji matengenezo hayo baada ya kutembelea umbali wa kilomita 5,000.
Katika matengenezo hayo benzi linagharimu kati ya Sh3 hadi 4.5 milioni na Vx kati ya Sh1.5 hadi Sh 2 milioni kwa viwango vya matengenezo ya serikali.
Katika uchunguzi huo, imethibitika kwamba baada ya Profesa Ndulu kuingia madarakani Januari 9, mwaka huu, alizuia matumizi yasiyo ya ya lazima ya magari hayo kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Imethibitika pia kuwa Profesa Ndulu ambaye amekuwa akiisafisha BoT, mara nyingi amekuwa akitumia gari aina ya Toyota Landcruiser Vx na kwamba huku siku moja moja ndipo hutumia benz tena katika matukio maalum hasa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa duru hizo za habari za uchunguzi za Mwananchi Jumapili, gavana baada ya kuingia na kukuta benki ikinuka ufisadi wa aina mbalimbali, alianza kuisafisha ikiwa ni pamoja na kubana matumizi.
Alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Profesa Ndulu alikiri kuzuia matumizi ya magari hayo pasipo na sababu za msingi.
"Ni kweli yapo mabenzi manne, yamekaa nilichozuia ni matumizi yasiyokuwa na msingi kwa magari hayo," alisema gavana Profesa Ndulu.
Hata hivyo, gavana Ndulu alisema magari hayo hutumika wakati wa wageni wa BoT wa kimataifa wanaokuja kwa mwaliko maalumu wa benki hiyo kama vile Shirika la Fedha la Duniani (IMF) au Benki ya Dunia (WB).
Gavana Ndulu alisema wakati mwingine kunapokuwa na matumizi ya msingi ndipo magari hayo hutumika.
Tangu kuingia gavana Ndulu BoT imekuwa katika mabadiliko ya kutaka kuirejesha heshima na imani yake kwa wananchi, ambayo ilitoweka kutokana na tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya.
Ukiacha EPA, kashfa nyingine ni ya matumizi ya zaidi ya Sh500 bilioni kwa ujenzi wa majengo pacha ya ghorofa 18 na ajira tata za watoto 16 wa vigogo.
Hata hivyo, hadi sasa tayari suala la EPA linashughulikiwa na maafisa wa BoT wanaodaiwa kuhusika katika sakata hilo walipandishwa kizimbani.
Suala lingine lilikuwa ajira tata za watoto wa vigogo ambali lishachunguzwa na kumalizwa, huku ukaguzi majengo pacha ukiendelea kufanywa na Kampuni ya wazalendo.
Magari hayo ya kifahari ambayo yalinunuliwa BoT ni sehemu ya magari 40,000 ya serikali, ambayo miongoni mwao 15 ni kati ya Vx na GX ambayo yanapaswa kupunguzwa.